Gavana Balali Ajiuzulu!

Je kuna mtu anajina la hospitali anayotibiwa huyu bwana hapa Boston,MA??? kama yes, basi weka hapa na kama ni siri ni PM hilo jina......then mie nitathibitisha kuwepo au kutokuwepo kwa mgonjwa huyo!!!!.
 
Balali nilikuambia last time hapa JF kuwa uombe msamaha kwa MUNGU na kwa watanzania kwa uliyofanya ukajifanya kichwa ngumu.

Hawa jamaa wamepania uondoke na mimi sitalia kabisa kwa yatakayokukuta. Hufai na umetumia nafasi kuu uliyopewa kujitajilisha binafsi, kusaidia CCM kushinda uchaguzi, kusaidia Mkapa na mkewe kuiba mapesa, kumsaidia Kikwete kupitisha mapesa kwenda kwa wadosi wake, na sasa ni time ya kulipa.

Omba msamaha wakati bado una dakika chache za kupumua, jamaa hawakutaki uendelee kuishi. Watanzania hawatakusamehe labda MUNGU atakusamehe.
 
...Mhhhhhhhh. Mhhhhhhh. Sasa hizo pesa zote alizochukua hapo Benki zina raha gani?? Wengine mnasema, maisha ya huyo gavana ni chokambaya, any time anaweza kurudisha namba. Tunapata fundisho gani hapa hasa?? Enyi wana wa adamu mnaowabia watanzania wenzenu kwa kushirikiana na mafioso wa kimataifa, mnajifunza nini kutokana na haya maswahibu yanayomkuta balali???
 
Sasa kwa nini hii imekuwa "KLH Breaking News"? Kwa nini isiwe 'Jamboforums' Breaking News? KLH News yenyewe imedoda siku hizi sasa habari zinavunjika hapa jamboforum halafu credit ziende KLH...wapi na wapi? Last time I checked, KLH News had 'Eid Mubarak' and not this so called breaking news here. Get it together people....
 
Alert JF...Telephone calls from abroad are being intercepted in light of this breaking news. Hivyo nyie watu huko ughaibuni mnaotupigia simu tulio nyumbani chukueni tahadhari basi... Ahsante.

SteveD.
 
Hapana, hatuwezi kukubali Ballali akimbie na pesa zetu hivi hivi, lazima aseme ilikuwaje vinginevyo wananchi tuna haja na haki ya kuendelea kumfuata kokote atakakokuwa.

Lazima huu uwe mwanzo wa kupambana na hawa mafisadi kwa faida ya nchi yetu.

Kama alilazimishwa lazima aseme akiwa hai kwanini hayo yalitokea, vinginevyo yeye ni mmoja wapo na hata akijificha USA
tutakuwa na haki ya kumpa kila aina ya kashikashi kwa faida ya mama na watoto wanaokufa kila siku hospitalini kwa kukosa matibabu huku hawa wajinga wanachota pesa bila huruma.

Nafikiri hata CCM wenyewe inabidi wawateme hawa wahuni, vinginevyo ama lao ama letu.

Kwa kweli mimi nimechukukia maana huu ni ujinga sasa. Watoe hiyo report ya BOT haraka ili tujue wanaotuchezea.
 
habari ya kujiuzulu kwa balali ilitegemewa ...tangu alipoondoka ilikuwa ni wazi kuwa kazi ya kikwete ilikuwa imemshinda...pamoja ya kwamba ni kweli ana MARADHI...

BALLALI sio mtu wa kumlaumu sana ...balali is just a victim of fourth phase CONSPIRACY....yeye mwenywe alikuwa akisema kuwa kashfa zinazomuandama zimepikwa na watu ambao " walikopa pesa benki kuu..na waliopoanza kudaiwa wanamuona mbaya!!"

kuna taarifa mbali mbali humu ndani na hata kashfa ya BOT inahusu makampuni ambayo mengine yako linked na mtandawo..yaliyokomba mabiolioni kwa ajili ya uchaguzi..

kuandamwa kwake kunahusu vigogo ambao walikosa fursa ya kuchotewa pesa BOT[kama mzindakaya alivyochotewa...]...amabao baada ya kukosa wakaaza kuumbuua network yote....

PIA kuna hisia kuwa wana mtandao walikuwa wanataka kuweka mtu wao pale na ukizingatia kazi ya gavana ni ya mkataba usiovunjwa ...njia pekee ya kuweka mtu pale ni kwa kumchafua gavana hadi aondioke mwenyewe..kama walivyofanya propaganda za kumlainisha mtu kama mahita na gen waitara kuandika barua za kustaafu ....

balali alisimamia uchumi vizuri ..ndio maana uchumi uliimarika,kwa niniubaya wake uanze baada ya kikwete kuingia???..PAMOJA NA MAPUNGUFU YAKE KIBINADAMU...MPAKA HAPO WENGI WATAKAPOGUNDUA ...DAUDI BALALLI ATABAKIA KUWA MMOJA KATI YA MAGAVANA WAZURI AMBAYO NCHI HII IMEPATA KUWA NAO...

kama kweli serikali ya jk wanataka kuwa clean kwenye hili basi watoe haradhani RIPOTI YA UKAGUZI WA BENKI KUU...
 
