Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic

Kuna mabwege nimebishana nayo hapa nayaelekeza yananibishia na kuniona mimi ninaongea nisichokijua.

Wakampigia fundi akasema ikiwaka taa ndio ipo On ikizima ndio ipo off. Nikasema duh....... Huu ni mtihani.

Huyo fundi atapoteza wengi, tena ukijaribu kumuelewesha ni wamoto balaa!
 
Hii concept ya taa ya OD/OFF kuwa on ikamaanisha umezima Overdrive na ikiwa off kumaanisha umewasha inawachanganya hata madereva wazoefu wa magari maana wengi huwa hawaijui ile kitu bali huwa wanaendesha tu gari.
Hii ni very confusing...., kwahyo kumbe napotembea kwenye mizunguko ya kawaida mtaani kwenye hizi speed za 30, 40, taa inatakiwa iwake kwenye dashboard...., nikiwa highway kwenye maspeed 80 huko ndo taa izimwe hapo kwenye dashboard..., ndivyo navyoelewa sasa.
Na je nini madhara ya kufanya vice-versa..., mfano niliaminishwa kwamba dashboard pasiwe na taa yyt inayowaka unapotembea, ni warning sign, na miaka 6 natumia gari kwa kuzingatia hilo, nini madhara mkuu?
 
View attachment 1220470
BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU
Wakuu naomba kufahamishwa, ni mahala au muda gani natakiwa kutumia OverDrive funcionality kwenye auto transmission. Ni kwa Ufahamu tu

Nawasilisha
---

---

---

UFAFANUZI WA JUMLA WA MATUMIZI YA OD

Overdrive ni nini?
Overdrive ni gia katika mfumo wa gari ambayo uifanya gari kuwa katika spidi kubwa huku mzunguko wa injini ukiwa mdogo. Kwa lugha rahisi, OD ni gia ya mwisho inayokupa mwendokasi ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.

Over drive ni kama gia ya ziada itakayokupa mizunguko mingi ya driving shaft kwa mizunguko michache ya engine yako. Unapaswa kuitumia ukiwa unatembea na mwendo mkubwa. Faida zake utatumia mafuta kidogo mana gari inakwenda kasi kwa mizunguko michache ya engine. Mfano katka gari ya kawaida yani 180km/h ili ufikishe speed 120km/h basi rpm inaweza kua 4000rpm. Katka barabara tambarare. ila ukiweka over drive unaweza tembea speed hiyo hiyo kwa rpm 2000 katika barabara tambarare.

Utajuaje kuwa Overdrive ipo On au Off?
Pindi uonapo kitaa cha overdrive kwenye dashboard ya gari yako inamaanisha kuwa Overdrive ipo off na pindi Kitaa cha overdrive kisipoonekana basi overdrive ipo on. Overdrive imewekwa Kama option yakutumia wakati ukiwa unatembelea speed chini ya 60km/h.

View attachment 1477985

Matumizi ya Overdrive ni yapi?
Unaweza kuitumia pia ikiwa unataka kuipita gari nyingine, mathalan, kwenye kilima ambapo nawe gari yako inakuwa imepungua nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4), na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka ukisha maliza tena matumizi yake.

Eneo lingine, ni mara gurudumu la motaklaa yako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa motokaa pia.

Watu wengine katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa motokaa, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogomea motokaa kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lilipasuka, nikiwa na maana kwamba hapo motokaa itakuwa inaacha njia na au kupinduka.

Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo.

Kitaa cha Overdrive kikiwa hakionekani kwenye dashboard yako maana yake Overdrive ipo Automatic au On na hivyo ndivyo inavopendekezwa na wataalam gari iwe automatic pindi upo mjini na unatembelea speed tofauti (sometimes less or more than 60)..kwa vile overdrive inatumia gear kubwa na speed less than 60km kwahio unaweza kutumia wakati unashuka milima mikubwa.

UFAFANUZI NA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU WA JF

---

---

---

---

---

---

---

---

---

---

---
Ssfi
 
Wengi wanaamini ikiwaka ni ishara kwamba O/D iko on!

sasa wanapokutana na habari ya kutakiwa kutoonekana kwenye dash basi wanavurugika!

Vilevile wengi hawaijui kabisa, akiiona inawaka halafu asikie gari inavuma anajua ndo inafanya kazi, pia akiiwasha ikatoweka kwenye dash anajua ndiyo ameizima!!
Mkuu mbona mm ikiwaka naona kama rpm huwa inapanda na nikizima rpm pia hushuka

Naomba ufafanuzi kidogo hapo maana saiv Hali ni Tete sana inabidi tubalance mafuta yasiyo na ulazima wa kutumika
 
Hii ni very confusing...., kwahyo kumbe napotembea kwenye mizunguko ya kawaida mtaani kwenye hizi speed za 30, 40, taa inatakiwa iwake kwenye dashboard...., nikiwa highway kwenye maspeed 80 huko ndo taa izimwe hapo kwenye dashboard..., ndivyo navyoelewa sasa.
Na je nini madhara ya kufanya vice-versa..., mfano niliaminishwa kwamba dashboard pasiwe na taa yyt inayowaka unapotembea, ni warning sign, na miaka 6 natumia gari kwa kuzingatia hilo, nini madhara mkuu?
Overdrive imewekwa hapo kukusaidia kuendesha gari efficiently kwa kubana uchomaji wa mafuta katika freeways.

