Wasimamizi Millennium Tower 2 wakiri changamoto ya lifti, waomba watumiaji kuwa wavumilivu marekebisho yakiendelea

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,818
11,996
Siku chache baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kudai 'lifti' tano kati ya sita kwenye jengo la Millennium Tower 2 hazifanyi kazi, wasimamizi wa jengo hilo wamekiri uwepo wa changamoto hiyo na kuwaomba watumiaji ikiwemo wapangaji kuwavumilia kidogo wakati wakifanya marekebisho ambayo wamedai yataleta muharobaini wa muda mrefu.

Akitoa ufafanuzi baada kuona taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa za JamiiForums baada ya kuibuliwa na mdau, Trude Henry ambaye ni Meneja Mwandamizi wa Prolaty Consult Ltd ambao ni wasimamizi wa jengo hilo, amesema lifti ambazo hazifanyi kazi kwa sasa zilipata tatizo na kuwa tayari walikuwa wameagiza lifti tatu ambazo tayari zimefika bandarini hivyo muda wowote wataanza mchakato wa kuziweka ili kupunguza changamoto iliyopo.

"Kuna mchakato ambao tunaupitia ili kuweza kununua lifti mpya, tumeuanza tokea mwaka jana (2023) ukakamilika tukampata mkandarasi utaratibu sambamba na taratibu zote za manunuzi na wakaagiza lifti tatu kwa ajili ya kuwa mbadala wa hizo ambazo zimepata matatizo," amesema Trude.

Ameongeza PSSSF baada kuagiza lifti tatu tayari pia kuna mchakato wa kubadilisha lifti tatu nyingine kwa kuwa zimekuwa zikisumbua kwa muda mrefu.
139.jpg
Pia amesema kama wasimamizi wa jengo taarifa za changamoto ya lifti na mikakati inayoendelea wanazo na wamekuwa wakiwasiliana karibu na wamiliki wa jengo hilo ambao ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuwajulisha kinachoendelea.

"Changamoto iliyotokea hivi karibuni tulikuwa na lifti mbili kwenye jengo lakini lifti moja ikapata changamoto na tukachukua hatua Mkandarasi aliyepo na Mkandarasi kutoka PSSSF pamoja na Mkurugenzi wa miradi wa PSSSF wote walikuja hapa kuongeza nguvu katika kuhakikisha miradi hii inaendelea na mpaka sasa hivi kuna timu inaendelea na jitihada za kuona kama lifti hiyo itafanya kazi," amesema.

Ameongeza "Lakini tuna lifti moja inayotumika ambayo ndio imekuwa ikitumika na ndio taarifa tuliyoiona JamiiForums ndio 'option' tuliyonayo na ile lifti mbadala inayoenda ghorofa ya sita.

"Tunachofanya wakati tukijitahidi kutatua tatizo kwamba tumeweka mtaalamu mmoja ambaye anasimamia Watumiaji wa lifti hiyo moja iliyopo kuhakikisha Watu wanakuwa salama, kuangalia kiwango cha watu wanaoingia maana kwa sasa presha ni kubwa unakuta watu wengi wanataka kwenda ofisini kwao kila mtu anata kuwai."

Aidha amesema kuwa wamewaomba wapangaji na watumiaji wa lifti hizo kuwavumilia na kuwashauri wanaopanda gorofa ya juu hadi ya sita ikiwezekana kutumia ngazi ikiwa jitihada mathubuti zinaendelea ili kuzifanya lifti kuwa salama kwa watumiaji.

"Tuwatoe wasiwasi sio kuwa kwa kukaa kimya tunadharau au hatufikirii kwamba kuna watu wanateseka ni kwamba lifti sio kitu kidogo ambacho unaweza kutoka kwenda ukakipata sehemu ni kitu kikubwa na kuna michakato"ameeleza Trude

Itakumbukwa Jengo hilo lina gorofa 24 na limekuwa na kumbi za mikutano na ofisi, hivyo mdau alidai kutumika kwa lifti moja imekuwa ikisababisha kero kwa watumiaji kutumia zaidi ya dakika 20 wakiwa wanasubiri lifti hiyo jambo ambalo alidai sio rafiki.

Soma - Millennium Tower 2, Lifti tano hazifanyi kazi inayofanya kazi ni lifti moja unaweza kusubiri zaidi ya dakika 20
 
Back
Top Bottom