Full mipasho bungeni

mpaka sasa wanaendelea kumuandama Tundu Lisu kwa kauli yake ya Raisi wa Kifalme
 
Wabunge 2 toka zanzibar wametoa maneno makali, matusi na dhihaka dhidi ya Lisu. Lisu akasimama kuomba utaratibu lkn spika Anne Makinda kamzuia kasema tuvumiliane. Rai yangu kwa spika..next time Mbunge toka CDM au upinzani wowote exluding CUF akitoa maneno makali na matusi kama haya dhidi ya CCM naomba pia tuvumiliane.

Vp mama Kommu na Mary Nagu?

Au mama kommu alikuwa na swaumu na vile bado mgonjwa?

Vumilianeni ndio mwendo huo.
 
Wabunge wa CCM kweli ze comedy..huyu mbunge wa CCM toka Zanzibar anajifanya yeye ndie Selina Kombani..anajibu hoja za Tundu Lissu..hivi anajua majukumu ya mbunge bungeni?!
 
Wabunge 2 toka zanzibar wametoa maneno makali, matusi na dhihaka dhidi ya Lisu. Lisu akasimama kuomba utaratibu lkn spika Anne Makinda kamzuia kasema tuvumiliane. Rai yangu kwa spika..next time Mbunge toka CDM au upinzani wowote exluding CUF akitoa maneno makali na matusi kama haya dhidi ya CCM naomba pia tuvumiliane.

Tafadhali 'reformer' tupatie huvyo vipande vya matusi ili tuvitumie kwenye kampeni kule Igunga.maana magamba wanazidi sasa.
 
mpaka sasa wanaendelea kumuandama Tundu Lisu kwa kauli yake ya Raisi wa Kifalme

Inashangaza sana kumshambulia Lissu kwa aliyoyasema
kwa kuwa huo ni msimamo wa Kambi rasmi ya Upinzani,
kwa nini wasiishambulie kambi yote, hapa inavyoonekana
kuna chuki binafsi dhidi ya Lissu...
 
Wabunge 2 toka zanzibar wametoa maneno makali, matusi na dhihaka dhidi ya Lisu. Lisu akasimama kuomba utaratibu lkn spika Anne Makinda kamzuia kasema tuvumiliane. Rai yangu kwa spika..next time Mbunge toka CDM au upinzani wowote exluding CUF akitoa maneno makali na matusi kama haya dhidi ya CCM naomba pia tuvumiliane.
Unajua maana ya tuvumiliane? ni kwamba mama Anna makinda anaufahamu vizuri uwezo wa Wabunge wa chama chake ndiyo maana anaomba tuwavumilie tuu hawajui watendalo, lakini kwa wabunge makini wa CHADEMA hakuna haja ya kuwavumilia huwezi ukamvumilia mtu mwenye uelewa mzuri wa jambo unapohisi amechemsha kitu.
 
Mbunge anatetea Zanzibar na kuonya "Mpuuzi' yeyote atakayejaribu kuifanya Zanzibar iwe inferior. - Hii lugha haina staha ndani ya Bunge

Mbunge mwingine kamponda waziwazi Waziri wa Sheria na Katiba kwamba sijui kasomea wapi ...na maneno mengine ya kukosa staha.

Hakuna juhudi ya kupunguza ukali huu ilizaa matunda... japo kuna wabunge kama Tundu Lissu..( aliyelengwa moja kwa moja na mipasho hiyo kwa kuitwa TUNDU LUSSU!) walisimama kutaka muongozo.

Haya ni kwa uchache...

Mh Spika kawataka wawe na uvumilivu..

Jamani kwani kusema Ukweli ni tusi au kosa.

kama ni kosa kusema Ukweli basi waZnz kila siku watakuwa wakosefu. Kwani kutetea maslahi na kutambulika kuwa Znz ni nchi kamili tena ene mamlaka ndani ya muungano ni wajibu wa wawakilishi na wabunge wote wa Znz. Kwani wapo pale kuhakikisha Znz inasimama kama nchi ndani ya muungano na kuhakikisha hakuna dharau wala kejeli dhidi yake.

Hongereni wabunge kutoka Zanzibar.
 
WOS tupe habari basi wajameni wengine sisi huku Mpitimbi hakuna TV mtandao mchina karahisisha internent tunapta kupitia visimu
 
Jaji mkuu Werema naye kasema TUVUMILIANE so naye ndo anaendelea kuichambua hotuba ya Tundu Lisu
 
Una hakika...?Udaku umekusibu tu... wewe umeshaambiwa kuna mipasho...ukita details tumia lugha yenye staha badala ya kutafuta mipasho na wewe!

Haya mama, lakini kuleta posti isiyo na maelezo ya kina ulimaanaisha nini,
unadhani watu wote wanaangalia TV?
 
Halafu spika anauchuna tu huku akijua ni kosa mbunge kumtusi mbunge mwengine awapo bungeni. Wadau huyo mbunge mdebwedo amesema huko zenji wanajua maana ya TUNDU LISSU (nahisi alimaanisha kuwa wanajua ni matusi)
 
Unajua maana ya tuvumiliane? ni kwamba mama Anna makinda anaufahamu vizuri uwezo wa Wabunge wa chama chake ndiyo maana anaomba tuwavumilie tuu hawajui watendalo, lakini kwa wabunge makini wa CHADEMA hakuna haja ya kuwavumilia huwezi ukamvumilia mtu mwenye uelewa mzuri wa jambo unapohisi amechemsha kitu.
Kuna ukweli hapo mkuu.
maana wawakilishi toka zenji mmhh...
 
"ni bora Dr Slaa nimpishe awe raish kuliko Tundu Lisu kuwa mbuge" Kikwete akikiri jinsi anavyomuogopa Lisu! Acheni wamtukane Lisu kwani hawawezi kushindana naye 'hoja nyepesi zinajadili watu wakati hoja zenye nguvu zinajadili uwezo'
 
maneno yenyewe yakoje hadi yawe matusi? ningependa nijue

Mpuuzi, mnafiki, elimu yake ni ya kubabaisha...Lastly kamalizia...wanzibari mnajua "tundu lusu" kule kwetu zanzibar manake nn.
Naomba mtusaidie wanaJF..kule unguja neno "tundu lusu" manake nn? Nimemnukuu kama alivotamka neno "lusu"..So I dont know kama ni mispronunciation or he twisted it to make the point he intended.
 
Jamani kwani kusema Ukweli ni tusi au kosa.

kama ni kosa kusema Ukweli basi waZnz kila siku watakuwa wakosefu. Kwani kutetea maslahi na kutambulika kuwa Znz ni nchi kamili tena ene mamlaka ndani ya muungano ni wajibu wa wawakilishi na wabunge wote wa Znz. Kwani wapo pale kuhakikisha Znz inasimama kama nchi ndani ya muungano na kuhakikisha hakuna dharau wala kejeli dhidi yake.

Hongereni wabunge kutoka Zanzibar.
Naona nawewe unaendeleza dhalau kwa Pinda, hivi aliposema Zanzibar siyo nchi hukutilia maanani eeh?
 
Na mwanasheria mkuu nae anang'ang'ania tindu lisu na yule wa zenji nao wamesahau kuwa wameolewa na magamba kwani si tunashida na muungano?
 
Back
Top Bottom