Gazeti la Mtanzania: Utetezi wa kikabila wa Lowassa haukubaliki

Tumechoka na maada za namna hii. Invisible nashauri ufunge maaada za namna hii zinaongeza traffic tu isiyo na tija.

Umechoka sio tumechoka....usiisemee mioyo ya wana JF

NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU
 
Mzee Mtei, hebu muulize mkweo Freeman kwa nini anaachia gazeti lake liwapambe mafisadi? Anajua kwamba wahariri wa Tanzania Daima wanamtumikia Fisadi Papa Rostam? Au na yeye ameshawekwa mfukoni? Hili gazeti lilipaswa kuwa mstari wa mbele kupambana na ufisadi.

Ni kweli kabisa -- huyo mhariri wake Kibanda ni ndumila kuwili, anauma na kupuliza - anawateteea kina Rostam kwa kiujanjajanja sana. Ni mtu hatari kwelikweli. Ni bora hili likaangaliwa ama sivyo Mbowe naye ataanza kutiliwa mashaka kwamba ni swahiba mkubwa wa RA. kama vile wale viongozi wa CUF -- Jussa na Professa walivyo katika uswahiba na RA.
 
====
Mzee Mtei
Shikamo na habari za siku nyingi.
Kama kweli ni wewe mwenyewe napenda kushauri kama nilivyoshauri wana Chadema wengine, kuwa kwa sasa ni vema mambo ya ndani ya chama yakajadiliwa huko chamani na siyo humu JF.
Utaitendea haki Chadema, Mbowe na sisi tunaoipenda ukitekeleza hilo na kuwaambia wengine wafanye hivyo. Natafuta simu kukupigia sasa hivi.

none sense! kuna mambo nyeti ya kujadili ndani ya vikao vya chama na yapo yanajadiliwa wala Mzee Mtei hajayaleta hapa. Mzee mtei amejibu hoja alizoulizwa na wana JF wakitaka kujua kwa hakika kile wanachokisikia magazetini....mara anaendesha chama kifamilia!...haya mambo hayana haja ya kujadiliwa ndani ya vikao vya chama. haya mambo tunataka tujue tulio nje ya michakato mbalimbali ya chama kuwa nini kinaendelea chadema na je ni sahihi kukipa dhamana ya kutuongoza?
sasa wewe unaona haya yakajadiliwe kwenye chama wakati wapiga kura tupo nje na tunataka kujua kinachoendelea chadema, tuwapime !
hebu acha siasa cha chama fulani cha kujifanya wanapenda kumaliza mambo ndani ya vikao bila kujali athari ya kisaikolojia unayowapata wanaowaongoza katika jambo hilo wanalotaka kujificha kulimaliza.
Amka kijana jiamini mbele ya jamii ya tz ukamate ridhaa ya kuongoza acha mambo ya vikao vya ndani katika ajenda za aina hii. Yapo mambo yakuishia ndani na yapo ya kutueleza kwa ufasaha ili tuwapime

MZEE MTEI HONGERA SANA KWA KUTUELEZA MAJIBU YA MASWALI YETU JUU YA CHADEMA......sasa tuna/nina nafasi ya kutafakari majibu yako na kuyatendea kazi ...pale ambapo tutapenda ufafanuzi zaidi usisite kutuhabarisha kwani muungwana ni vitendo

NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU
 
Ole Naiko aliwahi kutaka kumtetea Lowasa kwa kudai eti watu wa Arusha tunakuwa 'targeted.' nadhani aliona kosa lake mapema na kufunga mdomo.

Kama hilio ni gazeti la RA yeye mwenyewe kabila lake liko wapi kumpa kura za Igunga?

Narudia tena, EL lazima akubali kwamba U-Rais hapati tena. Ni ndege aliyeweza kumurudia maadamu Ufisadi hataki kuacha.

Pale Morogoro nasikia kajichukulia kiwanja cha Magereza kwa kusaidiwa na mkuu wa mkoa na sasa anajenga hoteli. huyu jamaa hakomi ngo! Kala nyama ya mtu tangu amfuriko ya Tanga.
 
Ukiona hivyo kuna mambo matatu kwa uchache: aidha gazeti lifilisika kimawazo au kisiasa, anayemtetea naye kakumbwa na tatizo la kufilisika na mtetewa (Lowassa) naye anaelekea kufilisika kiamwazo na hivyo wote hawa hawatufai kwenye hatima ya uongozi wa nchi yetu.
 
Pole Mzee Mtei: usisikitike sana kwani hili gazeti haliuzi nakala nyingi, limeporomoka kiasi kwamba jumla nakala zinazouzwa kwa wiki moja nzima ni chini ya theluthi moja ya nakala zinazouzwa na Mwanahalisi.