Sababu unapochochea gari bila overdrive engine inatakiwa kutumia RPM kubwa kupata mwendo kasi na kuifanya gari ibalance mwendo na gear.
 
Mkuu mbona mm ikiwaka naona kama rpm huwa inapanda na nikizima rpm pia hushuka

Naomba ufafanuzi kidogo hapo maana saiv Hali ni Tete sana inabidi tubalance mafuta yasiyo na ulazima wa kutumika
Ukiweka overdrive wakati unaanza from 0 speed, gari inakuwa nzito mwanzoni sababu inakuwa inawahi kutafuta gearr ndogo haraka haraka, and then ikishafika kwenye gear mfano namba 4 inakuwa tayari imeshafikia speed kubwa ya 60+km/h. Na hapo ndipo utaona RPM inaanza shuka tena na haipandi sana kwasababu Overdrive function yake ni kusaidia kupata mchanganyiko wa haraka wa speed kwa mzunguko mdogo sana wa engine ya gari na hivyo kupunguzia kiwango cha mafuta utakachochoma ukiwa unachanja mbuga.

Angalizo tumia Overdrive kwenye maeneo ambayo gari ipo free kikimbia na hakuna vikwazo katikati yaani highways na freeways.
 
Mkuu samahan kidogo hapo sijakuelewa
Mm gari yangu nikiwasha kile kitaa ndo rpm inakuwa kubwa na kikizima rpm inakuwa chini
Naomba nifafanulie kidogo hapo kwenye rpm.

Samahani kwa usumbufu mkuu
 
Mkuu samahan kidogo hapo sijakuelewa
Mm gari yangu nikiwasha kile kitaa ndo rpm inakuwa kubwa na kikizima rpm inakuwa chini
Naomba nifafanulie kidogo hapo kwenye rpm.

Samahani kwa usumbufu mkuu
Ile taa inapowaka na kukuandikia OD/OFF, then maana yake umezima Overdrive function. Sasa hapo ina maana engine itakuwa inafunguka kwasababu inatumia nguvu nyingi ambayo sio tatizo ni kawaida sana.

Yaani engine ya gari yako inabidi izunguke kwa kasi sana (RPM) kulingana na namna unakanyaga pedal ya acceleration yaani unavyokanyaga mafuta ili iweze kuivuta gari haraka na kupandisha gear kutoka moja kwenda mbili, tatu, hadi nne then pale inakuwa inasubiria uapply overdrive sasa usipoweka overdrive utaona RPM inakuwa juu na mvumo wa engine unakuwa juu pia kuashiria gari inataka gear inayofuata.

Na ndio maana ukiweka Overdrive utaona ghafla RPM itaanza kushuka na mshale wa speed utaanza kupanda kumaanisha sasa speed ya gari inaongezeka huku engine ikitumia nguvu ndogo yaani mzunguko mdogo (RPM) kumaanisha sasa gari inatembelea gear laini kuliko zote na engine inatumia mzunguko mdogo sana kulifanikisha hilo huku gear iliyopo ikilikimbiza tairi kwa kasi mara dufu zaidi.
 
Ile taa inapowaka na kukuandikia OD/OFF, then maana yake umezima Overdrive function. Sasa hapo ina maana engine itakuwa inafunguka kwasababu inatumia nguvu nyingi ambayo sio tatizo ni kawaida sana.

Yaani engine ya gari yako inabidi izunguke kwa kasi sana (RPM) kulingana na namna unakanyaga pedal ya acceleration yaani unavyokanyaga mafuta ili iweze kuivuta gari haraka na kupandisha gear kutoka moja kwenda mbili, tatu, hadi nne then pale inakuwa inasubiria uapply overdrive sasa usipoweka overdrive utaona RPM inakuwa juu na mvumo wa engine unakuwa juu pia kuashiria gari inataka gear inayofuata.

Na ndio maana ukiweka Overdrive utaona ghafla RPM itaanza kushuka na mshale wa speed utaanza kupanda kumaanisha sasa speed ya gari inaongezeka huku engine ikitumia nguvu ndogo yaani mzunguko mdogo (RPM).
Ubarikiwe sana kiongozi nimeelewa vema
 
Yaani hili somo najitahidi kulisikikiza kwa makini naishia kuvurugwa akili yaani unamsikiliza mdau mmoja unamuelewa ukimsikiliza mwingine anakuchanganya tena mara OVD iwe on mara iwe Off yaani duuh!.
 
