Gazeti la 'HabariLeo' na taarifa ya kifo cha Mh. Mtema

Inasikitisha kwa gazeti hili hasa kwa tukio hili,lakini haishangazi kwa imekua kawaida ya gazeti hili kudharau na kutozipa umuhimu au kuzipindisha hoja za upinzani hasa CHADEMA hata kama zina uzito,ukweli na umuhimu katika taifa inasikitisha gazeti hili ambalo linaendeshwa na kodi zetu linatumika kama gazeti la CCM.Naimani kama gazeti hili lingefutiwa ruzuku mawili yanaweza kutokea 1.Kufa baada ya matoleo mawili na 2.Kujirekebisha na kuanza kuandika habari balanced kutokana na umuhimu wake na nafasi yake katika taifa na pia kufanya kazi kwa ushindani na ufanisi zaidi kama yalivyo magazeti mengi ambayo yamejipatia sifa na yanauzika kwa umakini wake,kama vile Rai Mwema, Mwananchi,Tanzania Daima,Nipashe,Majira kuyataja machache.Tatizo hili liko kwa vyombo vyote vya habari vinavyoendeshwa na serikali.Na hii inatokana na chama tawala mbali na mabadiliko ya mfumo wa vyama vingi vya kisiasa bado inashindwa kufahamu kua CCM na serikali ni vitu tofauti.CCMni chama cha kisiasa kama vilivyo vyama vingine wakati serikali na nchi ni yaWATANZANIA WOTE.

Mkuu.....Si kwamba Habari Leo hawajaiandika habari ya kifo cha Regia,habari imeandikwa sema tatizo(kwa mujibu wa muanzisha thread) haijawekwa katika kipaumbele,yenyewe imewekwa ya pili katika kipaumbele na imewekwa na picha ya gari lililopata ajali na kusababisha kifo cha mpendwa wetu Regia Dotto Mtema....Tatizo liko wapi hapa?,mbona Habri Leo wameiandika Habari hii kwa mapana yake na ipo kwenye toleo la leo?....Mtoa Mada naona kama ana lengo la kupotosha katika hili maana nilichoona yeye tatizo lake ni Habari hii ya kifo cha Mpendwa wetu Regia kuwekwa ya pili katika kipaumbele na yeye alitaka iwe palepale katika front page ila iwekwe ya kwanza katika kipaumbele na ile(taarifa ya uchunguzi) iliyopewa umuhimu wa kwanza ndio iwe ya pili........

Poleni sana watanzania na wana JF kwa msiba huu wa mpendwa wetu Regia....

Habari yenyewe ni hii hapa chini:

Mbunge Chadema afa ajalini Ruvu

Na Oscar Mbuza, Ruvu.

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Regia Mtema amekufa katika ajali ya gari iliyotokea saa 5:15 asubuhi jana.

Katika tukio hilo, Mbunge huyo aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Landcruiser VX
(V8) lenye namba za usajili T 296 BSM, alipasuka kichwa na ubongo wake kutapakaa katika eneo la ajali mita chache kabla ya kulifikia Daraja la Ruvu kutokea Dar es Salaam.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Saleh Mbaga alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa ilitokana na hatua ya Mbunge huyo kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla likatokea roli la mafuta na
alipotaka kurejea upande wake gari hilo lilimshinda na kubiringita mara saba.

Mbaga alisema baada ya kutokea kwa ajali hiyo, polisi walifika na kumkuta Mbunge huyo akiwa tayari amekufa huku akibubujikwa na damu nyingi kutokana na kichwa kupasuka huku ubongo ukiwa umemwagika ardhini.

"Askari walipofika kwanza walianza kuwakimbiza majeruhi Hospitali ya Tumbi, waliwachukua
kwanza majeruhi watano halafu baadaye wakawachukua wengine wawili na baadaye ndio tukafanya mpango wa kuondoa mwili wa marehemu eneo la tukio kuupeleka Hospitali ya
Tumbi," alisema Mbaga.