Kuporomoka huko kumetokana na kuwekwa Deatus Balile kuwa mhariri kama miezi miwili sasa. Balile anasifika kwa kazi moja kubwa -- kulamba viatu vya RA pamoja na EL -- hadi anachefua kufuatana na ripoti kutoka hapo New Habari.

Ripoti pia zinasema kuwa siku hizi hata yule hussein Bashe -- wa kitengo cha usambazaji naye huingilia katika kuweka headline katika stori ya mbele.
Yeye huyu alifukuzwa Mwananchi kwa kuendesha genge la wizi wa magazeti. Msomali huyu ameahidiwa na RA kuwa atamrithi Selelii mwaka kesho.

Kichwa cha thread ni Mtanzania na ukabila, wanaolaumu Mtanzania wanafanya exactly the same na wanachopinga!
 
Geza Ulole said:
Utofauti wa makabila ya wanaoishi Manyara, Kilimanjaro na Arusha ni pale tu Missionaries walipokuja na kuamua ku-settle milimani kwa vile Massai were hostile, ambapo Wachagga na makabila mengine kama Wameru waliwapokea (wachagga walikuwa wakikaa milimani kwa kuogopa kukaa on plain grounds ambazo zilikuwa grazing grounds for those Massai) na as a result wakaingia Ukristo as some sort of seeking protection (si unajua Wild Massai walikuwa wanakanyaga kila mtu aliyekutwa in their territory n ku-raid kila kijiji kipindi cha kiangazi kukusanya ng'ombe wao waliopewa na Ainga (Massai God))! Ila haya makabila yote yana uhusiano ukiangalia vizuri kuanzia Warombo, Wameru n.k. within the region wanashaabihana na Wamassai kuanzia mila zinafanana ukiangalia vizuri walikuwa wanatoboa, kutahiri wanawake na kuvaa kama Massai those times! the rest is history jamani tusianze haya!

Geza Ulole,

..hujawatendea haki Watawala wa 'Kichagga' waliopigana vita dhidi ya Wakoloni.

..pia hujawatendea haki Wameru ambao waligombana na wazungu kuhusu ardhi mpaka kupeleka suala lao umoja wa mataifa.

..kama sijakosea Japhet Kirilo alikwenda UN kabla Nyerere,Tanu,na the rest of Tanganyika, hawajaelewa kwamba wanaweza kwenda huko kuwakilisha matatizo yao na Muingereza.

..Mangi wa 'Kichaga' waliungana na Wazungu kutokana na uchu wa madaraka, choyo na nia ya kuwamaliza wapinzani wao. kabla ya hapo walikuwepo Mangi walioungana na Waarabu kukamata utumwa jamii zilizowazunguka.

..pia nakuomba urejee historia ya Ngorongoro Conservation Area[eneo la malisho ya Wamaasai] utaelewa jinsi Mkoloni alivyokuwa mshe.nzi na jinsi ambavyo hakuwa na staha wala hishma kwa jamii yoyote ile ya Kiafrika.

NB:

..Wamisionari wali-settle milimani kwa kuogopa magonjwa maeneo ya tambarare, na kuvutiwa na hali ya hewa nzuri ya milimani.

..vilevile mazao mengi waliyo-introduce kama kahawa na chai yalikuwa yanastawi maeneo ya milimani na siyo tambarare.
 
Mtanzania na Rai naomba watanzania tusiyanunue ili hao akina bashe wakome.

Mkuu Magezi,

Mimi nilishaacha siku nyingi kununua Mtanzania na Rai ingawaje enzi hizo za`Generali Ulimwengu, nilikuwa siwezi kulala bila kusoma gazeti la Rai.

Watu wote wanaoitakia nchi hii mema, wanapashwa kutonunua magazeti haya (Mtanzania na Rai).

Tiba
 
Mkuu Ushauri wako Mzuri sana lakini Je Una uhakika haya lagazeti yanategemea Mauzo yake ili yajiendeshe?

Hata kama hayategemei mauzo ili kujiendesha.Mkuu, walau tuoneshe kuwakataa kwa kuacha kununua magazeti yao yasiyo tija.

Wote tuseme (na kutekeleza): namkataa FISADI na ufisadi wake wote,na fahari zake zote.
 
Pole Mzee Mtei:
Kuporomoka huko kumetokana na kuwekwa Deatus Balile kuwa mhariri kama miezi miwili sasa. Balile anasifika kwa kazi moja kubwa -- kulamba viatu vya RA pamoja na EL -- hadi anachefua kufuatana na ripoti kutoka hapo New Habari.

