ACT-Wazalendo wafunika Iringa Mjini. Zitto Ampongeza Filikunjombe, Msigwa bado

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
DSC_0074.JPG


KIONGOZI wa chama cha ACT Wazalendo amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) kuwa ni miongoni mwa wabunge wa mfano kutokana na utendaji kazi wake mkubwa badala ya maneno bila vitendo.

Huku aliyekuwa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa Chiku Abwao akimtaka mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (chadema) kuwaeleza wakazi wa jimbo hilo ndani ya miaka mitano ya ubunge wake amefanya nini zaidi ya maandamano na kutukana watu .

Kauli hiyo waliotoa wakati wa mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha wagombea ubunge wa jimbo la Iringa mjini na majimbo mengine ya mkoa wa Iringa na kuwa siasa si maneno matupu siasa ni kazi zaidi ya kuwakomboa wananchi waliokuamini katika maendeleo .

Alisema Bw Kabwe kuwa mbali ya kuwa yeye ni ACT wazalendo ila hata acha kuwazungumzia baadhi ya wabunge waliofanya kazi nzuri ya kuwatumikia wananchi wao na miongoni mwa wabunge hao ni pamoja na mbunge wa Ludewa Bw Filikunjombe kwani kazi aliyoifanya jimboni inaonekana na kazi aliyoifanya ndani ya bunge katika kupigania maendeleo ya wana Ludewa na Taifa kila mtazania anatambua mchango wake .

Kwani alisema kuwa kati ya manho makubwa ambayo Filikunjombe kama makamu wake mwenyekiti waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kamati liyoifanya ni pamoja na kuhakikisha ripoti ya Escrow inalindwa pasipo kuibiwa wakiwa wabunge watatu ambao walikesha wakilinda ripoti hiyo isiibwe na mawaziri waliokuwa wakizingira jengo walilokuwepo ili kuiba ripoti hiyo . '' Siku ile tulikesha na mashuka yetu ya kimasai kuhakikisha ripoti yetu haiibwi ili tuiingize bungeni na tukaiingiza bunge lakini ile ripoti hadi leo kuna mambo hayajamalizwa kwani kampuni ya IPTL ambao imenunuliwa na kampuni ya PAP ya Singa singa na kampuni hiyo ya PAP hadi leo bado inapokea Tsh bilioni 4 kila mwezi kutoka Tanesco hapo wazalishe ama wasizalishe'' alisema Kabwe Alisema kuwa kampuni hiyo asilimia 50 inamilikiwa na Seth Singa singa na asilimia 50 nyingine zinamilikiwa na kampuni inaitwa simba Trust iliyosajiliwa nje ya Tanzania na wamiliki wake hawafahamiki na kuwa hizo ndizo hoja ambazo ACT wazalendo wamejiandaa kutembea nazo katika kampeni ya uchaguzi mkuu.

Kabwe alisema kuwa sakata ya ECROW bado halijaisha kwani bunge liliagiza mtambo wa IPTL utaifishwe ila hadi leo bado kuna kigugumizi katika kuchukua hatua juu ya suala hilo la kampuni ya kitapeli kuendelea kulipwa mabilioni ya shilingi hivyo alisema kuwa haja ya chama cha kati kuingia Ikulu ili kuweza kupambana na mafisadi wa Richimond ambao leo wamejificha katika mwamvuli wa UKAWA .

Hivyo alisema kuwa kila sababu wabunge kufanya kazi wanayotumwa na wananchi wao kwa uadilifu badala ya kuwa wabunge wa maneno bila vitendo na kuwa wakati tukielekea katika uchaguzi mkuu ni vema wananchi kuwapima wabunge wanaowachagua kwa kueleza wamefanya nini majimboni badala ya kuwa na mbunge mpiga kelele zisizo za kimaendeleo kwa wananchi wake.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa ACT wazalendo jimbo la Iringa mjini Bi Abwao ambae amejiunga na chama hicho kutoka Chadema alisema mbunge wa jimbo hilo mchungaji Msigwa ajiandae kukabidhi jimbo hilo kwa ACT wazalendo kwani ameshindwa kuwatumikia wananchi wa jimbo la Iringa mjini kazi waliyomtuma bungeni .

Alisema kuwa kipindi cha miaka mitano ya mbunge mchungaji Msigwa jimboni hapo hakuna jipya ambalo amelifanya zaidi ya maandamano na vurugu ambazo wakazi wa Iringa mjini hawajapata kuziona na kuwa atazunguka kila moja hadi nyingine kuwaeleza wananchi jinsi ambavyo mbunge huyo alivyojaribu kuua nguvu ya vyama vya upinzani na kushindwa kuwajibika kwa wananchi waliomchagua.
 
Mkumbuke umati uliojitokeza wakati wa awamu ya kwanza na awamu ya pili ni tofauti sana.
 
Zitto ni mnafiki,leo tena anasema anaunga mkono ukawa ili kuiondoa ccm madarakani,mnafiki kabisa,tazama watu wanavyomsikiliza kwa tahadhari.
 
Zitto is a dead meat! hata yeye hajitambui anataka nini na anaelekea wapi? Nacheka sana eti Abwao apambane na Msigwa, ni kama kuchukua timu ya TOTO AFRICA ishindane na "MAN U". Na mtu yeyote mwenye akili timamu na anayeitakia mema nchi hii anapaswa kumuogopa zitto kama ukoma.
 
Chiku Abwao tangu enzi za Mrema hadi leo hachoki ?,tunataka mawazo mapya.
 
Nimekbuka jamaa walikuwa wanalalmika kuwa wanazomewa hapa Iringa mjini.....
 
siku akirudi kwenye kampeni atakuwa yeye na hawala yake chiku!! Hii ni aibu, watu wanapungua kila siku?

nyuma tu watu kibao je mbele ya jukwaa;

msingwa time will tell ; tumekupenda ila mungu kakupenda zaidi;
chiku na msingwa = kumraisishia mwakalebela na najua kamati iliyopo dododma itampitisha haitarudia makosa
 
hahaaaaaaa kila mkutano wa upinzani unafunika,haya twendeni majibu Oktober,muungane wote hamuambulii kitu kwa magufuli
 
Full bright politician.... Akisimamia zaidi utaifa kuliko chama..... Big up bro zitto
 
Wazalendo pekee ndie watakae liokoa taifa hili, kuliko mazuzu mengine yanapokea kivuli cha mufilisi wa nchi ajabukweli, TEAM WAZALENDO
 
Nimekbuka jamaa walikuwa wanalalmika kuwa wanazomewa hapa Iringa mjini.....

Hakika hawakuzomewa Iringa kwani ile tv iliopata mtonyo kwa EL(ITV) lazma wangeonesha maana hawa jamaa kuna mapato kwavyovyote,ukiona kimya tu ujue kimewangia
 
  • Thanks
Reactions: R.B

Similar Discussions

Back
Top Bottom