Alisema hata hivyo ajali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na hatua ya Mbunge huyo kuwa na ulemavu wa mguu na hivyo kuwa na mguu mmoja tu wa kushoto ambao alisema inadhaniwa ulimpa tabu katika kufanya uamuzi baada ya kutokea kwa lori hilo la mafuta mbele
yake.

"Kama mnavyojua pedeli za gari zipo upande wa kulia lakini yeye alikuwa anatumia mguu wa kushoto kwa hiyo inawezekana kutokana na mshituko wa kutokea gari mbele, alibabaika katika kuutumia mguu huo wa kushoto kufanya uamuzi na hivyo kusababisha gari kumshinda na kupinduka," alisema Mbaga.

Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mlandizi, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Emmanuel Bondo alisema
mbunge huyo alikuwa na abiria wengine saba ndani ya gari hilo ambao ni wa familia yake na walikuwa wakielekea katika kijiji cha Mperamumbi katika Tarafa ya Ruvu kukagua mashamba.

Alisema muda mfupi baada ya ajali hiyo, gari la Mbunge huyo liliondolewa kutoka eneo la ajali ili kuepusha msururu wa magari katika eneo hilo.

"Sasa hivi nasubiri kufika kwa Kamati ya Bunge ambayo nimeambiwa itafika mahali hapa wakati wowote ili kuja kutembelea eneo la tukio," alisema Mkuu huyo wa Kituo cha Polisi cha Mlandizi.

Naye Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alithibitisha kutokea kwa kifo cha Mtema aliyekuwa mmoja wa wabunge 48 wa chama hicho na akakiri kuwa Chadema imepata pigo kubwa kutokana na msiba wa ghafla wa mbunge huyo akisema kuwa, mchango wake ulikuwa ukihitajika kwa chama na taifa kwa ujumla.

Aliongeza kuwa, mipango ya mazishi ya marehemu ilikuwa inapangwa nyumbani kwa baba wa
marehemu, Estelatus Mtema, Tabata Chang'ombe, katika Manispaa ya Ilala na kwamba ratiba ya maziko itatolewa baada ya kukamilika kwa taratibu zilizotarajiwa kupangwa na familia ya marehemu, Ofisi ya Bunge na chama.

Kutokana na kifo hicho, salamu za rambirambi zimemiminika kwa Chadema na familia ya marehemu, zikiwamo kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.

Katika salamu zake za rambirambi kwa Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Rais Kikwete alisema amesikitishwa na kuhuzunishwa na habari za kifo cha mbunge huyo ambaye amepoteza maisha akiwa bado kijana na kwamba
pigo hilo siyo la Chadema pekee, bali ni kwa taifa zima.

"Nimepokea kwa masikitiko na huzuni nyingi habari za kifo cha Mheshimiwa Mtema katika ajali ya gari. Siyo kwamba ajali hii imechukua maisha ya kijana bali imelinyang'anya taifa mbunge hodari na kwa hakika, kifo chake siyo tu ni pigo kwa chama chako cha Chadema bali ni pigo kwa sote na kwa taifa letu kwa jumla. Nakutumia wewe binafsi, chama chako na wanachama wake salamu za dhati za moyo wangu kuomboleza kifo na msiba huu mkubwa."

"Napenda ujue kuwa niko nanyi katika msiba huu. Napenda vilevile uniwasilishie salamu zangu za rambirambi za dhati kabisa kwa wana-familia, ndugu na jamaa wa marehemu
Mheshimiwa Mtema. Wajulishe kuwa nimepokea habari hizo kwa uchungu mwingi na kuwa moyo wangu uko nao katika wakati huu mgumu wa maombolezo, " amesema Mheshimiwa Rais na kuongeza.

"Aidha, wajulishe kuwa nawaombea kwa Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, awajalie uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu kwa sababu yote ni mapenzi yake. Naungana nawe, Mheshimiwa Mwenyekiti, na wanafamilia wa marehemu kumwomba Mwenyezi
Mungu aiweke pema roho ya Mheshimiwa Regia Mtema. Amen."

