Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,614
Wanabodi,
Makala ya Leo ya Kwa Maslahi ya Taifa, Inaanza na A Declaration of Interest
  1. Kumezuka huu mtindo wa mtu akisifia jambo lolote kumhusu rais wa JMT, ananyooshewa vidole vya kutafuta uteuzi!. Niliwahi kuendesha darasa la kuwafundisha watu humu jinsi ya kutofautisha wasifiaji wa ukweli na wale wa kujikombakomba na kusaka uteuzi.
  2. Wasifiaji wa ukweli, watasifu kiongozi pale tuu anapofanya mambo mazuri ya ukweli yanayostahili sifa Kwa lengo la kumtia moyo as appreciation and encouragement aendeleze mazuri hayo.
  3. Wasifiaji wa kujikombakomba, wao kazi yao ni moja tuu, kusifu, kulamba, kuimba nyimbo za shangwe, sifa na mapambio, kwa kusifu kila kitu hata yale ya kijinga, wao watasifu tuu kama fanyavyo ma "chawa".
  4. Wasifuji wa ukweli, hawaishii kwenye kusifu tuu, kwa mazuri tuu, bali kukitokea huyo huyo kiongozi waliyemsifu akifanya jambo linalostahili ukosoaji watamkosoa ila ukosoaji huo hufanywa kwa constructive criticism kwa kutumia lugha ya staha. Mtafuta uteuzi kamwe hawezi kukosoa!.
  5. Huu mtandao wa Jamii Forums ulianzishwa enzi za JK, sisi wengine tulimsifu JK kwa mazuri yake, pia tulimkosoa kwa mapungufu yake, bila kutafuta uteuzi wowote. (Riz.1 ni rafiki, wa toka UDSM, ingekuwa ni kutafuta uteuzi, it would have been just a click)
  6. Alipoingia JPM, pia tulimsifu kwa mazuri yake ukiwemo uchapakazi wake na kumkosoa kwa madhaifu yake. Kwa maoni yangu, ukosoaji wa JPM ulimsaidia sana kuliko hata wasifiaji!.
  7. Sasa tuko na Rais Samia, kwa jinsi anavyoupiga mwingi, tutamsifu, ila pia yeye sio malaika.
  8. Hivyo mimi Paskali, naomba ku declare interest, namsifu Rais Samia kwa mazuri yake na wala sitafuti uteuzi wowote, na kumsifu rais Samia sikuanza leo, baada ya yeye kuwa rais wetu, tembelea HAPA! na HAPA!
  9. Tena ni mimi mwaka 2015 nilimtaja Samia Suluhu Hassan kuwa ni miongoni mwa ma best female presidential material HAPA!
  10. Hivyo pongezi zangu mbalimbali kwa Rais Samia, ni pongezi bonafide genuine kama hizi PONGEZI! PONGEZI!, SAMIA TUMAINI JIPYA! SAMIA MPONYAJI!
  11. Ila pia nelewa kuwa Rais Samia ni binadamu, na sio malaika, hivyo anaweza kukosea makosa ya kibinaadamu, sasa hatumsubiri Rais Samia akosee ndio tumkosoe, bali sasa tunamuangazia mwanga zaidi ili asikosee na akikosea pia tunamkosoa humu humu kama hapa jinsi nilivyo mkosoa RAIS SAMIA SIO MALAIKA, NI BINADAMU! na 2025 SIO LAZIMA SAMIA! na JAPO TUMEPANGA 2025 TWENDE NA MWANAMKE, KUNA HII SAUTI!
  12. Hata kwenye utengenezaji wa filamu ya Royal Tour, tangu mwanzo tunaiandaa, tulikosoa kwa kushauri, local producers wa ndani pia tushirikishwe, ili kuvuna utaalamu wa wazungu, na baada ya Mama kutengeneza filamu ya Royal Your kwa lugha ya kizungu kwa ajili ya wazungu, sisi local producers, tumtengenezee Mama "A Tanzanian Tour" kwa kwa lugha ya Kiswahili kwa ajili ya kuhamasisha na kukuza utalii wa ndani.
  13. Kabla ya uzinduzi wa Royal Tour, wengi wameishia kusifu tuu, akina sisi ambao tuko more objective, hatukuishia kusifu tuu bali pia tumekosoa! ROYAL TOUR TUNGE...!
  14. Hivyo msifu mtafuta uteuzi, atasifu tuu, kamwe hawezi kukosoa lolote, msifu ukweli, wa sifa bonafide genuine, atasifu panapostahili sifa na kukosoa panapostahili ukosoaji kwa kutumia constructive criticism.

