EWURA waridhia kupandisha bei mafuta, bei mpya hizi hapa!

Status
Not open for further replies.

Neng'uli

Senior Member
Aug 1, 2011
126
33
HUU NI UTHIBITISHO KUWA EWURA WALIDANGANYA NA KUTOA USHAURI POTOFU KWA SERIKALI, WANAPASHWA KUCHUNGUZWA NA KUFUNGULIWA MASHITAKA KWA KUSABABISHA HASARA KWA WANANCHI, SERIKALI AMKENI, ACHENI KUWATUMIA WATU WENYE ELIMU ZA KU-UNGA-UNGA, HAYA NI MATUNDA YAKE

Nilipotoa Mada zangu kuwa EWURA ndio Tatizo wengi mlipinga, mmeona ugumu wa maisha sasa!!!! Tupaze sauti zetu kwa nini wasinge tuachie zile bei zetu za mwanzo tulikuwa tunapata mafuta kwa 2040-2080 na wale wazee wa BP 2100-2150 sasa nini wamefanya?????

Costing Accountant.
katongo2002@gmail.com

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI ELEKEZI/KIKOMO ZA MAFUTA AINA YA PETROLI KUANZIA TAREHE 15 AGOSTI 2011

Aina ya Mafuta
Bei za Rejareja (TZS/L)
Bei za Jumla (TZS/L)
Kwa Formula ya zamani
Kwa Formula Mpya
Kwa Formula ya zamani
Kwa Formula Mpya
Petroli

2,298.33
2,114.12
2,230.07
2,046.62
Dizeli

2,213.36
2,031.31
2,140.80
1,963.81
Mafuta ya Taa

2,188.89
2,005.40
2,116.33
1,937.90

Point. As time goes on watu wenye elimu za mashaka na vyeti vya kugushi wanazidi kushika nafasi za maamuzi na matokeo ndiyo hayo. Vyuo vyetu sasa hivi ni viwanda vya kugawa vyeti na siyo kuimarisha taaluma. Watu wana vyeti ambavyo siyo wenywe walifanyia kazi bali kwa kuwa wana pesa waliwalipa wengine wawafanyie test, kuwaandikia thesis, kuwafanyia research. n.k. Ni matokeo ya mfumo wetu wa elimu. Tutakuwa nchi inayoendeshwa na vihiyo watupu muda si mrefu.
 
BP imefungiwa kwa miezi mitztu inz maana serikali imejifungia yenyewe? Kama ni hivyo basi EWURA ni mtori sana.
 
Sina imani na ewura nahisi kama vilaza ndo waliotulisha sumu namna ya kukokotoa kama namba zawagonga si muende udsm pale mkawape wazee wa maths wafanye mambo ya maana.
Msiona haya inaruhusiwa kuomba msaada
 
Maisha magumu magunmu magumu magumu ikifika 2015 petrol itakuwa 4000 kilo ya sukari 6000 maharage 4000
 
Mkuu mtoa mada ingekuwa vyema kama ungeainisha kwamba ni kwa kiasi gani kwa mfano walikosea kukokotoa kwa takwimu angalau mbili tatu hivi hii ingetufaa sana, heshima kwako na wapenda nchi wote.
Nawasilisha.
 
mtoa mada una uhakika kwamba wameridhia? bei hizo mpya za wk ijayo umeziona wapi? kama ungesikiliza kipima joto itv jana ungeelewa usanii wa wauza mafuta kwenye demurrage charges. ungeelewa kuwa hata sasa kwa kanuni hii mpya ewura ingetakiwa kubana tena kwenye hizo charges. with the current formula the determinant factors ni bei kwenye soko la dunia na exchange rate ya dola vs tshs.
 
Kwetu iringa umesema kweli, hiyo geresha tu, kama serikali ina hisa pasu kwa pasu na BP haiwezi kujifungia ila wameamua kutunza mafuta yao ili waje wauze kwa bei ya juu zaidi.
Watoto wawakubwa wabaki kuwa mameneja wa hoteli za baba na mama zao wasipewe nyadhifa kubwa kwenye maeneo hatari kama haya. Wakati ule watoto wa Mongela na wengine walikuwa benki kuu wakajaribiwa toka kukokotoa mahesabu mwisho wakaishia kugawa chai lakini kwa mishahara ya wakokotoaji na waandika cheque.
Nchi hii inachosha na kama sisi watanzania tusipoamua sasa hali inaelekea ndiko siko maana tunadidimia, tunafukarishwa na tunafirisiwa na watu wachache tu. Rostam, Ngoyayi, Ridhwani, akina mulamba na wengine hata mkapa si salama hafai, na huyu anayejifanya mtoto wa mkulima ipo siku yake yaja anadanganya watu tu
 
Maisha magumu magunmu magumu magumu ikifika 2015 petrol itakuwa 4000 kilo ya sukari 6000 maharage 4000
tatizo la kufikiria kutumia masaburi ndo hili. Kwani tuna visima hapa TZ? bei ya mafuta yanapangwa na soko la dunia na sisi ni sehemu yake. Hata akiongoza slaa hamna anachoweza kufanya labda kama atagundua visima kule kwao karatu. Think kwa kutumia upstairs.
 
Ni ukweli usiofichika kwa wale wote watalaamu wa Costing, kuwa EWURA waliishauri vibaya serikali na kusababisha wananchi kuteseka bila mafuta, Mgomaji wa kwanza ni serikali yenyewe kupitia kampuni yake ya BP ambayo inamilikiwa na serikali pamoja na PUMA Energy asilimia 50 kwa 50.

