Ex-girl friend wa rafiki yangu anataka tuoane

Mlati

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
207
60
Habari wana jf mimi nina rafiki yangu wa karibu sana alikua ana mpenzi wake walikua wanapendana sana.Ila hasa hasa alieonesha upendo wa dhati ni binti ambae alijitorea mambo mengi kwa ajiri ya huyu jamaa yangu kwani kwao na binti angalau mambo si mabaya na waliweza kukaa kwenye uhusiano takribani miaka minne na haikuwahi kusika au kufahamika kua huyu binti alikua na uhusiano na mtu mwingine pale mtaani kwetu hata siku moja.Huyu dada baada ya kumaliza kidato cha nne alikwenda Tanga ili kurudia mtihani wa kidato cha nne pindi tu ameondoka walikuja walimu wapya wa shule ya msingi ghafra jamaa yangu akawa ameanza mahusiano na mwalimu mmoja baada ya wiki mbili wakawa wameanza kuishi pamoja mpaka sasa ni mwaka wa tatu wako pamoja na wamesha zaa mtoto mmoja na jamaa yangu kisha toa mahari ili afunge ndoa na huyu mwalimu. Mara nyingi turiendelea kuandikana sms na huyu dada za kusalimiana na kutakiana maisha mema. Siku moja nikapokea ujumbe kutoka kwake kua ananipenda sana ila alikua anashindwa kuniambia na anataka tuoane. Nili mkataria nikamwambia ni swala ambalo hariwezekani kwani yeye alikua mpenzi wa rafiki yangu nita mueleza je? Jamaa yangu ili anielewe. Aliniambia mambo kama manne kuwa jamaa atakuwa mnafiki na kumzibia riziki kwani alimuacha hata bila kumtendea kosa lolote. Pili ingekua yeye ndio alimuacha alikua na haki ya kuraum. Tatu labda wangeacha kwa ajiri ya migogoro baina yao pia angelaumu. Bado anaendelea kunisisitiza nia yake ya kuishi na mimi nikafikia wakati kumuambia kua anatafuta njia ya kuripiza kisasi kwa ajiri ya kumuumiza jamaa yangu lakini amekataa vya kufa anadai yeye anacho angalia ni maisha yake ya baadae na sio visasi kwani mimi ninamfaa. Kiukweli kwangu mimi huyu binti nimetokea kumpenda ili niweze kuishi nae lakini tatizo ni huyu rafiki yangu atanichukuliaje? Jamani naombeni ushauri wenu
 
Mkuu unachanganya 'r' na 'l' sana. Hata hivyo umeleweka. Fuata moyo wako.
 
Nami nimemwambia kuwa kama hana kinyaaa kuwa mwenzake ameshavuruga aoe tu. Habari za Arusha by the way!
 
Mkatae unaemjua historia yake arafu umfuate usie mjua historia yake uone kama utakuwa unashinda MMU kulalamika mapenzi mabaya.
 
oa wewe unachelewa,kama yeye unaona itakuwa ni sehemu ya furaha yako usisite mdogo wangu,kuhusu jamaa yako huyo unaweza kumwepa kwa kuhamia sehemu nyingine, sio kwa kumwogopa bali kuepuka karaha
 
Moyo wa m2 ki kiza kinene, huwezi jua huyo bint ana nia gani hasa kutaka kuolewa na wewe. Labda mapenzi, labda na yeye aolewe kwa sababu aliyemwacha kashaoa. Kumbuka hisia za mapenzi kwa watu waliokuwa na uhusiano awali huwa hazifi hivyo lolote linaweza kutokea iwapo mazingira yataruhusu, kwa hiyo utakuwa na kazi ya ziada kuhakikisha kwamba penzilo kwake linakuwa bora kuliko alilokuwa anapata toka kwa rafiki yako hasa km mtakuwa wote mnaishi Ar, jitathmini chukua hatua.
 
We ndo mla mizoga eeh?

HA HA HA! PakaJimmy siku hizi sote tunakula mizoga tu ni kwa vile huwa hatujui fisi aliyewahi kupita katika mzoga hadi ukaufikia wewe. Shida ya huyu ni kwa vile anamfahamu fisi aliyemtangulia!!! Ila kama wanapendana ukweli nionavyo huyu binti ni mke safi!! Tena jamaa anamfahamu vizuri kwa kuwa alikuwa na rafiki yake huyo aliyemtosa!!
 
Kama na wewe unampenda oaneni. Hakuna sababu zozote za kumwacha huyo mrembo. By the way, huyo mrembo ana mapenzi ya dhati na mfano umeshauona. Usidanganyike kumwacha eti kwa sababu jamaa yako alikuwa anamla. Utampata wapi mrembo ambaye hajaliwa na mtu yeyote? Isitoshe, jamaa yako ameshaoa tayari, sasa kuna nini tena? Changamkia maisha kijana, kupata mke wa dhati ni kazi sana.
 
Moyo wa m2 ki kiza kinene, huwezi jua huyo bint ana nia gani hasa kutaka kuolewa na wewe. Labda mapenzi, labda na yeye aolewe kwa sababu aliyemwacha kashaoa. Kumbuka hisia za mapenzi kwa watu waliokuwa na uhusiano awali huwa hazifi hivyo lolote linaweza kutokea iwapo mazingira yataruhusu, kwa hiyo utakuwa na kazi ya ziada kuhakikisha kwamba penzilo kwake linakuwa bora kuliko alilokuwa anapata toka kwa rafiki yako hasa km mtakuwa wote mnaishi Ar, jitathmini chukua hatua.

Nani aliweka hiyo sheria? Au ni njia ya kuhalalisha ukahaba!
So mnapobwabwaja humu kila cku juu ya uaminifu mnamaanisha nn.
 
Acha kuwa MLAMBA MATAPISHI YA WENZIO!

Have some Honour and dignity to Mankind! Alikopita your Best Friend kunageuka OFF LIMITS automatically!

Hizo mambo zako za kulamba matapishi zitakutokea puani! We oa tu kila siku itakiwa ni COMPARISON kati yako na your Best (The Ex). Be expensive kidogo, dont be soo cheap! Kisa kaachwa ndo anakuona we wa maana????????
 
Back
Top Bottom