Exclusive: Ikulu hawataki MNF ijenge "twin towers" karibu yao

Kwa Point ya usalama hapa IKULU wanasababu ambazo kwa mtu yeyote rational atakubali kuwa ni risk sana kwa Ikulu kuzuungwa na majengo ya kibiashara yanayoizi urefu IKULU yenye, yaani mtu anaweza kuwa juu akaona what is taking placing on the ground of The State House.

kuna ubaya gani kuona kinachofanyika Ikulu? Majengo marefu hayazunguki ikulu yoyote duniani? Mtu anaweza kufanya nini kutoka kwenye jengo refu lililo karibu na Ikulu ambacho hawezi kukifanya mbali na Ikulu? Sioni kama kuna hoja ya usalama kwa kweli.


But Ili IKULU kuonesha kuwa hoja yao inanguvu walitakiwa ama kubomoa au kusimamisha majengo yote yaliyozidi ghorofa 6 katika perimeter ambayo wao wanaiona ni security zone. Vinginevyo watakuwa wanaruhusu Politics kuchukua mkondo wake na kwa kuwa hili halijafanyika basi inanilazimu kuamini hoja ya Mkjj kuwa wanaiogopa MNF.

Hakuna sababu ya kusimamisha majengo.. ambayo walishayapa kibali.. au walipotoa vibali na kumkubalia Nyerere walikuwa hawajui kuwa wako karibu na Ikulu au Ikulu imekumbuka kuwa ni Ikulu hivi majuzi?
 
Yaani hujanielewa MKKJ, mimi sipo dhidi ya MNF!! Ninachosema ni kuwa, kama wanazibiwa (au wanaona kuwa wanazibiwa) basi wakawekeze kwingine, Tanzania si moja?

Hapana nimekuelewa vizuri tu lakini ni lini watu watasema 'this is it' sisukumwi tena? maana ukienda huko unakoenda wakaja tena na kusema hapa hapafai utafanya nini? Kwa mfano wapate kiwanja karibu na Bunge pale Dodoma wakaambiwa huwezi kuwa karibu na Bunge wahame? Wakipata kiwanja kizuri pembezoni mwa mbuga moja wataambiwa hapo hapafai itakuwaje?

Kama kuna majengo mengine yanayojengwa na hayafuati utaratibu huo wa 'ghorofa 6 mwisho', basi ndiyo, na yenyewe yasitishwe!!

kwani magorofa ya chini ya gorofa sita siyo tishio kwa usalama?
 
kuna ubaya gani kuona kinachofanyika Ikulu?
Haa haa haaa! Nilikuwa kule feri napiga picha ufukweni karibu na ukuta wa Ikulu, lakini nilikuwa napiga upande wa bahari, jamaa wakaichukua kamera. Mimi ilikuwa still picture, tena lengo lilikuwa upande wa bahari (maji), sasa unadhani mtu akiwa anaangalia Ikulu continuously ataruhusiwa?
 
Uelewa wangu, eneo la kati ya jiji kuanzia kule Ikulu hadi Samora Askari Monument lilitakiwa kuwa na majengo ya urefu unaoanzia Gorofa tano-sita kuanzia kule shoreline na zikiongezeka hadi kufikia kilele katikati pale, yaani Master Plan ilikuwa inataka sura ya maeneo hayo iwe na muonekano wa majengo wenye sura ya kichuguu. Lakini nilipoona wamejenga Twin TOWERS ikawa imeshaharibu ile sura iliyokusudiwa. Na kama vile kule kwenye Manzese jiji la DAR linajengwa chochote tu.

Sasa MMJ anatueleza kumbe Jiji linataka kurejea lilikotoka. Wavunje magorofa yaliyojengwa kisagasaga kwanza ili hii MNF itendewe haki.

Usalama gani! Kwani siku hizi unahitaji nini kuingilia usalama wa mtu, sio ukaribu kamwe, mbona wanapiga picha kila kukicha wakiwa Marekani! Jiji lina sababu nyingine. MMJ kama uko karibu na MNF washauri wakate rufaa, rufaa za namna hii husikilikwa kwenye kadamnasi, wanaitwa wataalamu na wadau wanaizungumza. Haina mlongolongo mkubwa wa sheria kama mambo mengine. Sheria inayotumika ni ya Mipango Miji na ile inayohusiana na Building Regulations!
 
kuna ubaya gani kuona kinachofanyika Ikulu? Majengo marefu hayazunguki ikulu yoyote duniani? Mtu anaweza kufanya nini kutoka kwenye jengo refu lililo karibu na Ikulu ambacho hawezi kukifanya mbali na Ikulu? Sioni kama kuna hoja ya usalama kwa kweli.