  1. Screen Shot 2022-06-05 at 1.06.07 AM.png
    Screen Shot 2022-06-05 at 1.06.33 AM.png
    Utangulizi Kama kawaida, leo tana nimepata tena fursa ya kushuka na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" leo nazungumzia kuponywa kwa taifa na trends za kuelekea 2025 za Rais Samia. Rais Samia ameonyesha kwa kauli na matendo, yeye ni mtu wa haki, sio tuu ni muwaza haki, na msema haki bali ni mpenda haki na mtenda haki kukifanya kile anacho kihubiri, yaani by practicing what she is preaching
  2. Kwa haya anayoyasema sasa, na haya anayoyatenda sasa, tunaamini soon Rais Samia ataruhusu mikutano ya vyama vya siasa, ataifanyia marekebisho Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuifanya kuwa tume huru zaidi na shirikishi, na atazifanyia marekebisho sheria kandamizi zinazonyima haki ambazo licha ya kuwa ni sheria batili, kwasababu zinakwenda kinyumbe cha Katiba ya JMT, ubatili huo, bado umechomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!.
  3. Katiba yetu ya 1977 ilitoa uhuru kwa kila Mtanzania mwenye sifa na vigezo, kuwa huru kushiriki kwenye kuunda serikali toka serikali za mitaa hadi serikali kuu kwa sherti moja tuu la Utanzania wake. Hivyo kila Mtanzania ana haki na uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa!.
  4. Katiba hiyo imetoa uhuru wa kila Mtanzania kuwa huru kushiriki uchaguzi kwa kugombea nafasi yoyote na kushiriki kuwachagua viongozi wetu, bila vikwazo vyovyote. Hili ndilo lilikuwa lengo la mtunga katiba.
  5. Baadae kukajitokeza wataalamu fulani wa kufanya "mambo", wakafanya mambo!. Ile haki ya kila Mtanzania kuchagua viongozi Kwa kupiga kura kuwachagua viongozi, kwa uhuru, yenyewe bado ipo na inaendelea kuwepo, lakini haki na uhuru wa Mtanzania yoyote kushiriki kwenye kuunda serikali, yaani haki ya kugombea na kuchaguliwa, haki hii imeondolewa kwa ubatili fulani!.
  6. Japo Rais Samia ameunda timu ya "kikosi kazi" cha kumshauri, kikosi kazi hicho kinaita baadhi tuu ya watu, sijasikia kama sisi wananchi wa kawaida ambao ndio wamiliki wa katiba, pia tuko huru kufika mbele ya kikosi kazi, kuwasilisha mawazo yetu, ila mimi na haya mawazo yangu, nitayaandika na kuyawasilisha,
  7. Kwa vile tayari Rais Samia ameisha onyesha kwa kauli na matendio, yeye sio tuu ni muwaza haki na msema haki, bali mpenda haki na mtenda haki kwa kauli na matendo ya haki kuonekana, tunamuomba atutendee haki Watanzania, kwa kutuondolea ubatili huu wa ajabu kabisa, ndani ya Katiba Yetu!.
  8. Angalizo Bandiko hili, linauzungumzia ubatili fulani kwenye katiba yetu, kwa vile Watanzania wengi ni wavivu wa kusoma vitu vikubwa, virefu, vigumu, wanapenda vitu rahisi rahisi, na mabandiko mafupi mafupi, wale wa type hii, mnaweza kuishia hapa, halafu mkarukia moja Kwa moja kwenye hitimisho. Wale mastory mastory tuendeleeni na Mastori ya Pasco Mayalla.

