Eti inawezekana?...UVUMILIVU MPAKA LINI?

Nisipokiapa itakua kwa sababu nyingine sio hiyo! Kiapo ntakiweza kama mwenzangu ataniwezesha!Ndoa sio ya mmoja kwahiyo inabidi anisaidie mimi kumsaidia yeye!

Orayt

Tuchukulie kesi kama hii....

Mmeo kakuwezesha, amekusaidia, hajawahi kukuboa...yaani yote njema.

lakini ghafla lahaula...kapata mzinga yuko kitandani. Baioloji haitaamka mpaka anaingia kaburini. Na wewe una kiu yako. Utavumilia mpaka mwisho au uchakachuzi utafanyika japo kwa siri?
 
Kifo ni pale ambapo pumzi inagoma kutoka na kuingia
Moyo unagoma kufanya kazi
Baioloji inasizi kuibuka
Watu wanaweka matuirubai
Watu wanakula ubwabwa
Walevi wanachimba shimo la kukufukia
Kina mama wanaachia vilio, japo vingine vya kizushi
Na kazalika na kazalika

Kungekuwa na definishen 'nzuri' ya neno kifo (kwa ndoa).....labda iwe hivi...:
Kifo ni pale mmoja wa wanandoa anapokua katika hali ya kushindwa moja kwa moja utekelezaji wa majukumu ya kindoa, ilhali upande wa pili ukiwa mahitaji hayo.....
 
Kumbe ukweli ni kuwa kina baba wanafanya hadharani na kina mama mnafanya kwa siri?

Kwa hiyo KUFANYA kuko palepale?
Kusema wanawake hawafanyi ntakua muongo!Na wapo ambao wanabadili mapatna kama hawana akili nzuri...na watu wote wa karibu wanajua isipokua waume zao tu!Hii nimeona mwenyewe...ila mwisho wa siku ishu nzima inategemea na kutofautiana kati ya mtu na mtu!Kuna wengine wakichoka kabisa badala ya kwenda kuspaic mambo nje alafu arudi ataaga aondoke kabisa!
 
Babu acha ubaguzi wa kijinsia hapa jamvini, story yako imewalenga mke wa mtu kachakachuliwa na mume wa mtu, wote walikula viapo hawa, so suala la kuvunja viaapo ni la mtu binafsi na si jinsia, na kusema mpaka kifo kikutenganishe kwa hali hiyoo kifo c mpaka ufukiwe , kama umepalalaizi haf body wewe ni mfu ulie hai, ila suala la ubinadamu ndio linahitajika hapa, huwezi kumuacha mkeo au mumeo kalakala wewe unakula uroda, da cjui imekaaje, na huyo bwana X asijifanye eti kategwa huyo kaumindi mzitgo longi time kitambo sema ndio vile...............

Mkuu siyo ubaguzi....

Ila kuna dhana kuwa asilimia kubwa ya wnaume si waaminifu hata kama wake zao wapo na hawana matatizo....Ila wanawake siku zote wanaonekana ni wavumilivu (Hapa jamvini hakuna anayekubali hii kitu kuwa WANATOKA NJE YA NDOA ZAO)...Sasa ndio nlitaka kujua inapotokea hali kama hii watavumilia mpaka lini?

Kuparalaiz si kufa ndugu yangu....tema mate chini! Kile kiapo bana kinasema uvumilivu katika shida na raha....kuparalaiz si ndio shida zenyewe?
 
Habari zenu binafsi kwa ujumla wenu;

Jana wakati napata kifunga kinywa pale kingstaa kaunta ya juu wakaja wadada wawili wanapiga stori ya mwenzao waliyetoka kumwombea azidi kulala pahala pema peponi baada ya kumaliza mwaka mmoja akiwa chini ya dongo takriban tani saba. Walikuwa wanasikitika uamuzi wa rafiki yao huyo kujiua. Kwa unasaji wangu wa habari (siyo umbea) nikalazimika kuwajoin ili waninusishe yaliyojiri.

Ni hivi:

Kulikuwa jamaa marafiki wawili bwana X na bwana Y ambao walikuwa wameoa na bahati nzuri wake zao nao pia wakatokea kuwa marafiki wazuri. Katika pilikapilika za maisha siku moja bwana X akapata ajali iliyomgharimu kutenguka kiuno na kuparalaiz kuanzia kiunoni mpaka miguuni. Maisha ya Bwana X yakahamia kitandani rasmi, na baioloji yake ikawa haina mawasiliano na jinsia ya kike.

