FT: NBC Premier League | Young Africans 3-0 Coastal Union | Mkapa Stadium | YANGA BINGWA

Mzee Wa Kazi Chafu

JF-Expert Member
Jan 24, 2022
2,220
4,901
Yeeees! Karibuni Sana Wapenzi Wa Soka, Wapenzi Wa NBC Premier League Ama Kwa Hakika Leo Juni 15, 2022 Inapigwa Mechi Kali Hapa, Mechi Dume Kati Ya Dar Es Salaam Young Africans Dhidi Ya Coastal Union Wana Mangushi Ama "Wagosi Wa Kaya".

Ni Mechi Yenye Umuhimu Mkubwa Baina Ya Timu Zote Kupata Alama Zote Tatu Hasa Kwa Dar Es Salaam Young Africans Kwani Endapo Watafanikiwa Kupata Alama Zote Tatu Leo Hii, Ni Rasmi Watatangazwa Kama Ndio Mabingwa Wapya Wa Ligi Kuu Ya Soka Nchini Tanzania Na Kwa Upande Wa Coastal Union Wana Mangushi Kupata Alama Zote Tatu Ni Kuzidi Kujiweka Pazuri ili Kusalia Ndani Ya NBC Premier League.

Nini Kitajiri Hapa Je Young Africans Atafanikiwa Kutangaza Ubingwa Leo?, Ama Coastal Union Atatibua Mipango Na Kutibua Rekodi Ya Kutopoteza Mchezo Wowote Kwa Young Africans Mpaka Hivi Sasa?, Em Tutege Macho Na Masikio Kufuatilia Mtanange Huu Ndani Ya Dk Zote 90.

All The Best Dar Es Salaam Young Africans The Club Above All In Tz

Wananchi!!
FVTsm1wWQAEoEVt.jpg

Mchezo unaanza kwenye Uwanja wa Mkapa, leo Juni 15, 2022 Jijini Dar es Salaam

1' Mchezo umeanza
10' Yanga wanamiliki mpira muda mwingi
19' Coastal wanaonesha uhai wanajibu mashambulizi kadhaa
34' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Walinzi wa Coastal wanajichanganya, mpira unamkuta Mayele anapiga shuti linaingia wazuni
37' Yanga wanaendeleza kasi
40' Mayele anakosa nafasi ya wazi, shuti lake linatoka nje ya lango
45' Coastal wanaonesha utulivu licha ya kushambuliwa mara kadhaa
FVT-fW3XoAMWbXA.jpg

MAPUMZIKO
Kipindi cha pili kimeanza

47' Coastal wanapambana kutafuta bao la kusawazisha.
50' Mayele anapiga shuti la mbali linapaa juu ya lango
51 GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Chiko anaipatia Yanga bao la pili akimalizia krosi ya Mayele
60' Yanga wanaendelea kuliandama lango la Coastal
65' Mchezo ni mkali na Yanga ndio ambao wanatawala mchezo muda mwingi
67' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Mayele anaipatia Yanga bao la tatu, likiwa ni la pili kwake katika mchezo huu
80' Yanga wanaupiga mwingi, wanatawala mchezo
85' Coastala wajapiga pasi, wanaonekana hawana cha kupoteza
90' Zinaongezwa dakika 3
Full Time

YANGA BINGWAAA, kutokana na kufikisha pointi 67 inamaanisha kuwa Yanga imetwaa ubingwa
 
Kuna habari za punde zimetufikia zikidai Yanga mmejitoa kwenye shindano la NANI ZAIDI

Kwanini kibubu milicho nunua 5,000 mkivunje kikiwa na buku jero ndani?
 
Kuna habari za punde zimetufikia zikidai Yanga mmejitoa kwenye shindano la NANI ZAIDI

Kwanini kibubu milicho nunua 5,000 mkivunje kikiwa na buku jero ndani?
Tumesikia Mmoja Wa Viongozi Wenu Kaongeza Fungu La Kuboost Michango Yenu Maana Na Huko Pia Hali ilikuw Tete, Teh! Teh!
 
Tumesikia Mmoja Wa Viongozi Wenu Kaongeza Fungu La Kuboost Michango Yenu Maana Na Huko Pia Hali ilikuw Tete, Teh! Teh!
Maneno ya mkosaji

Nyie mlikosa viongozi wa kuwa bust?

Siku ya press mbona white alikuwa akiwapongeza azam kuwa zoezi la uhesabuji likiwa chini yao hakutakuwa na ujanja ujanja kama huo ambao wewe unausema hapa?

Kwa hiyo unataka kuwaaminiwha wana yanga kuwa azam wameshiriki kuwadhurumu Yanga?
 
Aya Chukueni Izo Pesa Mkanunue Kombe Lenu
 
Kuna habari za punde zimetufikia zikidai Yanga mmejitoa kwenye shindano la NANI ZAIDI

Kwanini kibubu milicho nunua 5,000 mkivunje kikiwa na buku jero ndani?
Habari za punde zimetufikia, zikidai kua hilo ndilo shindano pekee ambalo makolo wameshinda msimu huu. Hongereni sana!
 
Back
Top Bottom