Manabii wa Uongo, Tutawatambuaje?. Kwa Matendo Yao!. Na Viongozi wa Uongo Pia Tutawatambua kwa Matendo na Sio Kwa Kauli Zao!
Kwa Wakristu, Bwana wetu Yesu Kristu, kabla ya kifo chake, kufufuka kwake na kupaa mbinguni, alituasa kuhusu manabii wa uongo, akasema, “watakuja watu, watanya ishara kwa jina langu, watahubiri na kufanya miujiza kwa jina langu, lakini sii wangu”. Ndipo mmoja katika makutano akauliza, “ kama mtu atafanya ishara zote kwa jina lako na zikatokea, jee tutawatambuaje?”, akimaanisha hao manabii wa uongo.

Bwana Yesu akamjibu “Mtawatambua kwa matendo yao!” . Hili ni neno kubwa sana!. Bwana Yesu alitufundisha jinsi ya kuwatambua watu na kuwatofautisha wale wakweli, na wale wa uongo, fake na original. Huwezi kumtambua mtu mkweli kwa kauli tuu, utamtambua mtu mkweli kwa matendo yake!, hivyo Rais Samia ni mtu mkweli na matendo yake yanasadifu ukweli huu!.
Ulaghai wa Kauli Kwenye Mapenzi
Binadamu amepewa uwezo mkubwa wa kujifanyisha na kwa kutumia kauli. Mahusiano mengi ya mapenzi huanza kwa kauli, “nakupenda”, kwa huku Afrika, kwa kawaida ni mwanamume ndio humuanza mwanamke kwa kumwambia nampenda, ikitokea mwanamke ndio anapenda, sio desturi kwa mwanamke kumfuata mwanamume na kumuanza kwa kumwambia nakupenda, ikitokea ni mwanamke anapenda, anachoweza kufanya ni kujipitisha pitisha ili mwanaume husika amuone, amuanze!, wenzetu wazungu, wao wame advance kidogo, akitokea ni mwanamke anapenda, wao mwanamke huyo analianzisha tuu!.

Kwa vile neno "nakupenda" ni kauli tuu, na mwanamke akiishaambiwa "nakupenda", wengine wakiisha ambiwa tuu wanapendwa, unakuwa umeloga, hapo hapo hufungua mioyo yao na wao kuanza kupenda, hivyo hawezi kujua kama ni anapendwa kweli, ama ametamaniwa tuu na anadanganywa ili mhusika apate anachotaka!. Mwanamke unapotokewa na mwanamume akakuambia “nakupenda”, utamjuaje kama anakupenda kweli, au amekutamani tuu ili akutumie?. Mwanamuziki wa Marekani Whitney Houston, aliwahi kutunga wimbo kuuliza hili swali “How Will I Know” sehemu ya naneno ya wimbo huo ni “How will I know if he really loves me”, akimaanisha nitajuaje kama ni kweli ananipenda kiukweli?. Hili ni jambo gumu kulibaini kwa kauli tuu!.

Swali kwa dada zetu, mtu anapokuibukia na kukumbia anakupenda, utajuaje kama anakupenda kikweli, au anakudanganya tuu?. Jibu la swali hili kupitia yale mafundisho ya Bwana wetu Yesu Kristu , na kwa ndugu zetu Waislamu, nawaombeni msijisikie wazito kupokea mafundisho haya kwa kuyaona kama sio ya imani yenu, hapana, Yesu Kristu huyu wa kwenye Biblia Takatifu, ndiye yule yule Nabii Issa Bin Maryam, wa kwenye Quran Tukufu.

