Elections 2010 Eti Sitta ataka uspika, asema anafaa, Kweli ataliweza hilli Bungo La 10

Yeye anaongea kama nani sasa? kwa nini hao wanaodaiwa kuwa wapinzani wa SIX wasiseme wenyewe? au tuamini kuwa ndo ile kampeni ya kumuondoa SIX? Hebu waache uchafu wao huko
 
Sitta mwenyewe mnafiki tu, apite asipite haitusaidii lolote. Kwanza naona bora hata Chenge apite kwani tutakuwa tunajua moja kwamba FISADI anaongoza bunge, sio tunajua eti mtu makini na wa ukweli kumbe akibananishwa na vikao vya chama anapiga magoti kuomba msamaha!!
 
Nawambieni ukweli tupu, Spika ni chenge ama Makinda. labda kama wakibadili leo mpango wao lakini hizi ndio zimetoka kwao wenyewe. mmoja kati ya hao atakua naibu mwingine spika. na Rostam ndo anasuka mpango mzima na akina Lowassa. wanafanya haya wakijua uongozi ni dhaifu kwa hiyo wanapeta tu.
 
Ni bora chenge apite ili operesheni Sangara iendelee kwa kuwa wapinzania bungeni watakuwa hawana nafasi kwa Chenge.
 
Huo ndio mpango mzima wakuu. Hapo ujue zengwe-bin-fitna dhidi ya Sitta lishapikwa tayari,na hizo ni dalili tu za awali. kwa hali halisi ilivyo,uwezekano wa chama cha makuwadi kumrudisha mzee6 unafifia, maana wana uhakika kuwa sasa hv graph yao ya ufisadi especially kipindi hiki cha uchaguzi imepanda sana, kwahiyo wakimweka 6 as speaker ataruhusu wabunge kuongelea vitendo hivyo na kuhoji sheria ya gharama za uchaguzi ambayo kwa bahati mbaya imevunjwa zaidi na JK NA FAMILIA YAKE, ukiachilia mbali wabunge.
 
Kulikophao mafisadi bora six arudi,najua ni mwanaccm ila msukosuko anaoupata kutoka ccm kwa vyovyote atapata uchungu tu na kuweka maslahi ya taifa mbele.Hivyo atatoa maamuzi kwa matarajio ya wananchi.
 
Watu wengi hawaelewi au wanadharau ukweli kwamba hatuna tatizo la personality ya Spika tu, bali tuna tatizo la institutional structures za bunge letu, kuanzia supermaority ya CCM, mpaka nguvu kubwa sana katika "executive" hususan urais.

Kama hatutafanya institutional changes na kuweka balances zaidi kwa kubadili katiba na kupunguza supermajority ya CCM hata tumuweke Spika kutoka wapi hatutakuwa tumebadilisha kitu.
 
yAAANI inji hiii basi tena kwishneeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee:nono:
 
Watu wengi hawaelewi au wanadharau ukweli kwamba hatuna tatizo la personality ya Spika tu, bali tuna tatizo la institutional structures za bunge letu, kuanzia supermaority ya CCM, mpaka nguvu kubwa sana katika "executive" hususan urais.

Kama hatutafanya institutional changes na kuweka balances zaidi kwa kubadili katiba na kupunguza supermajority ya CCM hata tumuweke Spika kutoka wapi hatutakuwa tumebadilisha kitu.

Nashindwa kuelewa kwanini Watanzania hatuoni mambo ya wazi kama haya. Tunapoteza muda kujadili watu badala ya masuala kwa maana ya mfumo. Samuel Sitta kama JK ni watu wanaoonesha misimamo yao kwa kupima upepo. Leo utawasikia katika vyombo vya habari wakijidai ngangari kesho utawaona wakipambana na wapinga ufisadi. Huu ni mchezo.

Watanzania badala ya kujadili ujumla wa kiwango cha soka letu na mikakati ya kuboresha tunajadili namna ya kushinda mechi na Morocco, na ndiyo mitizamo yetu katika masuala ya kitaifa yalivyo.

