Tukimpa Rais Samia jukumu la kuwa mtalii namba Moja wa Taifa, tutakuza utalii wa kimataifa Kwa kiwango Cha juu. Tuwatumie mabalozi wamsaidie

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,602
Hongera na pongezi nyingi ziende Kwa Rais wa nchi yetu Mhe.Samia Suluhu Kwa kukubali kutangaza utalii kupitia filamu ya "THE ROYAL TOUR". Mengi ya kukatisha tamaa yalisemwa kabla ya matokeo ya filamu hiyo kuanza kuonekana lakini Sasa kinachosemwa ni ushindi na mafanikio.

Kulingana na takwimu zilizopo ndani ya mwaka mmoja ,filamu ya Royal Tour imechangia ongezeko la 57.7 ya watalii. Hizi ni takwimu za mwaka 2022 kulinganisha na za mwaka 2021. Haya ni matunda na matokeo makubwa sana katika sekta ya utalii.

Kitendo cha Rais kuchukua jukumu la kukuza utalii Kwa kufanya filamu ,ni kitendo cha kupongezwa na Kila mmoja Kwa sababu ya umuhimu mkubwa wa sekta hii kwenye uchumi. Ndio maana nimeanza Kwa pongezi kwake.

Jukumu alilobeba Mhe.Rais ni yeye kuwa mtalii Moja Kwa Moja maana ni mtalii anayeweza kutangaza utalii. Kwa mtazamo wangu ,tukimpa Rais Samia jukumu kubwa zaidi la kuwa mtalii namba Moja wa Taifa, naye akakubali jukumu hili jipya kutoka Kwa wananchi na wapigakura wake basi ninaamini atatusaidia sana kutangaza utalii wa kimataifa.

Wazi hili la kumpa jukumu hili Rais wetu limekuja kutokana na nafasi yake na ushawishi wake Kwa jumuiya na mashirika ya kimataifa na "exposure" kubwa aliyonayo kimataifa...Jukumu hili akisaidiwa na viongozi wenye "exposure " kubwa kimataifa litafanikuwa sana, wawe ni viongozi wastaafu ama wasio wa wastaafu.

Kwa kuwa Kuna filamu nyingine ya kutangaza utalii itatolewa na Rais Samia kaigiza tena,ninaamini filamu hizi zitakuwa na matokeo chanya kwenye utalii Kwa muda mrefu.

Filamu hiyo mpya na hii ya The Royal Tour zitangazwe kupitia mabango maalumu ya digital, naamini hii ni njia ya haraka zaidi kuwafikia watu. Mabalozi wetu wapewe jukumu hili huko wanapotuwakilisaha.

Rais kama mtalii namba Moja wa Taifa aandaliwe maonesho maalumu ya kuonesha na kukuza utalii wa nchi yetu. Matamasha hayo yaandaliwe hata nje ya nchi.

Rais atumie majukwaa ya kimataifa na kitaifa anapohutubia atumie sehemu ya hotuba yake kuonesha hata sehemu ya video inayoonesha vivitio vya utalii vilivyopo nchini. Mabalozi wanaweza kufanya jukumu hili huko wanapotuwakilisha na watanzania wanaoongoza mashirika ya kimataifa wasaidie kupitia nafasi zao.

Wageni wa kimataifa au watalii wa kimataifa wanapokuja kutembelea vivutio tulivyonavyo wakati wa kuondoka wapewe "USB flash' au CD ya Bure yenye sehemu muhimu za filamu zilizoigizwa na Rais wetu kukuza utalii naamini Kwa kufanya hivi taarifa za vivutio vyetu zitasambaa zaidi. Hapo itakuwa imetumika mbinu ya kuwavutia wengine wengi zaidi.

Kwa kufanya hivi ninaamini Rais wetu atasaidia kukuza na kuinua utalii wa nchi yetu Kwa haraka zaidi.

Tumuombe Mhe.Rais apokee jukumu hili la KUWA MTALII NAMBA MOJA WA TAIFA Kwa nia, lengo na kusudi la kusaidia kukuza utalii wa kimataifa
 
Back
Top Bottom