tumia ubongo kufikiri na sio macho tuu kusoma basi, huelewi kitu kaaa kimya, inawezekana huna hata gari so hujui uchungu wa sisi wenye kutumia fedha zetu, elezea bei imepandaje toka 2004 hadi 2114 nipe formula kama unayo, mimi nipo jikoni nasema ewura wanatudanganya, bisha kwa hoja, unasoma huo utumbo na unakubali??
Je unajua kama ewura waliwaomba wauza mafuta wauze kwa hasara na wiki hii watawafidia kwa kupandisha bei?
Walikuwa wana uza 2040, that means wakashushwa kwa tshs 36, na sasa wamerudishiwa ile 36 x 2 = 72 + ths ( ya usumbufu) bado unachekelea tuu ujinga unaofanywa na watu wachache
...Kweli tupu nilikuwa kigoma kilo ya sukari 2,800/= tena ya kutoka Zambia. Sijui Mtibwa na Kagera Sugar nao kwishney??Maisha magumu magunmu magumu magumu ikifika 2015 petrol itakuwa 4000 kilo ya sukari 6000 maharage 4000
<br /><font size="4"><span style="font-family: comic sans ms">BP imefungiwa kwa miezi mitztu inz maana serikali imejifungia yenyewe? Kama ni hivyo basi EWURA ni mtori sana.</span></font>
Pamoja na kwamba bei ya mafuta inapangwa na soko la dunia, tatizo kubwa la nchi yetu ni utitiri wa kodi, usimamizi mbovu wa uchumi wetu unaopelekea shilingi yetu kukosa nguvu ya soko na ufisadi, na kwa taarifa yako hivi vyote vinataka mtu makini, chama makini na serikali makini kuvisimamia (ambavyo havipatikani ccm) vinginevyo kwa "umasaburi" wenu mtabaki mkisema yeyote akiongoza ndivyo itakavyokuwa.tatizo la kufikiria kutumia masaburi ndo hili. Kwani tuna visima hapa TZ? bei ya mafuta yanapangwa na soko la dunia na sisi ni sehemu yake. Hata akiongoza slaa hamna anachoweza kufanya labda kama atagundua visima kule kwao karatu. Think kwa kutumia upstairs.
hivi mmemuelewa mtoa mada? au unabisha bisha, Ewura wali2mia formula iliyokuwa ikitumika hapo zamani kabla ya mgomo, na hiyo ni baada ya kugundua kuwa formula mpya imekosewa kitaalamu,.
[h=3]TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI ELEKEZI/KIKOMO ZA MAFUTA AINA YA PETROLI KUANZIA TAREHE 15 AGOSTI 2011[/h]
Kama ilivyo ada, na kulingana na Kanuni ya Kukokotoa bei za
bidhaa za mafuta ya petroli bei zimekuwa zikikokotolewa na kutangazwa na
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kila baada ya wiki mbili.
EWURA inatangaza bei elekezi/kikomo za mafuta ya petroli nchini zitakazoanza kutumika
kuanzia Jumatatu, Tarehe 15 Agosti 2011. Bei hizi zimekokotolewa kwa kuzingatia kanuni mpya
iliyoanza kutumika mwanzoni mwa mwezi huu. Pamoja na kutambua bei elekezi/kikomo za bidhaa
mbalimbali za petroli nchi nzima, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:
(a) Bei za jumla na rejareja kwa aina zote za mafuta zimepanda ikilinganishwa na bei zilizokokotolewa kwa ajili ya kuanza kutumika tarehe 1 Agosti 2011 ambazo zilitangazwa tarehe 3 Agosti 2011. Katika toleo hili bei zimepanda kama ifuatavyo: Petroli TZS 100.34 sawa na asilimia 5.51, Dizeli TZS 120.47, sawa na asilimia 6.30 na Mafuta ya taa TZS 100.87, sawa na asilimia 5.30. Mabadiliko haya ya bei za mafuta nchini yametokana na kupanda sana kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuendelea kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na dola ya Marekani (sarafu ambayo hutumika katika manunuzi ya bidhaa za mafuta kwenye soko la dunia).
Kwa mfano, kwa viwango vya bei zilizotumika katika chapisho hili, bei katika soko la dunia zimepanda kwa wastani wa asilimia 5.42 na thamani ya shillingi ya Tanzania imeshuka kwa shilingi 47.12 (asilimia 2.96) kwa dola moja ya Marekani. Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimepanda kama ifuatavyo: Petroli TZS 110.34 sawa na asilimia 5.70; Dizeli TZS 120.47 sawa na asilimia 6.54; na Mafuta ya Taa TZS 100.87 sawa na asilimia 5.49.
(b) Bei za rejareja na za jumla zingepanda zaidi endapo formula ya zamani ingeendelea kutumika. Kwa kulinganisha vigezo vilivyo katika fomula ya zamani na fomula mpya, bei za mafuta zingekuwa kama ifuatavyo:
Aina ya Mafuta Bei za Rejareja (TZS/L) Bei za Jumla (TZS/L) Kwa Formula ya zamani Kwa Formula Mpya Kwa Formula ya zamani Kwa Formula MpyaPetroli 2,298.33 2,114.12 2,230.07 2,046.62Dizeli 2,213.36 2,031.31 2,140.80 1,963.81Mafuta ya Taa 2,188.89 2,005.40 2,116.33 1,937.90
Kama inavyoonyesha kwenye jedwali hapo juu, formula mpya inaendelea kutoa unafuu kwa watumiaji ukilinganishwa na kama fomula ya zamani ingetumika. Ni dhahiri kuwa vigezo viwili vikubwa vinavyochochea kupanda kwa kasi kwa bei ya mafuta nchini ni kupanda kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania ukilinganisha na dola ya Marekani, sarafu ambayo inatumika kuagizia mafuta hayo.
