Je majengo yote yaliyoko Dar ya vitega uchumi yahamishiwe Dodoma au ni hili la MNF tu? Au mnapendekeza kuwa watu wasiwekeze tena Dar kwani tayari kumeshajazana au ni MNF ndio wataongeza kisichowezekana kuwepo? Hivi, ingekuwa taasisi ya kigeni ungeweza kusema security issue.. taasisi ya Mwalimu inatishia usalama wa Ikulu? really! Kwani walioenda kumtumia mkapa kuvunja sheria na waliopandikiza watu wao kwenye Ikulu ya JK leo hii walivunja wapi ili waingie? Usalama wa Ikulu hautishiwi na majengo!
Lakini si kila cha kumwenzi Nyerere ni halali, na ni kweli si salama kujenga hayo majengo marefu kuzunguka ikulu. Pia umesema Wachina ni wabia, hao ni hatari kabisa kua karibu na Ikulu. Halafu kwa kua ni biashara Ikulu itashindwa kuzuia wapangaji wasiowataka kupanga ndani ya hilo jengo karibu na Ikulu.
Uhusiano wa wahusika na CCJ si nongwa ili mradi CCJ imepewa uwanja halali wa kupambana kisiasa na uhuru wote kwenda kwenye vyombo vya sheria - kama ni kweli pia si nongwa maana ni ubinadamu tu kua hutampedelea mpinzani wako hasa unapojua unampa power mdomoni. CCJ wapo kutuonyesha uwezo wao wa kupambana na CCM wala si kuonewa huruma na CCM.