Kumbuka Sitta, Chenge, Lipumba, Slaa, Wewe na Mimi hatuna muda mrefu duniani, hivyo kujadili masuala ya matukio yetu hayana maslahi kwa Taifa. Maslahi kwa Taifa ni kujadili muundo na maono (vision) ya utawala, elimu etc katika nchi yetu, hapo sisi pamoja na vizazi vyetu tutapata faida. Si suala la Chenge na Sitta.

Bora hata Chenge kwa kuwa tunaufahamu kwa dhati msimamo wake kuliko Sitta ambaye ni chotara.
 
Nawambieni ukweli tupu, Spika ni chenge ama Makinda. labda kama wakibadili leo mpango wao lakini hizi ndio zimetoka kwao wenyewe. mmoja kati ya hao atakua naibu mwingine spika. na Rostam ndo anasuka mpango mzima na akina Lowassa. wanafanya haya wakijua uongozi ni dhaifu kwa hiyo wanapeta tu.

Namshauri Samweli 6 ccm wakimwaga awarudishie kadi yao, jimbo litakuwa wazi, achukue kadi ya chadema, cdm kitampa ridhaa akiwakilishe kugombea, wanchi wa tabora wataionyesha TZ kuwa tunatakiwa kuichukia ccm kuliko ukoma(wapige kura waliojiandikisha wote na wampigie samweli 6) naamini ndugu zetu wa tabora wanajua TZ ni bora kuliko ccm
watatusaidia kupata mpambanaji kama walivyofanya wananchi wa KARATU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA:israel:
 
MGOMBEA wa uspika wa Bunge, Andrew Chenge, amemshambulia Spika anayemaliza muda wake, Samuel Sitta kuwa ni mtu hatari aliyemwaga sumu kubwa kwa wananchi dhidi ya viongozi wa serikali katika miaka mitano ya uongozi wake bungeni.

Sumu hiyo kwa mujibu wa mgombea huyo, imesababisha majeraha kwa taifa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi na pia imezaa majeruhi wengi akiwamo yeye binafsi.

“Mimi kama walivyo wengine wengi, ni miongoni mwa majeruhi wa uongozi wa namna hiyo (wa Sitta). Kama Bunge, hatuna budi kukabiliana nalo kwa nguvu kubwa,” alisema Chenge katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari aliouitisha Dar es Salaam jana.

Moja ya majeraha hayo kwa CCM kwa mujibu wa Chenge, ni matokeo ya uchaguzi uliomalizika wiki iliyopita.

“Matokeo yake (ya uongozi wa Sitta), ni wananchi ambao siku zote wamekuwa na imani kubwa na viongozi wao, wamelishwa sumu mbaya na hilo limechochea chuki, hasira na kutoaminiana miongoni mwa jamii.”

Chenge, aliyejiita mwarobaini wa majeraha hayo na kuweka wazi kuwa Sitta ‘anatakiwa kuondolewa kwa nguvu kubwa’, mbali na kumshutumu Spika huyo ambaye ameshatangaza nia ya kutetea kiti hicho, pia alielezea uzoefu wake katika uongozi aliosema unatosha kumpa sifa ya kuwa Spika.

“Nimechukua fomu ya kugombea kiti cha uspika nikiamini kwamba, ninao uwezo wa kutibu majeraha makubwa yaliyoliumiza Bunge na Taifa, wananchi na chama changu (CCM),” alisema.

Kwa mujibu wa Chenge, majeraha hayo yamesababishwa na “kiongozi aliye tayari kujitafutia na kujitwalia umaarufu au ushujaa wake binafsi kwa njia ya kuwahujumu, kuwaumiza na kuwachafua wengine kwa kutengeneza tuhuma na kashfa za kila aina.

“Bunge limekuwa na changamoto kubwa katika miaka mitano iliyopita. Viongozi ambao wajibu wetu wa msingi ni kuonesha njia, badala yake tumekuwa vinara wa uzushi, uongo, fitina na majungu,” alisema Chenge.

Tiba ya uongozi wa aina hiyo kwa mujibu wa mgombea huyo, ni kuchagua kiongozi bora wa Bunge na njia bora ni kupata kiongozi mbadala mwenye uwezo na nia njema.

