Eti inawezekana?...UVUMILIVU MPAKA LINI?

Mkuu nimekuelewa sana tu, kamata sheria ya ndoa ya mwaka 1971, angalia factors zinazoonyesha kuvunjika kwa ndoa mojakwamoja(IRRIPARABLE BREAK DOWN OF THE MARRIAGE) ambapo talaka inaweza kutolewa, ni pamoja na mwanandoa kushindwa kutoa haki ya ndoa(INABILITY TO CONSUMATE) sasa ndio maana nikasema kuwa haya mambo ni ya ubinandamu, tuwe wakweli Babu, kama tendo la ndoa lisingekuwepo je tungekuwa tunafunga ndoa kweli?................. kisheria huyu mama angeweza kuomba talaka na kupewa japo mchakato wake ni mrefu, lakini kiubinadamu pia haileti maana kufurahia ndoa wakati wa neema tu, kiukweli amekosea huyu mama na Bwana X,...................., ila suala la uvumilivu ni matter of fact kama umezoea kuipata haki yako kila siku inapotokea jambo la kukunyima inakuwa balaa

Mkuu Sheria ya ndoa si ni hizi zimetungwa na binadamu?

Mi nazungumzia maandiko kwenye Bible. Yale yanayosema hata kumtamani tu mke wa mtu tayari umeshazini naye.

Tena imeandikwa...MKE HAACHWI ILA KWA ZINAA!...yaani kinachoweza kukufanya umtaliki mkeo ni zinaa...si magonjwa!
 
kwa hali kama hyi siwez msaliti as nakuwa nimeapa kwa mungu kuishi na kwa shida na raha bt namimi nitamsaliti pale tu nikijua nae kanisaliti au kaniletea za kuleta
 
Haya maswali ya Babu mpaka sasa bado sijaona mdada hapa jamvini aliye yachomoa kwa point inayoeleweka mpaka ikathibitisha kweli wao hawatokagi nje ya ndoa.

Babu naomba niweke dau utakalo chagua wewe. Mdada atakae tengua haya maswali namzawadia BILA ZENGWE. Tena nipo VERY SERIOUS.

Babu nifahamishe tu dau ni lipi kwa PM niiandae mapema.

Maana naanza kupata konklushen kwamba WANAUME NI WAWAZI na WANAWAKE NI WASIRI SANA ktk haya mambo
 
Babu...! Kwa style ya maisha ya sasa, hata bila mtu kuwa na hitilafu yoyote mwilini (kila kitu kiko active) watu wanatoka nje ya ndoa kwa sana tu. Si wanawake, si wanaume. Ni kama aina fulani hivi ya maisha ya kisasa (jinsi tunavyojidanganya). Ni asilimia chache sana ya wanandoa wanaotii kiapo walichoapa. Kwa wanawake wenzangu labda naweza sema hivi, hakuna aliyekamilika kwa asilimia zote, ni wachache sana wanaweza kumudu kuvumilia muda mrefu. Tuliobaki kwa issue kama hivyo, tunatoka nje lakini kwa staha. Kufanya mapenzi ndani ya nyumba unayoishi na mumeo, tena na mwanaume mwingine, ni aibu iliyopitiliza!

Buke ahsante kwa hii yuziful posti..... huo ndio ukweli halisi japo kina mama wengi humu ndani huwa wanaubishia sana.

Ahsante pia kwa hatimaye kujua kumbe wewe ni mwanamke. JF kaazi kwelikweli!

Ahsante kwa kuwa mkwelimama yangu
 
Sidhani kwa hali aliyonayo mumewe huyu mama kama anaweza kufikiria kuomba talaka i doubt, hata kwa mazingira ya sasa pia i doubt kama wewe mgonjwa halafu mkeo akakuomba talaka halafu ukampa, unless you don't love her

Ndio hapo waswahili wakalonga kuwa bora lawama kuliko fedheha......................, lazima tujifunze kuchagua moja kuliko kuishi kwa maigizo, ila ktk yote Mungu atangulizwe ili mtu uweze kufanya uamuzi sahihi, ni rahisi kunyoosha kidole na kusema mtu flani amekosea, lakini ujue kuwa ajuae kiatu kimembana ni yule aliekivaa, so mimi nachoweza kusema ni kumlaumu Bwana X sababu amemlia rafikiye wa karibu, lakini huyu mama nae da!!!! complicated jamani.................... tumwachie Mungu anajua (ALLAH KNOWS MUCH)
 
Haya maswali ya Babu mpaka sasa bado sijaona mdada hapa jamvini aliye yachomoa kwa point inayoeleweka mpaka ikathibitisha kweli wao hawatokagi nje ya ndoa.