Hakuna sababu ya kusimamisha majengo.. ambayo walishayapa kibali.. au walipotoa vibali na kumkubalia Nyerere walikuwa hawajui kuwa wako karibu na Ikulu au Ikulu imekumbuka kuwa ni Ikulu hivi majuzi?

Mkjj Ndiyo narudi pale pale kuwa kubomoa hawawezi kwani mwanzo wakati wanatoa vibali vya ujenzi hawakuona security risk, kwa ni dhahili kuwa hawa jamaa huwa wanafanya maamuzi kulingana na what's best for them but not what's best for the country. Ingekuwa nchi ni ya kifalme basi tungesema hayo ni makazi ya kudumu ya familia ya kifalme lakini IKULU ni nyumba ya wananchi na waliopo pale huenda mwaka huu baada ya uchaguzi ukawa ndiyo mwisho wa kukaa pale vinginevyo watuambie kuwa wamejimilisha na hawatoki kwa vyoyote.

Huu wote ni woga na kutojiamini na nafasi zao. Ni dhahiri kuwa if your enemy has a powerful weapon he will win the battle, na kwa Tanzania, viongozi wa sasa wanaona njia pekee ya kuwanyima nguvu wapinzani ni kuwanyima mianya ya kuweza kupata resources (Finance). Kama ikijadhihirika MNF is behind CCJ na wao wameshatoa kibali itakuwa ngumu sana kukifuta bila nchi kupata msukosuko.
 
MKJJ,

Mkuu ninachojua ni kuwa pale ni eneo ambalo liko ndani ya security zone ya IKULU. Ambacho sikifahamu ni "nini perimeter ya security zone as may be defined by the security people at the IKULU" Kama kuna mtu humu anyejua naomba nijuze.
 
From one side of a coin unawezaa kuhisi MNF wameonewa lakini pia ukingaliwa upande mwingine MNF ni taasisi huru isyo ya kiserikali. Na wanaubia kama unavyosema ni WACHINA, ADB etc. Hizi pia ni taasisi za nje inawezekana wakawa na maofisi ya kudumu kwenye huo mjengo yakikailika.na watakuwa na uhuru wa kumpangisha mteja yeyote ilimradi ana vijisenti. hili linaweza kuwa tatizo

Labda cha kujiuliza Eneo hilo kuna THREAT gani kujenga jengo la binafsi zaidi ya ghorofa sita. There could be a logic as far as system ya usalama wa magogoni state house unavyoendeshwa kwa style ambayo wengi nikiwemo hatujui ukoje. labda ni wa style ya mwaka 1960,1980 au ni kisasa kama

Majengo yaliyopo na mengine yanayojengwa yasitishwe au ni hii MNF ndiyo inatakiwa kubadilisha azma yake ?
Hayo majengo mengine ya karibu yenye ghorofa zaidi ya sita yana uhusiano na serikali may be ndio maana ni rahisi kupindisha sheria na kama sio kupindisha sheria labda wanaweza kuweka manual/computirised na logical/illogical or whatever security monitoring system za Ikulu yetu
 
De Novo.. CCJ haihusiani na ujenzi wa MNF wala MNF haihusiani na CCJ. NI watu wengine ndio wenye hofu hizo. Ninachozungumzia hapa ni MNF ambayo ni taasisi ambayo Nyerere mwenyewe aliianzisha na toka wakati huo alikuwa ameshapata na hilo eneo.. sasa kwa nini leo wahamishwe? Kisa CCJ?

Hakuna mtu anayelia lia kuhusu CCJ ila kama kudai haki na usawa ni kulia lia basi tutalia sana kwani hakuna aibu kulia ukidai haki yako. Unataka tukae tu kimya na kukubali kwa sababu "serikali imesema". Yaani serikali ije kutusukumiza halafu tukubali kusukumwa kwa sababu tukilalamika tutakuwa tunalia lia. Haya ndiyo mawazo yamewafanya watanzania kuwa wanasukumwa sukumwa na serikali yao.

kwenye CCJ mstari umeshachorwa hatuuvuki..

