Gazeti la Mwananchi kupanda bei

Hata mimi nimeshangaa sana kwani mapato ya magazeti, duniani kote, sio bei ya gazeti bali matangazo ya biashara ndani ya magazeti, na Mwananchi kwa hili wapo juu sana compared na magazeti mengine. Vinginevyo, unaweza hata kulitoa gazeti bure, ili mradi uwe na circulation nzuri tu itakayokupa good ratings.

Mchambuzi;
Ni kweli mapato ya magazeti hutegemea matangazo; kwa Tanzania kama gazeti lako halipambi habari za chama chetu na matangazo hupati; wafanyabiashara wengi wa Tanzania ni wababaishaji na wakwepaji kodi na wengi wamaejikinga nyuma ya mgongo wa chama chetu.

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Tatizo ni kwamba Mwananchi ndio wameanzisha huu utaratibu wa kupandisha bei za magazeti, tusubiri kidogo na media houses zingine zitafuata. Kwa hiyo tujiandae kwa ongezeko kama hilo kwa magazeti mengine. Hata hivyo, la kuzingatia ni iwapo ongezeko hilo litaenda sambamba na uongezaji na uboreshaji wa contents za gazeti husika? Tusubiri kidogo ili tuone.
 
Jamani kwa nini mnaumiza vichwa, Jamii Forums mbona kuna kila kitu, after every second unapata updated news.
Sio habari tu..magazeti yana kazi nyingi..sasa chapati, vitumbua na samaki wa kukaanga huku uswazi tutafungia nini?....teh! teh! teh!
 
Jamani mumesahau chain impact ya ongezeko la umeme?
Tutegemee kila bidhaa inayotumia umeme kuzalishwa ipande kwa 40% kama TANESCO walivyopandisha
 
kwani gazeti lipo moja tu?yapo magazeti kibao ambayo yana ubora kama kawaida.

we subiri kidogo tu na media house nyengine nazo zitatangaza ongezeko la bei sasa hivi.

usitarajie kwamba mwananchi wameamua kupandisha bei bila kuwasiliana na wenzao, walichofanya wao ni kukubali kupima kina cha maji kwa kuingiza miguu!! media house nyengine zikiona circulation ya mwananchi inakwenda vizuri nao wanapandisha mara moja.
 
Kutoka shilingi 5oo mpaka 8oo du ni kali sijui tunaenda wapi ?

Tutaenda kuhudhuria mihadhara ya dini, no entrance fee. Umeme umepanda bei, karatasi zimepanda bei, kodi za pango zimepanda, mafuta yamepanda bei, unga umepanda bei, mchele umepanda bei, sukari imepanda bei, nyama imepanda bei,nauli zimepanda, posho zimepanda, sitting allowance zimepanda, wauzaji wanadai ongezeko la posho, wasomaji wanazidi kuongezeka.................UNATEGEMEA NINI?
 
Mimi nilikuwa nanunua gazeti hili j3, j4, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi, kwa kweli siku hizo ilikuwa never miss! Jana kijana anayeuza kabla sijanunua akaniambia nisome juu kabisa kulia (paliandikwa: kuanzia tarehe 1/2/2012, bei ya gazeti itakuwa sh. 800/= ............. kutokana na gharama kupanda blah blah blah), ndipo nilipomwambia yule dogo kuwa jana ndo ilikuwa mwisho wangu wa kununua gazeti hilo! Kwa kweli ilikuwa ni mazoea tu maana si wazuri kiasi hicho na mara kwa mara typing errors na hata hicho kiswahili kilikuwa hakiandikwi vizuri! Kwa bei hiyo.........labda kama na mimi nitaongezewa posho ya angalau 200,000/= kwa siku ndo nitaweza kununua!
 
Wakuu tupunguze manunuzi. Badala ya mara 7 kwa wiki, tufanye mara 2 au 3 kwa wiki. Hapo naamini watakoma ubishi! Wa-Kenya wako kwenye shamba la bibi!
 
Hilo ni ongezeko la asilimia sitini (60%).

Sababu za ongezeko hili bila shaka zitakuwa ni hizi (wenyewe watathibitisha ama kukanusha):
1. Kupanda kwa posho na mishahara ya waandishi wao, wanaofanya kazi kubwa ya kwenda huku na kule kutafuta na kuripoti habari!
2. Kupanda kwa gharama za uendeshaji kufuatia ongezeko la bei ya umeme.

Uko sahihi kabisa ndg
 
Kabla ya juzi gazeti la MWANANCHI tumekuwa tukilnunua wa bei ya shs. 500.

Wakati likiongoza kutoa habari za upandanaji wa posho za wabunge, gazeti hilo nalo limeamua kujipandishia bei ili kukidhi gharama za uendeshaji kama wabunge wanavyojiongezea posho kukidhi gharama zilizoongezeka za kuishi Dodoma.

Wakati posho ya wabunge inajadiliwa nchi nzima kupanda toka shs. 70,000 kwenda 330,000 gazeti hili nalo limepandisha bei kwa 60%, kwani lilikuwa linauzwa shs. 500, sasa kulipata inabidi ujikamue shs. 800.

Imekuwa ikiulizwa, je gharama zimepanda kwa wabunge Dodoma tu. Sasa inawezekana swali lilelile likaulizwa, je gharama zimepanda kwa MWANANCHI tu na si magazeti mengine.

Natumaini mtaitendea haki hii thread yangu.
 
Back
Top Bottom