Eti asijue................How??

Penzi ni kikohozi kulificha huliweziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.................................

Huu wimbo sijui aliimba nani but mie nimecopy and paste @right reserved
 
Penzi ni kikohozi kulificha huliweziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.................................

Huu wimbo sijui aliimba nani but mie nimecopy and paste @right reserved

Fresh Jumbe nadhani.....hahahah
Dena bana kweli kabisa mapenzi hayafichiki ndio maana ninauliza uhalisia wa maneno hayo ya vijiweni??
Ni mara nyingi tunaambiwa na we nae.....ulimwonyesha kuwa unampenda sana ndio maana!! ..........sasa utakizuiaje kikohozi nacho kishafika kooni??!!
 
Ha ha ha huwezi kuficha lakini yako maneno mengi mno watu husema

Eti ooohhh na wewe ulimwonyesha unampenda ndo maana akakutenda hivyo
Ooohhh ukimwonyesha mwanaume unampenda sana atakunyanyasa
Ni maneno yakufikirika sana huwezi kuficha mapenzi kamwe utajaribu kupretend but you will never succeed
 
Hivi....eti nimpende mtu halafu niigize nampenda kidogo ili asiniletee mapozi? Haiwezekani. Nitasema juu ya wasichana:

  1. Si kweli kuwa ukimpenda msichana na ukamwonesha hivyo atakunyanyasa. Ukimwonesha umemfia atakunyanyasa. Nachomaanisha ni kuwa ukimwonesha umempenda kupiliza kiwango cha kutomwonesha dissatisfaction aki-misbehave atakunyanyasa kwa kuwa atakuwa anajua amekosea na huna uwezo wa kuchukua uamuzi wowote. Mvulana au msichana ni lazima amwoneshe mwenza wake kuwa anampenda na pia amwoneshe anaweza kuchukua hatua ya kuachana naye kama atafanya makosa na kuyarudia. Simaanishi umtishe kuwa utamwacha ila kuna namna ya kumwonesha kuwa umempenda na unajitambua katika kumpenda kwako. Namna mojawapo ni kumwambia kuwa unampenda kwa sababu unaamini anastahili kupendwa na kwa sababu unaamini atakuwa mwaminifu na mtiifu kwako. Mwambie, "Honey, kile utachokipata katika uhusiano wetu ni kile nachodhani unastahili na ninachoweza kukifanya juu yako. Kile nachostahili mimi ni kazi yako wewe kunipa. Kama kuna kitu ntachokosea usiache kuniambia nijisahihishe."

  1. I knew kuna hazina ya busara imejificha kwa 3D.....ulichokisema hapa ni ukweli mtupu. Penda kishujaa, usipende kidhaifu. Aksante sana mydia wengi tumenyanyasika sana kwa kuishi maisha ya namna hii.......... unajihisi kumpenda mtu mpaka unaogopa kumwambia akikukosea kisa asiudhike akakuacha loh................... ah mi ctaki

    [*]Tunachokosea ni kumruhusu mtu awe na wasichana wengine halafu "sisi" tunaishia kulia tu. Unamwambia unamwacha halafu then unarudi, hapo unategemea nini? Usiwahi kumtisha kuwa unamwacha, mwambie kuwa hauridhiki na anachokifanya. Mwambie pia japo hauna ushahidi lakini vitendo na ishara zake zinakunyima amani, mwambie aifanyie kazi hofu yako. Anayekupenda atakusikiliza, asiyekupenda ni kazi kwako kuendelea kumlilia kama moyo wako "umemfia."

  1. Hahahaha hapo ndo pabaya zaidi . Unajua/anakujulisha kuwa yupo mwingine bado wang'ang'ania tu ni mbaya.

    Nikimpenda msichana, kwanza ntamwambia, pili yeye mwenyewe ataona tu. Mimi naweza kuandika mashairi....... eti jamani nimpende mtu halafu niogope kumwandikia verse, sasa kipaji changu hiki ntakitumia wapi?
Hahahahaha nimeipenda hii 3D we kiboko eti bwana raha jipe mwenyewe ati. Wawezatunga nyimbo achia kipaji bana usikifiche...........Aksante leo umenifurahisha sana.

