Fatma Karume: Dk Shein Siyo Rais wa Zanzibar

Hivi kwani kavile kasema sasa siyo? Rais wa Zanzibar ni Dr. Shein hili mjadala wake ni wa kupotezea muda. Bi. Karume na wengine wenye mawazo kama ya kwake inabidi wajipange na kujiuliza ni vipi walipotea na kusababisha Shein arudi madarakani ili wajipange tena kwa 2020.

Wangefanya nini kuokoa jahazi kwa Katiba hii na Tume ya Jecha ?! Bora hata Fatuma sio mnafiki
 
Shein ni dikteta wa Zanzibar! Amejitwalia madaraka kinyume cha taratibu. Hawezi kueneza demokrasia na utawala bora Zanzibar! Anaungana na madikteta wenzake duniani!
 
Mbona hakusema kama ccm ya bara ndio inayoiharibu zanzibar wakati wawakilishi wa zanzibar walipomkataa baba ake katika mbioza urais alipata 9% za kura zazanzibar. Hiyo hiyo ccm ya bara ikamueka baba ake na kuja kuuhujumu uchumi wa zanzibar na kunyang'anya mashamba ya watu. Mnafiki mkubwa.
 
Hawa viongozi wengi wa kiafrika wanaamini kuwa wanaweza kufanya lolote kwenye nchi zao, hata kama kuvizunja waziwazi Katiba za nchi zao na wasiweze kufanywa lolote, kwa kuwa wanajiona wana impunity ya kuwa ABOVE LAW.

Wanaamini pia kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama ingawa vinaendeshwa kwa kodi za wananchi, lakini kwa kuwa wao watawala ndiyo 'wanaovimilikI' kwa hiyo mwananchi yeyote atakayepinga dhulma ya watawala (atakayeleta fyoko fyoko) wataviagiza vifaru hivyo vya kijeshi viingie mitaani na kuwapondaponda raia hao wasio na hatia.

Mambo yaliyofanywa na Gbagbo wa ivory Coast mwaka 2010 kule nchini kwake na mambo yanayofanywa na Nkurunziza kule Burundi na haya yanayofanywa na Dr Shein huko Zenji, yanathibitisha pasipo shaka yoyote kuwa viongozi wengi barani Afrika pale wanapoapa kuwa wanamwomba Mwenyezi Mungu awaongoze ili wazilinde Katiba za nchi zao huwa kumbe wanafanya maigizo ya hali ya juu ambayo hayana tofauti kabisa na maigizo yanayofanywa na vikundi vingine vya maigizo kama vile vikundi vya akina FUTUHI!
 
MJUKUU wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, amepinga hatua ya kumtangaza Dk. Alli Mohammed Shein, kuwa rais Visiwani, anaandika Pendo Omary.

Fatma Amani Abeid Karume, mtoto wa kwanza wa rais mstaafu, Amani Abeid Karume amesema, “Dk. Shein, siyo kiongozi halali wa Zanzibar. Amewekwa madarakani na jeshi na kinyume na Katiba na taratibu za nchi.”

Amesema, “Rais aliyewekwa madarakani na vyombo vya dola, siyo rais wa wananchi. Rais anayewekwa madarakani kwa nguvu za kijeshi na vitisho, hawezi kuwa rais wa wananchi. Anakuwa rais wa majeshi.”

Akiongea kwa sauti ya uchungu na MwanaHALISI Online, Jumatano wiki hii, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, Fatma amesema, “Chama Cha Mapinduzi, kisijidanganye. Zanzibar siyo shwari. Kinachotengenezwa sasa, siyo utawala. Ni muendelezo wa chuki, visasi na uhasama.”

Amesema, “CCM ya Tanganyika, ndiyo inayoiharibu Zanzibar. Wanalazimisha viongozi wasiokubalika na wananchi Visiwani kutawala kwa manufaa yao binafsi.”

Soma mahojiano kamili na mwanasheria huyo mashuhuri nchini, katika gazeti la MwanaHALISI Jumatatu wiki ijayo.

Mwanahabari Huru
nimetokea kumpenda huyu binti
Ile hoteli yake sijui iliungua kwa bahati mbaya?
ukute iliugunzwa badala ya kuungua
 
kwa mtu yeyote mwenye busara hawezi kukubali urais wa Shein isipokuwa mwenye akili ya kiccm, ila wakumbuke kwamba huu ushenzi unaofanyika kwa kupitia majeshi lazima watakuja kupata hukumu yao,kama sio wao watoto wao na kama sio watoto wao wajukuu wao na mambo haya yamishaanza kutokea kwa aliyekuwa rais wa awamu ya nne na hizo ni cha mtoto kisasi kinaanza kuonekana kwa wenyewe kwa wenyewe sasa mziki ni pale watakapokuwa wale wanaonyanyasika kwa sasa
 
Back
Top Bottom