Jibu la kuutambua ukweli kutoka kwenye kauli yoyote, ni utaubaini kwa matendo. Mtu akikuambia nakupenda, ili kumjua kama anakupenda kweli, atambaini kwa matendo yake. Na kwa kulijua hilo, wanaume ma laghai wa mapenzi, baada ya kukuambia anakupenda, hufanya pia ulangai wa matendo kama kukunulia soda na chips kuku, na kukuhonga pesa na tujizawadi ili tuu kuufungua moyo wako na kumpa anachotaka, akiishapata… huyoo ... humuoni tena!.

Ugumu huu wa kuujua ukweli bayana kwa kauli, umewaponza wengi na umewatesa wengi, kujikuta wameingia kwenye mahusiano ya mapenzi, na wengine hadi ndoa zimefungwa, na watoto hadi wamezaliwa, ndipo unakuja kubaini na kumtambua mwezi wako kwa matendo kuwa alikuwa mtu sio!. Kwa wanawake majasiri na mashujaa, baada ya kuutambua ukweli, huomba talaka zao, na kuendelea na maisha yao, lakini kwa walio wengi kutokana na utegemezi wa wanawake, na kwa wengine dini ambazo haziruhusu talaka, huishia kuishi kwenye ndoa za mateso!, lakini laiti wanawake hawa wangejipa muda ya kutosha kutafakari kwa kwa makini, kwa kuyachunguza matendo ya wenzi wao, kabla ya ndoa, wala wasingelikubali kuolewa!.
Ushauri kwa Watoto Wetu wa Kike na Wanawake Wote.
Ushauri kwa watoto wa kike na wanawake wote, mwanamume anapokutokea kukuambia anakupenda, kwanza furahi maana kupendwa raha, ila usimpe jibu la papo kwa hapo, kuwa na wewe unampenda bali mwambie asante kwa kunipenda, nipe muda nijitafakari. Kisha tumia muda wa kutosha kumchunguza, huku ukiushirikisha moyo wako kujiuliza “jee huyu ananipenda kweli, kwa dhati ya moyo wake?”, sauti toka ndani yako, “listening from yourself, the voices from within, itakuambia ukweli”. Futa hicho roho inachokuambia, hutapotea!, hutakosea!.

Kufikia hapa, wengi mnaweza kudhani darasa la “kwa Maslahi ya Taifa” ya leo, ni darasa la mapenzi!. No!. Hili ni darasa kutambua kauli dhabiti hufuatiwa na matendo.

Kama walivyo wanaume malaghai wa mapenzi, hutoa kauli za kilaghai kuwadanganya wenzao ili wapate wanachotaka, ndivyo ilivyo kwa baadhi ya wanasiasa na viongozi malaghai, hutoa kauli na ahadi kemkem za kuombea kura, kumbe ni kauli na ahadi za uongo! , wakiisha chaguliwa, na kupata walichotaka, huwaoni tena!, watakuja kuibuka baada ya miaka 5, ule mwaka wa uchaguzi. Na kuna viongozi ni wahubiri wazuri, good preachers, but they don't practice, what they preach!. Rais Mama Samia is a truth preacher, who practices what she preach!. Hongera sana kwa hili!.

Rais Samia na Kauli za Kweli, Zinazofuatiwa na Matendo.
Rais Samia, baada tuu ya kuapishwa, alitoa kauli njema ya maridhiano na kuliponya taifa “heal the nation”, zile hazikuwa ni kauli tuu, zimefuatiwa na matendo, amefanya matendo mengi makubwa ya kuliponya taifa, amekutana na wapinzani, akiwemo mpinzani machachari sana Tundu Lissu. Tangu Tundu Lissu alipopigwa risasi na kulazwa Nairobi Hospital, kuna watu wakadhani inakatazwa kwenda kumjulia hali na kumpa pole!, lakini kuna watu majasiri, wenye moyo wa huruma na upendo wa kweli, walikwenda kumjulia hali Tundu Lissu hospitalini Nairobi na kumpa pole, bila kugopa watu!.

