Mahakama Kuu yamhukumu Grace Mushi kunyongwa hadi kufa kwa kumchoma mpenzi wake ndani ya nyumba mpaka kufa

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
754
3,097
Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imemuhukumu leo kunyongwa hadi kufa Grace Mushi (25) maarufu kama Neema baada ya kumtia hatiani kwa kumuua mpenzi wake Abdallah Sekamba.

Grace alimuua mpenzi wake kwa kumchoma moto hadi kufa kwa kutumia mafuta ya petrol, baada ya kumfungia ndani ya nyumba tukio alilolitenda Julai 16, 2021 eneo la Mbezi Makabe Dar es salaam.

Mushi.png


Ilivyokuwa...

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilithibitisha kumshikilia Grace Mushi maarufu mtaani kwao kwa jina la Neema kwa tuhuma za mauaji ya mpenzi wake Hamis Abdallah ‘Zungu’ ambaye alimmwagia Petroli akiwa ndani kisha kumchoma moto.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro amesema tukio hilo limetokea Mbezi Makabe kwa Mzungu.

"Muda wa saa 8:30 usiku Mtuhumiwa huyu alimfungia ndani ya nyumba Hamis akammwagia mafuta ya Petrol na baadaye akachoma moto kitu kilichosababisha Hamisi kufariki”

“Hamis alikua ni Rafiki yake wa kiume (Boyfriend), Mtuhumiwa alijaribu kutoroka lakini Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wananchi tukamkamkata na uchunguzi umebaini kulikuwa na mgogoro mkubwa wa kimapenzi kabla kufanyika kwa tukio hili la Kikatili
 
Back
Top Bottom