Babu naomba niweke dau utakalo chagua wewe. Mdada atakae tengua haya maswali namzawadia BILA ZENGWE. Tena nipo VERY SERIOUS.

Babu nifahamishe tu dau ni lipi kwa PM niiandae mapema.

Maana naanza kupata konklushen kwamba WANAUME NI WAWAZI na WANAWAKE NI WASIRI SANA ktk haya mambo
Babu mdogo...hii ni ngumu kumesa....hilo swala la dau...huoni hiyo ni sababu ya kukutana Zero Pub leo kulijadili? Hebu msome msiri mwingine huyu hapa chini...LOL

kwa hali kama hyi siwez msaliti as nakuwa nimeapa kwa mungu kuishi na kwa shida na raha bt namimi nitamsaliti pale tu nikijua nae kanisaliti au kaniletea za kuleta
 
Habari zenu binafsi kwa ujumla wenu;

Jana wakati napata kifunga kinywa pale kingstaa kaunta ya juu wakaja wadada wawili wanapiga stori ya mwenzao waliyetoka kumwombea azidi kulala pahala pema peponi baada ya kumaliza mwaka mmoja akiwa chini ya dongo takriban tani saba. Walikuwa wanasikitika uamuzi wa rafiki yao huyo kujiua. Kwa unasaji wangu wa habari (siyo umbea) nikalazimika kuwajoin ili waninusishe yaliyojiri.

Ni hivi:

Kulikuwa jamaa marafiki wawili bwana X na bwana Y ambao walikuwa wameoa na bahati nzuri wake zao nao pia wakatokea kuwa marafiki wazuri. Katika pilikapilika za maisha siku moja bwana X akapata ajali iliyomgharimu kutenguka kiuno na kuparalaiz kuanzia kiunoni mpaka miguuni. Maisha ya Bwana X yakahamia kitandani rasmi, na baioloji yake ikawa haina mawasiliano na jinsia ya kike.

Bwana Y kwa upendo akawa anaisaidia familia ya Bwana X kwa hali na mali (kipato cha mke wa bwana X hakikutosha kuhimili mikiki ya maisha katika hali hii ya serikali ya awamu ya nne)

Mwaka ukakatika, mke wa X akaingiwa na shetani sehemu zake za siri. Akajikuta analazimika kujipitisha na kumimina mabode langueji ya malavidavi kwa bwana Y. Bwana Y uzalendo ukamshinda akalazimika kuliamsha pepo la ngono lililolala kwenye baioloji yake. Shughuli ikaanza wakanogewa na dhambi. Wakajivinjari bila ya mgonjwa X wala mke wa Y kujua mpaka Malaika wa Mungu alipoamua kuweka mambo hadharani.

Siku moja wamepiga ulabu, bwana Y akamsindikiza mke wa X mpaka nyumbani kwa Bwana X. Pepo likawaingia wakaanza kujivinjari sebuleni. Makelele ya malavidavi, Bwana X akastuka usingizini, sijui alipata wapi nguvu akajiangusha kitandani, akajiburuza mpaka sebuleni akashuhudia rafiki yake akimla uroda mkewe….. Akaachia yowe kwa mstuko, na Ziraili mtoa roho akaichukua roho yake kupitia njia ya mstuko wa Moyo…

Haikupita muda mke wa Bwana X nadhiri ikawa ikamsuta…. akaona isiwe tabu…… kwa hiyari yake tena bila ya kushauriwa wala kulazimishwa na mtu, akamwalika ziraili aje kuchukua roho yake kupitia mtaa wa sumu……. Naye akatangulia kuzimu. Yaliyojiri kwa bwana Y ni kuwa ndoa yake imekuwa historia. Na Bwana Y amekuwa kama kreze akiamini ameua watu wawili at a go! (Nadhani baioloji yake itakuwa imepata hitilafu flani)

