Full Text: Hotuba ya Rais Samia Suluhu ya kufunga mwaka 2021. Kirusi kipya cha Corona cha Omicron kimeshaingia Nchini Tanzania

Nenda kapitie hotuba ya Lissu uone alivyozungumzia suala la mbolea halafu njoo kwa Samia alivyozungumzia kuhusu mbolea, halafu walete wakulima waichambue, ndio utaelewa tuna rais wa kiwango gani cha chini cha upeo.

Wakulima wote wa Tanzania wanataka bei ya mbolea iwe chini, sio blah blah za Samia.
Wanataka kwani mbolea wanazalisha wao!!?
 
Tatizo ni kwamba mama hana uwezo wa kua rais, hana uwezo wa kuwa kiongozi wa Taifa.

Hili nawalaumu CCM, kuchagua tu mtu yoyote kua makamo wa rais, hii ni hatari.

Kuna yule mwingine enzi za JK alikua anatembea na mkasi mfukoni kwa ajili ya kukata utepe, ni PhD lakini hata kuongea ni shida.
Phd ya nyukilia fiziks
 
Wanaosifia Hotuba ya TL ni wale wale mashabiki wa Lissu na Chadema tuliowazoea humu..
Wanaosifia hotuba ya Mama ni wale wale mashabiki wa mama tuliowazoea humu...

Mama ni Rais wa nchi ambaye yuko Tanzania na anajua na kuona kila kitu kinachohusu hii nchi, kifupi kila anachoongea anaongea kama Rais wa nchi mwenye taarifa ya kila linaloendelea humu.

TL ni makamu mwenyekiti wa CDM na Mgombea Urais wa CDM 2020 ambaye anaishi ughaibuni baada ya kukimbia humu akiogopa usalama wake, mengi anayoongea ni taarifa anazopewa na watu wake na ili ayatekeleze ni mpaka awe Rais aka kiongozi wa dola...Ukiwa nje ya dola ni rahisi sana kuoma kila kitu ni rahisi..

Moja ya Tatizo kubwa la nchi hii ni Kodi, ulipaji wa kodi ni hafifu na hii inapelekea Serikali kushindwa kuendesha shughuli zake kwa ufanisi, Watanzia wengi hawalipi kodi na hawana shuguli rasmi na kipato rasmi...
 
Kuliko kupoteza muda kusikiliza utopolo SI heri muda huo mtu utumie kusukuma chapati na kupika na maharage.
 
Tanzania iliponywa na Mungu, endelea tu kujitisha mwenyewe,na kuvaa mibarakoa sisi thubutu.
Tunaendelea Kama kawa.

Mtatishwa Sana Jiwe alitjulisha mapema.
 
Huyu mama Samia kwenye hotuba ni sifuri kabisa. Hotuba nzima haina news, logics wala vibe. Yaani ni blah blah nyepesi za kurudia takwimu ambazo kila mtu anazijua, hata kuichambua huwezi
Ndo hivyo,yeye ndo Rais sasa; Subiri na wewe ukipewa angalau Ubalozi wa nyumba kumi utoe hotuba yenye logic kwa Wananchi wako.
 
Back
Top Bottom