Freeman Mbowe anamiliki jumba la kifahari Dubai!

mkuu, ipo siku CHADEMA watakuja kulikana hata gazeti lao Pendwa la Tanzania Daima

Daima binadamu hatabiriki huenda hata wewe kesho ukawa cdm hivyo sifa apewayo mtu ni kutokana na tendo lake la mda huo naaweza kuwa mwema kwako kumbe akuchimba undani wako
 
Mbowe ametokea familia tajiri....baba yake ni Kati ya matajiri wa mwanzo wazalendo......ambapo Mzee Ikaeli Mbowe,John Rupia,ally Sykes ...walikuwa wafadhili wa Tanu......
Mzee Mbowe alikuwa msaada mkubwa kusaidia Tanu kuingia Kanda ya Kaskazini .....ambapo baadaye kilpata makada Kama nsilo Swai,na Peter kisumo.....tofauti ni kuwa hawa Wazee wafadhili wao hawakutaka kabisa Siasa tofauti na wa Sasa ........kwa miaka yote Mzee Ikaeli Mbowe aliendelea kuwa rafiki wa Mwalimu .....na biashara akafanya.....,na Wazee hawa Ndio pekee ambao hawakukubaliana na azamio la Arusha na wakabakia marafiki wa Mwalimu na hata Mara Moja hawakujaribu kumuasi....
Mzee ally Sykes Amefariki na pia naye ameacha majumba hadi nje ya Nchi..........Mbowe amerithi utajiri sio kosa lake...labda Kama kosa ninkutumia vema pesa alizoachiwa...na vitega UCHUMI kwa kuongezaa vingine,...Watanzania wamezoea kuonaa watoto wakifuja Mali Za urithi Ndio Furaha Yao
 
Unachumia tumbo jamii Forum wewe, unaonekana ni kikaragosi cha viongozi wa cdm, jiendeleze, soma shule tafuta kazi ya profesional ulosomea ufanye hapo utaendeleza nchi na sio hivi unavyofanya sasa sio sustainable ni ushauri tu!!!

Umesoma shule gani wewe?Jenga hoja acha personal attack.
 
mkuu, ipo siku CHADEMA watakuja kulikana hata gazeti lao Pendwa la Tanzania Daima

Daima binadamu hatabiriki huenda hata wewe kesho ukawa cdm hivyo sifa apewayo mtu ni kutokana na tendo lake la mda huo naaweza kuwa mwema kwako kumbe akuchimba undani wako
 
Kwa mtu yeyote yule ambaye hata kama ana ufahamu wa darasani kwa kutumiatuu ule wa kufikirika ukiwa unazungumzia jina la bomani, kahama, au mbowe utakuwa unafamika mapema ni nini unachoongea...Kwa familia ya Mbowe ni nani asiyefahamu ni familia iliyofanikiwa na yenye jina kwa kipindi kirefu katiak masuala ya biashara hapa nchini, the same to Bomani au Kahama..sasa suala la Mbowe kumiliki jumba Dubai au Uk mimi kwa maono yangu sioni kuna ajabu hapo hapo..Hawa watu tangia nazaliwa nimekuwa nikiwasikia masikioni mwangu na sijaja kuawasikia kwenye siasa za leo za kuapakaza hila, ufedhui na matope. Itakuwa ni uendawazimu ulipoiitiliza kwa mtu kuyashangaa haya ikiwa kama haifuatilia historia ya familia hizi nilizozitaja na kuanza kohji au kusema nyumba hizo zimejengwa kwa ruzuku. Mwisho wangu kwa ninayoyajua na mimi nimeongea haya nikiwa kama mwananchi wa kawaida nisiye na tabaka la kusema niko upande gani katika vyama hivi vya siasa za kileo za kupakaziana matope.
 