Naye John Nditi anaripoti kutoka Kilombero kuwa, wananchi wa mjini Ifakara na vitongoji vyake wamepokea taarifa za msiba huo kwa mshtuko mkubwa kufuatia taarifa ya kifo cha mbunge huyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini Ifakara, kwa majonzi baadhi ya wananchi walisema kuwa wana-Kilombero wamempoteza mbunge kijana na mchapakazi aliyewatumikia wananchi wake bila kujali jinsia na itikadi ya vyama vya siasa.

Baba mkubwa wa marehemu Bartholomew Mtemanyenja alisema walipata taarifa za ajali hiyo, na baadaye baba mzazi wa marehemu, Estelatus Mtema alithibitisha akiwa njiani kwenda eneo la tukio akitokea Kilombero ambako juzi alishiriki katika maziko ya mmoja wa madaktari wa Hospitali ya St. Francis.

"Tulipata taarifa mchana wa saa saba na nusu saa baadaye, baba yake mzazi aliamua kuondoka kwa kupanda magari tofauti kwenda eneo la tukio, lakini akiwa njiani alituarifu kuwa Regia amefariki dunia," alisema baba mkubwa.

Awali, Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Abdul Mteketa alisema amesikitishwa na kifo hicho na
kumwelezea marehemu kuwa ni kijana mdogo, na mchango wake ulikuwa bado unahitajika kwa
wananchi wa Kilombero na Taifa kwa ujumla.

Naye Katibu wa Mbunge, Mashaka Manjoti alisema kuwa Wilaya ya Kilombero na Chama chao kimepoteza mpigania maendeleo ya wananchi wanyonge wakiwemo na watumishi wa nyanja mbalimbali.

Historia ya marehemu ambaye mwaka 2006 alihitimu Shahada ya Sayansi ya Uchumi na Lishe katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA).

Alizaliwa miaka 31 iliyopita na Aprili 21 mwaka huu angetimiza miaka 32. Alipata elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Mchikichini, Ilala kuanzia mwaka 1989 hadi 1995, huku elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne aliipata katika Shule ya Sekondari ya Forodhani kuanzia mwaka 1996 hadi 1999 zote za Dar es Salaam.

Alichaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa katika Mchepuo wa Kemia, Biolojia na Lishe (CBN) mwaka 2000, lakini aliomba uhamisho ili kwenda Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Bweni Machame, Moshi mkoani Kilimanjaro.
 
Hata kama mhariri angekuwaje,vyote tuseme lakini ukweli unabaki palepale,tukio hili ni kubwa sana maana aliefariki ni Mbunge wa JMT tena kwa ajali na eneo maarufu kwa ajali ni vipi habari hii isingewa uzito na kuwekwa front page?hapa tunajua kilichonyuma ya pazia,hata wanao yanunua magazeti hayo nao akili zao ziko kushoto.maana yanaendeshwa kwa kodi zetu halafu yanabagua habari
 
Ushauri huu uende hata kwa vyombo vingine vya uma mfano TBC, Daily News nk. kwani wanaona vyombo hivyo ni kama vya CCM peke yao mimi nafikiri CCM wanahaki ya kuvitumia vyombo hivyo lakini si wao tu kwani ni vyombo vyetu wote kama watanzania na tungependa kuona mambo muhimu yanayotugusa yatangaze navyombo hivyo ikiwemo taarifa za mikutano, misiba, na harakati mbalimbali za viongozi wetu wa kisiasa na kijamii wakiwemo wale ambao waliomo madarakani wanawaona kama mahasimu wao lakini sisi kwetu ni watu muhumu sana. kwa hiyo haki yetu isipuuzwe. Madhara ya kupuuziana ni mabaya ingawa viongozi wetu wanaona ni kama utani, ipo siku wataelewa maana ya hiki tunachokipigia kelele. Mh. Regia Mtema ni kiongozi wa kitaifa na ni kipenzi cha watanzania gazeti la umma linapopuuza habari ya kifo chake ni kama kuwapuuzia watanzania kwa mamilioni wanaothamini mchango wake katika maendeleo ya taifa. Hivyo nakubaliana na wewe kuwa hawa watu wajirekebishe
 
Mkuu.....