Ripoti pia zinasema kuwa siku hizi hata yule hussein Bashe -- wa kitengo cha usambazaji naye huingilia katika kuweka headline katika stori ya mbele.
Yeye huyu alifukuzwa Mwananchi kwa kuendesha genge la wizi wa magazeti. Msomali huyu ameahidiwa na RA kuwa atamrithi Selelii mwaka kesho.[/QUOTE]

Very serious!

Hao wana tabora watakuwa wajinga kumpa MSOMALI ubunge
 
Wewe acha kutisha watu, hapa JF tunaangalia pande zote, kama mtu ameleta hoja anapingwa kwa hoja zake. Sasa kama wewe unadhani hilo linahitaji kuwa na jina halisi mimi siwezi kukusaidia kwa hilo. Kwani una haki ya maoni yako

Hoja yako wewe nini au ndio unakodolea hoja za wenzako? TOA HOJA! Au hujui maana ya hoja
 
Haya mapambano yamefikia mahali pabaya sana; Ningependa kuisoma hiyo makala kwanza..

heshima mbele mkuu..

nadhani yamefikia mahali pazuri sana maana watu wanachukua upande hakuna kuwa katikati. hii inasaidia kujua nani ni nani, yuko wapi na anafanya nini kuendeleza au kupinga ufisadi.

kwa kimombo hii ni blessing in disguise.....
 
Wakuu zangu, kila mara nasikia kwamba kuna mtu alikwenda UN kabla ya Nyerere kudai Uhuru.. Je, mnaweza kuthibitisha maneno haya nipate kuelewa vizuri. Itakuwa vizuri kama mtaniwekea link yoyote inayothibitisha..
 
Geza Ulole,

..hujawatendea haki Watawala wa 'Kichagga' waliopigana vita dhidi ya Wakoloni.

..pia hujawatendea haki Wameru ambao waligombana na wazungu kuhusu ardhi mpaka kupeleka suala lao umoja wa mataifa.

..kama sijakosea Japhet Kirilo alikwenda UN kabla Nyerere,Tanu,na the rest of Tanganyika, hawajaelewa kwamba wanaweza kwenda huko kuwakilisha matatizo yao na Muingereza.

..Mangi wa 'Kichaga' waliungana na Wazungu kutokana na uchu wa madaraka, choyo na nia ya kuwamaliza wapinzani wao. kabla ya hapo walikuwepo Mangi walioungana na Waarabu kukamata utumwa jamii zilizowazunguka.

..pia nakuomba urejee historia ya Ngorongoro Conservation Area[eneo la malisho ya Wamaasai] utaelewa jinsi Mkoloni alivyokuwa mshe.nzi na jinsi ambavyo hakuwa na staha wala hishma kwa jamii yoyote ile ya Kiafrika.

NB:

..Wamisionari wali-settle milimani kwa kuogopa magonjwa maeneo ya tambarare, na kuvutiwa na hali ya hewa nzuri ya milimani.

..vilevile mazao mengi waliyo-introduce kama kahawa na chai yalikuwa yanastawi maeneo ya milimani na siyo tambarare.

Mangi wa 'Kichaga' waliungana na Wazungu kutokana na uchu wa madaraka, choyo na nia ya kuwamaliza wapinzani wao. kabla ya hapo walikuwepo Mangi walioungana na Waarabu kukamata utumwa jamii zilizowazunguka.

Massai land ilikuwepo na mpaka sasa ndo zilipo hizo mbuga na hamna kabila lililo ruhusiwa kukaa kwenye Massai Land na sio Wameru au wachagga walipenda kukaa milimani (huo ndo ukweli all steppe/Nyika/savannah land was Massai)! Kama kuna uchu wa Mangi wa Kichagga hilo unajua wewe ila historia inasema Missionaries couldn't spread the word of Gold to Massais cause they were not read to interact with foreigners na hao Wameru unaosema walienda UN kwa ajili ya masuala ya ardhi sijakataa ila ukweli upo hata early 80s koo za Kimeru zilikuwa na hata sasa zina-ugomvi juu ya ardhi wenyewe kwa wenyewe sijui ardhi ipi unayojitambia hapa! na Wamisssioanari waliingia huko ndo maana wengi wao ni Lutherans! sasa sijui unabisha nini? Hamna cha uchu wa Madaraka ni survival of the fittest hata Dubai, Saudi Arabia, Quatar na Kuwait leo hii wananunua usalama toka US japo ni matajiri wa kutupa! afterall Missionaries walikuwa hawagawi madaraka walikuwa wanafundisha dini na huduma kama elimu na hospital basi! Madaraka yalikuja baada ya kutawaliwa! Weka hoja ufahamishwe!
 