...Mhhhhhhhh. Mhhhhhhh. Sasa hizo pesa zote alizochukua hapo Benki zina raha gani?? Wengine mnasema, maisha ya huyo gavana ni chokambaya, any time anaweza kurudisha namba. Tunapata fundisho gani hapa hasa?? Enyi wana wa adamu mnaowabia watanzania wenzenu kwa kushirikiana na mafioso wa kimataifa, mnajifunza nini kutokana na haya maswahibu yanayomkuta balali???


THATS SADLY SOUND TRUE ..HAD ALSO THE NEWS FROM HIGHLY PLACED PERSON...wanasema maradhi yamemuandama sana...MUNGU ATAMSAIDIA!!!! SIJUI NA MAMA MUGANDA YUPO WAPI?
 
Alert JF...Telephone calls from abroad are being intercepted in light of this breaking news. Hivyo nyie watu huko ughaibuni mnaotupigia simu tulio nyumbani chukueni tahadhari basi... Ahsante.

SteveD.

SteveD,

Hata wanase simu wengine hatujali kabisa. Wanafikiri watendeleza huo upumbavu wao mpaka lini?

Akina Othman walikuwa hapa, wanaonekana waungwana kumbe ni pumbavu tupu.

Huyu Ballali tunaweza kumfungulia case hata huko huko USA. Watanzania wote dunia nzima, tuna uwezo wa kuchanga pesa za
kupambana na hawa mafisadi.

Tena siku hizi tunaweza kwa kila ambaye tunaushahidi basi tunafungua mashitaka nje na kusubiri tuakanyage Europe. Itafika mahali mpaka washindwe kutumia hizo pesa wanazoiba.
 
kuanzia sasa liwe somo kuwa ukiwaita waandishi wa habari na kuwafunga mdomo.. technolojia mpya wengine haitufungi... sasa hata taarifa ya habari ya saa mbili hawakuwaambia Gavana kajiuzulu.. hadi kesho watu wakiamka ndio wasikie amejiuzulu at that time.. sisi tutakuwa na habari nyingine kabisa kwani kama kawaida tena JF siyo tu inapakua habari na kuzionja kabla hazijafikishwa mezani Tanzania, inahakikisha kuwa habari hizo huenda na kachumbari...

don't forget Nyang'anyi naye nasikia amejiuzulu... (kama hawajamwomba aendelee kama walivyomfanyia Rashid)...
 
Calling a spade a spade,Balali ni mwathirika,na hilo lilikuwa likifahamika pale BOT kwa muda mrefu tu.Tatizo pale mahala (BOT),kama ilivyo kwenye visima vingine vya fedha,mafisadi wamekuwa wanaendekeza sana uzinzi to an extent ya kushindana miongoni mwao.Sasa unatarajia nini kama Balali alikuwa "anazungukana" (wanabadilishana vimada) na Liumba ( huyu ndie ambaye JK anadai "bunge litawatungia sheria watu wanaoambukiza UKIMWI kwa makusudi)

Wapo wengi wanaojua kuwa Balali,Liumba,and number of wakware hapo BOT ni waathirika lakini kwa vile "jamii yetu imestaarabika sana to an extent haiwezi kumnyanyapaa hata yule anayetumia fedha za ufisadi kuteketeza afya za dada zetu walio radhi kuukwaa kuliko kuendelea na umasikini" MAFISADI hawa wanaendelea kupata "kinga isiyo rasmi" ya kutajwa hadharani.

Inasemekana wakati wa kikao kilichopita cha Bunge,baadhi ya wabunge wanaojua afya ya Balali walikuwa wakitania kuwa "huyu jamaa aachwe tu ajifie kwa amani..." kumaanisha kwamba presha ndogo tu inatosha kumuondoa Balali duniani.Naamini kuna waliomuona namna alivyokongoroka,siku ile alipokutana na waandishi wa habari.


Kuhusu tuhuma za ufisadi,it goes without saying kwamba pamoja na kuwa mshiriki mkuu kwenye skandali nzima,Balali ni sawa tu na "ncha ndogo ya barafu inayoonekana usoni mwa bahari huku sehemu iliyofichika baharini ni mlima wa iceberg" (tip of the iceberg).Tunafahamu major players katika ufisadi huo kama walivyotawa na Dr Slaa,na kwa vile "ushirika wa wachawi huwa haudumu" si jambo la kushangaza iwapo Balali ataishia kuwa mbuzi wa kafara (na kwangu hiyo siyo adhabu anayostahili bali ni vema "akitangulia kwa Mwalimu" akawe kuni za kuchochea miili ya mafisadi wengine waliotangulia akhera).