Una uhakika Habari haipo Front page?.....
 
wataandika sana ikibid kila siku wakiisha tengeneza mgogoro kama ilivokuwa kwa chacha wangwe. maana mharir mkuu ndiye kamanda wa kutumia misiba kwa faida za kisiasa. tunamkumbuka vema alivokuwa majira alipotumia chombo hicho kutaka kuuaminisha umma kuwa wangwe aliuawa na chadema. lkn njia ya mnafik ni fupi

Akaliua Majira na habari za kupika za CCM ili watu wapate urais alafu akakimbilia Jambo leo,mpaka leo gazeti halijatulia linaweweseka tu halina hata mwelekeo.....kisa..huyo jamaa wa Habari leo
 
Nimepitia taarifa za kidogo cha mh. Mbunge Mtema, katika gazeti la habari leo si taarifa iliyopewa kipaumbele jambo ambalo nadhani si Sawa na hasa nikilinganisha na taarifa iliyopewa kipaumbele, taarifa ambayo haikuwa na uharaka wowote Kwani
1. Ni habari ya kawaida pamoja na yaliyoandikwa kuipa uzito. hapa nawakumbuka wastaafu wote hata walio vijijini.
2. Ni ya uchunguzi, so ingeelea kutafitiwa japo kwa leo, na ikaambatanishiwa na nyaraka kadhaa za utumishi wa umma zinazopelekea hali ngumu ya maisha kwa watumishi wasifanya ufisadi.
Kwa maoni yangu nashauri
1. Habari leo wajisahishe katika hili Kwani pamoja na mwelekeo wao kisiasi wakumbuke like ni gazeti la umma wa tz, linaendeshwa kwa kodi zetu, Kwani hata wasipouza litaendelea kuchapwa tu.
2. R. Mtema, marehemu sasa, Alikuwa mtanzania, Lakini mbunge wa JMT, hivyo ni msiba kitaifa, ni uungwana tukalia wote,
3. Ajali ile imechukua maisha ya watz wengine, Kama mlivyowahi jurist kipaumbele katika taarifa nyingine za aina hii, basi mngefanya vivyohivyo
4. Kofi zetu zinauma pamoja na madhira mnayotutendea nyie mlokabidhiwa dhamana ya utumishi wa umma.
Inasikitisha, mnaimba uzalendo, kuipenda nchi, kuwa wamoja ilihali ninyi mmejitenga na jamii ya watz. Naomba kwa hili tuwakumbushe Habari leo kwamba wamechemka.

Ingekuwa bora ungetueleza ni habari gani hiyo iliyopewa kipaumbele ili nasi tulinganishe. Maana si wote tunaosoma aina hiyo ya magazeti, na huku kwetu kazuramimba hayafiki.
 
Nyie Vijana wa JF: Msipende kukomalia siasa changa. Kuna hoja nzito iliyoandikwa kwenye Habari Leo. Ningetaka kuzungumzia au kuuliza kilichoandikwa kwamba Dereva wa gari marehemu Regia Mtema alikuwa na ulemavu wa mguu! This is very serious nijuavyo mimi walemavu wa miguu hawapewi leseni ya kuendesha gari ila wakiwa na gari maalum hupewa leseni for a specific use to easy there movement narudia mfumo wetu umeoza tena vibaya. Kwani leseni anayopewa mlemavu ni specific kutumia mjini tu na sio on a highway na pia haruhusiwi kubeba abiria. Nataka mamlaka iliyompatia marehemu Regia leseni ikiwa ni pamoja na TRA wote wajiuzulu. Kwanza nani alimruhusu as an amateur driver kubeba abiria tena 8. Huu ni upuuzi kwanza analipwa pesa kila mwezi za kuajiri dereva. We have a lot of un answered questions huyo dereva alikuwa wapi? This looks like a suicide mission why one with disability is allowed to recklessly drive a vehicle without a proper licence! Fine she is dead kinachobaki let us soberly learn this lesson and authorities have to take measures sio kukimbilia rambi rambi tu hazitatupunguzia hii road carnage. While driving from Dar to Chalinze professionals know when to overtake kuanzia Vikindu mpaka Vigwaza never attempt to overtake unless you can see 200 metres ahead clear don't forget to check your rear mirror for crazy drivers coming from behind!:A S 465:

Mokerema, kumbuka inayoendesha motokaa si leseni bali ni mtu! umetaja eneo linafahamika kwa ubovu wa barabara, serikali yako ya ccm inathubutu na kusonga mbele kuelekea kusikojulikana!!!!! nani anawajibika kuifanya barabara ipitike angalau kwa usalama. sheria ya utoaji wa leseni kwa wenye ulemavu inautata! kama haruhusiwi kupakia abiria kwa hofu atawaua, inamaana yeye kujiua ni sawa? SALUTE! REGIA MTEMA, R.I.P we’ll be mising U
 
ata majira wameweka ka kipande kadogo..eneo kubwa wamepamba picha za mbowe,zito na dr.slaa.ni upumbavu huu..kwani kifo ni kwa yeyote..shenz! Zao.
 
RIP regia.........inaniuma sana na tangu jana nina machungu...........siku yangu iliharibika. Maana tulichat wote juzi kuhusu mada ya kukusanya maoni. Hayo magazeti tuachane nayo kila mtu huwa na msiba wake
 
Nimepitia taarifa za kidogo cha mh. Mbunge Mtema, katika gazeti la habari leo si taarifa iliyopewa kipaumbele jambo ambalo nadhani si Sawa na hasa nikilinganisha na taarifa iliyopewa kipaumbele, taarifa ambayo haikuwa na uharaka wowote Kwani
1. Ni habari ya kawaida pamoja na yaliyoandikwa kuipa uzito. hapa nawakumbuka wastaafu wote hata walio vijijini.
2. Ni ya uchunguzi, so ingeelea kutafitiwa japo kwa leo, na ikaambatanishiwa na nyaraka kadhaa za utumishi wa umma zinazopelekea hali ngumu ya maisha kwa watumishi wasifanya ufisadi.
Kwa maoni yangu nashauri
1. Habari leo wajisahishe katika hili Kwani pamoja na mwelekeo wao kisiasi wakumbuke like ni gazeti la umma wa tz, linaendeshwa kwa kodi zetu, Kwani hata wasipouza litaendelea kuchapwa tu.
2. R. Mtema, marehemu sasa, Alikuwa mtanzania, Lakini mbunge wa JMT, hivyo ni msiba kitaifa, ni uungwana tukalia wote,
3. Ajali ile imechukua maisha ya watz wengine, Kama mlivyowahi jurist kipaumbele katika taarifa nyingine za aina hii, basi mngefanya vivyohivyo
4. Kofi zetu zinauma pamoja na madhira mnayotutendea nyie mlokabidhiwa dhamana ya utumishi wa umma.
Inasikitisha, mnaimba uzalendo, kuipenda nchi, kuwa wamoja ilihali ninyi mmejitenga na jamii ya watz. Naomba kwa hili tuwakumbushe Habari leo kwamba wamechemka.

Hiyo ni haki ya mhariri kuona umuhimu wa kila jambo na kulipa kipaumbele. Kwani Tz kuna wagonjwa, wenye njaa na hata waliojeruhiwana wengine wengi wamefariki kama Bi Regia. Hivyo muhariri ana haki kuona kipi muhimu kwake na jamii kukisoma.

Magazeti mengine mengi yameandika na yeye akaamua kuweka kipaumbee kitu kingine, Kwani nchi au serikali au hata Chadema haiwezi kusimama kwa sababu ya kifo chake Bi Regia.

Tumuombee kila lenye heir na fanaka na Mola amlaze pahala panapostahiki.
 