Kama kweli hizi mali zilikuwa declared tume ya maadili basi hata mimi binafsi imani yangu kwa Mbowe inaweza kuongezeka. Hii ni kwa sababu kuna watu tena wanajulikana ambao 'capacity charges' (waliyo) wanayochukua kwa mwezi inazidi thamani ya hizi nyumba zote na ukifuatilia hizo pesa zinakowekwa huwezi kuona majiana yao halisi bali 'kampuni za mfukoni'. Tusisahau kuwa Dr. Slaa aliwahi kutanabaisha juu ya kijana mdogo anayemiliki mali zisizoweza kuelezeka ikiwa ni majumba, malori, account za benki nk na hizi habari hazijawahi kukanushwa kikamilifu wala kupelekwa Mahakamani kama ilivyoahidiwa. Hivyo kitendo cha Mbowe kiziweka tume ya maadili ni wazi zinaweza kuwa halali na si za mashaka.

Labda tukikumbushana, mimi si mjuzi wa mji wa Dar es Salaam lakini kuna simulizi kuwa bustani ya Mnazi Mmoja ilikuwa inatenganisha eneo la 'waswahili' masikini waliokuwa wakiishi Kariakoo, Gerezani, Kidongo Chekundu, Ilala nk na eneo la matajiri wazungu, wahindi na wengineo. Nilisikia kuwa miongoni wa 'waswahili' wachache waliokuwa wanaweza kuishi maeneo ya Kisutu/Mchafukoge/Posta ni baba yake Freeman Mbowe pamoja na akina John Rupia, Bomani (mnaweza kunikosoa mnaojua vizuri). Na ni hawa waliokuwa wanaweza kusupport kipesa harakati za ukombozi. Sasa kwa trends hizo sishangai mtu kuwa na nyumba sehemu hizo. Tatizo ni muimbishaji jeshini au kwenye chama anapokutikana na mabilioni huku sote tukijua kuwa alivyoingia siasa akitokea aither chuoni alikuwa anaishi nyumba ya NHC!
Ujio wa Freeman kwenye siasa huku akiwa tajiri sio ajabu kwa maana anaweza kuwa anaelewa njia za wananchi wenzake kuondokana na umasikini kwa mikakati sahihi na si kuiba, na mind angelikuwa anaingia kwenye siasa kuendeleza 'wizi' ni wazi angejiunga na chama ambacho wenyewe walishasema wazi kuwa ukitaka utajiri wa haraka ujiunge nacho lakini yeye anatumikia chama cha ukombozi na mchango wake unaonekana kwa vitendo.
 
Ukifikiri kwa kutumia akili za mwenzako ujue utatumika kwa faida ya wenzako mpaka unakufa.Utumwa mbaya kuliko wote ni utumwa wa tumbo na tamaa.
 
-Mbowe ni Mfanyabiashara anayelipa kodi kwa Mujibu wa Sheria

-Kuna kasumba mbaya imeibuka inayojenga Taswira hasi kwa kila mfanyabiashara.Hatuwezi kujenga Taifa kubwa kwa mentality hizi

Sera ya CHADEMA kulingana na Mrengo wetu kiitikadi ni kuwa Mazingira mazuri ya Biashara na mfumo wa soko uendeshe uchumi ambapo individual efforts zinakua rewarded.

Umaskini si jambo la kujivunia.CHADEMA kimeweka msimamo wake very Clear.Kuweka mazingira mazuri ya kibiashara na kukuza uchumi kupitia uboreshaji wa maisha ya mtu mmoja mmoja.Tungefuata sera sahihi za kiuchumi na kibiashara basi nchi hii ingekua na mabilionea wengi zaidi na turnover ya wafanyabiashara tunaowaona leo hii ingekua tofauti na turnover zao kwa sasa.

Leo hii kutokana na kuwa na sera ya 'Kuchanganyikiwa" ya kiuchumi na kijamii hatuwezi hata kuweka estimation ya kuwa tutakua na Mamilionea au mabilionea wangapi in 5-15 years baadae.Tunapiga ramli kama waganga wa Kienyeji badala ya scientific forecasting

Hizi mentality za Kimaskini tunazoona zimejengwa kwa muda mrefu na kupaliliwa na mfumo na zinajenga chuki kwa kila mfanyabiashara lakini cha ajabu wanasiasa wezi wezi na waroho wa mali za Umma wanakua celebrated na kushangiliwa kuwa fulani ni Noma.Tunajenga taifa dogo la ovyo lenye uwezo wa kupiga reverse kimaendeleo tu na sio zaidi ya hapo.