  1. Hata hivyo ni vizuri kuweka kiasi katika mahusiano (Si kumwonesha kidogo unampenda). Kiasi maana yake usinunue kila kitu hata kama uwezo wako ni mdogo, kumbuka wenzi wetu wanajua uwezo wetu. Kama mwanamume una pesa na mwanamke akajua una pesa usimnunulie magari kila siku, atadhani unafanya hivyo kwa kuwa una uwezo, siku nyingine nunua pipi au mdoli. Bei ya mdoli si dalili ya utajiri ni dalili ya kupenda. Sasa kama ataweka nyodo ni juu yake. Ila naye ni lazima akununulie japo leso. Wavulana nawapasha leo: Kama mwanamke anakupenda nakuhakikishia atakuletea hata big g. Ukiona anaomba tu vocha, halipii nauli, halipii msosi, hapigi japo sekunde, anabipu tu, baba... hakupendi. Ndiyo ni mzuri sana. Ndiyo unampenda sana. Ndiyo "unashindwa" kumwacha. ndiyo alikuwa miss Tanzania. Ndiyo anaongea kiingereza. Ndiyo ukimwacha atachukuliwa na Diamond (sorry kwa kumtaja). Ndiyo yeye ni maarufu kuliko wewe. Ukweli ni mmoja tu hakupendi.
  2. MWONESHE UNAMPENDA. AKIRINGA ONGEA NAYE. ASIPOBADILIKA MWAMBIE TENA. ASIPOBADILIKA ACHANA NAYE. USIACHE KUMWONNESHA UNAYEMPENDA KUWA UNAMPENDA. Ila nayempenda naye...........
Anipende mimi kama mimi,​

Si kisa eti mi msanii,
Au labda naonejkana sana kwenye Tivii,
Ila wa kunishauri juu ya HIVii,
Si lazima awe na lipsi pana,
Si lazima akicheka awe ana mwanya.​

(Ubeti toka wimbo wa Daz Baba ft Mangwea - Wife)​

Aksante sana 3D. Thats all I can say to this useful post
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Penzi ni kikohozi kulificha huliweziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.................................

Huu wimbo sijui aliimba nani but mie nimecopy and paste @right reserved

Aliimba Fresh Jumbe.

Sikinde pia waliimba:

mtu chake apendacho,
hakina hila moyoni,
huridhika kuwa nacho,
japo hakina thamani,
mapenzi hayana kificho,
yaingiapo moyoni,
mwenye mapenzi haoni,
ingawa macho anayo!
 
MwanajamiiOne asante kwa hii topic
Asanteni sana wachangiaji wote mmemwaga point za vungu
Av learnt soo much from you guys

Muhimu kwangu,na hii naahidi kuipractise:
1. Love someone as much as your heart is willing
2. Show your love as much as you can
3. Ingia kwenye relationship na moyo na akili
4. Usionyeshe you are a desperate type
5. You still have a life even if you wont share it with him

Mbarikiwe sana
 
Hivi....eti nimpende mtu halafu niigize nampenda kidogo ili asiniletee mapozi? Haiwezekani. Nitasema juu ya wasichana:

  1. Si kweli kuwa ukimpenda msichana na ukamwonesha hivyo atakunyanyasa. Ukimwonesha umemfia atakunyanyasa. Nachomaanisha ni kuwa ukimwonesha umempenda kupiliza kiwango cha kutomwonesha dissatisfaction aki-misbehave atakunyanyasa kwa kuwa atakuwa anajua amekosea na huna uwezo wa kuchukua uamuzi wowote. Mvulana au msichana ni lazima amwoneshe mwenza wake kuwa anampenda na pia amwoneshe anaweza kuchukua hatua ya kuachana naye kama atafanya makosa na kuyarudia. Simaanishi umtishe kuwa utamwacha ila kuna namna ya kumwonesha kuwa umempenda na unajitambua katika kumpenda kwako. Namna mojawapo ni kumwambia kuwa unampenda kwa sababu unaamini anastahili kupendwa na kwa sababu unaamini atakuwa mwaminifu na mtiifu kwako. Mwambie, "Honey, kile utachokipata katika uhusiano wetu ni kile nachodhani unastahili na ninachoweza kukifanya juu yako. Kile nachostahili mimi ni kazi yako wewe kunipa. Kama kuna kitu ntachokosea usiache kuniambia nijisahihishe."
  2. Tunachokosea ni kumruhusu mtu awe na wasichana wengine halafu "sisi" tunaishia kulia tu. Unamwambia unamwacha halafu then unarudi, hapo unategemea nini? Usiwahi kumtisha kuwa unamwacha, mwambie kuwa hauridhiki na anachokifanya. Mwambie pia japo hauna ushahidi lakini vitendo na ishara zake zinakunyima amani, mwambie aifanyie kazi hofu yako. Anayekupenda atakusikiliza, asiyekupenda ni kazi kwako kuendelea kumlilia kama moyo wako "umemfia."
  3. Nikimpenda msichana, kwanza ntamwambia, pili yeye mwenyewe ataona tu. Mimi naweza kuandika mashairi....... eti jamani nimpende mtu halafu niogope kumwandikia verse, sasa kipaji changu hiki ntakitumia wapi?
  4. Hata hivyo ni vizuri kuweka kiasi katika mahusiano (Si kumwonesha kidogo unampenda). Kiasi maana yake usinunue kila kitu hata kama uwezo wako ni mdogo, kumbuka wenzi wetu wanajua uwezo wetu. Kama mwanamume una pesa na mwanamke akajua una pesa usimnunulie magari kila siku, atadhani unafanya hivyo kwa kuwa una uwezo, siku nyingine nunua pipi au mdoli. Bei ya mdoli si dalili ya utajiri ni dalili ya kupenda. Sasa kama ataweka nyodo ni juu yake. Ila naye ni lazima akununulie japo leso. Wavulana nawapasha leo: Kama mwanamke anakupenda nakuhakikishia atakuletea hata big g. Ukiona anaomba tu vocha, halipii nauli, halipii msosi, hapigi japo sekunde, anabipu tu, baba... hakupendi. Ndiyo ni mzuri sana. Ndiyo unampenda sana. Ndiyo "unashindwa" kumwacha. ndiyo alikuwa miss Tanzania. Ndiyo anaongea kiingereza. Ndiyo ukimwacha atachukuliwa na Diamond (sorry kwa kumtaja). Ndiyo yeye ni maarufu kuliko wewe. Ukweli ni mmoja tu hakupendi.
  5. MWONESHE UNAMPENDA. AKIRINGA ONGEA NAYE. ASIPOBADILIKA MWAMBIE TENA. ASIPOBADILIKA ACHANA NAYE. USIACHE KUMWONNESHA UNAYEMPENDA KUWA UNAMPENDA. Ila nayempenda naye...........

