Gari ipi itanifaa kati ya Spacio na Toyota Wish?

Mbayo wa Giika

JF-Expert Member
Apr 9, 2014
205
106
Wadau naombeni ushauri. Mimi si mtaalamu wa magari ila nahitaji kuwa na gari kwa ajili ya familia ya watu kama saba hadi nane na matumizi ya hapa na pale, safari za kazini na mara chache safari ndefu za mikoani na hasa vijijini.

Ninahitaji gari ambalo ni rafiki kwa matunzo na mafuta na linaweza kuhimili barabara za vijijini japo halitaenda huko mara nyingi na iwe ni 4W.

Katika pita pita zangu mtandaoni nimeona magari tajwa hapo juu yanaweza faa ingawa Wish nyingi ninazoziona zina CC nyingi (1900), Spacio ya 4W ina CC 1790.
Ni ipi itanifaa kati ya hizo au km kuna pendekezo lingine kulingana na matumizi niliyoainisha hapo juu?

Narudia tena, sina utaalamu na mambo ya magari hasa kwenye utofauti wa engine.

Ahsanteni!

1587105955860.png

Spacio

1587106050357.png

Toyota Wish
 
Mimi nakushauri chukua spacio tena 4wheel chukua wish nazionaga huku mtaani sinakera zilivyochoka then umbo la wish linatisha ni refu mnno then liko chini afadhali kwa urefu ule ingekuwa juu labda .CHUKUA. SPACIO MIMI NINAYO 4WD NAJIVUNIA KUWA NAYO PIA NI GARI KALI KULIKO HATA IST,PASSO,SIJUI SWIFT, SIJUI OPPA, kwa wenye familia na wa uchumi was chinii.kama nimekwaza mutu niwie radhiii.
 
Chukua SPACIO hakuna haja ya kujichanganya hiyo gari itakufaa Mkuu....
Kwa kukupatia elimu juu ya hizo gari ni kuwa SPACIO ndilo toleo la mwanzo kabisa kabla wish pia gari hii ilipendwa Sana na wajapan ikaingiza faida kubwa Kwa kampuni ya Toyota.

Baadae walichofanya Toyota walitengeneza IPSUM ili kuwavutia wateja hasa Kwa wale wanaopenda space kubwa kwajili ya familia,sasa Toyota wish ni zao la SPACIO na IPSUM kwahiyo limefiti katikati Yao yaani kama unataka gari kubwa Sana utaenda Kwa IPSUM na kama unataka size ya Kati utaenda Kwa wish..
 
Ahsante, ninazidi kupata uelewa zaidi juu ya haya magari.
 
Kwa sasa hayo siwezi kuyamudu ndio maana priority yangu ikawa kwenye Spacio na Wish.
Spacio ni nzuri sana tofauti na Wish...Ila kwa uwezo na nafasi ya kubeba watu kama 8 Wish inapata kipaumbele ila ubaya wa Wish inawahi kuchoka sana....ila kati ya hayo kweny ubora Spacio ni bora mara 79
 
Mimi nakushauri chukua spacio tena 4wheel chukua wish nazionaga huku mtaani sinakera zilivyochoka then umbo la wish linatisha ni refu mnno then liko chini afadhali kwa urefu ule ingekuwa juu labda .CHUKUA. SPACIO MIMI NINAYO 4WD NAJIVUNIA KUWA NAYO PIA NI GARI KALI KULIKO HATA IST,PASSO,SIJUI SWIFT, SIJUI OPPA, kwa wenye familia na wa uchumi was chinii.kama nimekwaza mutu niwie radhiii.
Wish body lake likichoka limaanza kufungwa na waya kama Nissan X-trail vile,pia Wish inafanana na panya(umbo lake).
 
Back
Top Bottom