Kuhusu Malicious intent kwa kuandika story zenye malengo mabaya kisiasa ni.jambo la hatari sana

Raia Mwema nimekua nikiliheshimu na hadi sasa nawapa benefit of doubt ili niwe rational.

Ukweli wa jambo lolote ni suala la Muda.Sidhani sasa kama Raia Mwema wamebadili dimension ya Legacy yao waliojenga kwa muda Mrefu kwa kuamua kwenda Gutter na irresponsible Journalism.

Jenerali Ulimwengu ana heshima kubwa nchini kitaaluma na katika weledi.Sidhani kama anaweza kuruhusu mambo haya

Wakati huo huo hatuwezi kupuuza kila lisemwalo maana kuna mambo mengi.Uchaguzi ndani ya CHADEMA unakaribia,Hoja ya Kuficha Mabilioni nje inaweza kuwa diluted kwa mbinu mbalimbali na pia kwa kuwa kuna wanasiasa wanahusika na hoja hii wanaweza kuitumia kisiasa kujinufaisha na kuwalenga maadui zao kwa sababu wanazozijua ambazo no doubt ni za Kisiasa

Najua wanapita wahariri hapa,Sasa sote tujiulize ;

Je,Tunapokubali kutumia vyombo vyetu kwa maslahi ya kisiasa ya watu wachache tunaitendea haki jamii?Je,misingi ya Demokrasia na mhimili wa media tunautendea haki?Tunakuza au tunafifisha tasnia ya Habari?

Asiyekuelewa hapo tena anahitaji maombi
 
Unachumia tumbo jamii Forum wewe, unaonekana ni kikaragosi cha viongozi wa cdm, jiendeleze, soma shule tafuta kazi ya profesional ulosomea ufanye hapo utaendeleza nchi na sio hivi unavyofanya sasa sio sustainable ni ushauri tu!!!

Aendeleze nchi inayopolwa na magamba. Umefanya nini kwa sehemu yako?
 
WanaJF,
Nilieleza hapa jukwaani kuwa hatuhitaji propaganda. Hatua ya kwanza ni 1) mtupatie taarifa ya ukaguzi mliyofanya kwa Eecretariat ya Maadili ya Umma. Gharama ya ukaguzi haizidi 1,500. lipeni hizo fedha, kagueni file lake, ndiyo muwe na uhalali wa kupiga propaganda hapa. Hili si swala la " nadhani", oh sijui nini. Fsnyeni homework yenu, ndipo watanzania watawaelewa. Vinginevyo, tutawaonya wachochezi, wazushi, watu wadioitakia nchi hii mema, kwa kujaribu kutuondoa kutoka kwa mapambano halisi ya ufisadi na kutuwekea mapambano feki.

2. Wameisha kusema wengi, kuwa na nyumba nje ya nchi, au akaunti siyo kosa, kosa ni ufisadi hasa wa kutumia fedha za umma au kuziiba na au kuhukumu na kuzificha kwenye benki za nje, na hasa Offshore Banks Kama walivyofanya Mafisadi wa ccm kwa fedha za EPA, Tangold, Meremeta ambazo mpaka CCM na Serikali yake wameshindwa kuzitolea Taarifa, siyo humu jamvini, lakini hata Bungeni ambapo Serikali inapaswa kuwajibika. Haya hapa ni propaganda tu, na Kama nilivyosema kwenye post nyingine, hizi propaganda zimefeli hata kabla hazijaanza. Upotoshwaji wowote, ni lazima ujibiwe, tena kwa hoja, na Kama hoja Great Thinkers msiingie kwenye mtego wa kishabiki, jibuni kwa hoja Kama wana nia njema watawaelewa, kama hawataki " hata ukimpigia Gitta Mbuzi haitasaidia".
Babuuuu naanzisha Kanisa langu nitakuchagua kuwa Baba Askofu wa kanisa langu. Usijali kanisa langu litaruhusu kuwa na mke na vimada.Pia nitakuomba umchague Mbowe kuwa muweka Hazina wa kanisa na Mzee Ndesamburo na Lowassa kuwa wazee wa kanisa.
 