Tuna mengi ya kushuhudia kabla ya Wadanganyika hawajafikia hatua ya kusema enough is enough,hasa ukizingatia kosa la kihistoria tulilofanya kumweka msanii pale Ikulu.
 
Ebana eeh hebu wanaojua hospitali aliyolazwa watuambie hapa. Kama namna gani mi na machizi wangu tunaweza kwenda kumfanyia wenyewe
 
Ngoja niweke kitu kimoja vizuri kabisa.. Gavana ametoka hospitali na anaendelea vizuri. Hata hivyo kutoka kwake hospitali ni kinyume na "matarajio" ya "wale wenye nguvu zilizopo". Na hata sasa hivi habari pekee ya furaha kwao itakuwa ni Gavana katuaga.. ndio maana mimi siombe afe nataka aishi atusimulie.. haya mambo ya viongozi kufa na siri zetu hatuna tena.
 
SteveD,

Hata wanase simu wengine hatujali kabisa. Wanafikiri watendeleza huo upumbavu wao mpaka lini?

Akina Othman walikuwa hapa, wanaonekana waungwana kumbe ni pumbavu tupu.

Huyu Ballali tunaweza kumfungulia case hata huko huko USA. Watanzania wote dunia nzima, tuna uwezo wa kuchanga pesa za
kupambana na hawa mafisadi.

Tena siku hizi tunaweza kwa kila ambaye tunaushahidi basi tunafungua mashitaka nje na kusubiri tuakanyage Europe. Itafika mahali mpaka washindwe kutumia hizo pesa wanazoiba.

Ahsante Mtanzania.
Ila ni tahadhari tu ndugu yangu, haswa kwa wale wanaopata 'inside story' na kutupatia hapa... najua monitoring lazima ifanyike, ila kwa habari kama hizi ambazo zina link kubwa hapa JF na zenye impact kwa taifa letu, lazima tukumbushane na kupeana tahadhari... ni rahisi kwa wengine kuanza kusema waliyo yasema hapa JF na jinsi wanavyotoa habari hizi hapa kwenye mawasiliano ya simu, na kama hilo linafanyika, wakifahamika ni sisi kukosa matoleo mengineyo ya 'inside story'. Ahsante.

SteveD.
 
Ebana eeh hebu wanaojua hospitali aliyolazwa watuambie hapa. Kama namna gani mi na machizi wangu tunaweza kwenda kumfanyia wenyewe

Nakubaliana na wewe, huyu anatakiwa kufanyiziwa ili iwe fundisho kwa wengine kwamba Watanzania wamechoka kuibiwa.

Ballali inatakiwa aseme ukweli wake kabla hajafa, vinginevyo
ataacha dhambi kubwa ambazo zitaiandama hata familia yake. When you are in a hole, stop digging, vinginevyo utafunikwa kabisa.

Inabidi aje clean kwa faida yake na familia yake.
 
Hii aliyosema Mlalahoi inafanana sana na habari ambazo mie pia nimebahatika kuzipata kutoka kwa wadau wa karibu. Lakini bado nadhani kuathirika "ngoma" si kinga ya kutomwajibisha mtu kwa ufisadi, maana waathirika wana haki na wajibu ule ule kwa taifa lao, sawa tu na waathirika wa maradhi mengine na watu wasio na ugonjwa. Ndio maana tunasema wasibaguliwe sehemu za kazi ili muradi wanamudu kazi zao. Na kama mtu anamudu kazi, hata ufisadi anaweza vilevile, na anastahili kuwajibishwa kwa hilo. Naomba kama yuko mtu mwenye ile ripoti ya ukaguzi wa hiyo BOT atusaidie, tuisome tujue kweli. Na kama huyo Gavana ni mtuhumiwa, ashitakiwe, kinachowezekana kuwa recovered kwenye assets zake kifanywe angao hasara ipungue, tusibakie tu kusema ana "ngoma" eti basi tumwache "ajifie"!
 
Nakubaliana na wewe, huyu anatakiwa kufanyiziwa ili iwe fundisho kwa wengine kwamba Watanzania wamechoka kuibiwa.

Ballali inatakiwa aseme ukweli wake kabla hajafa, vinginevyo
ataacha dhambi kubwa ambazo zitaiandama hata familia yake. When you are in a hole, stop digging, vinginevyo utafunikwa kabisa.

Inabidi aje clean kwa faida yake na familia yake.

Na maslahi ya walalahoi, walipa kodi, na taifa kwa ujumla.....
We need to make an example out of someone....enough is enough
 
Back
Top Bottom