Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Habari nilizonazo ni kwamba MNF (Mwalimu Nyerere Foundation) walitaka kujenga jengo la ghorofa 14 na 20 twin towers kama kitegauchumi kitakachoiwezesha taasisi kujiendesha yenyewe bila kutegemea michango ambayo kwa sasa haipatikani toka kwa mtu yoyote yule. Jengo hilo ilikuwa lianze kujengwa tangu mwaka jana lakini cha kusikitisha ni kwamba Wachina CRJE ambao ndio wajenzi walipotaka wapate building permit wajenge Halmashauri ya Jiji Ilala wakawaambia kwamba hawawezi kutoa building permit kwa sababu eneo hilo halipaswi kujengwa majengo yanayozidi gorofa 6 au tano sikumbuki vizuri.
Wakasema kwamba maagizo hayo yametoka kwenye kikao kilichofanyika Ikulu. Lakini ukiangalia katika eneo ambalo linadaiwa kwamba ni Security zone ya Ikulu yapo majengo mengine ambayo ni marefu na moja linaendelea kujengwa as we speak lina gorofa zaidi ya 20 pale karibu na Ocean Road.
Taasisi wamejaribu kupata waiver kwa kuwa ni mradi uliobuniwa na Baba wa Taifa mwenyewe wakati akiwa Mwenyekiti Mwanzalishi wa Taasisi. Ikulu imeziba masikio. wanadai Taasisi wapewe eneo jingine. Kama ni kupewa eneo jingine lazima liwe kwenye central area ili kuweza kupata wateja wauhakika kama ilivyodhamiriwa ili kuweza kurejesha fedha za Wachina na wabia wengine kama ADB, World Bank etc waliojitolea kuchangia ujenzi huo.
Ni wazi kwamba Ikulu wanakataa makusudi maana hakuna sababu yoyote ya kushindwa kuruhusu jengo linalobeba jina la Baba wa Taifa kujengwa katika eneo hilo kwa kuwa yapo majengo mengine marefu zaidi.
Vyanzo vya ndani vinasema watu wa Ikulu wanaogopa sana kuipa ujiko taasisi hiyo hasa kutokana na mwamko unaoendelea taratibu wa mawazo na fikra za Mwalimu kuhusu Taifa na hasa baadhi ya watu mashuhuri ambao sasa hawaoni tatizo kujipanga na fikra hizo. Lakini nyuma ya yote ni hofu kuwa yawezekana wakuu wa sasa wa MNF wanahusiana na CCJ na kama taasisi ikiweza kujijenga namna hiyo inaweza kuwa huru kweli na tishio hasa ikiwa karibu hivyo na Ikulu.
Hivyo, sitoshangaa endapo taasisi wakajikuta wanahamishiwa pembezoni mwa jiji...