Mbowe ametokea familia tajiri....baba yake ni Kati ya matajiri wa mwanzo wazalendo......ambapo Mzee Ikaeli Mbowe,John Rupia,ally Sykes ...walikuwa wafadhili wa Tanu......
Mzee Mbowe alikuwa msaada mkubwa kusaidia Tanu kuingia Kanda ya Kaskazini .....ambapo baadaye kilpata makada Kama nsilo Swai,na Peter kisumo.....tofauti ni kuwa hawa Wazee wafadhili wao hawakutaka kabisa Siasa tofauti na wa Sasa ........kwa miaka yote Mzee Ikaeli Mbowe aliendelea kuwa rafiki wa Mwalimu .....na biashara akafanya.....,na Wazee hawa Ndio pekee ambao hawakukubaliana na azamio la Arusha na wakabakia marafiki wa Mwalimu na hata Mara Moja hawakujaribu kumuasi....
Mzee ally Sykes Amefariki na pia naye ameacha majumba hadi nje ya Nchi..........Mbowe amerithi utajiri sio kosa lake...labda Kama kosa ninkutumia vema pesa alizoachiwa...na vitega UCHUMI kwa kuongezaa vingine,...Watanzania wamezoea kuonaa watoto wakifuja Mali Za urithi Ndio Furaha Yao

- Sawa sawa mkuu sana, naomba kuuliza in a very serious way hizi nyumba nje ya nchi zilinunuliwa mwaka gani? Halafu tuwekee wazi Mali alizoacha Mzee Mbowe kama kweli hizi nyumba zilikuwepo, hatuna chuki wala wivu ila ni standard mnazoziweka wenyewe kwa public, kubali kwamba for this mmejichafua sana mimi ni bepari by heart ila ninachukizwa sana na wanafiki na waongo hapa Tanzania, Mbowe kwa nini hajawahi kusema wazi kwamba ana majumba n je ya nchi kwa wananchi anaotaka kuwakomboa?

- Niliwahi kusema kwamba Chadema mmefikia mwisho wa your line of politics laid down by Serikali ya CCM, CCM ndio iliyoamua kuwepo na vyama vya upinzani pamoja na kwamba kura za maoni zilisema wazi kwamba 80% ya wananchi hawataki vyama vingi CCM walipokuwa wanakubali walijua sana kwamba hapa mlipo ndio mwisho wa siasa zenu. Sasa mmefikia wakati wa kujinyonga wenyewe and that is what you have been doing for the last one year na here you go, MWenyekiti wenu ana majumba nje baang, you are on the rope kujitetea na maneno mengi sana ya kitoto, as if mnawajibu watoto wadogo kumbe mnazidi kujichora ni bora mngenyamaza kuliko mnapojibu maana mnaziidi kujichanganya na kujivua nguo, kweli leo kuna mtu anaweza kusimama na kusema Mzee Mbowe alikuwa tajiri sana na kuwa na uwezo wa kumiliki majumba ya kifahari nje ya nchi? Eti aliacha utajiri wa kutosha kununua majumba ya kfahari nje please mnamdanganya nani hapa?

- Mnajichora bure, it is time now Viongozi wa juu wa Chadema wakajitoa na kuwaachia wengine hasa kina MWanakijiji na Kitila.