Thanks MMM, actually na mimi hupenda iwe hivyo... ila post yako ya kwanza nayo inakazia hayo mawazo ya watu wengine!!! yaani ile post usingetaja CCJ, basi ningeona hakuna bias kwenye concern yako, ila baada tu ya kugusia CCJ na mimi nikapata wasiwasi wa hiyo link kwani hata kama mnadhani ipo au haipo, inaihribia tu MNF

na najua angekuwepo, kusingekua na hizi myths or reality i dont know

i dont support serikali kuwanyima kibali MNF lakini pia siamini kuvunjika kwa koleo ndio mwisho wa uhunzi... hamisha tent weka ghorofa sehemu nyingine, hakuna asiyependa kuhusishwa na nyerere hata mie ningekua tycoon ningehakikisha ofisi zangu napeleka MNF complex

zidumu fikra za mwenyeheri!
 
Mtazamaji.. ina maana katika majengo yote yaliyo karibu wote wanaishi nakufanya kazi watanzania peke yao isipokuwa hili jengo la MNF litakapokuja ndio litasogeza wageni karibu na Ikulu?
 
As long as Kikwete ni rais Ikulu na as long as Salim Ahmed Salim na Joseph Butiku wako MNF kibali hakitatolewa.

you are damn right!!! kuna watu wanasahau baadhi ya binadamu tumeumbwa na visasi vya generations... ndiyo maana nasema watafute pengine

MNF imedumazwa na utawala uliopo sasa madarakani...
 
jengo jipya lililopo karibu oshean road hospital lipo karibu sana na ikulu kuliko la MNF.
Jengo la wizara ya ardhi lipo karibu sana na ikulu kuliko hayo majengo yote, ukiwa ghorofa ya tisa unaona ikulu lakini huoni kitu kwa ajili ikulu imetanda miti mitupu.
Jengo la mkemia mkuu ukiwa ghorofa ya tatu unaona ikulu lakini ni miti tupu huoni kitu.
Jengo la MNF liko mbali sana na ikulu na maghorofa yote ya eneo lile yanaona ikulu.

kama jengo la MNF limenyimwa planning kwa nini jengo jipya linalojengwa pembeni ya hospitali lisisimame
 
Je majengo yote yaliyoko Dar ya vitega uchumi yahamishiwe Dodoma au ni hili la MNF tu? Au mnapendekeza kuwa watu wasiwekeze tena Dar kwani tayari kumeshajazana au ni MNF ndio wataongeza kisichowezekana kuwepo? Hivi, ingekuwa taasisi ya kigeni ungeweza kusema security issue.. taasisi ya Mwalimu inatishia usalama wa Ikulu? really! Kwani walioenda kumtumia mkapa kuvunja sheria na waliopandikiza watu wao kwenye Ikulu ya JK leo hii walivunja wapi ili waingie? Usalama wa Ikulu hautishiwi na majengo!

Hilo eneo ni conservation zone. Hata kuvunja lile jengo walilokuwa nalo ilikuwa makosa ingawa si wao walioanza mchezo huo. Hilo eneo ndilo pekee lililobaki la kijani kati ya mji. Hapastahili kujengwa maghorofa yote hayo hasa ukiangalia litakavyokuwa limebanwa. Lile jengo karibu na Ocean Road, ambalo ni abomination lakini angalau linapakana na uwazi wa gymkhana. Ni kama vile najengo yanayozunguka Central Park nayo yanavyopumua. Mji wetu hauwezi kubeba hayo maghorofa hapo wanapokusudia. Impact yake kwenye traffic, giza (kivuli chake kinawanyima raha jirani waote), huduma ya maji, huduma ya umeme, huduma ya maji machafu n.k. Hali ya hewa ya mji wetu inahitaji majengo yanayopumua na yanayoruhusu hewa kupita. Huyo aliyewashauri hao wakina MWF alikosea. Wajenge jengo fupi na bora watapata kuliko hayo maghorofa wanayotaka kujenga! Si kila kitu kinachokataliwa ni kwa nia mbaya.

Amandla......
 
FM.. wewe umetoa sababu ambazo zinaweza kabisa kuwa ni za kiakili kuliko za usalama wa Ikulu. Sasa kwanini wao Ikulu wasitoe sababu kama hizo na wakizitoa zihusu wote siyo kwa jengo moja tu. Ama?
 
