Fujo za Iramba: Waliofanya fujo wanatoka Dar (soma majina)

@ Kurunzi acha tu uyu jamaa,sasa wameshtakiwa kwa kosa gani hasa? kama ni mauaji inakuweje wanatafutiwa dhamana?kesi za mauaji zina dhamana?au mie sijui sheria

Marehemu Ditopile alipewa dhamana kwa kifungu gani?
 
Watanzania, serikali yetu na Chama cha Mapinduzi wamezidi kutudharau, kutuonea, kutunyanyasa na kufanya hila za kila namna. Hii ni aibu kubwa, kati ya Vijana waliofikishwa mahakamani leo ambao polisi wamefanikiwa kuwafikisha mahakamani ni 12. Vijana watatu ni wa Ndago, Josia Israel (Katibu wa CHADEMA), na wenzake Abel Paulo wa Ndago, na Athumani Husein wa Ndago....

Duh! Nlishaanza kushangilia mwanzo mzuri kumbe UONGO!!kuna post nyingine hapo juu ina maelezo yaliyoshiba pamoja na picha,ina ku prove liar.
 
Pale CCM bado kuna watu wazuri .... Wahame chama haraka ... Waanzisha CCM yenye misingi na itikadi za Kweli Za TANU na ASP ... Wafanye Update ... Iwe ile CCM AZIMIO LA ARUSHA CCM AA the conservative CCM

.CCM ya Pili hii ya kina Kikwete na wenzake ... CCM AZIMIO LA ZANZIBAR CCM AZ The Liberal CCM.

Hawa Conservative CCM hawa ndio wanaweza kuokoa nchi kwa kuwatimua hawa liberal wasinii wakubwa wanohatarisha Taifa. Hawa CCM AA ndio wanaweza kuchuana ki ukweli na CHADEMA na kuleta upinzani wa kweli wenye tija na maendeleo.

..Ninaamuru hili litokeee!!




 
hakuna hata mtu wa dar vijana wote ni wa mkoani singida na ni wanachama wa chadema,chadema imewageuka haiwajui!
 
Tz at climax, now what follows is northing but to fall on the next side or falling back.
 
Watanzania, serikali yetu na Chama cha Mapinduzi wamezidi kutudharau, kutuonea, kutunyanyasa na kufanya hila za kila namna. Hii ni aibu kubwa, kati ya Vijana waliofikishwa mahakamani leo ambao polisi wamefanikiwa kuwafikisha mahakamani ni 12. Vijana watatu ni wa Ndago, Josia Israel (Katibu wa CHADEMA), na wenzake Abel Paulo wa Ndago, na Athumani Husein wa Ndago. (hao kwa mujibu wa maelezo ni Wafuasi wa CHADEMA), ni wakaazi wa ndago na wamedhaminiwa leo wapo nje kwa dhamana....
Wewe ndugu yangu acha kutunga story ya kibaguzi, mkuano wa hadhara ni ruhusa mtu yeyote awe CCM, CUF, CHADEMA au wengineo. Isipokuwa wanatakiwa wakasikilize sera sio kufanya vurugu hata km hawakubaliani na wazungumzaji, wao wasikilizaji ndo wakaamue upi ulikuwa mchele na zipi zilikuwa pumba.
 
Mkuu Madoro,
Me sijakuelewa unaposema Vijana hao Wanahudumiwa na CCM wakati TBCCM imetangaza waliokamatwa na kufikishwa mahakamani ni CDM!?

Shimbononi unakuwa mkorofi sasa hujaelewa nini wakati mwandishi amechukua walivyojieleza kituo cha polisi? TBC wanatangaza kwa sababu ya unafiki tu lakini ukweli ndiyo huo
 
Basically Huyo Kijana Mmoja Namjua na hiyo ndio Kazi yake!! Ambaye ni Mndengereko!! Katika chaguzi zote ndogo huwa anapelekwa!! Hadi Arumeru alikuwepo!! Anafanyia / Anajishughulisha Ubungo Maziwa!!!! Kazi yake nitabrief Baadae!!!
 
Mbona unaelewa yote, nenda kawapelekee list hao polisi, waache kutengeneza sinema nyingine. Polywood.tz imeanza kazi rasmi.
 

quote_icon.png
By Isango
Tupo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida kwa kamanda Mkoa Linus Vincent Sinzumwa, kusubiri Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo,John Mnyika na Dr. Kitila Mkumbo kuhojiwa kuhusu fujo zilizotokea Kijiji cha Ndago, Wilaya ya Iramba wiki iliyopita.