Rais Samia amezifuta kesi zote ambazo hazikuwa na haki, na nyingine japo ni kesi kweli, ila amezifuta tuu kwa ajili ya maridhiano. Licha ya mahakama kumthibitisha Mbowe ana kesi ya kujibu, lakini DPP akaifuta kesi ya Mbowe, na kwa vile kwa mujibu wa katiba yetu, mtu pekee mwenye uwezo wa kuifuta kesi ni DPP, hivyo wanaojua aliyefuta kesi ya Mbowe ni DPP, endeleeni kujua ni DPP, lakini wenye jicho la ndani, wanamjua aliyefuta kesi ya Mbowe ni nani, na Mbowe mwenyewe anamjua, ndio maana mara tuu baada kuachiliwa kutoka gerezan, kuna mahali alikwenda, wenye jicho hilo tunajua hapo Mbowe alipokwenda baada ya kuachiwa, alikwenda kufanya nini!.
Hitimisho
Jana kwenye mitandao ya kijamii, zimesikika habari, Tundu Lissu amelipwa haki zake zote alizo dhulumiwa, hivyo hapa ni uthibitisho tuu wa matendo ya haki na sio tuu kauli za haki.

Kufuatia matendo haya, naamini kabisa kupitia “kikosi kazi”, soon Samia ataruhusu mikutano ya vyama vya siasa, ataifumua na kuisuka upya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuifanya iwe shirikishi, pia atazifumua sheria kandamizi kuzifanyia marekebisho ili kufanya uchaguzi wa haki kwenye uwanja sawa wa ushindani na sio huu uwanja tenge wa uchaguzi wetu.

Tutunamuomba sana, sana, sana, Rais Mama yetu Samia, atuondolee na huu ubatili fulani ndani ya katiba yetu, uliochomekewa kiubatili, unao zioa haki ya kila Mtanzania kuwa na haki ya kuchaguliwa. Haki hiyo imenyofolewa kwa kuchomekewa kiubatili kipengele batili cha kudhaminiwa na chama na siasa!. Ubatili wenyewe nimeuleza hapa na jinsi ulivyochomekewa kiubatili
KATIBA YETU INA UBATILI, SHERIA YA UCHAGUZI INA UBATILI!. na SHURTI HILI KWENYE KATIBA YETU NI BATILI!

Hivyo mpaka sasa, Rais Samia, ameishathibitisha kwa kauli na matendo, kuwa yeye ni mpenda haki na mtenda haki. Analiponya taifa, hivyo kwa matendo haya ya haki, Rais Samia anayoyafanya, atabarikiwa sana, na taifa litabarikiwa na kupata ustawi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Nimalizie kumshukuru Mungu kwa kutuletea Samia: Ni muwaza haki, msema haki , mpenda haki na mtenda haki!. Soon ataruhusu mikutano ya siasa na kuiunda NEC Shirikishi, jee vipi kuhusu ubatili huu ndani ya Katiba yetu?

Asante Mungu kwa Rais Samia, ni Baraka kwa nchi yetu!, naomba lile jicho, liuone na ubatili huu ndani ya katiba yetu, lituondoshee kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025!.

Mungu Mbariki Rais Samia,
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.
 
Huo ubatilifu haupo kwa bahati mbaya... Ni fimbo ya kudhibiti nidhamu ndani ya vyama, na CCM wanaitumia vizuri sana. Mtu kama SH Amon angeweza kugombea Rungwe kama mgombea binafsi na akashinda.
 
Acha nao mkuu, mbona wao unakuta midume mizima iko humu kumsifu mwanaume mwenzao tena mume wa mtu, kisa tu huyo wanaemsifia ni kiongozi wao wa chama. Je na wao wanataka teuzi za kwenda kufanya kaz za ndani kwa mwenyekiti wao au wanasifia ili mwenyekiti aendelee kuwatumia kwa style ile ile ya kuwageuza chawa na nyumbu wa kisiasa kwa faida yake na familia yake.
 
