F.F.U wametapakaa kila kona ya manispaa ya Iringa Mjini!

Martoism

Member
May 31, 2012
36
21
IMG_0883.JPG

Huwezi amini kinachoendelea hivi sasa katika viunga vya manispaa ya Iringa mjini, Askari wasio na idadi wenye silaha nzito pamoja na magari yaliyofungwa vitaambaa vyekundu kuashiria hali ya hatari yanarandaranda kutisha wananchi, aidha wasifanye maandamano, fujo au wasihudhurie kabisa mkutano wa CHADEMA Unaotarajiwa kufanyika uwanja maarufu wa mwembetogwa.

Hivi sasa niko eneo moja linaitwa Kihesa, mbunge wa viti maalumu Mh, Chiku Abwao amezingirwa na FFU kwenye gari yake, huku Mh, Msigwa akikaririwa leo na kituo cha Redio cha Ebony FM kuwa chama chake hakitafanya maandamano bali watafanya mkutano wa hadhara kuanzia saa 8 mchana hadi 12 jioni.

Ntaendelea kuwajuza kila linalojiri wakuu.....
 
IMG_0886.JPG

askari wa FFU mkoani Iringa wakiwa wametanda eneo la uwanja wa Mwembetogwa ambalo Chadema ilipanga kufanyia mkutano wake leo wa kitaifa

IMG_0885.JPG

Mkuu wa FFU mkoa wa Iringa afande Mnunka akiwa eneo la uwanja wa Mwembetogwa kuzuia mkutano wa Chadema

IMG_0883.JPG

IMG_0889.JPG

Mfanyabiashara eneo hilo la Mwambetogwa akihamisha bidhaa zake kukwepa shari eneo hilo ambalo limetangazwa kuwa ni eneo la hatari na FFU

Picha kwa hisani ya blog ya Francis Godwin
 
Huwezi amini kinachoendelea hivi sasa katika viunga vya manispaa ya Iringa mjini, Askari wasio na idadi pamoja na magri yaliyofungwa na vitaambaa vyekundu kuashiria hali ya hatari yanarandaranda kutisha wananchi aidha wasifanye fujo au wasihudhurie kabisa mkutano wa CHADEMA Unaotarajia kufanyika uwanja maarufu wa mwembetogwa . Hivi sasa niko eneo moja linaitwa Kihesa mbunge wa viti maalumu Mh, Chiku Abwao amezingirwa na FFU kwenye gari yake , huku Mh , Msigwa akikariwa leo na kituo cha Redio cha Ebony Fm amesema kuwa chama chake hakitafanya maandamano bali watafanya mkutano wa hadhara kuanzia saa 8 mchana hadi 12 jioni . Ntaendelea kuwajuza kila linalojiri wakuu.....
Huu ni ukaburu Tanzania. Makaburu weusi wanajipambanua. CCM. Sensa ya Morogoro iliathirika vipi, na inatofauti gani na ya Iringa, Si wangetoa likizo ya shughuli zote mpaka sensa iishe?
 
.....[/QUOTE]
Mkutano kuanzia 8-12, jumanne, hayo si ni masaa ya kazi?
 
Morogoro walisema nane nane na jana siku ikaisha sijui kama hiyo sensa itaendelea hadi lini? maana nayo itaisha tu sioni swala la sensa na mikutano mbona wafanyakazi wanenda makazini? hii nchi sasa ni ya makaburu weusi
 
Huu ni utawala wa kiimla unaokuja Tanzania. Demokrasia sasa iko wapi?? Serikali Dhaifu inaendeshwa na matakwa ya chama cha siasa CCM?? Mwisho wao unakuja. Tutaizika pale Jangwani CCM miaka michache ijayo.
 
Tungemualika Mandela Iringa, ajikumbushie enzi zake, Nafikiri Babu wa Afrika atalia sana kuona kumbe kuna kaburu weusi.
 
Aiseeee babaangu naombeni mniabarishe hali ya ipogoro ikoje ni shwari au vita???
 
Serikali kumbe ina hela mwe! Hata kwa damu kumbe lazima ccm iwepo?
 
mkuu hebu endelea kutujuza maana wengine tuko mbali na maeneo na wakiwakataza kufanya mkutano basi mjue kuwa nguvu ya umma inaitajika zaidi.
 
Wana JF,Watanzania wote wapenda amani, hizi habari zinasikitisha na zinaudhi kuziona na kuzisikia!
Hivi CCM na serikali yake wanataka kutupeleka wapi nchi hii??? Inanikumbusha wakati wa enzi za Utawala wa Makaburu wa SA enzi za kina P.W.Botha yaani ni copy and paste kwa serikali ya CCM.

Hata hivyo mimi kama mpenda amani katika nchi hii napenda kutoa ushauri kwa Uongozi wa juu CHADEMA Taifa kutafakari hili tatizo. Kwamba ili kuepusha vurugu hizi kunusuru maisha na mali za Wananchi wa Iringa mjini basi kwa heshima na taadhima MAANDAMANO HAYA YAAHIRISHWE MPAKA BAADA YA SENSA. Najua itakuwa imevuruga ratiba nzima ya Operesheni Sangara lakini kwa muda.Watu wanasema, ''Never argue with a Fool,people may not notice the difference" Kwamba usibishane na mpumbavu watu wanaweza wasielewe yupi ni mpumbavu. Tunajua katika hilli CCM na Serikali yao ndo wapumbavu na wajinga wahedi,kwa hiyo ni kuachana nao mpaka hapo sensa itakapoisha sijui watasingizia kitu gani!

Baada ya sensa SANGARA na M4C viendelee kama kawa. Wanasema njia ya mwongo ni fupi leo watasema sensa,kesho watasingizia nini? CCM na Serikali yao wameshafulia. Inaonekana CCM kwa sasa hawali,hawanyi na hawalali kwa sababu ya mchecheto wa M4C!
 
Wana JF,Watanzania wote wapenda amani, hizi habari zinasikitisha na zinaudhi kuziona na kuzisikia!
Hivi CCM na serikali yake wanataka kutupeleka wapi nchi hii??? Inanikumbusha wakati wa enzi za Utawala wa Makaburu wa SA enzi za kina P.W.Botha yaani ni copy and paste kwa serikali ya CCM.

Hata hivyo mimi kama mpenda amani katika nchi hii napenda kutoa ushauri kwa Uongozi wa juu CHADEMA Taifa kutafakari hili tatizo. Kwamba ili kuepusha vurugu hizi kunusuru maisha na mali za Wananchi wa Iringa mjini basi kwa heshima na taadhima MAANDAMANO HAYA YAAHIRISHWE MPAKA BAADA YA SENSA. Najua itakuwa imevuruga ratiba nzima ya Operesheni Sangara lakini kwa muda.Watu wanasema, ''Never argue with a Fool,people may not notice the difference" Kwamba usibishane na mpumbavu watu wanaweza wasielewe yupi ni mpumbavu. Tunajua katika hilli CCM na Serikali yao ndo wapumbavu na wajinga wahedi,kwa hiyo ni kuachana nao mpaka hapo sensa itakapoisha sijui watasingizia kitu gani!

Baada ya sensa SANGARA na M4C viendelee kama kawa. Wanasema njia ya mwongo ni fupi leo watasema sensa,kesho watasingizia nini? CCM na Serikali yao wameshafulia. Inaonekana kanisa kwa sasa hawali,hawanyi na hawalali kwa sababu ya mchecheto wa M4C!
Hiyo kitu imeingiaje tena hapo?
 
Back
Top Bottom