Eti kadi feki za CCM!

Kyachakiche

JF-Expert Member
Feb 16, 2009
983
207
Kumekuwa na taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari kuwa kuna Wanaccm wanaotaka kupata nafasi za uongozi hususani ubunge katika uchaguzi ujao kusambaza kadi feki za chama hicho miongoni mwa wapiga kura.

Imeripotiwa kwenye gazeti la Majira la tarehe 22.09.09 na la leo tarehe 29.09.09 kwenye maoni ya mhariri kuwa huko katika jimbo la Moshi (V) kumesambazwa kadi nyingi feki na mmoja wa anayedaiwa kuutaka ubunge wa eneo hilo. Maeneo mengine kama Shinyanga pia yameripotiwa kuwa na maelfu ya kadi zinazodaiwa kuwa feki za CCM.

Hii ina maanisha nini? Ni kwamba hawa wanaozisambaza wameamua kununua mashine za kuchapa ama kudurufu, au mfumo mzima wa uchapaji na usambazaji hausimamiwi ipasavyo na wakuu wahusika, au kuna baraka kutoka juu?

Kama kila mtu anaweza kuchapa na kusambaza kadi za chama anaweza kufanya hivyo, kwa nini asiweze pia kuchapa na kusambaza vitambulisho vya wapiga kura na hata shahada za kupigia kura?
 
hilo swala linawezekana kabisa kwa hawa viongozi wetu

Kuna jamaa mmoja hapa nilipo kaenda kununua kadi za wapiga kura sehemu fulani na kuwakatia elfu kumi tu kila mmoja pesa za kitanzania ili shahada zao zikatumike sehemu na aweze kupita katika hizi chaguzi zinazoendelea sasa

Huyu mheshimiwa huyo!
 
mimi bado sijaelewa naomba kuelimishwa:

kama wanaogawa hizo kadi feki ni ccm, kwanini wagawe kadi feki? kwa nini badala ya kuingia gharama ya kuchapicha kadi feki wasingechapisha tu za kawaida?

kama wanaozigawa hizo kadi feki ni upinzani, inawapa faida gani?
 
hilo swala linawezekana kabisa kwa hawa viongozi wetu

Kuna jamaa mmoja hapa nilipo kaenda kununua kadi za wapiga kura sehemu fulani na kuwakatia elfu kumi tu kila mmoja pesa za kitanzania ili shahada zao zikatumike sehemu na aweze kupita katika hizi chaguzi zinazoendelea sasa

Huyu mheshimiwa huyo!
Kwa maneno mengine ni maandalizi ya kusambaza shahada feki za kupigia kura?
 
mimi bado sijaelewa naomba kuelimishwa:

kama wanaogawa hizo kadi feki ni ccm, kwanini wagawe kadi feki? kwa nini badala ya kuingia gharama ya kuchapicha kadi feki wasingechapisha tu za kawaida?

kama wanaozigawa hizo kadi feki ni upinzani, inawapa faida gani?
Hapo mkuu ndiko tunakopenda wenye mawazo zaidi kuhusiana na hili wayatoe.
 
Mimi mwenyewe nilipewa kadi kadhaa za sisiem na mwanachama mmoja mtaani kwetu ili niwape ndugu na marafiki, wamuwezeshe aweze kupita kwenye kura za maoni ndani ya chama kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
 
Mimi mwenyewe nilipewa kadi kadhaa za sisiem na mwanachama mmoja mtaani kwetu ili niwape ndugu na marafiki, wamuwezeshe aweze kupita kwenye kura za maoni ndani ya chama kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Ndugu yangu Katavi,
Utajuaje kwamba hii ni kadi feki na ile ni halali. Kwani huwa zinasainiwa na nani? Au saini nazo huwa wanazighushi!
 
Kumekuwa na taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari kuwa kuna Wanaccm wanaotaka kupata nafasi za uongozi hususani ubunge katika uchaguzi ujao kusambaza kadi feki za chama hicho miongoni mwa wapiga kura.

Imeripotiwa kwenye gazeti la Majira la tarehe 22.09.09 na la leo tarehe 29.09.09 kwenye maoni ya mhariri kuwa huko katika jimbo la Moshi (V) kumesambazwa kadi nyingi feki na mmoja wa anayedaiwa kuutaka ubunge wa eneo hilo. Maeneo mengine kama Shinyanga pia yameripotiwa kuwa na maelfu ya kadi zinazodaiwa kuwa feki za CCM.

Hii ina maanisha nini? Ni kwamba hawa wanaozisambaza wameamua kununua mashine za kuchapa ama kudurufu, au mfumo mzima wa uchapaji na usambazaji hausimamiwi ipasavyo na wakuu wahusika, au kuna baraka kutoka juu?

Kama kila mtu anaweza kuchapa na kusambaza kadi za chama anaweza kufanya hivyo, kwa nini asiweze pia kuchapa na kusambaza vitambulisho vya wapiga kura na hata shahada za kupigia kura?

Sielewi unashangaa nini hapa. hivi kelele zote ambazo huwa zinapigwa kwamba kura zinaibwa huwaga huzisikii wewe? kusambaza kadi feki si jambo gumu, hata wewe unaweza kwenda kwenye chama chako na kuwaambia viongozi wako kwamba umewahamasisha wananchi wajiunge na chama hicho, hivyo unaomba kadi 100 ukawagawie. nani asiyependa kuwa na wanachama wengi? watakupa tu. so ndugu yangu usishangae.
 
hawa ni kawaida yao kuiba kura ni afadhali kama hilo linatendeka ndani ya chama chao wenyewe.maana ukiwaambia wanaiba kura wanakuwaga wakali ,kiko wapi sasa
 
Sielewi unashangaa nini hapa. hivi kelele zote ambazo huwa zinapigwa kwamba kura zinaibwa huwaga huzisikii wewe? kusambaza kadi feki si jambo gumu, hata wewe unaweza kwenda kwenye chama chako na kuwaambia viongozi wako kwamba umewahamasisha wananchi wajiunge na chama hicho, hivyo unaomba kadi 100 ukawagawie. nani asiyependa kuwa na wanachama wengi? watakupa tu. so ndugu yangu usishangae.
Swala hapa si kushangaa bali ni kutwa kadi feki. Wewe kwa mfano wako ulioutoa wa kuomba kwenye chama chako kadi kama 100 kwa ajili ya kuwahamasisha watu wajiunge, je, utapewa kadi feki za kwenda kugawa? Na kama maana ni hiyo, kwanini uongozi wa chama Wilaya utoe tamko la kulaani kitendo hicho hadi kutishia kuwavua uanachama wale wote waliohusika!
 
"Shahada za kura 2010 kuchapishwa nchini "
Josh Michael
user_offline.gif
Today, 12:32 PM
"Na Sadick Mtulya


SERIKALI imetangaza rasmi kuwa kuanzia uchaguzi mkuu ujao wa Oktoba, 2010 itaanza kuchapisha nyaraka na karatasi za kura nchini kwa ajili ya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kupatikana kwa mitambo mipya na ya kisasa yenye uwezo wa kuweka alama za siri, namba na rangi katika karatasi za kura kwa usalama mkubwa.

Kazi hiyo itatekelezwa kupitia Idara ya Mpiga Chapa Mkuu ambayo iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Ununuaji wa mitambo hiyo ni mpango wa serikali wa kutaka kuimarisha idara hiyo tangu mwaka jana, ambapo serikali ilitoa zaidi ya Sh 1.7 bilioni na mwaka huu imetenga zaidi ya Sh 1 bilioni, ili kutekeleza mpango huo.

Pia ilielezwa kwamba mpango huo unalenga kuondoa utegemezi wa kuchapisha karatasi hizo nje ya nchi .

"Kwa sasa tayari umepatikana mtambo ambao utakuwa na uwezo wa kuweka alama za siri, namba na rangi katika karatasi za kura kwa usalama mkubwa. Na wakati huo huo upo uwezekano wa kuhakiki alama za siri zitakazowekwa," alisema Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera na Mipango) Philip Marmo.

Marmo aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kukagua mitambo ya zamani pamoja na huo mpya katika Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali.

Waziri huyo alifafanua kuwa mpango huo unaendelea kufanywa kwa ushirikiano wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(Nec).

Marmo alisema kutokana na hatua hiyo, serikali itakuwa imeondoa matatizo yaliyojitokeza katika chaguzi za miaka ya nyuma yakiwemo ya kukosewa kwa majina ya baadhi ya watu na kuilazimu serikali kutumia fedha nyingi kufanya marekebisho madogo.

"Pia itasaidia sana katika udhibiti wa siri za nyaraka hizo katika mikondo mingi na kuokoa pato la taifa, hivyo utaona zipo faida nyingi sana kwa uwekezaji huu unaofanywa na serikali," alisema Marmo.

Waziri huyo alisema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kuiboresha Idara ya Mchapaji Mkuu wa Serikali, ili iweze kuendesha shughuli na udhibiti wa nyaraka za siri kiujumla.

Alisema kwa kuanzia idara hiyo imeboreshewa kwa kupatiwa mgawo maalum wa bajeti ya maendeleo na kwa kila mwaka watakuwa wakipata mtambo mmoja au zaidi na kwamba, hivi sasa mitambo mipya saba iko bandarini na mingine inapakiwa kuja nchini.

"Serikali tumeanza mkakati huo na ndio maana hivi sasa tayari tumekwisha leta mtambo mmoja na mingine saba ipo bandarini na mingine inapakiwa huko kwa watengenezaji nchini Ujerumani.

"Hivyo serikali ina matumaini kuwa kabla ya bajeti ijayo, idara hii itakuwa na mabadiliko makubwa kabisa ambayo yanaweza pengine kuhitajika kwa zoezi la kupunguza watendaji wa baadhi ya sehemu za mifumo ya zamani isiyohitajika," alisema.

Waziri huyo pia alizungumzia mikakati ya kuimarisha idara hiyo kwamba ni pamoja na kujenga ofisi mpya na makao makuu mapya mjini Dodoma na mchakato umekwishaanza huku ukiambatana na hatua ya kumpata mtaalamu wa masuala ya uanzishaji wa kiwanda cha uchapishaji nyaraka za kawaida na siri.

"Hata hivyo katika makao hayo mapya, kutakuwepo pia chuo cha uchapishaji, karakana ya marekebisho ya mitambo yetu na pia viwanja vya kumbukumbu ya uchapishaji wa kale na asili vikiwa ni vivutio kwa wageni na pia sehemu ya mapumziko," alisema

Pia serikali imeanzisha mpango maalum wa kupata wataalamu zaidi na waliobobea katika fani ya uchapishaji ikiwemo kuendelea na ajira ya watumishi watakaomudu uendeshaji wa mitambo ya kisasa na uendeshaji wa vifaa vya elektroniki.

Katika hatua nyingine, jana hiyo, Marmo aliagiza Wizara, Idara za serikali, taasisi zake pamoja na watendaji wote katika Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuanzia sasa kuhakikisha nyaraka zote zinachapwa kwenye idara hiyo.

Sambamba na agizo hilo, alizitaka Wizara, na Idara ya halmashauri zote nchini kurejesha nyaraka zote za serikali pamoja na nyenzo zake kama mihuri kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, ili ziandikwe kwenye daftari maalumu.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya serikali kwa sasa kutaka kuhakikisha kuwa inakuwa na taarifa ya nyaraka zake zinazochapishwa kwa Mpigachapa Mkuu wa Serikali na pia nyaraka zake zote zitakazokuwa na ulazima wa kuchapishwa nje ya idara hiyo, ziandikwe kwenye daftari maalumu la mzunguko wa nyaraka za serikali.

