FBI ndani ya Tanzania, kazi ipo

Yawezekana FBI wakaja na wasifue dafu(tusipate jibu)- tuna mifano mingi, kwani Scotland yard walipata nini kuhusu moto wa BOT au kifo cha Dr Ouko kule Kenya. Hapa uchunguzi ni wa kufunika siyo kufumbua.
 
MAOFISA wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), wamekubali kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri Evaristus Mushi yaliyotokea Zanzibar Februari 17, mwaka huu.

Kwa mujibu wa habari za kuaminika zilizopatikana jana maofisa hao wako nchini na tayari wamekutana na baadhi ya viongozi wa Serikali kwa ajili ya kuanza kazi hiyo.

Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa maofisa hao walikutana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kwa ajili ya kuangalia ni namna gani watafanya shughuli zao katika upelelezi huo.

Kutua kwa maofisa hao kumekuja baada ya kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete katika salamu zake za rambirambi baada ya mauaji ya Padri Mushi kuwa ameliagiza Jeshi la Polisi kutumia nguvu zake zote pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama vya hapa nchini na mashirika ya upelelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji hayo.

Pamoja na ushiriki wa FBI, pia Serikali inazungumza na nchi nyingine rafiki ili kushirikiana nao katika upelelezi ya matukio mengine ya mauaji ya hivi karibuni.

Taarifa zinaeleza kuwa maofisa wa Serikali wamezungumza na taasisi za upelelezi za nchi tano ili kuongeza nguvu katika kazi hiyo.
Taasisi nyingine inayotajwa kwamba huenda ikashiriki katika uchunguzi huo ni Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Uingereza ya Scotland Yard.

Hatua hizi zinakuja baada ya Dk Nchimbi kutoa tamko la Serikali, Jumapili iliyopita, akidai kuwa mauaji ya Padri Mushi yalikuwa ya kigaidi hivyo Serikali itachukua hatua kali kuhakikisha waliohusika wanakamatwa.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa Serikali ya Tanzania kushirikiana na asasi za kimataifa katika ku chunguza matukio ya uhalifu na yale ya kigaidi.
Hii itakuwa mara ya pili kwa FBI kuja nchini kufanya operesheni kubwa ya upelelezi. Mwaka 1998, walifika kuchunguza kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani na kugundua ilikuwa kazi ya Kundi la Al-Qaeda.

Pia mwaka 1984 walikuja wapelelezi kutoka Scotland Yard kuchunguza kuungua kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima alithibitisha Serikali kuanza mazungumzo na mashirika mbalimbali ya upelelezi duniani kwa ajili ya kushirikiana nayo kuchunguza mauaji ya Padri Mushi.

Alisema tayari wameanza kufanya mazungumzo na mashirika hayo kutoka nchi mbalimbali, lakini alisema ni mapema mno kuyataja... “Ilatukikamilisha kila kitu tutawaiteni na kuwaeleza hatua tuliyofikia, ila tumeanza kufanya mazungumzo nayo. Kama unavyojua Rais Kikwete alitoa agizo hilo, sisi tumeanza kulitekeleza.”

Waziri Silima alisema kwanza wataanza kuchunguza mauaji ya Padri Mushi... “Tutaanza kuchunguza kwanza chanzo cha mauaji haya ili tujue kila kitu.”

Watuhumiwa wakamatwa
Polisi Zanzibar inawashikilia watu kadhaa wakihusishwa na mauaji ya Padri Mushi.

“Tumekamata watu kadhaa kuhusiana na kifo cha Padri na tunaendelea kuwahoji na wengine tutawaachia,” alisema Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa jana.

Source: Mwananchi

watanzania wakirudisha misingi ya amani ilyowekwa na waasisi wa Taifa hili wala fbi/scotland yard hawahitajiki. kuna mtu jana alisema ccm imefanya mambo mengi mazuri sana ila uzee imeipa mkono hivyo ipewe baibai
 
Sasa maadamu FBI wapo Nchini ni fursa pia kuwatumia kuchunguza waliomteka ulimboka kama ni magaidi au lah, maana SERIKALI ilisema haijui na kama kuna chenji itabaki katika kuwagaramia FBI basi sio vibaya wakachunguza na mauaji ya mwandishi Mwangosi tukajiridhisha ili jeshi letu libaki safi mioyoni mwa Wananchi.
 
MAOFISA wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), wamekubali kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri Evaristus Mushi yaliyotokea Zanzibar Februari 17, mwaka huu.

Kwa mujibu wa habari za kuaminika zilizopatikana jana maofisa hao wako nchini na tayari wamekutana na baadhi ya viongozi wa Serikali kwa ajili ya kuanza kazi hiyo.

Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa maofisa hao walikutana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kwa ajili ya kuangalia ni namna gani watafanya shughuli zao katika upelelezi huo.

Kutua kwa maofisa hao kumekuja baada ya kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete katika salamu zake za rambirambi baada ya mauaji ya Padri Mushi kuwa ameliagiza Jeshi la Polisi kutumia nguvu zake zote pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama vya hapa nchini na mashirika ya upelelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji hayo.

