Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
Makabila hayatofautiani lugha pekee, ila mila na desturi pamoja na mahusiano kwenye ndoa zao pia huwa ni jamii inayojitofautisha na jamii ya kabila au makabila mengine.
Kuchepuka kwa wanandoa kwa baadhi ya makabila ni jambo la kawaida na wala halileti misukosuko mikubwa kwenye mahusiano katika jamii yao, limezoeleka na laonekana ni la kawaida tu. Usiyezoea desturi hiyo usioe/kuolewa huko, la sivyo utajimaliza kwa blood pressure kwa jambo ambalo katika desturi zao ni la kawaida sana.
Kuna rafiki yangu moja aliwahi kuniambia kuwa, kama ukimpenda mke wangu mchukue tu, niliduwaa na sikuamini kama mwanaume mwenzangu tena msomi aweza kuniambia hivyo na kuiachia green light kwa mke wake. Ikabidi nipunguze ukaribu kwao maana nimeanza kuzoeleka mno na ni kinyume kabisa na desturi zetu na kidini.
Kuna desturi twaambiwa katika jamii fulani ya wafugaji, jamaa ukifika nyumbani kwako na kuona jamaa kaweka mkuki mlangoni, we subiri amalize shughuli humo ndani, akitoka mpishe aende zake nawe maisha yaendelee na mke wako. Hilo likitokea kwa baadhi ya makabila itafumuka vita kali kati ya wasaksoni na wabaribariani✍🤣🤠
Matatizo ya ndoa nyingi kuvunjia mikanganyo mingi ni kutokana na kutofanyia utafiti wa tofauti za desturi zenye kupata mikanganyiko katika mahusiana, upekee wa desturi za mwenzi na mila zao. Tunakutana tu mijini na kuanza maisha bila kufanya utafiti na kufahamiana kutosha, na yatakayojilia, Lord God have mercy on us.