"Mtindo huu wa kufanyia usaili na kuwekwa kwenye rekodi za nyaraka za serikali unatumika pia na nchi zilizoendelea na zenye mafanikio makubwa ya kiuchumi na kiulinzi, hivyo ninamuagiza Mpigachapa Mkuu wa Serikali kufungua regista hiyo kama hakuwanayo," alisema Marmo.

Akizungumzia utendaji kazi katika idara hiyo, Marmo aliwataka wafanyakazi hao kufuata maadili ya kazi na kwamba, wafanyakazi waache mifarakano, wizi wa nyaraka ili kuimarisha utendaji kazi.

Alisema serikali haitawavumilia watumishi wanaochafua utulivu maeneo ya kazi.
Awali, Mpiga Chapa Mkuu, Casian Chibogoyo alimshukuru waziri kwa kufika na kuahidi kuwachukulia hatua mara moja wafanyakazi watakaojaribu kuiba nyaraka na kusababisha mifarakano kazini."

ZILICHAPISHWA NJE YA NCHI, WAKAZIIBA; JE KAMA WANAZICHAPISHA WENYEWE SI NDIYO BALAA? TUTARAJIE YA AFGHANISTAN AMBAKO IDADI YA KURA ZILIZOPIGWA IMEZIDI IDADI YA WAKAZI.! TZ NADHANI ITAKUWA MARA MBILI YA AFGHANISTAN
 
Watu wanapata vyeti feki vya PhD, madawa feki na karibu kila kitu kwenye nchi yetu leo hii ukitaka unaweza kupata feki version...sembuse kadi za CCM..!!!
 
Ni nini maana ya kadi feki? Kama ccm wanatoa kadi bure, kwa nini mtu achape kadi feki kwa pesa? Ili kadi iwe feki ndio tuambiwe ina vigezo gani. Sina sababu ya kupokea kadi feki ilhali ya halali nikiitaka leo tu napata tena bureeeeee!

Leka gwe.
 
Ni nini maana ya kadi feki? Kama ccm wanatoa kadi bure, kwa nini mtu achape kadi feki kwa pesa? Ili kadi iwe feki ndio tuambiwe ina vigezo gani. Sina sababu ya kupokea kadi feki ilhali ya halali nikiitaka leo tu napata tena bureeeeee!

Leka gwe.
Haya ndiyo yakujadili Leka. Ni kwanini ziitwe kadi feki? Je, zina mfumo tofauti katika usambazwaji wake au ni za kughushi kama ambavyo vyeti mbalimbali hughushiwa?
 
Thousands of fake CCM cards printed




AN elaborate 'internal' plot to remove from leadership corruption-free Chama Cha Mapinduzi (CCM) members and replace them with those who embrace the vice is said to have been uncovered as the ruling party braces for next year's presidential and parliamentary elections.

According to reports reaching THISDAY from reliable sources within CCM and also in various state organs, some leading ruling party cadres are believed to have launched an underground scheme where fake CCM membership cards are being printed in the thousands and 'strategically' distributed in regions like Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mbeya and the 'Lake Zone'.

The aim is to facilitate the ouster of all CCM legislators and councilors seen to be riding the anti-corruption bandwagon, and pave the way for the 'greedier' (fisadi) elements to replace them and entrench themselves around the country, the sources say.

CCM membership cards are supposed to be sold to aspiring members, even at negligible prices. But sources say the fake cards are being given away for free, and the recipients instructed not to vote for certain candidates for parliamentary and local council seats.

State organs are understood to have been informed about this development and an undercover investigation is now underway in Kilimanjaro and Dar es Salaam regions, where the first fake CCM cards were discovered.

According to our sources, preliminary findings strongly suggest that the individuals behind the clandestine printing operation are amongst the richer CCM members.

