Eti mabadiliko ni machafuko?

Voice of Wisdom

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
537
240
Sitaki kuzungumza kishabiki na ni vyema kujadili bila hisia za chama.
Mara kadhaa tumemsikia mgombea wa chama chenye sirikali akisema kuwa tukifanya mabadiliko tutakuwa kama libya na Misri.
Misri na Libya walifanya mabadiliko kwa kutumia silaha sisi tunafanya mabadiliko kwa kutumia bullet box.
Siku zote chama cha sirikali kimekuwa kikishindaa na Amani inakuwepo.
Kama amani inatoweka kwa sababu chama cha sirikali kimeshindwa nani atahusika kuleta machafuko???

Kwa tafsiri yangu mimi juha nahisi chama cha sirikali kikishindwa ndicho kitakacholeta machafuko.

Ni hatari sana kufananisha mabadiliko ya bullet box na mabadiliko ya silaha za kivita/bunduki. Ujuha wetu usiwe sababu ya kutuaminisha kuwa tukichagua upande wa pili amani itatoweka vinginevyo mmejipanga kuleta machafuko mkishindwa.
Ni hayo tu kwa leo.
 
Back
Top Bottom