Eti akina Dada/Wanawake huwa hawapendani wenyewe kwa wenyewe, ni kweli?

jamani hii kitu kweli......
mie mmoja wapo napenda kuhudumiwa na wahudumu wa kiume.....:) kwa sababu hizi;
huwa nahisi wahudumu wa kike wanakuwa na complications nyingi, labda atakung'ang'aniza ununue kitu japo huna interest (anajaribu kuku convince sana)
pili, naona tabu kumtuma sana mhudumu mwanamke. Nimezowea nikienda madukani ulaya nakaa ktako, natuma tu nipe kiatu kile, nipe nguo kaa ile size fulani, mwanamme anaenda kuniletea (sipendi kumtuma mwanamke naona yupo weak)
na lastly, naweza kum-charm mwanamme akanipa huduma kwa u-smooth zaidi kuliko mwanamke....:) na pia huwa sioni haya kuuliza suala la kipuuzi kuhusu bidhaa kaa mhudumu mwanamme kuliko mwanamke

nb: sio kama nna chuki kwa mwanamke
 
kweli Mtu B,mimi mwenyewe nipo kwenye profession yenye wanaume wengi,hivyo napata shida kukubalika.Lakini hili pia la manyanyaso hata wanaume nao wanatunyanyasa,sijui sometimes wanakuwa na tabia kama hizo za masekretary?

Pole dadangu. Mimi pia nilishawahi kufanya kazi katika ofisi yenye mkurugenzi mkuu (DG) na wakurugenzi wasaidizi 3. Yule DG alikuwa mwanaume, na wale wengine 3 wote ni wanawake. Basi story zilizokuwa zinasambazwa na wanawake wengine pale ni kwamba wale wakurugenzi 3 wote walikuwa hawara za DG, na walipata nafasi hizo kutokana na uhawara huo! Lakini wale wanawake 3 wana elimu kubwa, mmoja ana PhD, wawili wana masters katika fani zao. Lakini wanawake wambea hawakukubali, wakawa wanadai hizo elimu zao wamepata pia kwa kugawa uroda!

Kichekesho ni sasa kimetokea, DG kaondoka kapata dili Ulaya, wamebaki wale wanawake. Ni bifu daily! Yule mmoja anayekaimu yuko radhi kuchukua ushauri wa mwanaume wa cheo cha chini kuliko kuwasikiliza wale mabosi wenzie, maana nao wameanza vikao vya majungu dhidi yake, ni majungu kila mahali! Hapakaliki, kisa ni mwanamke mwenzao kawa DG. Wivu tu, maana siku zote alipokuwepo yule DG mwanaume hatukuwahi kuwasikia mabosi wetu hao (wa kike) wakisengenyana. Sasa wanasengenyana kweupe kwa wahudumu, wafagiaji, madereva, na yeyote anayeweza kusikiliza. Ni aibu tupu!
 
Ukikutana na wenye self esteem hawana muda wa kuchukiana...
Kwa sasa nimezungukwa na watu wenye mapenzi ya kweli...ni muda toka ni feel kushushwa na mwanamke mwenzangu...

tatizo ni kwenda kwenye ofisi za watu au kwa manesi...unakutana na watu wasio wa class yako...na wana tatizo la kutojiamini...

Nina experience ya kuletewa dharau; lakini na wanawake nisowajua nilokutana nao maofisi ya watu...
Lakini hizo hizo ofisi ukifanikiwa kuonana na mkurugenzi wa kike utaona utofauti na kuktana na say secretary au lower level employees wa kike...

Kuna dada mmoja ofisi fulani mkoani alinikwaza sana nikapania kuandika barua kwa RAS wa huo mkoa...ana bahati niliporudi Dar hasira zilikuwa zimeisha...lakini ndio nasema mtu analeta dharau wakati mwingine sababu hakujui
 
Back
Top Bottom