Bwana Y kwa upendo akawa anaisaidia familia ya Bwana X kwa hali na mali (kipato cha mke wa bwana X hakikutosha kuhimili mikiki ya maisha katika hali hii ya serikali ya awamu ya nne)

Mwaka ukakatika, mke wa X akaingiwa na shetani sehemu zake za siri. Akajikuta analazimika kujipitisha na kumimina mabode langueji ya malavidavi kwa bwana Y. Bwana Y uzalendo ukamshinda akalazimika kuliamsha pepo la ngono lililolala kwenye baioloji yake. Shughuli ikaanza wakanogewa na dhambi. Wakajivinjari bila ya mgonjwa X wala mke wa Y kujua mpaka Malaika wa Mungu alipoamua kuweka mambo hadharani.

Siku moja wamepiga ulabu, bwana Y akamsindikiza mke wa X mpaka nyumbani kwa Bwana X. Pepo likawaingia wakaanza kujivinjari sebuleni. Makelele ya malavidavi, Bwana X akastuka usingizini, sijui alipata wapi nguvu akajiangusha kitandani, akajiburuza mpaka sebuleni akashuhudia rafiki yake akimla uroda mkewe….. Akaachia yowe kwa mstuko, na Ziraili mtoa roho akaichukua roho yake kupitia njia ya mstuko wa Moyo…

Haikupita muda mke wa Bwana X nadhiri ikawa ikamsuta…. akaona isiwe tabu…… kwa hiyari yake tena bila ya kushauriwa wala kulazimishwa na mtu, akamwalika ziraili aje kuchukua roho yake kupitia mtaa wa sumu……. Naye akatangulia kuzimu. Yaliyojiri kwa bwana Y ni kuwa ndoa yake imekuwa historia. Na Bwana Y amekuwa kama kreze akiamini ameua watu wawili at a go! (Nadhani baioloji yake itakuwa imepata hitilafu flani)

Sasa ndugu zangu, (kina mama safari hii hebu kuweni wakweli japo kiduchu):

1.Hiki kiapo kwamba "nitakuwa mwaminifu mpaka kifo kitutenganishe" kinatekelezeka? Is it practical kwa wanawake? (Kwa wanaume sitii neno hapo, kwa sababu liko wazi kabisa)

2.Eti mwaweza kwenda kuliwa uroda ilhali mumeo unayempenda sana mpaka ukaamua kuhamia kwake yu kitandani hoi? Nadhiri haziwasuti? (Ningekuwa Mungu mngenitambua hakyanani)

3.Je mwaweza kuvumilia muda gani wakati mnajua kabisa huyu unayelala naye kitanda kimoja baioloji yake ishakuwa si rizki? Mwaweza kuvumilia mpaka ziraili mtoa roho afanye kazi yake? (Hapa mnaweza kuniambia kwa PM manake najua wengine mwaogopa kusema hadharani)

Babu ako konfyuzdi na ameanza kuogopa kutenguka kiuno….Bibi bado anadai wasije wakanichakachulia kwenye hili banda nililojenga kwa pesa za mkopo;

Angalizo: Hii mada ni serious na atakayeenda Ofu Topic….nambwenga makwenzi afu anakula BAN!

Babu...! (Naomba nikuite kama wengine wanavyokuita)
Naomba ufafanuzi kidogo hapo kwenye red, labda nitaweza kuchangia kidogo.
 
Orayt

Tuchukulie kesi kama hii..

Mmeo kakuwezesha, amekusaidia, hajawahi kukuboa...yaani yote njema.
lakini ghafla lahaula...kapata mzinga yuko kitandani. Baioloji haitaamka mpaka anaingia kaburini. Na wewe una kiu yako. Utavumilia mpaka mwisho au uchakachuzi utafanyika japo kwa siri?
Kusema ukweli ntaweza nikitaka!Ila kama nimejawa na tamaa ni bora kumuacha kuliko kumletea mwanaume mwingine ndani...au popote pale!Maana hata hiyo raha nnayoitafuta sitaifaidi!
 
Kungekuwa na definishen 'nzuri' ya neno kifo (kwa ndoa).....labda iwe hivi...:
Kifo ni pale mmoja wa wanandoa anapokua katika hali ya kushindwa moja kwa moja utekelezaji wa majukumu ya kindoa, ilhali upande wa pili ukiwa mahitaji hayo.....
Aisee we RR...ile wanasema till death do us apart kwa kiinglish...wanamaanisha kifo cha kutoa roho..... Na hii kushindwa kutoa utekelezaji wa maswala ya kindoa wakati mmoja wapo bado anahitaji, si ndio hapo kiapo cha KUVUMILIANA KATIKA TAABU NA RAHA kinapokuja?....Hiyo si ndio Taabu au?

Kusema wanawake hawafanyi ntakua muongo!Na wapo ambao wanabadili mapatna kama hawana akili nzuri...na watu wote wa karibu wanajua isipokua waume zao tu!Hii nimeona mwenyewe...ila mwisho wa siku ishu nzima inategemea na kutofautiana kati ya mtu na mtu!Kuna wengine wakichoka kabisa badala ya kwenda kuspaic mambo nje alafu arudi ataaga aondoke kabisa!

Aisee Lizzy,

Sina swali la kukuuliza tena mama. Nimekuelewa fika!
 
Nakusubiri...ole wako ulete uongo wako hapa!

Kwanza hapo kwenye red umeniudhi na nimekusamehe kabla hujasema samahani.

Narudi kwenye mada: Umekuwa umeegemea upande mmoja wa mama kutoka nje ya ndoa wakati mumewe mgonjwa je huyo baba na mkewe nyumbani hajatoka nje ya ndoa?? Umekuwa kama unaonea upande mmoja.

Kiukweli ukiona mwanamke anafikia hatua ya kutoka nje ujue mambo yamemfika shingoni yanakaribia puani kumkosesha pumzi si rahisi sana wanawake kufanya hivyo na atafanya kwa siri kubwa mno ili mumewe asijue kitu wala kutambua hata kidogo all in all wanawake wanatoka nje ya ndoa.

Asanteni kwa kusoma post yangu.

Naomba kuwasilisha
 
Aisee we RR...ile wanasema till death do us apart kwa kiinglish...wanamaanisha kifo cha kutoa roho..... Na hii kushindwa kutoa utekelezaji wa maswala ya kindoa wakati mmoja wapo bado anahitaji, si ndio hapo kiapo cha KUVUMILIANA KATIKA TAABU NA RAHA kinapokuja?....Hiyo si ndio Taabu au?

Naijua hiyo mzee mwenzangu...ila iko very unjust.....hivi kama ikitokea ajali (inayoharibu bayoloji) siku moja baada ya ndoa inakuwaje?
 
Babu...! (Naomba nikuite kama wengine wanavyokuita)
Naomba ufafanuzi kidogo hapo kwenye red, labda nitaweza kuchangia kidogo.

Ni hivi Buke:

Kuna kiapo watu huwa wanaapa wanapoingia katika mikataba ya ndoa (hapa ni wakristo zaidi) Kuwa ndoa yao itakuwa ya mke mmoja na mme mmoja mpaka kifo kiwatenganishe....Katika tabu na raha..... Tumezoea mara nyingi, hata hapa jamvini wanaume wakionekana au kujionyesha kuwa si waaminifu katika ndoa zao. Ila wanawake siku zote wanasema na kushikilia misimamo yao kuwa wao ni waaminifu katika ndoa zao provided kwamba waume zao hawawachakachui.

Sasa likitokea tukio kama hili ambapo mme ndo hivyo tena baioloji imeshasizi, watavumilia wasimegwe nje huko mpaka kifo kifanye kazi yake? tatizo hawataki kunijibu, kanijibu mmoja tu. Kina mama bana!
 
Kwanza hapo kwenye red umeniudhi na nimekusamehe kabla hujasema samahani.

Narudi kwenye mada: Umekuwa umeegemea upande mmoja wa mama kutoka nje ya ndoa wakati mumewe mgonjwa je huyo baba na mkewe nyumbani hajatoka nje ya ndoa?? Umekuwa kama unaonea upande mmoja.

Kiukweli ukiona mwanamke anafikia hatua ya kutoka nje ujue mambo yamemfika shingoni yanakaribia puani kumkosesha pumzi si rahisi sana wanawake kufanya hivyo na atafanya kwa siri kubwa mno ili mumewe asijue kitu wala kutambua hata kidogo all in all wanawake wanatoka nje ya ndoa.

Asanteni kwa kusoma post yangu.

Naomba kuwasilisha
Ahsante kwa kunisamehe.

Hapo Bold sijawaonea kwa kuwa kila siku nyie huwa mnatubishia kuwa hamtoki nje ya ndoa zenu, wakati wanaume wamekuwa wakikiri kuwa huwa wanatoka....ndo maana nimewaulizeni mama zangu, katika situation kama hiyo bado hamtatoka?

Naijua hiyo mzee mwenzangu...ila iko very unjust.....hivi kama ikitokea ajali (inayoharibu bayoloji) siku moja baada ya ndoa inakuwaje?
Kwa mujibu wa imani, shida ndiyo imeanzia hapo, omba mwenzio afe haraka ukamate kifaa kingine vinginevyo .....VUMILIA MAZEE!
 
Bwana Y kwa upendo akawa anaisaidia familia ya Bwana X kwa hali na mali (kipato cha mke wa bwana X hakikutosha kuhimili mikiki ya maisha katika hali hii ya serikali ya awamu ya nne)

Hili halikuwa baya sana...LAKINI HALIKUPASWA KUENDELEA KWA MUDA MREFU SANA!muendelezo wake umejenga mazingira ya ''tamaa za kimwili'' baina ya hao watu wawili

Mwaka ukakatika, mke wa X akaingiwa na shetani sehemu zake za siri. Akajikuta analazimika kujipitisha na kumimina mabode langueji ya malavidavi kwa bwana Y. Bwana Y uzalendo ukamshinda akalazimika kuliamsha pepo la ngono lililolala kwenye baioloji yake. Shughuli ikaanza wakanogewa na dhambi. Wakajivinjari bila ya mgonjwa X wala mke wa Y kujua mpaka Malaika wa Mungu alipoamua kuweka mambo hadharani.

hili mimi silishabikii sana kwakweli......
kibinaadamu nalitafsiri kama ''tamanio'' au tamaa za kimwili baina ya hao wawili.HILI NI KOSA!NA NI KOSA KUBWA KUTUMIA UDHAIFU WA RAFIKIYE AU KINYUME CHAKE KUTUMIA UWEZO WAKE WA KUISAIDIA FAMILIA kumlala mke wa nduguyo.....

kama vile haitoshi kuna upuuzi mkubwa ulifanyika huu hapa:

Siku moja wamepiga ulabu, bwana Y akamsindikiza mke wa X mpaka nyumbani kwa Bwana X. Pepo likawaingia wakaanza kujivinjari sebuleni. Makelele ya malavidavi, Bwana X akastuka usingizini, sijui alipata wapi nguvu akajiangusha kitandani, akajiburuza mpaka sebuleni akashuhudia rafiki yake akimla uroda mkewe….. Akaachia yowe kwa mstuko, na Ziraili mtoa roho akaichukua roho yake kupitia njia ya mstuko wa Moyo…

aisee hapo juu kuna kosa la pili huyo ''mgoni'' kalifanya.....DHARAU!ukishapita mwaka hujalala na mkeo kwa maradhi ya aina hiyo ni dhahiri kwamba mume anajua wazi kuwa kuna vijana wanamkazia mkewe.....!LAKINI KUFANYA KITU HICHO MBELE YA MACHO YAKE AU MAZINGIRA KAMA YALE NI DHARAU KUBWA......!unachukua mke wa mtu SAWA....JARIBU KUWA NA PRIVACY KIDOGO BASI....au?

Wahenga wanaposema ''malipo ya dhuluma zote chini ya jua HULIPWA CHINI YA JUA hawakukosea.....angalia kilichoendelea sasa:

Haikupita muda mke wa Bwana X nadhiri ikawa ikamsuta…. akaona isiwe tabu…… kwa hiyari yake tena bila ya kushauriwa wala kulazimishwa na mtu, akamwalika ziraili aje kuchukua roho yake kupitia mtaa wa sumu……. Naye akatangulia kuzimu. Yaliyojiri kwa bwana Y ni kuwa ndoa yake imekuwa historia. Na Bwana Y amekuwa kama kreze akiamini ameua watu wawili at a go! (Nadhani baioloji yake itakuwa imepata hitilafu flani)

...ukiwa smart zaidi unaweza predict kitakachojiri kwa huyo bwa mkubwa....!DEATH OFCOURSE

SASA MIMI TEAMO NASEMA HIVI:
1)-ukiamua kutoa msaada toa kwa moyo
2)-ukiamua kuifanya kazi ya Bwana Mungu Wako IFANYE KWA MOYO
3)-MSAADA HAUNA RISITI
4)-mke wa mtu achana nae kabisa NI ZAIDI YA HATARI AISEE
5)-tuiepuke ZINAA!maisha bila zinaa yanawezekana
6)-ndo hivo yani mi ndo nimemaliza yani
 
1.Kiapo kinatekelezeka kwa msaada wa Mungu na hofu ya Mungu na zaidi kujiheshimu kwa mwanamke.....!

2. Roho zinasuta huwezi muacha mwanaume uliyempenda kitandani mgonjwa ukaenda kufanya kitu kibaya nadhiri isikusute...sisi tuna roho ya kuumia sana pia!

3.Ukweli wa Mungu na kwa msaada wa Mungu asiyeshindwa jambo,kwasababu zinazoeleweka za kushindwa kupata tendo la ndoa....nitavumilia hado mwisho,uwezo upo kama nia ipo!
 
Mkuu siyo ubaguzi....

Ila kuna dhana kuwa asilimia kubwa ya wnaume si waaminifu hata kama wake zao wapo na hawana matatizo....Ila wanawake siku zote wanaonekana ni wavumilivu (Hapa jamvini hakuna anayekubali hii kitu kuwa WANATOKA NJE YA NDOA ZAO)...Sasa ndio nlitaka kujua inapotokea hali kama hii watavumilia mpaka lini?

Kuparalaiz si kufa ndugu yangu....tema mate chini! Kile kiapo bana kinasema uvumilivu katika shida na raha....kuparalaiz si ndio shida zenyewe?

Mkuu nimekuelewa sana tu, kamata sheria ya ndoa ya mwaka 1971, angalia factors zinazoonyesha kuvunjika kwa ndoa mojakwamoja(IRRIPARABLE BREAK DOWN OF THE MARRIAGE) ambapo talaka inaweza kutolewa, ni pamoja na mwanandoa kushindwa kutoa haki ya ndoa(INABILITY TO CONSUMATE) sasa ndio maana nikasema kuwa haya mambo ni ya ubinandamu, tuwe wakweli Babu, kama tendo la ndoa lisingekuwepo je tungekuwa tunafunga ndoa kweli?................. kisheria huyu mama angeweza kuomba talaka na kupewa japo mchakato wake ni mrefu, lakini kiubinadamu pia haileti maana kufurahia ndoa wakati wa neema tu, kiukweli amekosea huyu mama na Bwana X,...................., ila suala la uvumilivu ni matter of fact kama umezoea kuipata haki yako kila siku inapotokea jambo la kukunyima inakuwa balaa
 
1.Kiapo kinatekelezeka kwa msaada wa Mungu na hofu ya Mungu na zaidi kujiheshimu kwa mwanamke.....!

2. Roho zinasuta huwezi muacha mwanaume uliyempenda kitandani mgonjwa ukaenda kufanya kitu kibaya nadhiri isikusute...sisi tuna roho ya kuumia sana pia!

3.Ukweli wa Mungu na kwa msaada wa Mungu asiyeshindwa jambo,kwasababu zinazoeleweka za kushindwa kupata tendo la ndoa....nitavumilia hado mwisho,uwezo upo kama nia ipo!

This really mean something to me

The Following User Says Thank You to Michelle For This Useful Post:

The Finest (Today)​
 
Hili halikuwa baya sana...LAKINI HALIKUPASWA KUENDELEA KWA MUDA MREFU SANA!muendelezo wake umejenga mazingira ya ''tamaa za kimwili'' baina ya hao watu wawili

hili mimi silishabikii sana kwakweli......
kibinaadamu nalitafsiri kama ''tamanio'' au tamaa za kimwili baina ya hao wawili.HILI NI KOSA!NA NI KOSA KUBWA KUTUMIA UDHAIFU WA RAFIKIYE AU KINYUME CHAKE KUTUMIA UWEZO WAKE WA KUISAIDIA FAMILIA kumlala mke wa nduguyo.....

kama vile haitoshi kuna upuuzi mkubwa ulifanyika huu hapa:

aisee hapo juu kuna kosa la pili huyo ''mgoni'' kalifanya.....DHARAU!ukishapita mwaka hujalala na mkeo kwa maradhi ya aina hiyo ni dhahiri kwamba mume anajua wazi kuwa kuna vijana wanamkazia mkewe.....!LAKINI KUFANYA KITU HICHO MBELE YA MACHO YAKE AU MAZINGIRA KAMA YALE NI DHARAU KUBWA......!unachukua mke wa mtu SAWA....JARIBU KUWA NA PRIVACY KIDOGO BASI....au?