LE Mutuz
 
Hivi wewe na ukubwa wote huo..still your brain is functionless..
Inamaana hata Jomo Kenyatta alipoacha mali mtoto wake Uhuru Kenyatta asiendeleze mali..?
Mzee Mbowe ameacha biashara..mtoto wake Freeman ameendeleza na kuleta super profit..na ameeleza kwamba kwa kipato chake halali anamiliki nyumba sehemu kadhaa kama Dubai..
Sasa major point ambayo CCM hawataki iguswe ni viongozi wa umma ambao wanafanya mikataba ya siri na kupata hela na kukimbiza Uswisi..
 
OK I LOVE THIS, NAOMBA NIKUONYESHEE UTOTO WA MAJIBU YENU KAMA NILIVYOSEMA MWANZONI:-

- Unasema sina brain na kwamba I am functionless, great una maana umekuja mbio kumjibu mtu ambaye ni no brain na functionless? Sasa what that tells about you?

- Eti ni mjinga gani Duniani anayeweza kulinganisha utajiri wa Mbowe na Mzee Kenyatta? Hivi wewe kweli ni mzima Uhuru familia yake ya Kenyatta inamiliki 50% ya Ardhi yote ya Kenya ambayo ni the best collateral kwa ajili ya benki kumpa mikopo ndio maana ameweza kuendeleza zile pesa kama vile Donald Trump, ambaye na yeye aliachiwa Ardhi nyingi na baba yake so ikawa rahisi kwake kukopa na kuendeleza mali za USD 200, Million alizoachiwa na baba yake, lakini sio Mzee Mbowe nasema bila kuogopa kwamba hakuacha mali mtoto wake leo kuwa na majumba nje nchi kama Dubai, USA na South Africa ambako ni lazima ulipie kodi kubwa sana ya property ama sivyo Serikali za huko zinakunyanga'nya ardhi au jumba.

- Unasema Disco la pale Mbowe ndilo limempa hela za kununua majumba ya kifahari nje ya nchi? Really? So huu ndio utetezi wako kwamba hizo nyumba ameweza kuzinunua kwa kuendeleza utajiri alioachiwa na baba yake, atakuwa ndio Mtanzania wa kwanza kuwa na akili namana hiyo bro, kwamba baba yako anakuachia Disco unalendeleza mpaka unaunua majumba ya kifahari nje ya nchi, that is the best joke of this week!!

- Mwenyekiti wenu bado ana kazi kubwa ya kujieleza amepata wapi hayo mapesa ya kununulia hayo majumba ya kifahari huko nje? Mali alizoachiwa Kenyatta na baba yake hazifanani hata robo na alizoachiwa Mbowe, halafu bado kuna swali kubwa kwamba mbona hmajawahi kusema to the public kwamba anamiliki majumba nje aliyonunua kwa hela za halali? Kwa nini tumejua sasa baada ya Zitto kumkomalia nyani giladi, poleni sana haya sasa nendeni mkawaaambie wananchi vijijini kwamba Mzee Mbowe alikuwa tajiri sana alimuachia mtoto wake ambaye ameuendeleza ndio maana sasa anamiliki majumba ya kifahari nje!!

VERY CHILDISH!!

Le Mutuz
 
Sijawahi kuona kiongozi mzalendo kama mhe.Freemani Mbowe; amezaliwa tajiri na mfanyabiashara mkubwa hadi leo.Ebu tujiulize alikoswa nn hadi akaamua kuwa mpinzani tangu Chadema kikiwa chama kichanga, kwa historia ya familia yake angekuwa ccm asingekuwa kigogo mkubwa sana ndani ya serikali?

Kwani kuwa na nyumba Dubai ni kosa, je ni Mbowe tu ana nyumba huko kama mfanyabiashara, je aliiba pesa kajenga huko au ni kipato chake halali?
Tuache mitazamo ya kimaskini, kama tunategemea kuwa na viongozi maskini tu, tutakuwa tunajidanganya!!

Hongera sana Mhe. Mbowe kwa uwezo mkubwa wa kusimamia biashahara zako vizuri na kuendeleza mapambano ya kuwakomboa Watanzania kutoka kwenye umaskini uliosababishwa na CCM.
 
Wakuu JF amani iwe Nanyi.

