maneno yenyewe yakoje hadi yawe matusi? ningependa nijue
pole kwa nitakaowaudhi lakini yamesemwa kama ninavyokumbuka------
kwamba Tundu Lisu pengine haelewi maana ya ufalme kwa kuwa nchi inaendeshwa kidemokrasia (mbunge wa donge)
Tundu Lisu sijui alihitimu namna gani chuoni kwake
Tundu lisu ni wakili sijui anawakilisha vipi hao wateja wake
Tundu Lisu kwa zanzibar ina maana ambayo wazanzibari wanaelewa kwa hiyo wazanzibari wajue huyo ndiyo tundu Lusu kwa hiyo wasiwe na tabu
wanasema upuuzi huu ukizidi wataufanya usifike zanzibar utakuwa unaishia sehemu fulani ambayo ameitaja -----jina sijalikumbuka
mwingine anasema sidhani kama ni mtazamo wa kambi ya upinzani nategemea ni mtazamo wake ..............
nimeyataja bila mpangilio ili kwa wakati tofauti yamesikika hivyo
hayo ndiyo ninayokumbuka, yote hayo yalikuwa yanaumiza hasa kama ungepata nafasi ya kuwasikia wanavyoongea kwa hisia. Ilimlazimu Lisu kusimama mara kadhaa lakini spika akazuia kwa kauli kuwa tuvumiliane.