Geza Ulole,

..ninachokueleza mimi ni kwamba Wamisionari na Wakoloni hawakuvutiwa na ardhi ya Wamaasai na ndiyo maana mpaka leo Wamaasai wamebahatika kuwa na ardhi yao hapa Tanzania. Kenya mkoloni aliitamani ardhi ya Wamaasai,Wanandi,Wakikuyu, na aliichukua kwa nguvu.

..Watawala wa Saudia,Kuwait,..wananunua usalama kwa USA ili waendelee kukaa madarakani. kwa msingi huohuo Mangi wa Kichagga nao walikuwa wananunua usalama toka kwa Wageni[Waarabu,Wazungu] kutokana na uchu wa kuendelea kukaa madarakani. katika hili naona tunakubaliana.

..by the way, Mzungu pia hakuchukua ardhi ya Wachagga. alipofika Uchagani alibaini kwamba ilikuwa rahisi kuwatumia Wachaga kwa kuwalimisha kahawa bila kutaifisha ardhi yao. Hali hiyo ni kinyume na kwenye maeneo ya Wameru ambapo Mzungu aliamua kunyang'anya ardhi.
 
Bora ya hao Wachagga waliolimishwa na kupata hata angalau hela ya kujikimu hata ikiwa ya kubabaisha zaidi ya kunyang'anywa kama ulisema hapo juu! nathani hii topic imekosa mwelekeo maana naona hapa swala ni kuhusu Wachagga ndo limewasisimua wengi zaidi ya ukweli kwamba gazeti la Mtanzania linatia uchochezi! Na jamii hizi zote wameru, Wachagga na Wamassai zimeishi huko kwa muda mrefu (Wamassai wakitawala sehemu kubwa) na mtu kudai Wamassai wanaonewa ni sawa na kujipiga risasi mguuni wakati ni serikali hiyo hiyo anayoitetea ndo inaongoza ukwapuaji wa ardhi huko umassaini na sio jimbo la Arusha Mjini pekee! Huo ndo utetezi wangu!
 
Kafiribangi

Pole Mzee Mtei:
Kuporomoka huko kumetokana na kuwekwa Deatus Balile kuwa mhariri kama miezi miwili sasa. Balile anasifika kwa kazi moja kubwa -- kulamba viatu vya RA pamoja na EL -- hadi anachefua kufuatana na ripoti kutoka hapo New Habari.
Ni kweli, huwa anachefua kama wengine wanavyochefua kwa kuwaandika ama kuwaita kila wasiotaka kudandia kile wakiitacho "vita ya ufisadi" ama wanaohoji usafi na umakini wa wanaoitwa "wapiganaji wa ufisadi" kuwa nao ni mafisadi.

Ripoti pia zinasema kuwa siku hizi hata yule hussein Bashe -- wa kitengo cha usambazaji naye huingilia katika kuweka headline katika stori ya mbele.Yeye huyu alifukuzwa Mwananchi kwa kuendesha genge la wizi wa magazeti. Msomali huyu ameahidiwa na RA kuwa atamrithi Selelii mwaka kesho
Kosa lake ni ahadi ya ROSTAM, tuhuma za wizi wa magazeti ya MWANANCHI ama usomali wake?

Very serious!

Hao wana tabora watakuwa wajinga kumpa MSOMALI ubunge

Which is serious, kuwaona wajinga watakaompa ubunge "MSOMALI" ama watakaomnyima na kuwashutumu watu wa Tabora kuwa wajinga kwa kumpa ubunge MSOMALI ambaye ni raia halali wa Tanzania?

omarilyas
 
Ukiacha Mtanzania, kuna Rai la kila wiki ambalo nalo kazi yake kubwa ni kuwatetea RA na EL na mafisadi wengine kwa ujumla. Mhariri wake ni Boniface naye pia ni hodari kulamba viatu vya RA kwa namna ya kutia kichefuchefu. Kwa ujumla pale New habari kuna mtandao wa waandishi wa RA ambao unaundwa na Muhingo, Mwakiteleko, Balile, Manyerere, Makene, Sarah Mossi, Matinyi, na Mayage. Mtandao huu unashirikiana kwa kiwango fulani na Kibanda wa T. Daima.

Mtandao huo umesaidia sana kuporomoka kwa mauzo ya magazeti (ukiacha yale ya michezo) kiasi kwamba hata mishahara ni matatizo makubwa -- tofauti na ilivyokuwa wakati Rosemary Mwakitwange akiwa CEO.

Nadhani hata Tanzania Daima nayo mauzo yameporomoka. Inashangaza sana kuona watu kama Kibanda nao wameingia kwenye genge hilo la kulifanyia Taifa ufisadi kwa kalamu zao! Kwa maana hiyo hiyo hata makala za 'Rais Wangu' za kila Jumatano zinakosa mvuto.
 
Back
Top Bottom