Wale ndugu zetu wa Buku 7 Project wameamua kumbebea Bango Mbowe kwa kumiliki kwake Nyumba ya Kifahari Dubai.
Hawa jamaa hawataki kabisa kuhoji kama Mbowe kama Mbowe ana uwezo wa kumiliki Nyumba hiyo ama la.
Cha ajabu zaid, Ndugu zetu hao wanasahau Kabisa kuwa hapa kwetu Tanzania (Shamba la Bibi) kuna wageni wanamiliki Majumba na vitega uchumi vingi kabisa.
Wanasahau kuwa kuna Mwarabu kule Loliondo kamilikishwa Ardhi ya wa Masai.
Hivi hawa Ndugu zetu nikiwaita wana akili za Misukule nitakuwa nimewatendea haki kweli jamii ya watu wenye akili za Misukule ???
 
OK I LOVE THIS, NAOMBA NIKUONYESHEE UTOTO WA MAJIBU YENU KAMA NILIVYOSEMA MWANZONI:-

- Unasema sina brain na kwamba I am functionless, great una maana umekuja mbio kumjibu mtu ambaye ni no brain na functionless? Sasa what that tells about you?

- Eti ni mjinga gani Duniani anayeweza kulinganisha utajiri wa Mbowe na Mzee Kenyatta? Hivi wewe kweli ni mzima Uhuru familia yake ya Kenyatta inamiliki 50% ya Ardhi yote ya Kenya ambayo ni the best collateral kwa ajili ya benki kumpa mikopo ndio maana ameweza kuendeleza zile pesa kama vile Donald Trump, ambaye na yeye aliachiwa Ardhi nyingi na baba yake so ikawa rahisi kwake kukopa na kuendeleza mali za USD 200, Million alizoachiwa na baba yake, lakini sio Mzee Mbowe nasema bila kuogopa kwamba hakuacha mali mtoto wake leo kuwa na majumba nje nchi kama Dubai, USA na South Africa ambako ni lazima ulipie kodi kubwa sana ya property ama sivyo Serikali za huko zinakunyanga'nya ardhi au jumba.

- Unasema Disco la pale Mbowe ndilo limempa hela za kununua majumba ya kifahari nje ya nchi? Really? So huu ndio utetezi wako kwamba hizo nyumba ameweza kuzinunua kwa kuendeleza utajiri alioachiwa na baba yake, atakuwa ndio Mtanzania wa kwanza kuwa na akili namana hiyo bro, kwamba baba yako anakuachia Disco unalendeleza mpaka unaunua majumba ya kifahari nje ya nchi, that is the best joke of this week!!

- Mwenyekiti wenu bado ana kazi kubwa ya kujieleza amepata wapi hayo mapesa ya kununulia hayo majumba ya kifahari huko nje? Mali alizoachiwa Kenyatta na baba yake hazifanani hata robo na alizoachiwa Mbowe, halafu bado kuna swali kubwa kwamba mbona hmajawahi kusema to the public kwamba anamiliki majumba nje aliyonunua kwa hela za halali? Kwa nini tumejua sasa baada ya Zitto kumkomalia nyani giladi, poleni sana haya sasa nendeni mkawaaambie wananchi vijijini kwamba Mzee Mbowe alikuwa tajiri sana alimuachia mtoto wake ambaye ameuendeleza ndio maana sasa anamiliki majumba ya kifahari nje!!

VERY CHILDISH!!

Le Mutuz

Wewe hujui chochote...kwa akili yako unafikiri Mbowe anamiliki Bilcanas peke yake...?
Au wakati anajaza fomu ya maadili ameorodhesha vitu vyote hivyo..kwakuwa anajua ni kipato halali...
Waambie mafisadi wenzenu CCM kama kuna mtu anaweza kiweka wazi mali zake...open kama Mbowe.. Ndio maana Mwenyekiti wenu Kikwete kasema 2015 hamponi na mkinusurika 2020 ...ni mazishi
 
Back
Top Bottom