Overdrive inatakiwa kuwa off kwa kawaida . Kwa wale wanaoishi kwenye Theluji wanatakiwa waweke overdrive on ili kukabili utelezi. Overdrive ikiwa off gari yako ina ingia gia ndogo haraka badala ya kuchambua Gia moja baada ya nyingine hadi kuingia namba 4 au 5. Inasaidia mafuta pia. Huna sababu ya kuchanganyikiwa. Maelezo mengi hapo juu si ya kweli.
 
Mmmh mkuuu
 
Yaani hili somo najitahidi kulisikikiza kwa makini naishia kuvurugwa akili yaani unamsikiliza mdau mmoja unamuelewa ukimsikiliza mwingine anakuchanganya tena mara OVD iwe on mara iwe Off yaani duuh!.
Ni hivi over drive ni button iliyopo kwenye gari yenye traditional automatic gear box...sasa kazi ya switch ya over draft ni kuruhusu gari imalize gear zote au isimalize gear zote..sasa kawaida gari inatakiwa imalize gear zote for better fuel economy (yaan gari iwe kwenye perfect gear ratio at any desired speed).na ili gari imalize gear zote inatakiwa over drive iwe "off" yaan sasa unaondoa limitations yakutoifanya gari isishindwe kumaliza gear zote...ngoja ntoe mfano unipate vizuri (mfano Traditional automatic gear box iliyopo kwenye Toyota-IST ina gear nne, sasa kama over drive ipo off basi gari ita badiri(change) gear ratio kadri speed inavoongezeka mpaka kufika gear ya nne for top speed at low engine RPM, but ukiweka "OD ON" ambapo taa itawaka kwenye dashboard maana yake unaizuia gari isifike mpaka kwenye gear ya nne(top gear) ambayo ndo ipo design for high speed so matokeo yake gari iligari ifime speed za juu itabidi RPM ndo iwe juu ndo upate high speed is speed above 80kmh matokeo yake speed ya 90kmh unaipata kwenye rmp 4 badala ya rpm 2. Kinachotokea hapa ni kwamba when "OD ON" gari inaishia gear ratio za chini mfano mpaka gear ya tatu kwa ist na gari nyingi za automatic zenye traditional automatic gear box.....

Matokeo ya Kuendesha gari huku "ODE ON". Ni gari kunywa mafuta mengi sana kwakua utakua unalazimisha engine kufanya kazi kubwa at higher rpm ku attain high speed (cruise speed) ie kupata speed ya 80 at 3000RPM..

Pia kama cooling system haipo vizuri driving at higher RPM kwa muda mrefu with low speed ambayo hai match na rpm ya engine basi gari inaweza Over heat.

Driving higher speed with "ODD ON" inasababisha oil kuungua haraka because of excessive heat,,,so when engine temperature is excessive(na unatumia thin oil hzi za kileo mfano 5w-30), possibilities ya thin oil kupoteza thickness yake kua kama maji ni very likely...this bring us to another point where prolonged driving of car with "ODD ON" may potentially cause premature wearing of internal engine part.

Note: changamoto hii haipo kwenye gari za automatic zinazokuja na CVT transmission system.... By the way let me declare my interest...I love cars with CVT gear boxes...they drive so nicely ila zinataka umakini.. they are so mooth on road..no gear-shifting shocks, no gear hunting problem like in traditional automatic gear box,, because with CVT transmission has gapless shifting (continuous shifting) basi acceleration is very quick.. and car is always at perfect gear ratio hence better fuel economy..

I know kuna automatic gear boxes nyingi nzuri kama DSG(Direct shift gearbox/DCT(dual clutch transmission), but mh hizi nazo zina majanga yake mengi ya mechatronics..tuwaachie wanaopenda gari za ulaya waangaike nazo.
 
Overdrive inatakiwa kuwa off kwa kawaida . Kwa wale wanaoishi kwenye Theluji wanatakiwa waweke overdrive on ili kukabili utelezi. Overdrive ikiwa off gari yako ina ingia gia ndogo haraka badala ya kuchambua Gia moja baada ya nyingine hadi kuingia namba 4 au 5. Inasaidia mafuta pia. Huna sababu ya kuchanganyikiwa. Maelezo mengi hapo juu si ya kweli.
Kuhusu issue ya utelezi gari nzuri zinakua na button imeandikwa snow/ETC hii button kazi yake ni ku alter input za accelerater /gas pedal ilikuzuida gari zisi slip pale dereva anapokanya mafuta..hata kama akifanya sudden pressing of gas pedal basi tairi zi slip na sio kazi ya ODD button mkuu...na kwa gari zisizo kua na "snow button" basi dereva mwenye manually anataka kujipimia pressure atayo tumia ku press gas pedal ili kuzia slipping ya tairi anapokua kwenye barafu ili asipoteze control.
 
Back
Top Bottom