Asije akakudanganya MTU; Wanawake Hawapendani na hawatakuja kupendana

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
ASIJE AKAKUDANGANYA MTU; WANAWAKE HAWAPENDANI NA HAWATAKUJA KUPENDANA.

Anaandika, Robert Heriel
Mwanasaikolojia.

Wanawake wenyewe hili wanalijua fika, wala hawahitaji mtu wa kuwaambia au kuwakumbusha. Kwa sababu kiasili tangu wanazaliwa wanajua Jambo hili fika.

Wanawake kiasili hawaaminiani nafikiri wanajijua zaidi mioyoni mwao vile walivyo. Wanawake hata wakiwa marafiki vipi elewa kuwa urafiki wao niwa machale machale. Ni viumbe ambao wanaishi Kwa kuviziana. Hawaaminiani. Muda wowote wanaweza kubadilikiana na kugeukana Kwa kiwango cha kutisha.

Linapokuja suala la mwanaume hapo ndio kabisa Wanawake kamwe hawawezi kuwa kitu kimoja.

Bado haujanielewa sio? Mimi Taikon ninakuambia Kwa sababu ni Mwanasaikolojia, Mtibeli niliyejaliwa kusoma Akili na tabia za viumbe hasa kiumbe aitwaye Mwanadamu.

Wanawake hata kama hawajuani, elewa kuwa wakikutana wataoneana Wivu tuu. Wivu huo ndio huwafanya wasipendane.
Elewa kuwa kutopendana Kwa Wanawake kunatokana na tabia ya ubinafsi wa asili wa Mwanamke. Mwanamke hataki azidiwe Kwa Jambo lolote zuri na Mwanamke mwenzake. Na akizidiwa hataki kukubali kuwa kazidiwa.
Jambo hili huwafanya wasiheshimiane na wachukiane.

Elewa kuwa, Mwanamke haoni shida kuzidiwa na Mwanaume. Unajua Wanawake kiasili wanajua Sisi wanaume tunawapenda, na wanajua hilo natural. Lakini wanachotaka ni tuwapende zaidi kuliko Wanawake wenzao. Lengo Lao ni kuwakomoa na kuwakalia kooni Wanawake wenzao.

Mwanamke akikutana na Mwanamke mwingine aliyemzidi labda Mwenye shepu, mtoto tako au Sura nzuri, hapo chuki itaanza mara moja. Hilo sio kwamba wanaamua Noop! Inatokea natural. Wivu! Tunaita Wivu wa Kike.

Ukitaka utukanwe na Wanawake basi jaribu kumsifia Mwanamke mwenzao Mbele Yao. Hakika utatukanwa lakini hautachukiwa kivile kama vile huyo Mwanamke atakavyochukiwa na wenzake.

Elewa kuwa, Wanawake wengi hawapendi Wakiona Mwanamke mwenzao anapendwa kuliko wanavyopendwa wao na Waume zao. Yaani wewe umpende Mkeo kuliko utashangaa Wanawake wengine akiwemo Mama yako, dada zako na majirani wakike.

Utasikia, huyu naye kalogwa, hicho kimwanamke ni kichawi Sana, chenyewe sio kizuri alafu kinampelekesha kaka/baba wa Watu.

Wanawake wakiwa maofisini hata wakichekeana usiwaamini, Kwa sababu wenyewe wanajijua kuwa wanachekeana za kinafiki.
Wanawake wenyewe hupenda hata wakiwa viongozi waongoze wanaume Kwa sababu kwao ni rahisi na hakuna competition yoyote na wataheshimiwa na wanaume na wanaamini heshima ya mwanaume kuliko ya Wanawake wenzao.

Wanawake wakienda kwmeye maofisi wanatamani zaidi wahudumiwe na wanaume wenzao kuliko kuhudumiwa na Wanawake wenzao.
Hata mahospitalini Wanawake wengi hupenda kuhudumiwa na Madaktari WA kiume ikiwezekana kuzalishwa na Madaktari WA kiume.
Wanajua mziki wa Wanawake wenzao.

Wanawake wanajua fika kabisa ni rahisi Kupata msaada na kujaliwa na Mwanaume kuliko Wanawake wenzao.

Muonekano wa Mwanamke ni silaha take namba moja awapo popote pale. Wanawake huhukumiana zaidi Kwa mwonekano kuliko Jambo lolote.
Mwanamke akiwa na mwonekano mzuri anajiamini na kuwa na dharau kuliko Mwanamke mwenye kipato. Hasa wakikutana ana Kwa ana.
Mwanamke mzuri hatishwi na Mwanamke asiye na muonekano mzuri hata angekuwa ni Tajiri au kiongozi mkubwa. Ni Kwa sababu Wanawake wanajua Jambo pekee ambalo Sisi wanaume tunalipenda na kulitaka Kutoka kwao ni jinsi wanavyoonekana.

