FT: Ligi Kuu Bara | Tanzania Prisons 1-0 Simba SC | Uwanja wa Sokoine | Juni 26, 2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Wanajulikana kuwa ni watalaamu wa kusakata Kabumbu Maridhawa Nchini Tanzania kwa viwango vya Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF, na Klabu yeye kuvuta hisia mujarabu kwa Wadau na Mashabiki wa Kabumbu, Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, leo Juni 26, 2022 yupo ugenini kuwakabili Wajelajela Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Tanzania Prisons kuwepo kwenye uwanja wao wa nyumbani, huenda wakazidisha upinzani haswa hivyo kupelekea kufanya mchezo kuwa ngumu sana, huku Simba SC wakihitaji ushindi murua ili kuendelea na furaha ya kuumwagilia moyo kuelekea kumalizika kwa msimu.

Anakayejiandaa vema kwenye mchezo huu ndiye ambaye ataweza kuibuka na furaha.. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10: Jioni, Usikose Ukaambiwa.

Kulipewa Mwana....Kulitaka Mwana


===================

Naaam mpira umeanza kwa kasi Uwanja wa Sokoine | Tanzania Prisons 0-0 Simba SC.

05' Timu zinagawana mashambulizi katika dakika hizi za mwanzo

10' Milango bado ni migumu hakuna timu imeona nyavu | Prisons 0-0 Simba SC.

15' Kakolanya anafanya Kazi nzuri kuokoa hatari langoni kwake, Prisons walikuja vizuri sana eneo la Simba SC

20' Shuti kali la Banda lambabatiza mchezaji wa Prisons kwenye mkono ndani ya box, refa anasema hapana.

25' Kona inapigwa kuelekea Prisons lakini golikipa anatoka na kupangua mpira ule.

30' Pambano linaendelea huku Jimmyson akikosa nafasi ya kufunga baada ya kazi nzuri ya Mhilu

35' Almanusura Simba wapate bao baada kichwa cha Lwanga kutoka njeee

Free Kick inapigwa na Banda golikipa wa Prisons anasafiri na kupangua na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao

40' Inapigwa Free Kick kuelekea Prisons, Bandaaa looo, golikipa anafanya Kazi nzuri kuokoa hatari na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao

Prisons wanacheza faulo nyingi kipindi hiki, ni wakati wa Simba kufanyia kazi mipira hii ya kutengwa

Prisons wanakosa nafasi ya kufunga ilikuwa Shambulizi kali mno, ambapo Beno anadhihirisha ubora wake baada ya kuokoa hatari mbili

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko ambapo hakuna timu imeona lango

HT: Prisons 0-0 Simba SC

Kipindi cha pili kimeanza kama kipindi cha kwanza, mpira wa kasi huku Asukile anakosa nafasi nzuri ya kufunga.

50' Timu zote zinacheza uangalifu sana huku wakikosa kutumia Kona kwa pande zote mbili.

53' Asukile Goooooooooooooaaal

Asukile anafungua ukurasa baada ya kufunga bao, ambapo mpira uliopigwa na kuokolewa na Beno, hatimaye unamkuta mfungaji.

60' Hatariii, golikipa wa Prisons anasafiri kwa mara nyingine tena na kuokoa hatari langoni kwake, nyota wa mchezo leo.

Kagere anapiga kichwa lakini mpira unatoka nje, ilikuwa nafasi murua ya kusawazisha.

Kadi ya Njano kwa Kagere baada ya kumchezea madhambi mchezaji wa Prisons

Simba wanatafuta nafasi ya kusawazisha, lakini Kimenya anakaa imara.

67' Ametoka Lwanga na ameingia Mzamiru upande wa Simba SC | Prisons 1-0 Simba SC

75' Mchezo unaendelea huku muda unazidi kuyoyoma, huku Simba wakisaka nafasi ya kusawazisha, lakini mipango yao bado.

Wachezaji wa Prisons wameanza kulala kupoteza muda kuelekea dakika hizi za mwisho.

82' Je, Simba wataweza kusawazisha? Ametoka Mudathir na ameingia Mkopi upande wa Prisons.

Prisons wanacheza kwa nidhamu ili kulinda lango lao, Juma anatoka na kuingia Ismail upande wa Prisons

Kagere anapiga kichwa lakini golikipa andaka, hata hivyo refa anasema Offside.

90+3' Kuelekea kumalizika kwa mchezo, huku Simba wakielekea kupokeza mchezo huu.

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Prisons wanaibuka na ushindi wa bao moja kwa bila

FT: Tanzania Prisons 1-0 Simba SC

...... Ghazwat.....
 
Kupakana tu jasho sasa wanacheza ili iweje
kombe la yanga.jpg
 
Ulienda Airport kwenye kupokea...!?
Au design wa lile Kombe amekukera

adriz
Kombe lile ni kali sana , aliyebuni apewe tuzo ya heshima ameleta kitu mikali cha utofauti

Kama Man U tu , jezi za punda milia kipindi zinatambulishwa zilipokea comments negative nyingi lakini baadae mdogo mdogo watu wakazoea na kuongoza kwenye mauzo na watu kufanya za mtoko.
 
Samahani Wakuu,
Naomba Kujua Wafungaji wa mechi ya Yanga na Mbeya City.
Na Hadi sasa Nani anaongoza kwa Ufungaji NBC ligi
 
Back
Top Bottom