Itabidi hao kwenye red waunganishwe na watuhumiwa wenzao

Usipate shida anzeni kumkamata OCD.....La sivyo mtaumbuka

Hii nimeipata humu…. NOLNIZ

Mimi ni mtumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Kiomboi, Singida katika idara ya elimu. Nilishiriki katika mikutano miwili ya CHADEMAiliyofanyika Ndago na Kinampanda na nilishiriki kupokea msafara kuanzia Mbelekese.

Ukweli ni kwamba utaratibu wa kuvuruga mikutano ya CHADEMA uliandaliwa mapema kwa kuwashirikisha OCD, Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Iramba Magharibi, na jambo hili tuliwaeleza viongozi wa CHADEMA kabla hawajafika Ndago. Mpango uliokuwepo na utakaokuwepo katika mikutano ya leo ni kuwaandaa vijana wasio pungua 50 wakiwa wamelewa chakari.

Wao kazi yao ni kuhakikisha kwamba viongozi wa CHADEMA hawahutubii mikutano na wakijifanya hawaelewi basi maweyapopolewe. Jambo hili halijawafurahisha watumishi wengi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wanaopenda haki, na kuna malumbano makali yanaendelea chini kwa chini.


Sasa jana, mara msafara ulipofika Ndago na kabla mkutano haujafunguliwa wale vijana walikuwa wamekaa pembe tatu tofauti nyuma ya Mnyika, mbele kabisa karibu na barabarani na kushoto wakiwa wamejichanganya na maaskari. Lengo ilikuwa ni kumlenga mawe Mnyika moja kwa moja ili ionekana kwamba hatakiwi kabisa Iramba.

Bahati nzuri aliposimama Waitara akaanza na tahadhari kali sana kwamba tunafahamu mipango yote haramu na akawaambia maaskari wanawajibika kulinda mkutano kwa sababu mkutano ni halali na una baraka zote za Jeshi la Polisi.

Moja ya wale vijana alimpigia simu Mwigulu kwamba mpango wao umeingia mkenge kwa sababu jamaa wa CHADEMA wanaujua mpango mzima. Mwigulu alimfokea yule kijana kwa ukali sana na akamwambia anataka kuona mawe yanapigwa ndani ya dakika tano vinginevyo ajiandae. Moja kwa moja yule kijana akawaambia wenzake kwa ishara na wakatoa mawe mfukoni wakaanza kurusha. Purukushani ziliendelea na vijana wa CHADEMA wakawa wanajihami na kuwalinda viongozi waliokuwepo kwa karibu kabisa.

Vurugu ziliendelea kwa takribani kati ya dk 20-30, na wananchi wengi kusambaratika. Waitara na Mnyika walionekana wakiwasiliana kwa simu na kuwalaumu polisi waliokuwepo, ambao wao walikuwa wanachekacheka tu. Ndipo utulivu ukarejea na wananchi walirudi kwa kasi ya ajabu, na mkutano ukajaa tena na Mnyika akaendelea kuhutubia. Mnyika alipokuwa anamalizia hotuba yake, ndipo landrover ya FFU ikaingia ikiwa imesheheni maaskari. Mnyika akawaambia wananchi kwamba maaskari wameingia lakini baada ya fujo kutokea na wananchi wamejilinda wenyewe.


Mkutano uliisha kwa amani, na kisha msafara ukaelekea Kinampanda palipokuwa na Mkutano mwingine. Tukiwa pale Kinampanda ndipo habari zikaanza kusambaa kwa kasi kwamba kuna kijana ameuawa. Mkutano wa Kinampanda uliisha salama na hapakuwa na kurushwa mawe. Wananchi walihudhuria kwa wingi ukizingatia pale ndipo palipo Chuo cha Ualimu cha Kinampanda.

Taarifa nilizozipata baadaye ni kwamba yule kijana aliuawa ndani ya nyumba ya mtu kando kidogo na mkutano ulipokuwa unafanyika. Mtu huyo pia anatajwa kuwa kada wa CCM aliyekuwa anagombea ukatibu kata na ndiye aliyepewa fedha na Mwigulu kuratibu shughuli nzima ya fujo.


Sina uhakika kama mikutano ya leo ya CHADEMA itafanyika kwa sababu vijana wameshaanza kukamatwa na kuna hatari polisi wakazuia mikutano ya leo. Pamoja na yote haya, Mwigulu watu wanamchukia sasa hivi kwa mambo ya kihuni anayoyafanya. Hatujuwahi kuwa na Mbunge wa namna hii katika Jimbo hili".
 