EWURA walikosea makadirio ya Demmurrage charges, na kutaka kwa wauza mafuta wauze chini ya gharama ambazo hata kichaa hawezi kuuza kwa bei hiyo, matokeo yake watu tumeuziwa uchafu wa mafuta na sio mafuta tena kwa bei mara 3 ya bei ya kawaida, tumefedheheshwa, tumeshuka kiuchumi, na hata wengine kukosana na wakubwa wetu wa kazi.

SERIKALI IFANYE UCHUNGUZI NA ITAKAPO BAINI MWENYE HATIA AFUNGWE KWA HESHIMA YA NCHI, EWURA WATAFUTE WATAALAMU NA SIO VIJANA AMBAO WANA ELIMU ZA KU-UNGA UNGA, NA KUTULETEA KERO.

WAKISHINDWA WAWACHUKUE VIJANA KWENYE MAKAMPUNI BINAFSI, TUPO WENGI.

KATONGO ACCOUNTS SERVICES
katongo2002@gmail.com
nilichokisikia ni kuwa watapandisha bei elekezi kulingana na soko la dunia si kwamba watajipandishia tu. source kipima joto ITV jana usiku.
acha kuongopa. Au wewe ndo wale wanaofikiria kwa kutumia masaburi?
 
Bado wengi wapo nyuma sana kuhusu ili suala Nenguli(katongo accounts services)alishusha hesabu husika hapa jf,Nenguli big up jk na serikali yake wanadhani watanzania wote ni wajinga,wala hawajamfungia mtu hapo, huyu masebo na vijana wake wanamfurahisha ngereja ili apitishe bajeti yake ipite waliowengi hawajui kuwa kiini cha tatizo sio makampuni ya mafuta bali ni EWURA wengi waliangalia zaidi uhaba wa mafuta bila kujikita kwenye kiini cha tatizo,haiwezekani kampuni zote zigome kwa wakati mmoja bila ya sababu ya msingi. Lipumba nae juzi alitahadhalisha juu ya athali za kutumia ubabe kuamua juu ya jambo hili , kwa uelewa wa watz wameisha sahau suala hilo sasa bei inapanda j3 au j4 huku kesi ipo mahakamani.hakika huu ni utoto.
 
Hapa ni kichekesho kwani hao ewura baada ya kugundua makosa wamejichukulia hatua gani, kuifungia BP ni kuinyima serikali mapato inawezekana ni nkwa sababu haikutoa chochote kwa hao ewura maana ni makampuni mengi yaliyogoma kuuza mafuta. Hapa kuna harufu ya Ufisasi. Tusubiri tuone.
 
mtoa mada una uhakika kwamba wameridhia? bei hizo mpya za wk ijayo umeziona wapi? kama ungesikiliza kipima joto itv jana ungeelewa usanii wa wauza mafuta kwenye demurrage charges. ungeelewa kuwa hata sasa kwa kanuni hii mpya ewura ingetakiwa kubana tena kwenye hizo charges. with the current formula the determinant factors ni bei kwenye soko la dunia na exchange rate ya dola vs tshs.
mkuu huyu mleta maada ninavyoona ni kam vile anafikiria kwa kutumia masaburi. Yaani haelewi ila anakurupuka tu, sijui kalewa mbege? Aggghhhh!!! nashindwa hata kumjaji.
 
Kwetu iringa umesema kweli, hiyo geresha tu, kama serikali ina hisa pasu kwa pasu na BP haiwezi kujifungia ila wameamua kutunza mafuta yao ili waje wauze kwa bei ya juu zaidi.<br /> Watoto wawakubwa wabaki kuwa mameneja wa hoteli za baba na mama zao wasipewe nyadhifa kubwa kwenye maeneo hatari kama haya. Wakati ule watoto wa Mongela na wengine walikuwa benki kuu wakajaribiwa toka kukokotoa mahesabu mwisho wakaishia kugawa chai lakini kwa mishahara ya wakokotoaji na waandika cheque.<br /> Nchi hii inachosha na kama sisi watanzania tusipoamua sasa hali inaelekea ndiko siko maana tunadidimia, tunafukarishwa na tunafirisiwa na watu wachache tu. Rostam, Ngoyayi, Ridhwani, akina mulamba na wengine hata mkapa si salama hafai, na huyu anayejifanya mtoto wa mkulima ipo siku yake yaja anadanganya watu tu
<br /> <br / umenena
 
Ni ukweli usiofichika kwa wale wote watalaamu wa Costing, kuwa EWURA waliishauri vibaya serikali na kusababisha wananchi kuteseka bila mafuta, Mgomaji wa kwanza ni serikali yenyewe kupitia kampuni yake ya BP ambayo inamilikiwa na serikali pamoja na PUMA Energy asilimia 50 kwa 50.

EWURA walikosea makadirio ya Demmurrage charges, na kutaka kwa wauza mafuta wauze chini ya gharama ambazo hata kichaa hawezi kuuza kwa bei hiyo, matokeo yake watu tumeuziwa uchafu wa mafuta na sio mafuta tena kwa bei mara 3 ya bei ya kawaida, tumefedheheshwa, tumeshuka kiuchumi, na hata wengine kukosana na wakubwa wetu wa kazi.

SERIKALI IFANYE UCHUNGUZI NA ITAKAPO BAINI MWENYE HATIA AFUNGWE KWA HESHIMA YA NCHI, EWURA WATAFUTE WATAALAMU NA SIO VIJANA AMBAO WANA ELIMU ZA KU-UNGA UNGA, NA KUTULETEA KERO.

WAKISHINDWA WAWACHUKUE VIJANA KWENYE MAKAMPUNI BINAFSI, TUPO WENGI.

KATONGO ACCOUNTS SERVICES
katongo2002@gmail.com

Ebu toa ufafanuzi una maana EWURA ilileta mgomo wote kwa mambo yasiyo na uhakika? Mbona itakuwa kashfa kubwa sana?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom