FIKRA PEVU EDITORIAL: Watanzania tutume SMS kwa watawala wajue.. namba hizi!

@mwanakijiji

jamaa wameweka mfumo wa kuchuja sms zinazowafikia wao, katika namba hizo ni zile tu zitazokuwa kwenye phone book zao ndizo zitaweza kupeleka sms mpaka kiganjani kwa wakuu uliowataja, lakini kama hauko kwenye phonebook zao itakuonyesha sms zimepokelewa lakini hazitafika kiganjani kwa wakuu bali zitaishia kwa wachujaji
Acha kuwadanganya watu.
 
Ngoja nipime kama viongozi wetu wanashukuru ngoja niwatumie M pesa nione watafanya nini
 
tukituma nyingi na wakijua kila wakishika simu kuna sms zinaingia watajua kuwa Watanzania wako serious. BInafsi sihitaji majibu, nahitaji wasikie! Majibu yatakuwa kwenye vitendo vyao.. Watanzania hatupendi kuwasumbua na kuwakera watawala hii ni njia mojawapo ya kuwafanya waogope kushika simu au wazizime kwani wakizifungua ni sms za mgomo tu!

Wakiona usumbufu watabadili namba za simu. Halafu tungepata na namba anayotumiaga JK anapokua nje ingesaidia maana muda mwingi hayupo nchini.
 
Kamwe hili siwezi kulifanya ww MM upo hulo detroit, unataka unichome mie mwana wa mwenzio kisa nn? Unataka unipoteze kwenye ramani.

Mkuu una maana MMM anapigana hii vita akiwa ng'ambo? Mimi siku zote nadhani tunaye hapa nchini. Mimi nimeishatuma nifanyeje sasa mkuu?
 
Mkuu una maana MMM anapigana hii vita akiwa ng'ambo? Mimi siku zote nadhani tunaye hapa nchini. Mimi nimeishatuma nifanyeje sasa mkuu?

ukituma ya kuwataka wewe makini hautaathirika, lakini ukituma ili kuwa kashifu na kuwasemea mabaya sana, ushahidi ni simu yako utakamatwa tu
 
Kikwete hasumbuliwi na sms zenu.

Alishasema kelele za mlango hazimsumbui mwenye nyumba kulala
 
Mpango mzima wa sekta ya afya ni janga la taifa, umejaa ufisadi wa hali ya juu kuliko wengi tunavyofikiria. Muda mwingi Madaktari wetu wengi wanautumia katika Hospitali zao binafsi vivyo hivyo maduka ya madawa mengi yanamilikiwa na Madaktari, Wauguzi na baadhi ya watumishi wa Idara za Afya. Vipato vya watumishi wa Afya hapa Tanzania ni vikubwa ukilinganisha na vile vya Watanzania walio kwenye sekta nyingine.

Kwa maoni yangu naona migomo ya Madaktari ina nia kuu ya kuendeleza kudumaza huduma za Afya ziltolewazo na Hospitali za Umma ili huduma hii iende kwenye Hospitali na Maduka yao binafsi.

Ni jambo la kawaida kwenye Hospitali nyingi za Umma huduma hazipatikani kulinganza na Pesa inayowekezwa na Serikali katika sekata hii. Hii inatokana na sababu tu ya undumila kuwili kwa upande wa watumishi hawa wanaojionesha wameajiriwa huku mipango yao ni kuimarisha miradi yao binafsi.

Inabidi Serikali iangalie upya muundo wa utumishi katika Idara za Afya. Ni vema ikaangalia na kuboresha viwango vya malipo kwa watumishi hawa na ikibidi kuwepo na maamuzi kwamba watumishi wanaohitaji kuendesha huduma ya Afya binafsi wasiwe watumishi katika Idara za Umma period.
 
Ngoja nipime kama viongozi wetu wanashukuru ngoja niwatumie M pesa nione watafanya nini

Haya matatizo yanayosemwa wewe hayakuhusu? au ni mmoja wa mafisadi? Bila shaka utakuwa mmoja wa watoto waliofilisi mashirika ya umma lakini hawayaoni hayo zadi ya kumlaumu JK tu....aaargh!
 
Toka jana najiuliza swali hili na sipati jibu naomba msaada wenu then ntatuma sms,

1-Kikwete 754 xxxxxx
2-Pinda 754 xxxxxx
3-Makinda 754 xxxxxx
4-Lowasa 754 xxxxxx
5-Rostam 754 xxxxxx
 
Mwanakijiji, shukrani kwa wazo mahili. Watanzania tumeni tu hizo text zinafika bila matatizo. Mimi nimesha tuma na zimefika na nimejibiwa mbili.
 
Toka jana najiuliza swali hili na sipati jibu naomba msaada wenu then ntatuma sms,

1-Kikwete 754 xxxxxx
2-Pinda 754 xxxxxx
3-Makinda 754 xxxxxx
4-Lowasa 754 xxxxxx
5-Rostam 754 xxxxxx

Ndugu, kwani mpaka sasa hujajua connection iliyopo kati ya Vodacom vs Rostam and Rostam vs Serikali iliyopo madarakani??
 
Mbona hizi namba tunazo siku nyingi? wewe umechelewa wapi kuzileta????? Lakini pia mwanakijiji wewe umeshapeleka maoni na kero zako kupitia namba hizi.... ulijibiwa??

VGL,

Kwani "siku nyingi" kulikuwa na huo mgomo wa madaktari?

Different scenes demands different schmes.
 
MM tunashukuru kwa kuhamasisha maandamano haya ya SMS.

Maana kila tukitaka kuandamana mitaani wanatuma PoliCCM wao wanatuzuia, kutupiga marungu na ujumbe wetu haufiki.

Nimetuma kwa wote ila ime'deliver kwa Makinda tu, nasubiri kwa hawa waheshimiwa wengine wawili.

Mimi ninashukizwa na kila kitu cha serikali, hakuna kilichokaa sawa, kila sehemu shida matatizo tupu naserikali haifanyi chochote kutatua. Sasa wanacheza na uhai wa raia waliowachagua na kuwaweka madarakani. Hawajui kwamba aliyekuchagua kukuweka madarakani akitaka atakutoa?

Nimeshangaa sana wakati madaktari wamegoma na raia walio wengin wasio na uwezo wa kutibiwa hospitali za kulipia wanakufa, rais anaenda kwenye mkutano davon sijui wapi anaongea pumba. Hii nimeifananisha na katika familia mwanao anaumwa hoi hoi wewe unavaa unaenda kumsalimia jirani.

Naomba wafungue simu zao ili mafuriko ya sms yaingie hadi waone kero na kuchukua maamuzi ya haraka yatakayokuwa profitable kwa pande zote mbili ya madaktari na wagonjwa.
 
MMUnatumia silaha mbovu it is not going to work. Hawa jamaa wote ni wagonjwa. Wanapmbana na moto wao. We need people like Malema. Just give me my AK45 or an RPG ndiyo lugha watakayoelewa. Empty words hazivunji mifupa. Hapa tulipofikia no retreat no surrender daraja nyuma limevunjwa? Shauri yenu come what may as a diehard soldier niko tayari kufa hata leo- Ebenezer! Kanyaga twende tune na Occupy Magogoni Huko Dodoma hakuna kitu lile Bunge bora ya Mirembe mental hospital yaani wanapiga makofi kwa kutokujadili mgomo shame on all MP's.
 
Back
Top Bottom