As long as Kikwete ni rais Ikulu na as long as Salim Ahmed Salim na Joseph Butiku wako MNF kibali hakitatolewa.

Mambo ya ccm-mwalimu vs ccm whateever!ccj msipoimega ccm nani mwingine wa kufanya hivyo,ebu fanyeni mambo shala tuone bana....
 
Tupende au tusipende, jina la Nyerere ni kubwa sana katika historia ya nchi hii na halitakuja lifutike kirahisi hata tukikesha tunapiga ngoma kuimba nyimbo za kumtukana. Viiongozi wa kitaifa watafanya makosa sana kujaribu kujenga uhasama na Nyerere au taasisi yake kwa sababu watakuwa wanajiweka sememu mbaya sana ya historia. Jengo lile litakuwa na lifespan ya takriban miaka 50 na zaidi likiweka kumbukumbu ya uasisi wa taifa hili. Kikwete ana miaka mitano tu ya kuendelea kuwapo Ikulu, Butiku na Salim wana muda usizidi miaka kumi ya kuendelea kuwa active kwenye MNF. Kwa nini Ikulu haiwezi kuona mambo yote hayo kwa mbali, na badala yake waone jambo hili kwa upeo mfupi namna hii? Huenda ndiyo maana tunashindwa kuendelea kwa vile viongozi wetu wanaona mambo yote kwa upeo mfupi tu.
 
mwalimu wanaangalia mambo yote through a prism of power.. tunaona the same thing in Rwanda as we have seen it other parts of the world where people in power wanaamini mambo ambayo nje ya madaraka huwezi hata kuyafikiria.
 
Kwa kuongeza ladha ya mjadala, mnaweza kugonga HAPA

Kwa hii stori ya Kwenye Mwanahalisi, nadhani unaweza kuona tofauti kati ya MNF na TB. Hapa inaonekana kuwa TBA wanao wanatumia kivuli cha kutekeleza Mpango Mkakati wa Serikali ya JK mwenyewe ambapo yaonekana walikwisha mpiga changa la macho kwa kuingiza katika Bajeti yao ya Mwaka. Sijui kama kisheria ipo hivyo, hapa Mwandishi anaonyesh kuwa hata Mamlaka husika zinasema TBA wamejipa Kibali wenyewe kujenga hilo jengo karibu na IKULU na IKUKU imekuwa "kondoo" katika kulizuia lisijengwe.

Kimsingi, matumizi ya jengo la TBA na hilo la MNF ni yale yale ya Kibiashara kama ilivyo kwa TT la BOT.
lakini hapo kinachowapo kiburi wale wa Seikali ni kuwa hayo yatakuwa ya Serikali pasipo kuangalia kuwa yananaweza kutumika kumchungulia mzee na kuhatarisha usalama wake akiwa humo IKULU.

Hii ni matokeo ya Serikali yake Mwanyewe JK ya kuwaachia watu wa Mipango Miji wakae kwenye madawati wakila mishahara pasipo kazi yeyote, sasa ataingiliwa huko aliko kwa kuwa maeneo ya mitaani kwetu hayafai tena, hayapitiki tena kutokana na ujenzo holela na usiofuata mipango endelevu.