Sasa ndugu zangu, (kina mama safari hii hebu kuweni wakweli japo kiduchu):

1.Hiki kiapo kwamba “nitakuwa mwaminifu mpaka kifo kitutenganishe” kinatekelezeka? Is it practical kwa wanawake? (Kwa wanaume sitii neno hapo, kwa sababu liko wazi kabisa)

2.Eti mwaweza kwenda kuliwa uroda ilhali mumeo unayempenda sana mpaka ukaamua kuhamia kwake yu kitandani hoi? Nadhiri haziwasuti? (Ningekuwa Mungu mngenitambua hakyanani)

3.Je mwaweza kuvumilia muda gani wakati mnajua kabisa huyu unayelala naye kitanda kimoja baioloji yake ishakuwa si rizki? Mwaweza kuvumilia mpaka ziraili mtoa roho afanye kazi yake? (Hapa mnaweza kuniambia kwa PM manake najua wengine mwaogopa kusema hadharani)

Babu ako konfyuzdi na ameanza kuogopa kutenguka kiuno….Bibi bado anadai wasije wakanichakachulia kwenye hili banda nililojenga kwa pesa za mkopo;

Angalizo: Hii mada ni serious na atakayeenda Ofu Topic….nambwenga makwenzi afu anakula BAN!

ndo maana wajukuu zako bado tunasoma mchezo!
ngoja wanawake watupe experience
 
Ndio hapo waswahili wakalonga kuwa bora lawama kuliko fedheha......................, lazima tujifunze kuchagua moja kuliko kuishi kwa maigizo, ila ktk yote Mungu atangulizwe ili mtu uweze kufanya uamuzi sahihi, ni rahisi kunyoosha kidole na kusema mtu flani amekosea, lakini ujue kuwa ajuae kiatu kimembana ni yule aliekivaa, so mimi nachoweza kusema ni kumlaumu Bwana X sababu amemlia rafikiye wa karibu, lakini huyu mama nae da!!!! complicated jamani.................... tumwachie Mungu anajua (ALLAH KNOWS MUCH)

Hili ndio jambo la msingi hasa.
 
Asprin babu yangu najiuliza swali moja kabla sijapata majibu ..
Hivi kama Mtu unaweza kuishi forever and ever bila kupata hiyo kitu ?Mwili kwanza unakuwa hauko active au ume -expire ?
Hii ni mitihani mikubwa sana ya maisha
Lakini kwa kesi ya huyu dada hata sijui nisemeje mie?
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atusaidie na aendelee kutupa rehema na hekima zake kama mfalme Suleiman
 
Mkuu Sheria ya ndoa si ni hizi zimetungwa na binadamu?

Mi nazungumzia maandiko kwenye Bible. Yale yanayosema hata kumtamani tu mke wa mtu tayari umeshazini naye.

Tena imeandikwa...MKE HAACHWI ILA KWA ZINAA!...yaani kinachoweza kukufanya umtaliki mkeo ni zinaa...si magonjwa!

Babu hata wanadamu wamewekwa na Mungu, Hivyo chochote halali kitokacho kwa mwanadamu, kimetoka kwa mungu, Suala la dini na sheria japo vinakinzana lakini vinaenda sambamba, lengo ni kutoa migogoro isiyo ya msingi, na Islamic law inakubali kabisa hili suala tatizo la Bible wakristu tulio wengi hatujui kuwa inatupasa kuisoma na kuijua kwa maana inakila kitu, tunapick vijimistari na kuvitumia kuacomodate matakwa yetu(TUNACHAKACHUWA)....................., ila twende mbele turudi nyuma hata kama na dini yako bado uanadamu ndio suluhisho hapo
 
Babu, nami niseme hivi,
mambo haya ya viapo yanafanyika mbele ya Muumba; na inategemeana na hawa wawili wanamheshimu vipi huyu Muumba. Kweli kama unamcha Mungu na unampenda mume/mke wako, utavumilia. Ni kweli jaribu hili ni gumu sana, lakini kwa msaada wake Mungu utaweza kama umedhamiria. Kwa wanadamu haiwezekani, lakini kwa Mungu yote yanawezekana.
Mbarikiwe na nawatakia siku njema.
 