They are believed to be taking advantage of loopholes in the internal CCM 'opinion polls' process of selecting its contestants for parliamentary and councilorship positions.

Under the process, initiated by President Jakaya Kikwete in his capacity as party chairman, all CCM members are supposed to be given the chance of equal involvement at the nominations stage.

It is however, understood that only genuine CCM members will be allowed to vote in the primaries. Genuine members will be determined through a verification process to be done before June next year. Details of this process are not yet known.

Sought out for comment, CCM's ideology and publicity secretary John Chiligati acknowledged that there was some truth in the reports of fake party cards having been printed, but said the only area where this had been concretely confirmed was Moshi Rural District in Kilimanjaro Region.

The district has two parliamentary constituencies: Vunjo and Moshi Rural itself. Both incumbent legislators are CCM members; Cyril Chami (Moshi Rural), who is currently Deputy Minister for Industries and Trade, and Aloyce Kimaro (Vunjo), recognized as one of the party's more outspoken anti-corruption campaigners.

Chiligati said the fake CCM cards were found at the following locations in Moshi Rural: Kimochi, Okaoni, Uru Kaskazini and Longuo.

CCM secretary general Yusuf Makamba said when contacted for comment that he was on leave. But according to his deputy, George Mkuchika, the problem of fake membership cards being distributed around the country has been presented to relevant local government authorities for investigation, and a findings report will be released �at the conclusion of an in depth search for the truth.�

It is understood that the Moshi Rural CCM district chairman, Gabriel Masenga, is leading the probe and has vowed to take stern action against culprits who will be found, including stripping them of their own CCM membership, and written warnings sent to all party branches in the district about the presence of the fake membership cards.

But according to our sources, the fake cards are believed to have already been used in the recently-held primaries for local government leaders in the district.

According to Chiligati, legitimate party cards are henceforth to be dispatched to new members straight from CCM headquarters in Dar es Salaam, via regional party secretaries who will hand out the cards according to lists prepared by district party secretaries.

He said special member registers are currently being printed by the Government Printer, which will be used to register genuine party members to vote in next year's primaries.

Every voter will only vote at the location where his or her name is listed in the special register, and nowhere else, Chiligati further explained.

The CCM primaries are scheduled to take place before August next year, to nominate CCM contestants for councilorship and parliamentary seats in the general election a couple of months later.

Source: http://www.thisday.co.tz/News/6339.html



CCM yawashtukia 'wajanja', yatoa masharti
Imeandikwa na Gloria Tesha; Tarehe: 21st September 2009
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka masharti ya watu kujiunga na chama hicho kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao ili kuwaepuka watu watakaojiunga na chama hicho kwa lengo la kuwapitisha watu wao wakati wa kura za maoni.

Chama hicho kimesema, masharti hayo yanawahusu wagombea wa udiwani na ubunge.

Kutokana na mfumo mpya wa kupiga kura za maoni, chama kimepata wasiwasi kwamba kuna watu watafanya ujanja na kuzua tafrani wakati wa kura za maoni mwakani.

Miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na kutoingizwa mwanachama mpya yeyote kuanzia Juni 30 mwakani na pia kuandikisha majina ya wanachama wote katika rejesta kupitia matawi kuanzia mwezi huu au ujao hadi mwakani (Juni) ili kuepuka watu kuingia kiholela.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, CCM, John Chiligati amesema, uamuzi huo ulipitishwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM hivi karibuni na kwamba hiyo itasaidia kudhibiti wanachama watakaoingia kwa lengo baya.

Chiligati amesema leo kuwa, uamuzi huo wa NEC ulianza kuzungumzwa tangu kikao cha mwaka jana Butiama mkoani Mara na umepitishwa ili kupunguza vurugu za kuharibu haki katika kura za maoni ambazo zingetokea kama utaratibu huo usingepitishwa.

