From Karimjee Hall: Public Hearing ya Kamati ya Bunge toka kwa wadau wa Dar es Salaam

Thanks for the updates. Hivi wazungumzaji wanachaguliwa kwa kufuata priorities gani? Ni kila mtu anaweza kuchangia hapo ukumbini au ni wale waliopangwa tu?
 
Kufikia hapa, wanabodi wenzangu, naombeni niishie hapa nikaendelee na mambo mengine.

Ningetamani sana nikae mpaka mwisho, nisemeheni, sisi watanzania wenzenu, tunajikuta tunafanya shughuli za kitumwa, haswa tunapofanya kazi na wazungu, eti baadhi ya sikuu zetu, wao hawazitambui hivyo leo kwetu ni siku ya kazi, sio siku ya mapumziko, hivyo nawajibika kurudi jela kuendelea kutumikia kifungo cha hiyari kwa wazungu ili siku ipite.
 
Kumradhi Pasco na wengineo, nimeihamishia Jukwaa la Siasa; unawajua watu wetu... Hawakawii kuanzisha same thread hukuhuku; tutairejesha kwenye forum ya Katiba baadae (after a week or two).

Shukrani kwa updates mkuu wangu
 
Thanks for the updates. Hivi wazungumzaji wanachaguliwa kwa kufuata priorities gani? Ni kila mtu anaweza kuchangia hapo ukumbini au ni wale waliopangwa tu?
Utaratibu, ni kwa Mwenyekiti kuita watu mbele. Kipindi cha wawakilishi wa vyama vya siasa walishamalizika, CCM ilisahaulika, mwakilishi wa CCM Tambwe Hiza amesimama, kwanza anapigiwa makofi, anaanza kwa kumwaga masifa kwa JK, anazomewa
 
NCCR Mageuzi wamesema wao hawaitaki kabisa hiyo Tume ya rais, bali wanataka Bunge litunge sheria ya kuunda Baraza la Kutunga katiba, na baraza hilo ndilo liunde tume ya kukusanya maoni ambapo rais has nothing to do na katiba mpya.
Mbatia amemaliza, anafuatia Mzee kijana wa APPPT-Maendeleo, Peter Kuga Mziray.

Kuna namna simuamini huyu mbatia... !!!
 
Kufikia hapa, wanabodi wenzangu, naombeni niishie hapa nikaendelee na mambo mengine.

Ningetamani sana nikae mpaka mwisho, nisemeheni, sisi watanzania wenzenu, tunajikuta tunafanya shughuli za kitumwa, haswa tunapofanya kazi na wazungu, eti baadhi ya sikuu zetu, wao hawazitambui hivyo leo kwetu ni siku ya kazi, sio siku ya mapumziko, hivyo nawajibika kurudi jela kuendelea kutumikia kifungo cha hiyari kwa wazungu ili siku ipite.
Hii ni habari MBAYA kwetu
 
Pasco sina budi kukushukuru kwa kutujuza kama nilivyoomba mwanzo utujuze, pia sina budi kukushukuru kwa kuwa unaenda kumtumikia huyo mzungu. Umejitoa kwa moyo wote hata sisi ambao tuko mbali tumeweza jua kinachoendelea nyumbani. Kila rakheli na kazi njema.
 
Dr. Slaa anaubomoa muswada top down, left right, inside out, kwa hoja kuwa kama katiba ndio baba na ndio mama na katiba hiyo ni ya wananchi, rais ni zao la katiba, hivyo ni mtoto wa katiba husika, hivyo mchakato hauwezi kuongozwa na rais, kila kitu rais, ndio mwenye maamuzi ya mwisho, amesisitiza mamlaka yawe kwa wanachi kupitia wawakilishi wao waliowachagua bungeni.

Huyo rais si mchaguliwa? mi sioni tofauti kati ya raisi na mbunge. Mangapi wameboronga huko, I have no trust na wabunge, wamepitisha mangapi? Na je rais si sehemu ya bunge? watz tutalonga weee but tutabaki palepale we have no trustable people in everywhere.
 
ndugu zangu mie niko tabora lakini hata umeme huku hatuna kwahyo cna ili wala lile ...niwashukuru sana wana J.F nawaombeni mtupe mengi zaidi
 
Mkuu Pasco, wamesema pia ni lini watakuja huku kijijini kwetu ili nasi tutoe maoni yetu ama ni huko huko tanzania (dar) tuu?
 
Huyo rais si mchaguliwa? mi sioni tofauti kati ya raisi na mbunge. Mangapi wameboronga huko, I have no trust na wabunge, wamepitisha mangapi? Na je rais si sehemu ya bunge? watz tutalonga weee but tutabaki palepale we have no trustable people in everywhere.

Remmy .. I totaly understand you ..

...but please lets talk and talk .... always its for nothing!!
 
Huku Dodoma tumepigwa mabomu na pia wanafunzi walikuwa wamekusanyika wametawanyika sana na kukimbia huku na kule na hivyo kufanya taharuki kubwa sana katika mji wa Dodoma
 
haya sasa! kumekucha, FFU wamewasha risasi za mpira na kuanza kufurusha watu toka kwenye geti la bunge hapa mjini dodoma.....

wanasafisha njia yote, vijana na wanaharakati wamevuka na kuingia upande wa pili wa barabara, askari wanaranda randa.

it has been an embarasment kwa umma kwani mh godbless lema aliitwa aje azungumze na vijana. akapewa pendekezo kuwa chimwaga hall itumike, vijana wametaka jamhuri stadium instead...

vijana wametaka waliomo ndani wasitishe zoezi na lifanyike upya mara moja hapo jamhuri stadium....

vijana na wanaharakati wana sababu ya msingi.....

1. wakina mama waliopewa dozi na mama kombani washaingia ukumbini

2. watu wanaingia kwa kuwa identified.....eg viongozi wa ccm

3. mbunge wa dodoma mjini mheshimiwa malole mapema asubuhi alileta champion mbili zilizojaa wanafunzi wa shule yake ya city kuja kuunga mkono muswaada. (ikumbukwe kuwa mheshimiwa malole aliwatumia hawa hawa wanafunzi kushinda kura za maoni na kuteuliwa kuwa mbunge)

4. vijana na wanaharakati wamefika tangu saa moja asubuhi na kuambiwa kuwa ukumbi umejaa....

ntaendelea kuwajuza!
 
Jamani kuban Radio na TV ni kutunyima haki sie wa mikoani kujua kinachoendelea :disapointed:, kweli serikali yetu haina nia njema na huu muswada kwani katiba ni wananchi na wananchi wana haki ya kujuzwa nini kinaendelea ili wasijejikuta wanakurupushwa, anyway bado nguvu ya umma ipo tutapambana tuuu...
 
Back
Top Bottom