Anipende mimi kama mimi,
Si kisa eti mi msanii,
Au labda naonejkana sana kwenye Tivii,
Ila wa kunishauri juu ya HIVii,
Si lazima awe na lipsi pana,
Si lazima akicheka awe ana mwanya.

(Ubeti toka wimbo wa Daz Baba ft Mangwea - Wife)

:A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose:
 
Hapana si kunyanyasika......kuna baadhi ya vitu ambavyo pale mnapokuwa mmezoeana huwa vinapungua na pale mwenzi wako anapojaribu kuquestion huwa kama vile tunapuuza.......akiifyumu huwa tunaignore na hapo ndo ule usemi wa usimwonyeshe kama umefika saaaana huapply lol.

Mfano hun wako anatamani wenda cinema, na alikwambia muda mrefu tu then siku ya siku unachomoa, akinuna ,,,,,,,,,,,,,,we kwa vile ukionyesha kuhudhunika kwako na kumwomba samahani unajiona kama vile umekwenda an et\xtra mile........na washkaji hawakawii kukwambia unamuendekeza usimwonyeshe kuwa unampenda saaaaaaaaaaana

Alrite alrite, sasa nimekupata mjukuu mtiifu, hapo sasa hata mimi napinga, penzi sio kuoneshwa tu bali kukolezwa pia ni muhimu, penzi linatawaliwa na hisia na hisia ni lazima ziamshwe kwa vikorombwezo ili penzi liwe active and alive, hauwezi kusema unampenda mwenza wako halafu unaona tabu kumuomba msamaha pale unapokosea au unapofeli kutimiza ahadi.

Na hapa ndipo ninapoona waswahili tunatafsiri mapenzi kwa lugha ya kigeni, ni lazima tujue kwamba kuna vitu ni vya msingi katika mapenzi (eg kutimiza ahadi, outing, kushauriana, zawadi, romantic enviroment, kuwa responsible etc etc), kufanya vitu hivi ni lazima ili penzi lithaminike, lakini waswahili wanatafsiri kufanya vitu hivi ni kuonekana umemilikiwa au kuwezwa kimapenzi au the so called unaonesha mapenzi. big NO.

NINACHOPINGA MIMI.

Mtu kujionesha kuwa yuko very weak katika mahusiano kiasi kwamba mwenza akajua kwamba hata nikileta kidumu/nyumba ndogo ndani basi jamaa atalia tu halaf atanyamaza na hawezi kuniacha. Amini usiamini MJ1, binadamu tukiwekwa juu tunakuwa na kiburi na dharau (hii ni human nature, refer to viongozi wa siasa),
kwahivyo, give love but show strength as well.

THE END
 
MwanajamiiOne asante kwa hii topic
Asanteni sana wachangiaji wote mmemwaga point za vungu
Av learnt soo much from you guys

Muhimu kwangu,na hii naahidi kuipractise:
1. Love someone as much as your heart is willing
2. Show your love as much as you can
3. Ingia kwenye relationship na moyo na akili
4. Usionyeshe you are a desperate type
5. You still have a life even if you wont share it with him

Mbarikiwe sana

Na hii ndio ilitakiwa iwe conclusion ya hii sred. umeipanga vizuri kweli daughter. aiseee! unafanya kazi ya kupanga ratiba za safari za rais nini? lol
imetulia kweli
 
Wanajamii
Natumaini wote wazima.........................