Wanabodi,

Declaration of Interest
Kumezuka huu mtindo wa mtu yoyote humu, akisifia jambo lolote kumhusu rais wa JMT, ananyooshwa vidole vya kutafuta uteuzi, niliwahi kuwafundisha watu humu...
Ni rais aliye muwazi sana, katika nchi hii tangu imeumbwa hatujawahi na sidhani kama tutakuja kupata rais aliye systematic, anayesikia empathy, sympathy na anayewapenda watu wake kama Rais Samia. Huyu ni rais anayefanya mambo kwa uwazi sana, tunaona maendeleo...Hakuna siri kwenye hilo.
 
Wanabodi,

Declaration of Interest
Kumezuka huu mtindo wa mtu yoyote humu, akisifia jambo lolote kumhusu rais wa JMT, ananyooshwa vidole vya kutafuta uteuzi, niliwahi kuwafundisha watu humu
Pascal Mayalla

Nakusalimu tuu huko ulipo

lkn naomba niweke kumbukumbu kwamba wewe mwenyewe umeshawaikusema umestaafu uandishi wa mabandiko ukasema unaenda kugombea ubunge


sasa hili bandiko lako limetoka wapi
 
Mimi Mkenya hapa, napenda sana kusoma makala yako, huwa very deep, insightful and thought provoking, sema ndugu zako wazembe wa kusoma, comments zao zinaonyesha hawasomi kitu na kuelewa, wanajibu tu moja kwa moja.
 
Pascal Mayalla
Nakusalimu tuu huko ulipo
lkn naomba niweke kumbukumbu kwamba wewe mwenyewe umeshawaikusema umestaafu uandishi wa mabandiko ukasema unaenda kugombea ubunge
sasa hili bandiko lako limetoka wapi
Mkuu kibori nangai , baada ya wale ndugu zetu "wajumbe" kufanya yao!, nilikubalimatokeo na nikatoa taarifa ya kurejea mnipokee na kueleza
Kila kitu hapa!
P
 
Ukweli Raisi amejitahidi sana kwenye swala la haki. Alionekana mtu wa haki tangu hajawa Raisi. Ikumbukwe ndie kiongozi pekee alieweza kumtembelea Tundu lisu akiwa hospitalini Nairobi. Mungu ni mwema akamwinua kuwa kiongozi mkuu wa nchi. Ameweza kutenganisha vizuri Mamlaka makubwa aliyonayo na Ubinadamu. Anaweza tofautiana na wewe kisiasa lakini kwa sababu ya ubinadamu bado mtaendelea kuwa marafiki.

Anastahili kupongezwa na tuna paswa kujifunza kuwa Ubinadamu lazima utangulie mamlaka makubwa katika maisha yetu.
Tusitende mabaya sababu ya madaraka kwani huja na kupita.
 
Neno HAKI limeanza kutamkwa baada ya Mbowe kukutana na Rais na kutangaza walichokubaliana kukihubiri badala ya kuhubiri amani wakati haipo. Hii kuwa ni msema kweli na mtenda haki itajulikana pale mazungumzo Kati yake na Chadema, na CCM yake kama mwenyekiti yatakapokamilika.

Sehemu kubwa ya ulahaghai wa siasa za Tanzania ni ya kitaasisi zaidi(CCM) kuliko mtu kama unavyochukulia.
Hapa CCM kama taasisi ndiyo kivuli cha uovu wote, maana huo ubatili wa kwenye katiba un aousema upo kwa sababu CCM ndiyo ngao yao katika kulinda maslahi yao.

Ni vigumu sana kwa mwanaccm kujitoa katika kibano hiki, ndiyo maana Chadema wakaona ni Meza ya mjadadala na makubaliano ambayo yanaweza Kuwa fanya CCM wakajipindua na hapo Mamlaka ya Rais kama taasisi nayo ikawajibika kwa kile kitakachokuwa kimekubaliwa na pande zote.

Hata hivyo bado tuna tatizo la kimfumo, kwa CCM kuwa Rais ndiye mwenyekiti wa chama. Kuna namna hata chama hakiwezi kuiagiza serikali katika baadhi ya mambo, kwani Mwenyekiti kujiagiza, Rais, na au kujisimamia ni ngumu kibinadamu.
 
Back
Top Bottom