Asprin babu yangu najiuliza swali moja kabla sijapata majibu ..
Hivi kama Mtu unaweza kuishi forever and ever bila kupata hiyo kitu ?Na kwa nn iliwekwa kwanza
Mwili kwanza unakuwa hauko active au ume -expire ?
Hii ni mitihani mikubwa sana ya maisha
Lakini kwa kesi ya huyu dada hata sijui nisemeje mie?
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atusaidie na aendelee kutupa rehema na hekima zake kama mfalme Suleiman

Hahahaha...mama wakwanza moja bana!
Usisikitike, changia mada hapo bana.
Yaani jamaa limeshakunjesha utamu. Ushajua raha yake, haipiti siku mbili unaihitaji...mara ghafla imebuma...nawe ndo kwanza una miaka miwili katika ndoa. Bado mbichi na vijana mtaani hawakomi kukukonyeza...

Hutamuacha mmeo anagumia kwa maumivu kitandani ukamegwe mtaani huko?
 
mmh!ama kweli inasikitisha lkn uvumilivu hapo ni utata mtupu,huyo mama kuvumilia lazma ingekuwa ngumu kwa vile ana hisia na analala kitanda kimoja na mumewe wakati mwingine kile kiapo kimekuwa nadharia zaidi.
 
Babu, nami niseme hivi,
mambo haya ya viapo yanafanyika mbele ya Muumba; na inategemeana na hawa wawili wanamheshimu vipi huyu Muumba. Kweli kama unamcha Mungu na unampenda mume/mke wako, utavumilia. Ni kweli jaribu hili ni gumu sana, lakini kwa msaada wake Mungu utaweza kama umedhamiria. Kwa wanadamu haiwezekani, lakini kwa Mungu yote yanawezekana.
Mbarikiwe na nawatakia siku njema.

Hahahahah....Keren..

Leo kina Mama mmemtumia Mungu sana kujikinga LOL

Tunapokuwa wazima mnaenda kuchakachuliwa huko mnajifanya hamfanyi! Tunapokuwa wagonjwa mnasema Mungu atawasaidieni....babu ako konfyuzdi!
 
.......Hutamuacha mmeo anagumia kwa maumivu kitandani ukamegwe mtaani huko?

Ikitokea katika umri mkubwa ndoa inavumilika.....ila wanandoa wako chini ya miaka 40 inakua haiwezekani (angalao kwa nguvu za kibinadamu)....
 
Ahsante kwa kunisamehe.

Hapo Bold sijawaonea kwa kuwa kila siku nyie huwa mnatubishia kuwa hamtoki nje ya ndoa zenu, wakati wanaume wamekuwa wakikiri kuwa huwa wanatoka....ndo maana nimewaulizeni mama zangu, katika situation kama hiyo bado hamtatoka?

Tutatoka hata kama si kwa situation kama hiyo peke yake zipo nyingi mf. Maudhi, kunyimwa ile kitu inamesa mwenzake, jamaa kutokuwepo home hadi midnight nk

BTW: Sababu zipo nyingi za kukufanya utoke nje ukawa na mpango wa kando wa kiume
 
Aisee Michelle kama haya uliyoyaandika hapa ni ya kweli na ukweli mtupu......Najuta kwanini nilichelewa kukufahamu. NINGEKUOA!

Una mke mwema,wajua hilo acha story zako hapa.....ni kweli,si chakula kile au pumzi kwamba ukikosa unakufa Babu!
 
Haya maswali ya Babu mpaka sasa bado sijaona mdada hapa jamvini aliye yachomoa kwa point inayoeleweka mpaka ikathibitisha kweli wao hawatokagi nje ya ndoa.

Babu naomba niweke dau utakalo chagua wewe. Mdada atakae tengua haya maswali namzawadia BILA ZENGWE. Tena nipo VERY SERIOUS.

Babu nifahamishe tu dau ni lipi kwa PM niiandae mapema.

Maana naanza kupata konklushen kwamba WANAUME NI WAWAZI na WANAWAKE NI WASIRI SANA ktk haya mambo

Umenifurahisha sana leo CPU unajua nachoongelea pata haki yako

The Following 2 Users Say Thank You to CPU For This Useful Post:

Asprin (Today), Dena Amsi (Today)​
 
Back
Top Bottom