Sitta alipotafutwa kwa njia ya simu, ilipokelewa na mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mlinzi wake na kusema kuwa anafahamu kinachotafutwa ni kuhusu Chenge lakini Sitta hatajiingiza katika malumbano hayo.

“Mzee hatuwezi kumruhusu ajibu, tumemzuia asijibu, hawezi kuingia katika malumbano,” alisema mlinzi huyo na kuendelea, “watu wanaona, subirini wakati wa kampeni.”

Chenge alisema Sitta aliendesha mijadala kwa kuwafanya wabunge wa chama tawala na wa Kambi ya Upinzani upande mmoja na serikali upande mwingine.

“Mimi nikiwa spika siwezi kuruhusu kitu kama hicho.” Alifafanua kwamba demokrasia ya kibunge, inataka wabunge wa chama tawala na serikali wawe upande mmoja na kambi ya upinzani upande mwingine na kusisitiza kuwa, pamoja na kuwa majeruhi wa uongozi wa Sitta, hatalipiza kisasi katika uongozi wake.

Kwa mujibu wa Chenge, wabunge wa chama tawala wanaruhusiwa kuzungumza lolote kuhusu utendaji wa serikali katika kamati yao ya chama na wakiingia bungeni, wanapaswa kuikosoa Serikali kwa lengo la kuboresha utendaji wake kwa staha.

Kuhusu kambi ya upinzani, alisema yenyewe ndiyo inayopaswa kuikosoa serikali ikibidi iiondoe madarakani kwa kuwa hilo ndilo lengo lao kuu.

Mbali na kuwageuza wabunge wa chama tawala na kambi ya upinzani dhidi ya serikali, Chenge alisema pia Sitta hakutekeleza wajibu wake kama mwamuzi (referee) kwa kuzingatia sheria na kanuni, badala yake aligeuka shabiki na aligeuza Bunge sehemu ya kutoa maoni yake binafsi.

Alipoulizwa kama ametumwa kugombea uspika, Chenge alihoji mbona alipokwenda kugombea ubunge Bariadi Mashariki, hakuna mtu aliyehoji nani aliyemtuma?

Alisisitiza kuwa uzoefu wake kama Mwanasheria Mkuu wakati wa uongozi wa awamu ya pili na ya tatu ndio kilichomsukuma.

Waandishi walipotaka awataje majeruhi wengine na kuhoji kama ni mkakati wake na wa majeruhi hao wa kuingia katika siasa za kusaka uongozi kwa mwaka 2015, Chenge alisema kila mtu aliyekuwa akifuatilia mambo ya Bunge, anafahamu majeraha na majeruhi wengine. Hata hivyo hakutaka kufafanua kuhusu kampeni za 2015.

Alipoulizwa kama aliwahi kufanya jitihada zozote kunusuru hali hiyo akiwa kama Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya chama hicho, alisema chama chake kimefanya kazi kubwa katika hilo, ikiwemo kuundwa kwa Kamati ya Mzee Mwinyi.
 
Yani huyu mzee wa vijisent hafai hata kidogo. Inamaana yeye anaenda bungeni kutetea tena ufisadi? Nilifikiri atakuwa amejifunza kumbe hakuna kitu kabisa. Sijui kwa nini wanachi wa barihadi wamemrudisha tena huyu jamaa
 
pfff!!!!!!!!!!!!!!!!! hata sijamaliza kuisoma .....anatetea mafisadi liveeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!! hatufiki ..ok ngoja niimalizie
 
ccms' true color starts revealing.....
 
  • Mgaya na wanachama wote wa TUCTA

  • Vyama mbadala vyote vya kisisiasa

  • Makonda ,Wapiga debe ,madereva
  • Na hata wale madada wauza "utamu"
  • NGO
  • I mean wananchi wote

Chenge akiwa Spika tunaomba wenye uwezo waorganise migomo na maandamano. Tunapoeleka People's power inahitajika. Wabunge wa upinzani sauti yao bado ni ndogo.

Chenge hajashiinda uspika lakini kitendo cha yeye kugombea ubunge na sasa kuchukua fomu ya spika ni tusi kwa watanganyika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom