Gazeti la 'HabariLeo' na taarifa ya kifo cha Mh. Mtema

Nipo tangu jana mkuu.

Hivi Tabata Chang'ombe gani hiyo. Kwani mimi nakumbuka niliwahi kufika mpaka kwenye kota za VETA. Je unaweza kuwajuza wengine wanaotaka kufik huko.

Tunakuomba uwe una update kwani sote tunapenda na tungependa kuwa hapo na hata mazikoni lakin ndio hivyo tena.

Kila la kheir na utuwakilishe vyema.

 
Wajameni huu ndio uhuru wenyewe wa habari ambao hiki ni kipengele kinachoitwa "Editorial Independence"!. Hii inahusisha uhuru wa wahariri kujiamulia ipi ndio iwe habari muhimu kwao!.

Nimeangalia mapitio ya magazeti yote yameiweka habari ya kifo cha Regia kwenye front page zake. Mengi ya magazeti hayo yameipa uzito wa juu, mengine uzito wa kati na machache yameipa uzito mdogo likiwemo Daily News na Habari Leo kwao msiba huu is not big deal!.

Hili halishangazi, gezeti hili halina mhariri mkuu kwa zaidi ya miaka 3 sasa huku anaekaimu ni full kujipendekeza kwa serikali akijiaminisha ataukwaa huo uhariri mkuu!. Kukaimu mwisho ni miezi 9 tuu ikipita hujateuliwa, inamaana hufai!. Sasa unapokaimu kwa miaka 3 na kujipendekeza kote bila kuteuliwa, then kujikombaring haisaidii katika uteuzi.

Nashauri it's high time magazeti haya ya serikali ya Daily News na Habari leo yapatiwe competent chief editor!.

Angalau kwa leo nikuunge mkono katika hili, saafi good observation.
 
Nimepitia taarifa za kidogo cha mh. Mbunge Mtema, katika gazeti la habari leo si taarifa iliyopewa kipaumbele jambo ambalo nadhani si Sawa na hasa nikilinganisha na taarifa iliyopewa kipaumbele, taarifa ambayo haikuwa na uharaka wowote Kwani
1. Ni habari ya kawaida pamoja na yaliyoandikwa kuipa uzito. hapa nawakumbuka wastaafu wote hata walio vijijini.
2. Ni ya uchunguzi, so ingeelea kutafitiwa japo kwa leo, na ikaambatanishiwa na nyaraka kadhaa za utumishi wa umma zinazopelekea hali ngumu ya maisha kwa watumishi wasifanya ufisadi.
Kwa maoni yangu nashauri
1. Habari leo wajisahishe katika hili Kwani pamoja na mwelekeo wao kisiasi wakumbuke like ni gazeti la umma wa tz, linaendeshwa kwa kodi zetu, Kwani hata wasipouza litaendelea kuchapwa tu.
2. R. Mtema, marehemu sasa, Alikuwa mtanzania, Lakini mbunge wa JMT, hivyo ni msiba kitaifa, ni uungwana tukalia wote,
3. Ajali ile imechukua maisha ya watz wengine, Kama mlivyowahi jurist kipaumbele katika taarifa nyingine za aina hii, basi mngefanya vivyohivyo
4. Kofi zetu zinauma pamoja na madhira mnayotutendea nyie mlokabidhiwa dhamana ya utumishi wa umma.
Inasikitisha, mnaimba uzalendo, kuipenda nchi, kuwa wamoja ilihali ninyi mmejitenga na jamii ya watz. Naomba kwa hili tuwakumbushe Habari leo kwamba wamechemka.

Sina hisa wala interest na magazeti haya ya Umma lakini nataka tu kuweka wazi, maana taarifa za utendaji wake husomwa bungeni.

Magazeti ya Umma yalikoma kupewa ruzuku na serikali tangu 2003 na yanajiendesha yenyewe kibiashara na kulipa kodi serikalini.

Sasa swala la kujikomba ama kwa viongozi au kwa chama ni la mtu binafsi (iwe mwandishi au mhariri) na hii ni ile kawaida ya waafarika kudhani kuwa ukilamba miguu ya mtu aliye madarakani utapewa safari za nje, au (Kicheko) U-DC au U-RC. Umasikini wa mawazo.