Hata hivyo hawa vijana wamejitambulisha katika hati ya Mashtaka kuwa ni Abdala Mbwana Kingwande, (Mndengereko), ana Miaka 36, Mwislamu, Mfanyabiashara na Mkaazi wa Segerea Dar es Salaam.Wa Pili Ni Nasri Salehe (Mnyamwezi), ana umri 28, Mwislamu, anakaa karikaoo, na ni mfanyabiashara. Wa tatu ni Laizimu Njama, ni MMakua, ana miaka 42, Mwislamu, anatokea Tandika/Temeke Dar es salaam. Wa Nne ni Mohamedi Abdalaa, Mluguru, ana miaka 34, Mwislamu, anakaa Kibamba Dar es Salaam, wa Tano ni Rudoviki Muganyizi, Mhaya, ana miaka 32, Mkristo, Ni Injinia. Wa Sita ni Justini Sangu, Mfipa, ana miaka 40, Mkristo anakaa Dar na ni mfanyabiashara. Wa Saba ni Salumu Ali Rashidi, ni Mmwela, ana miaka 26, Mwislamu, ni Mkaazi wa Tandika Jijijini Dar.

Well well well.....we all have ghosts don't we?
 
Maswali:
1. Hao vijana waliingia lini Singida? na walipanga kuondoka lini? WALIKUJA SIKU NYINGI ZILIZOPITA NA WATAONDOKA PINDI WAKIPATA DHAMANA .

2. Walisafiri pamoja? NDIYO Na wanajuana?NDIYO kama ndio kwa muda gani? TOKEA WALIPOANZA MAFUNZO YA MGAMBO KULE ULEMO

3. Walishafika Singida kabla? NDIYO Kama jibu ndiyo, lini na kwa shughuli gani? KABLA YA UCHAGUZI MDOGO WA IGUNGA Walikuwa wote? NIMESHASEMA NDIYO!!!

4. Dar es Salaam wanafanya biashara pamoja, na eneo lao la biashara liko mahali gani? HAKUNA BIASHARA HAPO BALI NI UUAJI.

5. Walisikia toka kwa nani kwamba CHADEMA walikuwa na mkutano?MWIGULU MZINZI na waliambiwa na viongozi gani watahutubia?WAITARA, DR. K. MKUMBU na MNYIKA

6. Mbali na kuhudhuria mkutano wa CHADEMA, walifanya nini kingine siku/kabla ya mkutano huo? WALIKUNYWA VALUUUUUUUU!!!!!

7. Wanamjua Mwigulu Nchemba? NDIYO x 1000! au walishasikia hilo jina?ZAIDI YA x 10000000! na wanafikiri ni nani? MBUNGE MZINZI

8. Wametembelea sehemu gani nyingine ndani na nje ya Tanzania kwa miezi 12 iliyopita? ARUMERU KATIKA NJAMA ZA KUIBA KURA

9. Mbali na mkoa wa Singida ni mkoa gani mwingine huwa wananunua mazao, na lini mara ya mwisho wamenunua huko? HAKUNA MAZAO WANAYONUNUA

10.Wanaweza kusema huu ni msimu wa mazao gani Singida? BANGE KATIKA SHAMBA LA MWIGULU Na mkoa gani unazalisha nafaka kwa wingi zaidi hapa Tanzania?HAPA HAWANA JIBU KWANI HAWAFANYI BIASHARA
 
Si UMASKINI unaochangia hali hii bali Elimu inayotolewa haijengi uwezo wa kufikiri na kuamua bali inajenga udhaifu wa kufikiri na kuamini wengine wenye mamlaka ndiyo wenye fikira sahihi.
Bado kuna maswali ya kujiuliza kutokana na sakata hilo; Je
1. Mbali na kujitambulisha kuwa wanatoka Dar, wanatokea kweli huko, au wametayarishwa hivyo ili kupoteza ushahidi? Waweza kuwa ni wa hapo hapo. Ugizaji ukaendelea kama wa Dr, Wafanyabiashara wa Madini, Kesi za EPA nk.
2. Wanaotajwa kuwahudumia hata sasa bado ni wa-ccm
 
Mh ipo kazi kwelikweli walazimishwe wataje ninani aliwatuma?
 
mmmh kuhonga watu ili wafanye fujo..ni tuhuma nzito hizi aise

na pia tujadili akaunti alowafungulia vijana 32 wa kiomboi ili baadae awatumie kuvaa jezi zake na kuleta fujo. Ntarudi kuwapa tape na sauti ya mmojawapo aliyekiri wazi
 
Back
Top Bottom