Fainali Uzeeni!....

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,752
7,846
Kumekucha jamani, shime tukajiandalie pensheni zetu...fainali Uzeeni.

Tunavyowapiga vikumbo wastaafu wa Jumuiya ya Africa mashariki, na hata wengine kuwadhihaki, ina maana hatukumbuki ipo siku nasi twaweza angukia
kwenye mzunguko huo huo. Mwenye macho haambiwi ona, na mwenye masikio halazimishwi sikiliza.

What goes around comes around.... Usipojiwekea akiba ya uzeeni, ujue unachezea shilingi chooni.
Tujiandae! Ujana ni moshi...unafuka huoooo wenda zake!...kufumba na kufumbua utajikuta marafiki wanapungua
kwa rate ya mafungu ya 10%...na kujikuta mkiwa...

Je, umejiandalia nini uzeeni? Una japo kibanda cha kujistiri? au unabahatisha maisha wewe? wanao ni Insurance, lakini pia usiitegemee 100% ipo siku watakusaidia....Jiandaee...fainali uzeeni!


Old+Age+Sri+Lanka+Daily+Mirror210709.jpg


"Old age is like everything else. To make a success of it, you've got to start young."

elderly-couple.jpg


"When marrying, ask yourself this question: Do you believe that you will be able to converse well with this person into your old age?
Everything else in marriage is transitory."

...Maisha ya uzee ni ukiwa!...story zako hazitakuwa na mvuto tena. Twaona wazee wengi wa miaka ile wamepitwa na wakati. hawawezi hata kuwapigia hata hadithi wajukuu sababu ya hizi Big Brother, Egoli, etc... watoto wa kisasa hawadanganywi na hadithi za sungura na fisi...

anza sasa kujijengea mahusiano mazuri na mkeo uwe na mtu wa kujifariji nae miaka hiyo ya ukiwa, ....fainali uzeeni!
 
Kuna mzee mmoja alikuwa anaponda raha tu hataki hata kujenga kisa akifa ataacha mali zake. Kufa hajafa hadi sahv na maisha yanambana.
Mbu ahsante kwa kutukumbusha.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mh Mbu hii kwa kweli inatia huruma kwa jinsi wazee wetu wengi wanavyoishi! Nakumbuka kulikuwa na mkutano mmoja ulioandaliwa na HelpAge International ambao waliainisha kuwa katika wazee wote nchini ni asilimia 4 tu ya waliokuwa covered na hizo pension zao!

But najiuliza hii fainali uzeeni kwa mkulima wa kijijini!! Mbona tutakuwa tunamwonea? Tukumbuke hiyo asilimia 4 ni wale waliokuwa wanafanya kazi za kuajiriwa!! Ambao wanastahili pension!!
 
kweli fainali uzeeni, mhhh cku hizi kuuona huo uzee imekuwa ishu kweli.

Hahaha kweli lakini nyamayao
Afu eti ni kweli kuwa watu wa huko Kasikazini wanaishi muda mrefu kwa sababu wanakula maparachichi kwa wingi?? Niliwahiuliza nikajibiwa hivi sa sijui niliingizwa mkenge!! But kule wazee wenye umri mkubwa naona kama wako kwa wingi (I might be wrong tho)
 
Sipendi kufikiri uzee,halafu kukubali kwamba umezeeka ni kazi.

Hivyo viajuza hapo juu vimenikosha kweli.

Asante kwa kutukumbusha sijui babu ASPRIN kama anafurahia uzee wake.
 
...kumbuka, pensheni yako haitokutosheleza kulipia;

1. kodi ya nyumba/chumba
2. ada ya shule kwa mwanao/wanao.

Ugumu wa maisha unaoupata sasa ni 'ishara' ya huko unakoelekea, na huenda yakazidi ugumu, upweke na ukiwa.

Wakati huo ushapoteza kazi, marafiki, na hata ndugu ulowainua kwa pesa zako za ujana. Wahenga walisema, ' mtumai cha ndugu...' Hala hala usijekimbiwa hata na wanao.

Jiwekee 'akiba'...jenga, nunua hisa kama unaamini, nunua pensheni, jiwekee bima ya afya, jipangie maisha...Muda unakuacha mkono.
 
Asante sana Mbu ndo maana mie naumiza kichwa changu hapa kama mungu atanijalia uzee kweli ujana maji ya moto
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
...kumbuka, pensheni yako haitokutosheleza kulipia;

1. kodi ya nyumba/chumba
2. ada ya shule kwa mwanao/wanao.

Ugumu wa maisha unaoupata sasa ni 'ishara' ya huko unakoelekea, na huenda yakazidi ugumu, upweke na ukiwa.

Wakati huo ushapoteza kazi, marafiki, na hata ndugu ulowainua kwa pesa zako za ujana. Wahenga walisema, ' mtumai cha ndugu...' Hala hala usijekimbiwa hata na wanao.

Jiwekee 'akiba'...jenga, nunua hisa kama unaamini, nunua pensheni, jiwekee bima ya afya, jipangie maisha...Muda unakuacha mkono.

Naona Mbu leo umepata ufunuo asante
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Naona huyu ndugu yetu (mosquito...sorry Mbu) anajitafutia ugonjwa wa moyo...Kwa bongo mambo yanaenda kwa Vodafasta tu...Unahangaika nini na watu hao au mambo hayo? Mla mla leo bwana!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Asante Mbu, sasa hapa wazazi wetu ambao ni wakulima tuwasaidie je?

Hongera sana mjukuu wangu kama bado unawafikiria wazee wako...May be ndo maana wengine mmejaziwa mibaraka!!

Kwa tulio wengi akili zetu zimegota kwenye matanuzi...makunywa kunywa kwa saaana tena, kula kula na totoz (apply to mitu ya aina zote!!)!!!


Mhhh.....Hata sijui kama tunaelewa tunakotoka na kinachotusubiri huko mbele ya safari!!
 
  • Thanks
Reactions: LD
Back
Top Bottom