Mwanamke anaweza asimhudumie Mwanamke mwenzake vizuri kisa tuu kamzidi Tako au kisa kavaa kapendeza kumliko.
Au Mwanamke Kwa muonekano wake au mavazi yake dhaifu anaweza kujisikia vibaya akihudumiwa na mhudumu wa kike mrembo, ni lazima atamuona anaringa au anamishauzi.

Elewa kuwa Wanawake wao wanapenda kufanya ujinga na wanapenda Entertainment, yaani uwa-entertain. Wanawake hawathubutu kuleta ujinga Kwa Wanawake wenzao Kwa sababu kamwe hawatavumiliwa.
Mwanamke anakuwa na hofu akiwa Mbele ya Mwanamke mwenzake Kwa sababu hatavumiliwa Kwa vyovyote akileta Makosa ya kijingajinga, hatachekewa, na kamwe hataonewa huruma. Ni ngumu Sana Mwanamke kumuonea huruma Mwanamke mwenzake Kwa Sababu kosa lolote hata kama liwe la bahati Mbaya Mwanamke hulihesabu kama ni umefanya Makusudi na umemdharau au umemchukulia pouwa!

Elewa Mwanamke hataki kuchukuliwa pouwa na Mwanamke mwenzake.

Ni ushindani. Ni vita. Ni mapambano ya Wanawake na kamwe hawawezi kukaa Sawa.

Binti mdogo WA miaka mitatu mpaka Mitano akikuta Wanawake na wanaume wamekaa ni lazima Aende Kwa wanaume Kwa sababu Huko ndio atakuwa na Amani na uwezo wa kufanya utoto na ujingaujinga na wanaume watakavumilia. Lakini Wadada au Wanawake hawatakagi mambo ya kijingajinga.
Kudekeza dekeza ujinga Wanawake hawavumilii Ila wao ndio wanataka wadekezwe.

Kitendo cha Mwanamke kupendeza kuliko Wanawake wenzake kinaweza kumuingiza katika vita kubwa na Wanawake wenzake. Chuki na husda na ikiwezekana kulogana kunaweza kufuatia.

Ukitaka Mkeo akupende na kukusifu basi waponde na watukane Wanawake wengine, Kwa kweli atajisikia Raha mustarehe na kujiona salama. Sema; unajua MKE wangu wewe ni Malaika, yaani sijui ilikuwaje nikakupata, hakika nilibahatisha kuwa na Mtoto mkali kama wewe, umewashinda Wanawake wengine, alafu Wanawake wengine ni kama midoli au katuni Fulani hivi"
Hapo atacheka Mno na asipokupikia chakula kizuri niite Mbwa!

Lakini ukitaka Mkeo aanze chuki za kijinga ndani ya nyumba basi uwe unasifia wengine au kuwaangalia Wanawake wengine, Wanawake wanajua miangalio, kisaikolojia Wanawake wanauwezo WA kusoma Kwa upesi body language ya wanaume na Wanawake wenzao. Utashangaa tuu Mkeo au Mpenzi wako amebadilika.

Hakunaga umoja WA dhati wa Wanawake, hiyo hakunaga. Umoja wowote Wanawake wanauchukulia Kwa tahadhari kubwa. Umoja wa kuviziana.

Wanawake kuibiana wanaume ni Jambo la dakika moja. Lengo Lao ni kukomoana, kushushana hadhi au kumkera Mwanamke mwenzao ikiwezekana kuiharibu familia ya Mwanamke mwenzake. Hili Wanawake wanalijua fika Kwa sababu Wanawake wanajuana.

Wanawake huweza kujitongozesha Kwa mwanaume wa Shoga yake ili kumkata ngebe mwenzake, alafu utasikia; eenhee! Alikuwa anaringa sana, alikuwa anajishaua Sana. Nimemkomesha.

Wanawake hawapendani.
Huko shuleni mabinti hasa wale mabinti Wazuri waliowazidi waalimu wa kike hupata joto la jiwe Kwa madamu wa kike. Maneno ya karaha Kutoka Kwa waalimu wa kike kwenda Kwa Wanafunzi wakike waliowarembo ukiyasikia unaweza Baki mdomo wazi. Ni kama wake wenza.

Acha nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hili silipingi .Kuna sehemu niliwahi fanya kazi ya uwakala kipind cha likizo moja hiv. Sasa nilikuwa nafanya na kischana fulani hivi. Sasa katika huduma ya transactions kina mama au wadada mara mia bora wanikute mimi sio hako kaschana. Yaani wengne bora wadiriki kunisubiri kam sijaenda mbali yaani.
 
Ukweli mtupu.
 
Nyodo
Huduma mbovu
Kutokujali
 
Back
Top Bottom