Chiligati amesema, katika mchakato wa kampeni na uchaguzi unaoendelea wa Serikali za Mitaa, mambo hayo hayajaonekana kwa kuwa wapiga kura wanawafahamu wagombea hivyo si rahisi ujanja kufanyika kama ilivyo katika nafasi za ubunge na udiwani.

"Kwenye vitongoji na vijiji hakuna shamrashamra kama kwenye udiwani na ubunge, mshikemshike upo huko juu bwana, huko watu wanacheza ‘rafu', na ujanja ujanja ni mwingi mno hasa kutokana na utaratibu huu mpya, ndiyo hasa lengo," alisema Chiligati.

Alipoulizwa udhibiti huo utawezekana vipi hasa ikizingatiwa kuwa kuanzia sasa hadi Juni mtu yeyote anaruhusiwa, Chiligati amesema, kadi kwa ajili ya wanachama wapya zitachukuliwa makao makuu ya chama.

Amesema, makati wa CCM wa mikoa watakabidhiwa idadi ya wanachama wapya na Katibu wa Wilaya kutoka kwa Katibu wa Tawi.

"Kwa sasa mtu yeyote atakayetimiza utaratibu wote wa kuomba uanachama katika chama ambaye amechunguzwa kwa utaratibu wa kawaida na kuridhika na tabia yake, atapokewa katika kipindi hiki hadi Juni, ukifika muda huo,

hakuna mwanachama mpya atakayeingia katika chama na kadi za wanachama zinachukuliwa makao makuu na Katibu wa Mkoa tu," amesema Chiligati.

Amesema, utaratibu wa kupokea wanachama wapya utaendelea tena Agosti mwakani baada ya kura za maoni ili mambo yafanyike kwa haki na kwamba katibu wa ngazi hizo mbili (mkoa na wilaya), atakayebainika kufanya hujuma, atafukuzwa kazi au kupewa adhabu kali.

Kuhusu rejesta, amesema hivi sa,sa zinaandaliwa kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, mwanachama ataandikishwa katika tawi lake anakoishi na ambako mwakani atapiga kura katika tawi hilo hilo na si vinginevyo.

Kura hizo za maoni zitapigwa mwakani kabla ya Agosti na kwa mujibu wa utaratibu huo mpya wa CCM, kila mwanachama katika tawi lake ataruhusiwa kupiga kura hizo kumchagua mtu atakayesimama kuwania udiwani na ubunge kupitia chama hicho.

Kabla ya utaratibu huo, wajumbe wachache wa chama ndio waliohusika kupiga kura za maoni jambo lililojadiliwa katika vikao vya NEC kwamba linawanyima wanachama demokrasia na wakati mwingine inachangia kupitishwa mtu ambaye hakubaliki katika jamii.


http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3679
 
UCHAGUZI 2010

Mafisadi waibuka
na mkakati mpya

*Wachapisha kadi bandia kuwang'oa wapambanaji
*CCM yawashitukia, makachero nao waingia kazini

MWANDISHI WETU
Dar es Salaam

WATUHUMIWA wa ufisadi pamoja na kuzidi kubanwa kila kona, bado wanaendelea na mikakati yao ya kimajitaka safari hii, wakitumia mbinu ya kuingiza watu wao katika nafasi za ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na sasa wamebainika kuchapisha kadi bandia za CCM kutimiza azma hiyo.

Tayari vyombo vya dola vimekwishajulishwa na vimeanza kuzifanyia kazi taarifa hizo baada ya kukamatwa kwa kadi kadhaa katika mikoa ya Dar es Salaam na Kilimanjaro.

Habari za ndani ya vyombo vya dola zimethibitisha kubainika kwa mkakati huo wa kihalifu ambao ulianza kutumika katika baadhi ya maeneo ya nchi, washiriki wakielezwa kuwa na nguvu kubwa ya kiuchumi.

Ofisa mmoja mwandamizi wa serikali ameliambia KULIKONI kwamba kumekuwa na mshituko ndani ya vyombo vya usalama kutokana na uhalifu huo kuwa na nia ya kuvuruga mfumo mzima wa uongozi wa nchi.