ikulu_1.jpg



FARAGHA ya ikulu iko mashakani. Ujenzi wa majumba makubwa na marefu karibu na Kitalu Na. 1, Mtaa wa Luthuli, Dar es Salaam ambako ni makao ya rais, unatishia faragha hiyo.
Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam walioongea na mwandishi wa habari hizi wamesema kuna uwezekano wa kila kinachofanyika ikulu kuonekana kwa walio katika majumba hayo marefu.
"Sasa ikulu watachunguliwa kama tunavyotendewa na wenye maghorofa mitaani; maana kule tunaonekana watupu," amesema Leticia Magasha mkazi wa Magomeni aliyekutwa karibu na jumba refu lililo mita chache kutoka ikulu.
Mkazi mwingine wa Dar es Salaam ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini amesema, "Kuonekana unaoga siyo hoja sana; lakini kuna suala la usalama wa ikulu.
"Wanaojenga waweza kuwa na nia njema, lakini watumiaji je?" aliuliza huku akitingisha kichwa mbele ya jengo ambalo linaota kwa kasi.
Hoja za wakazi wa jiji zinatokana na ujenzi wa jengo linalotarajiwa kuwa na ghorofa 19 lililoko pembeni mwa hospitali ya Ocean Road, Barabara ya Chimara, Kata ya Kigamboni, katika wilaya ya Ilala.
Taarifa zinasema jengo litaendeshwa kwa ubia kati ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na kampuni ya Palm Residency Limited.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Evance Balama, alipoombwa kusema lolote juu ya jengo hilo, alisema kwa kadri anavyojua, kibali (building permit) cha ujenzi huo hakikutolewa na Manispaa ya Ilala.
"Kibali kimetolewa na TBA wenyewe maana ndiyo wanaomiliki jengo hilo," alieleza Balama.
Kuhusu suala la usalama, Balama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani, alishikwa "kigugumizi" kulielezea hilo.
"Kwa kweli kuwepo kwa jengo hilo kwenye eneo lile, si jambo zuri sana. Hadi sasa naendelea kumtafuta meneja wa miradi wa TBA anieleze kwa kina jambo hilo; pia vijana wa Usalama wa Taifa wanaendelea kulishughulikia," alieleza mkuu wa wilaya.
Jengo linalohusika liko karibu na ikulu kiasi kwamba ni dakika tatu hadi tano kwa mwendo wa miguu wa kawaida.
Afisa Uhusiano wa TBA, Segolena Francis alipotakiwa kuelezea, pamoja na mambo mengine ubia huo, alitaka MwanaHALISI kuandika maswali na kumwachia ili "yafanyiwe kazi na wahusika," na kwamba majibu yangetolewa wakati wowote wiki hii.
Ujenzi wa jengo hilo ni utekelezaji wa "mpango wa kujiendeleza na kujiimarisha kiuchumi" unaoelezwa kwenye taarifa ya utekelezaji kazi za TBA, kwa miaka mitatu ya uongozi wa serikali ya awamu ya nne, kuanzia Desemba 2005 hadi Septemba 2008.
Katika taarifa yake ya Januari 2009, wakala huyo anasema ameingia ubia na wadau mbalimbali katika sekta ya ujenzi wa majengo makubwa, kwa kuzingatia sera yake ya uwekezaji.
Jumla ya miradi sita inaelezwa kutekelezwa ambapo mmoja kati ya hiyo ni huo wa ujenzi wa jengo lenye gorofa 19 jirani na ikulu. Miradi yote inatarajiwa kugharimu jumla ya Sh. 65 bilioni.
Taarifa zilizopatikana baadaye zimeeleza kuwa TBA imetoa ardhi ambayo ni kiwanja namba 45 na 46 huku mbia wake akigharamia ujenzi wa jengo hilo.
Taarifa zilizopatikana kutoka chanzo cha uhakika ndani ya ofisi za TBA zinasema mradi ukikamilika, jengo linatarajiwa kutumiwa kibiashara.
Eneo la chini litatumiwa kwa maduka ya bidhaa mbalimbali (shopping centre) huku eneo la juu likikodishwa kwa ajili ya makazi (apartments).
Baadhi ya wafanyakazi kwenye mradi huo wamesema karibu kila anayefika kwenye ujenzi huo na kuambiwa zitajengwa ghorofa 19, huwa anauliza iwapo ikulu imeridhia.
Hata hivyo, wafanyakazi hao wamethibitisha kuwa hawajawahi kuona yoyote akitishia au kushauri usimamishaji wa ujenzi. "Tunafanya kazi kwa kujiamini," alieleza mmoja wao.
Hadi sasa maghorofa yaliyo karibu na ikulu ni ya urefu wa wastani ya wizara za Elimu na Ardhi na hayatumiki kwa biashara au makazi.
 
Mk.. nadhani mengi usemayo ni mtazamo wako so vibaya kuwa na mawazo yako...security ni fani kama wengine wanavyosomea kuandika habari
 
Mtazamaji.. ina maana katika majengo yote yaliyo karibu wote wanaishi nakufanya kazi watanzania peke yao isipokuwa hili jengo la MNF litakapokuja ndio litasogeza wageni karibu na Ikulu?

Mwanakijiji sidahni kama tatizo ni jengo la karibu na ikulu kuwa na wageni. Tatizo naloliona mimi ni jengo la ghorrofa nyingi karibu na ikulu ambalo serikali sio mdau. I still think wana logic
 
Back
Top Bottom