Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 42
Ni jambo la kusikitisha kuwa gazeti la Mtanzania lipo si kwa ajili ya maslahi ya taifa bali kuangamiza nchi.
Katika habari iliyotoka leo 21.11.09 kwenye gazeti hili wanamtetea Lowasa kuwa kuna watu wanazungukia jimbo lake kutaka kugombea. Kibaya zaidi ni pale utetezi wao wa Lowasa unapoingiza mtazamo wa kuleta ubaguzi wa kikabila.
Gazeti hili linaandika eti Wamasai wameonewa vya kutoka sasa basi, kwani Lowasa ni Mbunge wa Wamasai? Jimbo la Lowasa kwa vyovyote vile kuna makabila mengine pia, na utetezi wa kupandikiza ubaguzi wa kikabila haukubaliki katika nchi yetu. Mbunge vilevile yupo kwa ajili ya taifa zima, siyo kwa ajili ya makabila yao, ndio maana huapa.
Hili ni gazeti linalostahili kupuuzwa na watanzania wote. Jukwaa la wahariri nalo pia litoe karipio lake kwa gazeti hili kwa kutoa utetezi wa kikabila.