Siku za mwanzo za uongozi wa Rais Jakaya Kikwete katika serikali yake na ndani ya CCM, alionyesha waziwazi kukerwa na utaratibu ambao unatoa mwanya wa rushwa na alianzisha mchakato wa kukabiliana na hali hiyo.

Dhamira hiyo njema ya Kikwete ilikisukuma chama hicho kubadili mfumo wake wa upigaji kura za maoni pamoja na udhibiti wa kadi za wanachama wapya wanaojiunga nacho kuepusha kuingizwa kwa ‘mapandikizi' yatakayovuruga, ukiwa unafanyiwa kazi, mafisadi wameiasi azma hiyo.

Maofisa Usalama wa Taifa wameelezwa kuingia kazini sasa baada ya kubainika kuwapo kwa kundi kubwa la wahalifu lililoanza kusambaza kadi bandia kwa nia ya kupandikiza wanachama wengi watakaoshiriki upigaji kura za maoni za udiwani na ubunge kwa matakwa ya wanaozichapisha kadi hizo ambao wana historia ya ufisadi na hata uhalifu mkubwa wakiwamo majambazi.

Kwa mujibu wa mwenendo wa kisiasa nchini, huenda mkakati huo ulilenga kuwang'oa wabunge na madiwani wa CCM ambao ni kikwazo kwa mafisadi kutokana na msimamo wao mkali wa kusimamia maslahi ya Taifa kwa kupinga rushwa na ufisadi.

Tayari wanamkakati hao walionekana kutaka kufaidika na utaratibu mpya kwa wanachama wote wa CCM wenye kadi halali ndio walioruhusiwa kupiga kura za maoni katika maeneo yao badala ya utaratibu wa zamani ambao kura hizo zilipigwa na viongozi wachache katika kata.

Uongozi wa juu wa CCM akiwamo Katibu wa Itikadi na Uenezi, CCM, John Chiligati, umethibitisha kupokea taarifa za kuwapo kwa kadi bandia katika baadhi ya maeneo lakini wamesema eneo ambalo kuna ushahidi ni wilaya ya Moshi Vijijini yenye majimbo mawili la Moshi Vijijini na Vunjo.

Majimbo hayo sasa yanaongozwa na Cyril Chami, ambaye ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko na Aloyce Kimaro, ambaye amekuwa mwiba kwa watuhumiwa wa ufisadi na wote sasa wanaandaliwa mikakati ya kung'olewa kwa gharama yoyote.

Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba alisema kwa sasa yuko likizo na kazi zake zinafanywa na Naibu wake, George Mkuchika, ambaye kwa upande wake alidai hakuwa na taarifa rasmi kuhusiana na kuwapo kwa kadi bandia zinazosambazwa bila kufuata taratibu mpya za chama hicho tawala.

Mkuchika alionekana kutofahamu yanayoendelea katika chama kwani Chiligati yeye si tu alikiri bali alionekana kufahamu hata hatua zilizokwishachukuliwa kwa kusema tayari suala hilo limeripotiwa na linafanyiwa kazi na viongozi wa wilaya husika na majibu yatatolewa wakati wowote baada ya uchunguzi wa kina kukamilika.

Wilayani Moshi Vijijini, imebainika kwamba kadi hizo zimekamatwa katika maeneo ya Kimochi, Okaoni, Uru Kaskazini na Longuo na uongozi wa CCM wilayani humo wamekwishachukua hatua ya kufuatilia suala hilo.

Mbali ya kuchukua hatua kuhusiana na usambazaji wa kadi bandia, uongozi wa wilaya hiyo umetoa karipio kali kwa baadhi ya watu walioanza kufanya mikakati ya kuwavuruga wabunge wa sasa kwa nia ya kuwazuia kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho ya 2005.