Nyie Vijana wa JF: Msipende kukomalia siasa changa. Kuna hoja nzito iliyoandikwa kwenye Habari Leo. Ningetaka kuzungumzia au kuuliza kilichoandikwa kwamba Dereva wa gari marehemu Regia Mtema alikuwa na ulemavu wa mguu! This is very serious nijuavyo mimi walemavu wa miguu hawapewi leseni ya kuendesha gari ila wakiwa na gari maalum hupewa leseni for a specific use to easy there movement narudia mfumo wetu umeoza tena vibaya. Kwani leseni anayopewa mlemavu ni specific kutumia mjini tu na sio on a highway na pia haruhusiwi kubeba abiria. Nataka mamlaka iliyompatia marehemu Regia leseni ikiwa ni pamoja na TRA wote wajiuzulu. Kwanza nani alimruhusu as an amateur driver kubeba abiria tena 8. Huu ni upuuzi kwanza analipwa pesa kila mwezi za kuajiri dereva. We have a lot of un answered questions huyo dereva alikuwa wapi? This looks like a suicide mission why one with disability is allowed to recklessly drive a vehicle without a proper licence! Fine she is dead kinachobaki let us soberly learn this lesson and authorities have to take measures sio kukimbilia rambi rambi tu hazitatupunguzia hii road carnage. While driving from Dar to Chalinze professionals know when to overtake kuanzia Vikindu mpaka Vigwaza never attempt to overtake unless you can see 200 metres ahead clear don't forget to check your rear mirror for crazy drivers coming from behind!:A S 465:

Bit too hash!!!
 
Hiyo ni haki ya mhariri kuona umuhimu wa kila jambo na kulipa kipaumbele. Kwani Tz kuna wagonjwa, wenye njaa na hata waliojeruhiwana wengine wengi wamefariki kama Bi Regia. Hivyo muhariri ana haki kuona kipi muhimu kwake na jamii kukisoma.

Magazeti mengine mengi yameandika na yeye akaamua kuweka kipaumbee kitu kingine, Kwani nchi au serikali au hata Chadema haiwezi kusimama kwa sababu ya kifo chake Bi Regia.

Tumuombee kila lenye heir na fanaka na Mola amlaze pahala panapostahiki.

Hiyo ndiyo furaha yako.Unacheka kijino pembe.Unaona tu aibu ungeelezea furaha uliyo nayo.Endelea.......
 
Ushauri huu uende hata kwa vyombo vingine vya uma mfano TBC, Daily News nk. kwani wanaona vyombo hivyo ni kama vya CCM peke yao mimi nafikiri CCM wanahaki ya kuvitumia vyombo hivyo lakini si wao tu kwani ni vyombo vyetu wote kama watanzania na tungependa kuona mambo muhimu yanayotugusa yatangaze navyombo hivyo ikiwemo taarifa za mikutano, misiba, na harakati mbalimbali za viongozi wetu wa kisiasa na kijamii wakiwemo wale ambao waliomo madarakani wanawaona kama mahasimu wao lakini sisi kwetu ni watu muhumu sana. kwa hiyo haki yetu isipuuzwe. Madhara ya kupuuziana ni mabaya ingawa viongozi wetu wanaona ni kama utani, ipo siku wataelewa maana ya hiki tunachokipigia kelele. Mh. Regia Mtema ni kiongozi wa kitaifa na ni kipenzi cha watanzania gazeti la umma linapopuuza habari ya kifo chake ni kama kuwapuuzia watanzania kwa mamilioni wanaothamini mchango wake katika maendeleo ya taifa. Hivyo nakubaliana na wewe kuwa hawa watu wajirekebishe

Angekuwa amekufa mwenyekiti wa wilaya wa CCM basi habari hiyo ingeongoza kwenye vichwa vya magazeti ya Habari leo,Jamboleo na ndugu yao Majira.
 
Hiyo ndiyo furaha yako.Unacheka kijino pembe.Unaona tu aibu ungeelezea furaha uliyo nayo.Endelea.......

Kama wewe unavyofurahia. Lakin kumbuka kuwa Kifo cha Bin'Adam sio kama cha kuku. Kwa muungwana yoyote yule hata kama mnatofauti lakin muswiba ni kitu tofauti sana. Acha roho mbaya hata kama ulikuwa na bifu nae.

Hakika sote ni vizuri tusahau tofauti zetu na kumuombea tena kwa dhati sana Mola amlaze pahala panapostahikhi. Na ndio maana nikasema nipo Japan Kikazi lakin ningekuwa Doha pasi na shaka yoyote ningekuja kuhudhulia muswiba huo.

