Gazeti la Mwananchi na Habari ya Kiudaku kuhusu Dr. Slaa.

Mie bado gazeti hili sitalisamehe kwa kutulazimisha kuchagua raisi mbovu kwa kumsingizia Dr Salim U- Hizbu!! eti alishiriki kumuua Karume!!
Naona wana benefit tukiwa na raisi mbovu kama hivi!

Kwanza hata hivyo kwani kuna ulazima gani kusalimia!!!?? Yeye ni raisi kweli sawa, lakini ni raisi haramu kwani aliupata kwa njia haramu pia.....

Jambo lingine wa Tanzania tusiwe wepesi wa kusahau...Mwakyembe alisema kuna watu wanataka kumuua yeye na watu wengine akiwemo Dr Slaa...na watu hao wanashirikiana na usalama wa taifa vijana wa JK! Na ni wazi JK anajua kila kitu na kipango yoote inayoendelea kwenye idara hiyo ya usala wa nchi inavyopanga kumuua pi DR Slaa. Lakini JK kauchuna tu..... hachukui hatua..hii maana yake nini kwa mtu anaefikiri kama Slaa!? JK ni muuaji anae muwinda Dk Slaa, sasa unafiki wanini? kumchekea namsalimiasalimia mtu anayetaka kukuua??

Unafiki huu ndiyo uliyo mponza Mwakyembe kumchekea na kukubali post ya mtu anayeiwinda roho yake!!
 
Mwananchi linaanza kuwa non credible paper kama uhuru kama hawatakuwa makini na waandishi makanjanja, toka wametishiwa wamekuwa waoga kweli. Hiyo habari ilitakiwa isomeke hivi "JK amkwepa Dr.waukweli ktk mazishi ya Regia Mtema". Kudos mleta mada.:poa
 
Nimegundua ule usemi kuwa Ajali ikitokea na wakiwepo waandishi wa habari karibu hakuna atakayeokolewa kwani wote watabakia kuchukua picha za tukio kuliko kuokoa..Kumbe wajamaa hawakuenda kumsindikiza mpambanaji walikwenda kutafuta yanayojiri.....Kidonda ndugu
 
Hii ni January sasa gazeti la Mwananchi wana renew kibali cha kufanya kazi nchini, kwa kuwa walimtoa babu wa Bunda (Tyson a.k.a) kauchapa usingizi, sasa babu alikasirika akasema mtakoma kibali kikiexpire.

Ndio maana wanajikomba kwa government, ili waonekane wako upande wao, lakini nawaambia ngoja walambe kibali mwendo mdundo kumchora babu kalala.
 
Mwenye macho haambiwi tazama! We unajua kinachoendelea? Wengi wao hawajui kinachoendelea, kuna watu humu naona kama wanagusa ukweli kwa mbali, najizuiya na kuchelea kusema kama si kuandika mengi. Ukifuatilia kwa makini utakapoona kama unaelewa basi kaa kimya, tafakari moyoni. Hi nchi sina hamu nayo!
 
Gazeti la Mwananchi leo limeandika habari inayosema kuwa Dr. Slaa alimkwepa rais JK jana kwenye mazishi ya Marehemu Regia Mtema. Kwanza mwandishi anasema ilikuwa nyumbani ambako Dr. Slaa aliamua kujichanganya na wabunge badala ya kukaa sehemu ya watu maalum, hata hivyo JK hakuwepo.

Mara ya pili ni baada ya kwenda uwanjani pia Dr. hakukaa sehemu maalum na JK hakuwepo vile vile. Ukiisoma kwa undani habari hii utagundua kuwa imeandikwa kiudaku sana!

Naliheshimu sana gazeti la Mwananchi lakini naona sasa linazidi kupoteza Credibility kadri siku zinavyozidi kwenda. Kama hata rais hakuwa jukwaani ni nani alimkwepa mwenzie?

Mwananchi jirekebisheni kabla hamjaharibika zaidi!

Udaku mtupu, Hawa wamiliki wa magazeti wanajua wasipomwandika Dr Slaa hayanunuliwi
 
Kwa takribani wiki nzima, The Citizen na Mwananchi zimekuwa kama Uhuru.