Wahenga wanaposema ''malipo ya dhuluma zote chini ya jua HULIPWA CHINI YA JUA hawakukosea.....angalia kilichoendelea sasa:

...ukiwa smart zaidi unaweza predict kitakachojiri kwa huyo bwa mkubwa....!DEATH OFCOURSE

SASA MIMI TEAMO NASEMA HIVI:
1)-ukiamua kutoa msaada toa kwa moyo
2)-ukiamua kuifanya kazi ya Bwana Mungu Wako IFANYE KWA MOYO
3)-MSAADA HAUNA RISITI
4)-mke wa mtu achana nae kabisa NI ZAIDI YA HATARI AISEE
5)-tuiepuke ZINAA!maisha bila zinaa yanawezekana
6)-ndo hivo yani mi ndo nimemaliza yani

Aisee Dogo!

Leo nimekukubali vibaya sana!
 
1.Kiapo kinatekelezeka kwa msaada wa Mungu na hofu ya Mungu na zaidi kujiheshimu kwa mwanamke.....!

2. Roho zinasuta huwezi muacha mwanaume uliyempenda kitandani mgonjwa ukaenda kufanya kitu kibaya nadhiri isikusute...sisi tuna roho ya kuumia sana pia!

3.Ukweli wa Mungu na kwa msaada wa Mungu asiyeshindwa jambo,kwasababu zinazoeleweka za kushindwa kupata tendo la ndoa....nitavumilia hado mwisho,uwezo upo kama nia ipo!

Aisee Michelle kama haya uliyoyaandika hapa ni ya kweli na ukweli mtupu......Najuta kwanini nilichelewa kukufahamu. NINGEKUOA!
 
Mkuu nimekuelewa sana tu, kamata sheria ya ndoa ya mwaka 1971, angalia factors zinazoonyesha kuvunjika kwa ndoa mojakwamoja(IRRIPARABLE BREAK DOWN OF THE MARRIAGE) ambapo talaka inaweza kutolewa, ni pamoja na mwanandoa kushindwa kutoa haki ya ndoa(INABILITY TO CONSUMATE) sasa ndio maana nikasema kuwa haya mambo ni ya ubinandamu, tuwe wakweli Babu, kama tendo la ndoa lisingekuwepo je tungekuwa tunafunga ndoa kweli?................. kisheria huyu mama angeweza kuomba talaka na kupewa japo mchakato wake ni mrefu, lakini kiubinadamu pia haileti maana kufurahia ndoa wakati wa neema tu, kiukweli amekosea huyu mama na Bwana X,...................., ila suala la uvumilivu ni matter of fact kama umezoea kuipata haki yako kila siku inapotokea jambo la kukunyima inakuwa balaa
Sidhani kwa hali aliyonayo mumewe huyu mama kama anaweza kufikiria kuomba talaka i doubt, hata kwa mazingira ya sasa pia i doubt kama wewe mgonjwa halafu mkeo akakuomba talaka halafu ukampa, unless you don't love her
 
Ni hivi Buke:

Kuna kiapo watu huwa wanaapa wanapoingia katika mikataba ya ndoa (hapa ni wakristo zaidi) Kuwa ndoa yao itakuwa ya mke mmoja na mme mmoja mpaka kifo kiwatenganishe....Katika tabu na raha..... Tumezoea mara nyingi, hata hapa jamvini wanaume wakionekana au kujionyesha kuwa si waaminifu katika ndoa zao. Ila wanawake siku zote wanasema na kushikilia misimamo yao kuwa wao ni waaminifu katika ndoa zao provided kwamba waume zao hawawachakachui.

Sasa likitokea tukio kama hili ambapo mme ndo hivyo tena baioloji imeshasizi, watavumilia wasimegwe nje huko mpaka kifo kifanye kazi yake? tatizo hawataki kunijibu, kanijibu mmoja tu. Kina mama bana!

Babu...! Kwa style ya maisha ya sasa, hata bila mtu kuwa na hitilafu yoyote mwilini (kila kitu kiko active) watu wanatoka nje ya ndoa kwa sana tu. Si wanawake, si wanaume. Ni kama aina fulani hivi ya maisha ya kisasa (jinsi tunavyojidanganya). Ni asilimia chache sana ya wanandoa wanaotii kiapo walichoapa. Kwa wanawake wenzangu labda naweza sema hivi, hakuna aliyekamilika kwa asilimia zote, ni wachache sana wanaweza kumudu kuvumilia muda mrefu. Tuliobaki kwa issue kama hivyo, tunatoka nje lakini kwa staha. Kufanya mapenzi ndani ya nyumba unayoishi na mumeo, tena na mwanaume mwingine, ni aibu iliyopitiliza!
 
Back
Top Bottom