Pamoja na ushiriki wa FBI, pia Serikali inazungumza na nchi nyingine rafiki ili kushirikiana nao katika upelelezi ya matukio mengine ya mauaji ya hivi karibuni.

Taarifa zinaeleza kuwa maofisa wa Serikali wamezungumza na taasisi za upelelezi za nchi tano ili kuongeza nguvu katika kazi hiyo.
Taasisi nyingine inayotajwa kwamba huenda ikashiriki katika uchunguzi huo ni Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Uingereza ya Scotland Yard.

Hatua hizi zinakuja baada ya Dk Nchimbi kutoa tamko la Serikali, Jumapili iliyopita, akidai kuwa mauaji ya Padri Mushi yalikuwa ya kigaidi hivyo Serikali itachukua hatua kali kuhakikisha waliohusika wanakamatwa.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa Serikali ya Tanzania kushirikiana na asasi za kimataifa katika ku chunguza matukio ya uhalifu na yale ya kigaidi.
Hii itakuwa mara ya pili kwa FBI kuja nchini kufanya operesheni kubwa ya upelelezi. Mwaka 1998, walifika kuchunguza kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani na kugundua ilikuwa kazi ya Kundi la Al-Qaeda.

Pia mwaka 1984 walikuja wapelelezi kutoka Scotland Yard kuchunguza kuungua kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima alithibitisha Serikali kuanza mazungumzo na mashirika mbalimbali ya upelelezi duniani kwa ajili ya kushirikiana nayo kuchunguza mauaji ya Padri Mushi.

Alisema tayari wameanza kufanya mazungumzo na mashirika hayo kutoka nchi mbalimbali, lakini alisema ni mapema mno kuyataja... “Ila tukikamilisha kila kitu tutawaiteni na kuwaeleza hatua tuliyofikia, ila tumeanza kufanya mazungumzo nayo. Kama unavyojua Rais Kikwete alitoa agizo hilo, sisi tumeanza kulitekeleza.”

Waziri Silima alisema kwanza wataanza kuchunguza mauaji ya Padri Mushi... “Tutaanza kuchunguza kwanza chanzo cha mauaji haya ili tujue kila kitu.”

Watuhumiwa wakamatwa
Polisi Zanzibar inawashikilia watu kadhaa wakihusishwa na mauaji ya Padri Mushi.

“Tumekamata watu kadhaa kuhusiana na kifo cha Padri na tunaendelea kuwahoji na wengine tutawaachia,” alisema Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa jana.

Source: Mwananchi
heee,makubwa!yaan hatuwezi jambo lolote..!mpaka tukawaombe mabwana zetu!at least tunaweza kusambaratisha maandamano,na kuwashughuulikia "magaidi"akina dokta Ulimboka na kuua mwanahabari
 
Bora wawalete hao ma FBI,CIA na MASCOTLAND YARD waje watuchimbulie hawa magaidi wanaotaka kuharibu nchi yetu.Kama hofu kama ni kuchukua gas,mbona Ma-CCM wameuza madini yote,mbuga zote na rasilimali nyingine nyingi lakini bado hatuwachukulii hatua zozote zile.
 
Ingekuwa maandamano ya Chadema ungesikia, Tumepata TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA. Hivi kwenye unyama kama huu huwa hampati hizo taarifa.

Huu ni upuuzi bhana.
 
Nchi hii haiishi vichekesho. Tuna taasisi za upelelezi na ujasusi kibao (CID,TISS,DMI) zenye vijana weledi lakini hata viongozi wetu hawaziamini. Au ndiyo kufunika kombe mwanaharamu apite? Tuangalie yasije tokea yale ya Det. Insp. John Troon( Scotland Yard) na serikali ya Kenya..
 
Jamani watanzania hatuna jema,wangesema watafanya UWT na polisi tungekuja juu na kusema hatuna imani nao.Wamewaleta tunaofikiri wanauwezao,nguvu na technologia ya kisasa tunailaumu serikali kwa nini wamewaita,hebu tujiulize tunaopenda kulalamika tunataka serikali ifanyeje?

hawa ni wale vigeugeu kama NAPE na SHONZA.
 
Ingekuwa maandamano ya Chadema ungesikia, Tumepata TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA. Hivi kwenye unyama kama huu huwa hampati hizo taarifa.

Huu ni upuuzi bhana.

Ningekuwa nakujua nakutupia ofa, kwa kuongea ukweli. Nimekugongea like
 
Hv n upelelez wa mauaji au ndio wanaanza kusogea kisa wameckia kuna gec!huwa cwaamn hawa watu na tuwe makn yacje yakawa yale ya pakistan maana nchi zenye utajir wa asili hawa ndio wanasaidia pekee
 
Bora wawalete hao ma FBI,CIA na MASCOTLAND YARD waje watuchimbulie hawa magaidi wanaotaka kuharibu nchi yetu.Kama hofu kama ni kuchukua gas,mbona Ma-CCM wameuza madini yote,mbuga zote na rasilimali nyingine nyingi lakini bado hatuwachukulii hatua zozote zile.
Inaelekea ni namna ya kujitoa ktk lawama kwa kuwasakizia hao FBI.
 
Back
Top Bottom