Nation Media Group inayomiliki Mwananchi ipo ku protect interest za Kenya rejea jinsi magazeti hayo yalivyomshambulia Dr Kamala wa EAC kisa tuu amewawekea ngumu katika suala la ardhi.
Shauri yao hao wanayoyashabikia kama Mazuzu... fools
 
Kama ni muhimu sana kwa JK kuonana na Slaa amzukie nyumbani kwake na ving'ora na wapiga picha!
Heeheeeheeee...! Asante mkuu. Maana watu wanataka kujinyonga kwa sababu wamekosa salaamu ya Dr. Slaa. Kuna HEKIMA inayosema ukimpa salaamu mtu mbaya, unayashiriki mabaya yake! Kazi kwenu wapenda salaamu za mikono.
 
mwananchi siku hizi kweli limeanza kufulia, mimi nilianza kuridharau siku lilipo andika habari za URAIS 2015 hasa ndani ya CDM ikiwataja hata akina J.Mnyika, Wenje nk, nachelea kusema limeshanunuliwa na mafisadi. wanapoteza weledi wao pole pole
 
Gazeti la Mwananchi leo limeandika habari inayosema kuwa Dr. Slaa alimkwepa rais JK jana kwenye mazishi ya Marehemu Regia Mtema. Kwanza mwandishi anasema ilikuwa nyumbani ambako Dr. Slaa aliamua kujichanganya na wabunge badala ya kukaa sehemu ya watu maalum, hata hivyo JK hakuwepo.

Mara ya pili ni baada ya kwenda uwanjani pia Dr. hakukaa sehemu maalum na JK hakuwepo vile vile. Ukiisoma kwa undani habari hii utagundua kuwa imeandikwa kiudaku sana!

Naliheshimu sana gazeti la Mwananchi lakini naona sasa linazidi kupoteza Credibility kadri siku zinavyozidi kwenda. Kama hata rais hakuwa jukwaani ni nani alimkwepa mwenzie?

Mwananchi jirekebisheni kabla hamjaharibika zaidi!

nilipoanza kusom habari hizi kwenye gazeti ambalo tulikuwa tunaamini lilikuwa gazeti lisiloegemea upande wowote ule wa kisiasa zaidi ya kuandika ukweli, mimi binafsi kilewo sikupata fursa ya kwenda kumuaga dada yangu kipenzi Regia so kilichosemwa na mwananchi hakihitaji ushahidi wa uwepo wa mtu katika tukio fulani ndiyo auelewe ukweli,

Akili ya kawaida ya binadamu inatosha kuchambua habari hiyo na mpaka kwenye makala iliyoandikwa na NAibu katibu mkuu wangu wa chama bwana ZItto pale alipo elezea ukaribu wake na marehemu kitu ambacho hakipingiki kipo wazi kuhusu hilo, ila katika makala hiyo hiyo kuna mambo ya msingi yametajwa yakihusu kamati kuu ya chama juu ya uamuzi wa kwenda kumuona Rais juu ya mswaada wa sheria ya katiba, ukisoma kwakina makala hiyo utagudua ya kuwa sasa mwananchi imegeuka kuwa gazeti la udaku na lenye niambaya ya mabadiliko ya taifa hili kwasasa. Gazeti hili kwasasa haliendeshwi kwa maadili ya taalum ya uandishi ya kuhakiki habari toka upande mwingine zaidi ya kuchukua habari kiushikaji ushikaji na kuupindisha ukweli,

Sikuona sababu za msingi kichwa cha habari kusema : Siri ya chadema kwenda kumuona Rais ya fichuka. Hii habari ukiisoma ukairudia mara tatu amazaidi kisha ukatafakari utajua nijinsi gani sasa Ukweli umeanzwa kuminywa na gazeti hilo. Haiwezekani ishu ya kamati kuu ya chama isemwe kuwa fulani ndiyo aliyesema, hapana huu ni upuuzi na chama kinapaswa kichukue hatua zaidi za watu kama hawa . Japokuwa mimi siyo mjumbe wa kikao hicho ila naamini yalikuwa siyo maamuzi ya mtu mmoja bali hoja hiyo ilikuwa ni moja kati ya maadhimio ya kamati kuu ya kuadhiamia kuhusu maswala ya kukijenga chama na ushiriki wa chama katika shughuli la kulijenga taifa nasiyo maamuzi ya mtu mmoja bali ni maoni ya watu yaliyokusanywa na kuwekwa kwenye mpangilio wa kitaasisi. Mwananchi kwasasa ni udaku halina maana tena na hiliswa nilazima watu mbalimbalimtuliliripoti kwenye makao makuu yao kenya
 
Back
Top Bottom