Ni mara nyingi nimekuwa nikisikie kuwa ..Kama unataka mwanaume/mwanamke wako kimapenzi asikuchoke basi usimwonyeshe kuwa kwake umefika............yaani hata kama unampenda sana basi unatakiwa usionyeshe!!!

How do people do that?? Mapenzi si wanasema ni kikohozi, hayajifichi?? sasa hapa inakuwaje au inakuwagaje?

Mhhhh! MJ1 mie mwenzenu haya ya kuficha mapenzi sijui hata unafanyaje fanyaje ili kumficha mpenzio kwamba unampenda sana! Kama huo wasiwasi wa kutendwa kwa kuwa anajua unampenda sana si bora tu akutende mapema badala ya kuwa nae kwa muda mrefu kisha ukaja kugundua kwamba penzi lake kwako lilikuwa ni usanii tu na si penzi la kweli?

Nimeshaona hapa katika mijadala kama hii wachangiaji wengine walidai wanampenda mpenzi kwa 60% or even less than that! huu si ndio uchakachuaji wa mapenzi!? kama huwezi kumpenda mtu 100% naye akajua hivyo kwanini upoteze muda wako na muda wake kufanya usanii wa mapenzi!?
 
Jamani ukweli ni kuwa if you love someone tell them. Watakuja wengine wataonyesha wanapenda utaachwa kwenye mataa. Hamna haja ya kuficha mapenzi kwani mapenzi ni vitendo sio maneno.
Suala la kuanza kutoonyesha kuwa hujamfia kiasi hicho nadhani ni MATOKEO tu baada ya kuona kuwa hakujali pamoja na kuwa unampenda sana na umemwonyesha hivyo. Yani baada ya kuonyesha upendo wako wote na bado hajali unaweza ukaacha kumwonyesha upendo na ikiwezekana kuachana naye kabisa.
Ila la msingi hapa ni kuwa mtu hawezi jua unampenda kiasi gani mpaka umwonyeshe. Na lazima ajue kuwa akizingua unamtema. Kumpenda kwako sio tiketi yake ya kukudharau na kukunyanyasa.
UKIPENDA ONYESHA, AKIZINGUA ACHANA NAYE FASTA TU.
 
Wanajamii
Natumaini wote wazima.........................

Ni mara nyingi nimekuwa nikisikie kuwa ..Kama unataka mwanaume/mwanamke wako kimapenzi asikuchoke basi usimwonyeshe kuwa kwake umefika............yaani hata kama unampenda sana basi unatakiwa usionyeshe!!!

How do people do that?? Mapenzi si wanasema ni kikohozi, hayajifichi?? sasa hapa inakuwaje au inakuwagaje?
Mimi nashanga sana! hata kuna rafiki yangu mwanaume alimpa ushauri rafiki yangu wa kike eti ajifanye hampendi bwana wake ili jamaa ampapatikie, mie nikipenda nataka ulimwengu mzima ujue including mhusika
 
Na hii ndio ilitakiwa iwe conclusion ya hii sred. umeipanga vizuri kweli daughter. aiseee! unafanya kazi ya kupanga ratiba za safari za rais nini? lol
imetulia kweli

Haaahaha mbavu zangu jamani kuloro,
Ratiba za raisi ntaziwezea wapi mtu mwenyewe alivyo kiguu na njia ivo,
si ntakuwa nawork overtime kila siku.........
 
man-on-a-leash-5.jpg
cimg0292-1.jpg

...so long as hakutakuwa na kudhalilishana i.e "nimemuweka na amejaa kwenye kiganja!," "hapa amefika hafurukuti!"
nadhani ni muhimu na sahihi kuonyeshana mapenzi kwa vitendo!
 
in an intimate relationship the power lies whith who cares less. unampenda,be kind,play ur part.bt signs of desperation nadhani zinamfanya mwenza akimbie.nadhani nimeona hii,unapompenda mwanaume hadi unaskia kama unapata kichaa,anaanza kuleta maringo.when u almost give up,ana-notice na kuanza kukufukuzia tena.i guess chilling out and take life as it is ndo unaambiwa usimuoneshe.dont go over the roof over petty stuff.what am i saying again,sorry im half asleep,lol!

Si kweli. Most likely, hajakupenda from the beginnning.
 
mapenzi ni kikohozi...huwezi kujificha au kujiigiza...litaonekana wazi au la kuzuga huwezi kujificha
 
Nadhani kwa kupretend utakuwa unajitesa sana!

However, love using head more than your heart, keep a a door open, you may need it one day.....!
 
Back
Top Bottom