Sagini asimikwa Uchifu Butiama apewa jina la Mshora

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Wazee wa Mila Wilayani Butiama Mkoani Mara wameiomba Serikali iweze kuwachukulia hatua Wanasiasa ambao wamekuwa wakileta ukabila, ukanda na udini kwenye mambo ya maendeleo hali inayoweza kuleta machafuko baina yao.

Wameeleza hayo wakati wakimsimika uchifu Jumanne Sagini ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kumpatia jina la Chifu Mshora.
Naibu.JPG

Naibu 2.JPG

Wakizungumza katika hafla hiyo baadhi ya Wazee wa Mila wamesema kuna Wanasiasa wanatengeneza matabaka baina ya Wazanaki na Wakwaya huku Rais wa kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere alipinga vikali vitendo hivyo.

"Sisi kama Wazee wa Mila Wakizanaki tunakemee vikali vitendo hivi vya kibaguzi vya kikabila, kidini na kikanda kwani ubaguzi hauwezi kuleta maendeleo na tunaahidi kuwa bega kwa bega na Mbunge wetu katika kufanikisha Maendeleo ya Wilaya yetu ya Butiama," wamesema.

Akizungumza baada ya kusimikwa kuwa chifu wa Wazanaki na kupewa jina la Chifu Mshora Mhe. Sagini amesema yupo tayari kushirikiana na Wazee katika jambo lolote hasa ukizingatia kuwa wao ndio waanzilishi wa Taifa hili.

"Wazee wangu nimepokea kwa mikono miwili uongozi huu mliyonikabidhi leo hakika siwezi kuisahau siku hii adhimu katika maisha yangu nitashirikiana nanyi kwa kila jambo katika kuiletea Maendeleo Butiama yetu na niwaonye wale wote wanaodharau Wazee wa Mila kuacha tabia hiyo mara moja kwani hawa ndiyo waliyotulea mpaka tumefika hapa."

Ameongeza kuwa maji hayawezi kuletwa na udini, miundombinu haiwezi kuletwa na ukabila wala vituo vya afya haviwezi kuletwa na ukanda sisi wote ni ndugu kwa pamoja tuijenge Butiama yetu.
 
Sasa mbona wao ndio wanapenda ukabila, huyo Jamaa kawajaza sana serikalini wa Kabila, hasahasa idara ya elimu Karibu kila wilaya Kuna Aisha afisa elimu Au takwimu Au taaluma tokea huko
 
Wazee wa Mila Wilayani Butiama Mkoani Mara wameiomba Serikali iweze kuwachukulia hatua Wanasiasa ambao wamekuwa wakileta ukabila, ukanda na udini kwenye mambo ya maendeleo hali inayoweza kuleta machafuko baina yao.

Wameeleza hayo wakati wakimsimika uchifu Jumanne Sagini ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kumpatia jina la Chifu Mshora.
View attachment 2844373
View attachment 2844375
Wakizungumza katika hafla hiyo baadhi ya Wazee wa Mila wamesema kuna Wanasiasa wanatengeneza matabaka baina ya Wazanaki na Wakwaya huku Rais wa kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere alipinga vikali vitendo hivyo.

"Sisi kama Wazee wa Mila Wakizanaki tunakemee vikali vitendo hivi vya kibaguzi vya kikabila, kidini na kikanda kwani ubaguzi hauwezi kuleta maendeleo na tunaahidi kuwa bega kwa bega na Mbunge wetu katika kufanikisha Maendeleo ya Wilaya yetu ya Butiama," wamesema.

Akizungumza baada ya kusimikwa kuwa chifu wa Wazanaki na kupewa jina la Chifu Mshora Mhe. Sagini amesema yupo tayari kushirikiana na Wazee katika jambo lolote hasa ukizingatia kuwa wao ndio waanzilishi wa Taifa hili.

"Wazee wangu nimepokea kwa mikono miwili uongozi huu mliyonikabidhi leo hakika siwezi kuisahau siku hii adhimu katika maisha yangu nitashirikiana nanyi kwa kila jambo katika kuiletea Maendeleo Butiama yetu na niwaonye wale wote wanaodharau Wazee wa Mila kuacha tabia hiyo mara moja kwani hawa ndiyo waliyotulea mpaka tumefika hapa."

Ameongeza kuwa maji hayawezi kuletwa na udini, miundombinu haiwezi kuletwa na ukabila wala vituo vya afya haviwezi kuletwa na ukanda sisi wote ni ndugu kwa pamoja tuijenge Butiama yetu.
Mmmmh Pesa ni adui Mbaya SANA
 
Back
Top Bottom