(c) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.
(d) Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na fomula iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 5 la tarehe 9 Januari 2009 na marekebisho yaliyofanywa mwezi Julai 2011.
(e) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.
(f) Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa.
A: BEI ZA REJAREJA
Bei Elekezi Mji Petroli Mafuta ya Taa Dizeli (TZS/LT) (TZS/LT) (TZS/LT)Dar es Salaam 2,114 2,005 2031Arusha 2,198 2,089 2115Arumeru 2,198 2,089 2115Karatu 2,216 2,108 2133Monduli 2,203 2,095 2121Ngorongoro (Loliondo) 2,275 2,166 2192Kibaha 2,119 2,010 2036Bagamoyo 2,125 2,016 2042Kisarawe 2,121 2,013 2038Mkuranga 2,124 2,015 2041Rufiji 2,142 2,033 2059Dodoma 2,173 2,064 2090Kondoa 2,205 2,096 2122Kongwa 2,170 2,061 2087Mpwapwa 2,174 2,065 2091Iringa 2,178 2,069 2095Kilolo 2,183 2,074 2100Ludewa 2,244 2,135 2161Makete 2,237 2,128 2154Mufindi 2,188 2,079 2105Njombe 2,206 2,098 2124Bukoba 2,329 2,220 2246Biharamulo 2,303 2,194 2220Karagwe 2,345 2,236 2262Muleba 2,320 2,211
tatizo la kufikiria kutumia masaburi ndo hili. Kwani tuna visima hapa TZ? bei ya mafuta yanapangwa na soko la dunia na sisi ni sehemu yake. Hata akiongoza slaa hamna anachoweza kufanya labda kama atagundua visima kule kwao karatu. Think kwa kutumia upstairs.
Wewe una matatizo binafsi, Elimu ya kuungaunga una maana gani? We ndo mshamba unayejisikia una elimu ambayo haikukufungua akili.Au ndo ulikaa darasani peke yake. Watu wamesoma kutokana na historia za wazazi wao. Wengine wamepata vibarua ndo wanatumia hizo pesa kujisomesha. We mshukuru mungu wazazi wako walikuwa na uwezo wa kukulipia ukasoma bila kusimama.
Mi nasikitika kwamba kukosa uwezo wa kufikiri na kubwatuka maneno yasiyo chujwa, ni ishara tosha ulifauru kwa kudesa. Hekima kichwani hamna.
HUU NI UTHIBITISHO KUWA EWURA WALIDANGANYA NA KUTOA USHAURI POTOFU KWA SERIKALI, WANAPASHWA KUCHUNGUZWA NA KUFUNGULIWA MASHITAKA KWA KUSABABISHA HASARA KWA WANANCHI, SERIKALI AMKENI, ACHENI KUWATUMIA WATU WENYE ELIMU ZA KU-UNGA-UNGA, HAYA NI MATUNDA YAKE
Nilipotoa Mada zangu kuwa EWURA ndio Tatizo wengi mlipinga, mmeona ugumu wa maisha sasa!!!! Tupaze sauti zetu kwa nini wasinge tuachie zile bei zetu za mwanzo tulikuwa tunapata mafuta kwa 2040-2080 na wale wazee wa BP 2100-2150 sasa nini wamefanya?????
Costing Accountant.
katongo2002@gmail.com
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI ELEKEZI/KIKOMO ZA MAFUTA AINA YA PETROLI KUANZIA TAREHE 15 AGOSTI 2011
Aina ya Mafuta
Bei za Rejareja (TZS/L) Bei za Jumla (TZS/L)
Kwa Formula ya zamani Kwa Formula Mpya Kwa Formula ya zamani Kwa Formula Mpya
Petroli 2,298.33 2,114.12 2,230.07 2,046.62Dizeli 2,213.36 2,031.31 2,140.80 1,963.81Mafuta ya Taa 2,188.89 2,005.40 2,116.33
1,937.90
Kama inavyoonyesha kwenye jedwali hapo juu, formula mpya inaendelea kutoa unafuu kwa watumiaji ukilinganishwa na kama fomula ya zamani ingetumika. Ni dhahiri kuwa vigezo viwili vikubwa vinavyochochea kupanda kwa kasi kwa bei ya mafuta nchini ni kupanda kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania ukilinganisha na dola ya Marekani, sarafu ambayo inatumika kuagizia mafuta hayo.
A: BEI ZA REJAREJA
Bei Elekezi
Mji Petroli Mafuta ya Taa Dizeli
(TZS/LT) (TZS/LT) (TZS/LT)Dar es Salaam 2,114 2,005 2,031
Arusha 2,198 2,089 2,115
Arumeru 2,198 2,089 2,115
Karatu 2,216 2,108 2,133
Monduli 2,203 2,095 2,121
Ngorongoro (Loliondo) 2,275 2,166 2,192
Kibaha 2,119 2,010 2,036
Bagamoyo 2,125 2,016 2,042
Kisarawe 2,121 2,013 2,038
Mkuranga 2,124 2,015 2,041
Rufiji 2,142 2,033 2,059
Dodoma 2,173 2,064 2,090
Kondoa 2,205 2,096 2,122
Kongwa 2,170 2,061 2,087
Mpwapwa 2,174 2,065 2,091
Iringa 2,178 2,069 2,095
Kilolo 2,183 2,074 2,100
Ludewa 2,244 2,135 2,161
Makete 2,237 2,128 2,154
Mufindi 2,188 2,079 2,105
Njombe 2,206 2,098 2,124
Bukoba 2,329 2,220 2,246
Biharamulo 2,303 2,194 2,220
Karagwe 2,345 2,236 2,262
Muleba 2,320 2,211