Natoa pole kwa waTz wote kwa kumpoteza binti mpambanaji mkubwa wa kutetea wanyonge.

Acha fitina wewe.Si umefurahi jinsi Habari leo lilivyoripoti? Kama una huzuni ya kweli kwanini ufurahie upuuzi huu wa Habari leo? Kweli we barubaru.....
 
Angekuwa amekufa mwenyekiti wa wilaya wa CCM basi habari hiyo ingeongoza kwenye vichwa vya magazeti ya Habari leo,Jamboleo na ndugu yao Majira.
Mkuu wangu Molemo.......

Hebu japo kwa siku mbili tatu tuachane na haya mambo ya kutumia kifo cha Regia kuonesha hisia zetu za kisiasa na badala yake tuungane katika kuomboleza,kumuombea mpendwa wetu pamoja na kumuandalia makao yake ya kudumu....

Hizi habari za u CCM, u CHADEMA, u CUF etc hauna nafasi katika kipindi hiki.....Msiba huu ni wetu sote wana JF, ni wa watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama.....Regia alikuwa ni Mbunge wa bunge la JMT so alikuwa ni Mbuge wa watanzania wote.....

Inawezekana ni kweli Mhariri wa Habari Leo amekosea kwa kutoipa kipaumbele Habari ya Regia(japo mimi sijaona kosa lake maana kama ni Habari ya Regia bado ipo ukurasa wa mbele wa Habari Leo sema haijapewa kipaumbele kama wengi humu JF tulivyotaka)....Tunachotakiwa sisi kama Great Thinkers ni kuwasamehe Habari Leo na Menejimenti yote ya TSN na kuendelea kumuombea mpendwa wetu Regia Dotto Mtema apumzike kwa amani......

Niaminivyo mimi Habari za kifo cha mpendwa wetu Regia zimesambaa(jana) nchi nzima kwa msaada mkubwa wa mitandao(hasa JF), TV, Redio na ujumbe wa simu za mkononi......Haya magaezti ya leo yamekuja kukazia tu Habari ambayo kimsingi ilisambaa na kuwafikia watanzania tangu jana.....Kwa hiyo tusisikitike sana kwa magazeti kama Habari Leo, majira n.k kutoipa kipaumbele habari hii ya kifo cha mpendwa wetu Regia,tunachotakiwa kufanya ni kuwaombea nao wabadilike......

Btw: Siku hizi hatuna Waandishi wa Habari,tulionao ni waandishi wa majungu na wachochezi....Wengi wanapika Habari kwa motive ya kupata pesa(Rushwa n.k) na kuzichapa pasipo kufuata misingi ya uandishi wa Habari.......

Upumzike kwa Amani Regia....
 
Acha fitina wewe.Si umefurahi jinsi Habari leo lilivyoripoti? Kama una huzuni ya kweli kwanini ufurahie upuuzi huu wa Habari leo? Kweli we barubaru.....

ndio nikakwambia ni uhuru wa mwandishi kuangalia kipaumbele. Pasi na shaka magazeti yote wameweka mbele kama habari kuu lakini na wengine wana haki ya kuweka habari kuu nyingine na hii ikawa kama habari ya pili au Tatu. Hiyo ni choice ya Muhariri na sio kosa kisheria au hata kiuandishi.

Sasa unapolazimisha lazima habari hii iwe ni habari kuu pekee hilo ni la kwako ndio maana nakwambia hata Chadema, Nchi au hata Serikali au Bunge halijafunga ofosi zake kwa huu muswiba, kinachofanyika mabo yanaendelea na utaratibu wa maziko unaendelea sambamba ili kuleta tija na uswawi wa jamii nzima.

Cha msingi hapa ni kumuombea tu kwa Mola ampokee na kumuweka pahala panapostahiki na sio kusimamisha shughuli zote za Serikali, chama au hata Bunge.

Kumbuka kifo kimeumbwa na sote tutakuf
a kilicho siri ni kuwa hatujui muda gani.

Vipi umshaanza safari ya kuelekea kwao tabata Chang'ombe?
 
Nipo tangu jana mkuu.
 
Back
Top Bottom