Kila rafiki nayempata anataka vita na mimi

Friedrich Nietzsche

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
1,145
1,911
Huwa najiuliza hii inakaaje yaan kila rafiki au marafiki nao wapata wanataka mashindano na vita namm.
Mwanzo nilijua ni coincedence baadae nilipofanya Tathmini nikagundua ni pattern kabisa kua kila rafiki lazima awe ni mnafiki au anachukua vitu kwa ajili ya kunitandika navyo baadae.

Nikiwa Advance nilikua na rafiki benet sana tulikua tumereport siku moja shulen hapo na tulikua tunasoma combination moja.Jamaa ni mwana kila mahali tuko wote sasa siku ikatokea nimefanya jambo fulani la aibu mbele ya shule tukiwa parade but ilikua kama comedy fulan watu walicheka sana.

Sasa uyo rafiki yangu yeye akawa ananiigiza kabisa tena ndo wa kwanza kunicheka na kukumbushia watu.Yaan watu washasahau hawana hata time na hiko kitu ye kwene vigenge anakumbushia ili grup lianze kunicheka na kunikejeli.

Kifupi n ile jamii ya watu wanaofurahia mtu kudharirishwa au kuandamwa au kuumizwa.Daah nilijiona mnyonge si kwasababu ya watu ila kwasababu yake sikutegemea yy ndo awe mwiba.
Yaan badala yy apotezee ye ndo akawa kubwa la maadui na wala hajishtukii bado anakuja kwangu na anaendelea na mawasiliano kama kawaida najiuliza huyu mwana ana Gut.

Nilivoenda chuo kuna jamaa tena alikua mwana tunasoma wote misele na kila kitu .Tunashare shida na raha
Siku Kuna kitu tumezinguana na wana rum sijui kitu gan si unajua mkiishi vijana laziam mpishane.Si ghafla kawatumia picha zangu nikiwa nimelala bila boxa

Waweza cheka ila 😂😂Ila inasikitisha likiwa jambo lako.Kuna siku kulikua na joto afu boxa chafu Vijana mnajua boxa chafu na joto visivopatana.Basi usiku nikaamka nikatoa nikalala zangu. Sasa yy sijui alikua anaamka saa8 usiku kusoma.Sasa kaniona kanipiga picha kazitunza kimya kimya.Akawatumia jamaa siku iyo tumezinguana Daah zilitrend chuo kizima.

Sasa nikajiuliza huyu jamaa alikua na lengo gan majibu sipati.Na aliowatumia si kua ni marafiki zake no ni room mate tu. Basi nikafanya kama yakikua masihara njapotezea.Lakini nikapunguza ukaribu tukawa tu marafiki wa kawaida sana.

Miaka mitatu baada ya kumaliza shule nakuja kugungua alikua ana file langu la picha na video za ajabu. Za ajabu naamanisha maisha ya chuo mara utoke kuoga uchi( si unajua kiumeni) , Kucheza miziki vibe, maigizo tunayofanya yaan kifupi ni ule ushenzi ushenzi.

Nikajifunza kuna watu ni hatari na ukimuona hatuna ugomvi wala hatujawai zinguana kusema analipa kisasi no.Tunaishi tu poa mara nyingine ananitumia kazi au kusaidia kitu Lakini shida ni huu upande wa shilingi alionao sifahamu anamalengo gani.

Kuna muda alikua anasema ukiwa maarufu tutafukua makaburi yako .Nilimpuuza kwasababu sijawai waza nitakua maarufu kumbe alikua anarecod kila details.
############%


Nilimind sana.

Yaan imefika sehemu nimekua insecure.
 
Huwa najiuliza hii inakaaje yaan kila rafiki au marafiki nao wapata wanataka mashindano na vita namm.

Yaan imefika sehemu nimekua insecure.
Kuna kipindi Nilivoona marafiki walivyo Niliamua kutoamua kuwa na marafiki ila kuwa na watu Ninaofahamiana nao..
Yaani nikiwa kazini kuna watu naofahamiana nao kazini ila sio marafiki zangu..TunaHangout na vitu kama hivyo..
Nyumbani na sehemu nyingine pia..
Ilinisaidia sana..

Kwa sababu si kila Rafiki atapenda Mambo yako kuna wengine wanakuja kutafuta Yo weakness Part ili wakuumize kwa makusudi
 
Sasa hiko ndio kinachonipa wakat mgumu sikua najua kweli mtu anakuja mnakua wote huku na huko kumbe anatafuta vitu vya kukutandika navyo baadae utadhan kana kwamba ametumwa
 
Marafiki wapo kaka ila ina tegemea na marafiki inshort kama mimi now sina rafiki officially maana nilishapigwa tukio hilo na rafiki zaidii ya ndugu kwao wanani faham pia home wanamfahamu yanii tumeanza urafiki tangu tupo chekechea imagine mpk now kila mtu ana twenty 25
 
Marafiki wapo kaka ila ina tegemea na marafiki inshort kama mimi now sina rafiki officially maana nilishapigwa tukio hilo na rafiki zaidii ya ndugu kwao wanani faham pia home wanamfahamu yanii tumeanza urafiki tangu tupo chekechea imagine mpk now kila mtu ana twenty 25
Alikupga tukio gan
 
Marafiki wapo kaka ila ina tegemea na marafiki inshort kama mimi now sina rafiki officially maana nilishapigwa tukio hilo na rafiki zaidii ya ndugu kwao wanani faham pia home wanamfahamu yanii tumeanza urafiki tangu tupo chekechea imagine mpk now kila mtu ana twenty 25
Duh alikufanyaje miaka yote hoyo
 
Back
Top Bottom