Kujikomba si kwa magazeti ya serikali tu, (Tena ukiangalia kwa makini yana afadhali kuliko mengi tunayoyafahamu ambayo waandishi wake hata kama ni wanaume utadhani wameolewa na wanasiasa fulani).
 
Habari Leo ni sawa na Uhuru na Mzalendo. Ukinunua Habari Leo huhitaji kununua Uhuru and vice versa kwani habari ni zilezile.
 
Yote munayosema ni sawa lakini hata Habari leo wanafahamu kuwa, gazeti lao si chaguo la wanaharakati, wapenda mageuzi na wengine wenye 'calibre' kama hiyo, kwa hiyo wakaipa uzito kama walioipa kwa kujua kuwa hao wateja wao wanaonunua na kusoma magazeti yao watakutana nayo wanaposoma hilo gazeti lao. Japokuwa walivofanya si sawia kwa sababu marehemu alikuwa kiongozi katika taifa na Mbunge wa JMT, kwa hiyo taarifa hii ilipaswa iwafikie watanzania wote popote walipo bila kujali itikadi zao, kwa kuwa mtetezi wa masilahi yao na Mbunge wao hatunaye tena. RIP Mh. Mtema
 
vyombo vya habar ni lazima viwe huru na kuonyesha uzalendo kwa jamii yote ya watanzania bila kujal itikad ya aina yeyote.Regia Mtema ni mtanzania na Mbunge wa watanzania wote.Nashangaa Habar Leo,Daily Newz,Channel Ten,Star Tv na RFA kuipuuza habar ya Mbunge wa Watanzania aliyekuwa mstar wa mbele kutetea Watanzania wote.Mungu Mkumbuke Regia, M Mbunge wa Watanzania wote katika Maisha ya Raha ya Milele.
AMEN
 
Hivi Tabata Chang'ombe gani hiyo. Kwani mimi nakumbuka niliwahi kufika mpaka kwenye kota za VETA. Je unaweza kuwajuza wengine wanaotaka kufik huko.

Tunakuomba uwe una update kwani sote tunapenda na tungependa kuwa hapo na hata mazikoni lakin ndio hivyo tena.

Kila la kheir na utuwakilishe vyema.


Mkuu,anayekuja aje na njia ya Tabata Relini afike bar ya Barakuda kisha aulizie eneo la Msimba.Atakayekwama apige namba hii 0713756924.Mimi pia nipo msibani.Asante.
 
Kwani Daily news na Habari leo kuna tofauti? kama ni wale wale mnashangaa nini? mmesahau walishajifanya Tume ya uchaguzi wakatangaza wazi kuwa Dr Slaa hatakuwa raisi wa awamu ya tano! maana wao inaonesha walishiriki hata vikao vya uchakachuaji matokeo. Wamejihakikishia kufa pamoja na ccm.
 
Nilisema ms utendaji wa magazeti yetu unatia kinyaa, yapo magazeti hukaa madirsiha ya msikiti kuangalia nani kamkosa nani. Likija swala la maendeleo ya waislam wanakataa kuhudhuria. Haya ndio matunda yake. Sikuona sababu ya gazeti la serekali hasa ukizingatia jk katoa salamu za pongezi kutoa habari kiduchu. Anaglikuwa wa ccm habarileo lingalifanya kituko hicho? Tuungane chadema kupinga ubaguzi huu hata kwa waislam na sio kwenu tu
Safi tuko pamoja! waambie CUF wawe wanatupa support sie na kuachana na ccm maana sie ndo tuna sera zinazo kidhi mahitaji ya jamii zote za kitanzania.
 
Hata wasipo ipa kipaumbele habari ya ndugu yetu mpendwa Regia Mtema aliepoteza maisha poteleambali, kwani yumo mioyoni mwetu hata kama amekufa tutaendelea kumuenzi kwa kutimiza yote aliyokuwa akifanya. kifo cha Regia ni pigo kwa familia, wapenda maendeleo, pia ni pigo kwa cdm na jf. Lakini yote tunamwachia Mungu
 
Mbona hili ni zaidi ya gazeti la Uhuru - angalia jinsi lilivyo behave kwenye chaguzi zote. Hili si gazeti la serikali ya wananchi bali ni gazeti la serikali ya magamba - shame!!!!
 
Back
Top Bottom