Hatua ambazo zimeelezwa kuchukuliwa na kamati ya siasa Wilaya chini ya Mwenyekiti wa CCM Moshi Vijijini Gabriel Masenga ni pamoja na kuagiza uchunguzi ufanyike na wote watakaobainika wachukuliwe hatua kali ikiwemo kuvuliwa uanachama.

Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Cosmas Kasangani pia ameamriwa kuandika barua kutahadharisha kata zote kuhusu ukiukwaji huo wa taratibu na usambazwaji wa kadi bandia pamoja na kuwakemea wanachama waliotajwa kuhusika na matukio hayo.

Mbali ya uchaguzi mkuu wa mwakani, imebainika kwamba kadi hizo baadhi zimetumika katika mchakato wa kuwapata wagombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Kilimanjaro, kadi hizo bandia zimeelezwa kusambazwa katika mikoa ya kanda ya ziwa na Nyanda za Juu Kusini, kwa lengo la kuwang'oa wabunge wanaoonekana kuwa mwiba kwa mafisadi na wahalifu wengine.

Baada ya mchakato wa muda mrefu ulioanzishwa na Rais Kikwete na watendaji wake, Halmashauri Kuu ya Chama hicho (NEC) iliweka masharti ya watu kujiunga na chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu ujao ili kuwaepuka watu watakaojiunga na chama hicho kwa lengo la kuwapitisha watu wao wakati wa kura za maoni.


Miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na kutoingizwa mwanachama mpya yeyote kuanzia Juni 30 mwakani na pia kuandikisha majina ya wanachama wote katika rejesta kupitia matawi kuanzia mwezi huu au ujao hadi mwakani (Juni) ili kuepuka watu kuingia kiholela.

Imeelezwa kwamba uamuzi huo wa NEC ulianza kuzungumzwa tangu kikao cha mwaka jana Butiama mkoani Mara na umepitishwa ili kupunguza vurugu za kuharibu haki katika kura za maoni ambazo zingetokea kama utaratibu huo usingepitishwa.

Hata hivyo taarifa rasmi ya CCM iliyotolewa na Chiligati ilikanusha kuwapo kwa kadi bandia katika mchakato wa kampeni na uchaguzi unaoendelea wa Serikali za Mitaa.


Kuhusu uwezekano wa watu kutumia mwanya huo kujiandikisha kabla ya Juni, Chiligati alisema kadi kwa ajili ya wanachama wapya zitachukuliwa makao makuu ya chama na kwamba makatibu wa CCM wa mikoa watakabidhiwa idadi ya wanachama wapya na Katibu wa Wilaya kutoka kwa Katibu wa Tawi kwa utaratibu maalumu utakaowekwa.


Chiligati alinukuliwa akisema kwamba utaratibu wa kupokea wanachama wapya utaendelea tena Agosti mwakani baada ya kura za maoni ili mambo yafanyike kwa haki na kwamba katibu wa ngazi hizo mbili (mkoa na wilaya), atakayebainika kufanya hujuma, atafukuzwa kazi au kupewa adhabu kali.

Alisema kwa sasa rejesta zinaandaliwa kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali na kila mwanachama ataandikishwa katika tawi lake anakoishi na ambako mwakani atapiga kura katika tawi hilo hilo na si vinginevyo.

Kura hizo za maoni zitapigwa mwakani kabla ya Agosti na kwa mujibu wa utaratibu huo mpya wa CCM, kila mwanachama katika tawi lake ataruhusiwa kupiga kura hizo kumchagua mtu atakayesimama kuwania udiwani na ubunge kupitia chama hicho.

Kabla ya utaratibu huo, ni wajumbe wachache wa chama ndio waliohusika kupiga kura za maoni jambo lililojadiliwa katika vikao vya NEC kwamba linawanyima wanachama demokrasia na wakati mwingine inachangia kupitishwa mtu ambaye hakubaliki katika jamii.


Chanzo:KULIKONI Namba 758, Ijumaa, Septemba 25, 2009 __________________
 
Back
Top Bottom