Esoteric: Uhusiano wa Zitto, JK, Salim A.S, Ridhwan, Omar Ilyas & then some Islams?

Status
Not open for further replies.
Hizi takwimu za kweli? Kama za kweli inabidi hii anomaly Zitto aitolee maelezo.

Ze thinker Abduhalim:

Wanasema nchi zilizoundwa na wakoloni na kuunganisha jamii na imani nyingi tofauti, haziendelei. Ingekuwa watanzania wote tuna kabila moja na dini moja, mjadala huu usingekuwepo. Na tungekuwa tunawaza maendeleo. Anyway wacha wengine tuendelee kudunda huku viwanja.
 
1. . Kisiasa hapana.
Kaisha kiri kuwa kisiasa alikosea na Chadema ni chama cha kisiasa

 
Zitto,

Nakubaliana na wewe hapo kwenye BOLD. Ila msimamo wako ungelikuwa wa maana kama Tanzania ingelikuwa inaruhusu mtu kugombea bila chama. Unakuwa Mbunge bila chama na kushirikiana na Vyama vingi na zaidi Chadema. Ukija kwenye mkutano kama huo na kusema hapa na wenzio wakapiga kura na Wengi Wakashinda, basi unaweza kutoka na maneno kama hayo kuwaambia wanachama wako waliokupigia kura. Kwa sasa huwezi kusema wote waliokuchagua, walikuchagua wewe kama Zitto na si Zitto na Chadema.

Watu wengi sasa wanaanza kujenga IMANI na chama chenu. Kama mtaanza kila mtu kuja na msimamo wake, basi mtakiuwa na kukimaliza. Kama ingelikuwa uamuzi wa kiongozi mmoja, hapo ungelikuwa sawa. Ila kama watu walipiga kura na wengi wakashinda na Matokeo hayakuchakachuliwa, mie sioni tatizo maana ndiyo Demokrasi

Kama unakumbuka ugomvi wa Serikali Tatu, Malecela alikuwa upande wa Serikali tatu. Nyerere alipoitwa Dodoma, aliwaambia msimamo wa Serikali na wawaambie nini Wabunge. Malecela aliongea, Mwinyi aliongea na Nyerere aliyekuwa kasubiriwa kwa hamu amalize Mgogoro alikuja na kusema "yote yameongewa na PM Malecela na Rais Mwinyi, mie sina la kuongeza......" Malecela ikaonekana yeye pia ana msimamo wa Serikali yaani Serikali mbili na si tatu kama alivyokuwa akitaka zamani.

Kwenye kipindi hiki kigumu, ukiwa wewe Zitto kama Mwanachadema, tunategemea kukuona ukitetea Wananchi wa Tanzania, kudai katiba mpya, tume huru ya Uchaguzi, Mahakama huru nk. Ukiwa viwanjani, hatutakulaani kama tukiona unagonga Glass na hao Mafisadi. Ila kusikia ukiwasifia na kuwapongeza kwa kufanya mambo kwa kutumia kodi yetu na kazi ambayo wanalipwa hela nyingi tu, kwa kweli ni aibu sana. Huo ndiyo wajibu wao na si kuwa wanachukua hela zao mfukoni.

Kwenye Swala la Udini, mhhhhh hili naweza kukutetea hata mie. Nimesoma habari zako nyingi na kwa hili nina uhakika wa asilimia kubwa sana kuwa huhusiano nalo. Na uendelee hivyo...... Jamaa yako Omar ni MDINI haswaaa na hilo hawezi kujificha. Nimeshamuambia hata yeye moja kwa moja kwenye majadiliano humu JF. Hutetea kila hoja ambayo Muislaam ameshambuliwa. Ukisema fulani Mwizi yeye atakuja na kuandika "tunamshambulia kwa sababu yeye ni Muislaam...." Siku hizi hata kumsoma sitaki.

Kuna mpango wa kujenga kiwanda cha Mawese Kigoma? Nilisoma kwenye maelezo yako juu ya Trip yako huko Asia. Kuna mshikaji wangu mmoja ana nia sana ya kusaidia Kigoma kwenu huko. Yeye anaishi Uholanzi na amekuwa katika kuwasiliana na ndugu, jamaa na Marafiki. Kama utakuwa na nia ya kweli ya kuwasiliana naye ili kuangalia kama mtaweza kuunganisha nguvu kusaidia watu wa kwenu, basi nijulishe kwa PM. Kama una kazi nyingi sana na hutataka kuingia kwenye mzigo mwingine, basi wala usijisumbue na kujiongezea mzigo. Uandike au usiandike PM, hiyo itabaki siri yangu hapa ndani ya JF.

Swadakta.

Nakubaliana na wewe Zitto siamini kama ni mdini, ila huyu Tanzanianjema it is obvious ni al Qaeda fanatic..soma posts zake tu utaona muelekeo wake.
 
Hivyo ndio unavyosema ama unavyoona wewe. Lakini je ndio sababu hasa ya kususia hotuba rasmi ya kufungua bunge ya RAIS HALALI KIKATIBA ambaye ndiye sehemu ya pili ya Bunge hilo na ndiye pekee mwenye kuwezesha ama kudumaza/kukandamiza hoja hiyo? Ukweli ni kuwa it was pure improvised strategy iliyolenga misguided short term political interests za mtu kuliko chama na wala Taifa.....
Hi Omary
Heshima Mbele Mkuu

Mimi nionavyo , ile ilikuwa best way kuonyesha Dunia kwamba " katika uchaguzi uliopita kulikuwa na uchakachuaji mkubwa"
kwani altenative zingine zingekuwa zipi ? ebu tuzichambue chache hapa chini

1 kutoingia bungeni siku hiyo , = Jumuiya ya kimataifa isingejua
2.kugomea vikao vya bunge kabisa= wangewanyima wananchi haki yao na kukwamisha utashi wao
3.kuandamana nchi Zima = damu ingemwagika

4. kuwasilisha hoja binafsi = Chama kushika hatamu, matakwa ya CCM yangelindwa na sio wananchi
5.Kubembeleza CCM isikie na kuka kwa meza 4 discussion hii isingewezekana kwa sababu hizi hapa chini:




Historia inaonyesha kwamba , katika Nchi zinazoendelea , Pale ambapo kutoa haki kunamaanisha kupoteza madaraka au kujenga mazingira ya kuyapoteza siku za usoni ,watawala huwawia vigumu ku-part away/kuhatarisha madaraka yao. Na huo ndo ukweli hata kwa CCM. ifuatayo ni mifano inayoonesha jinsi CCM isivyo sikivu hadi zitumike mbinu mbadala kuwaleta mezani kwa mjadala:
  • Mapendekezo Marehemu Jaji Nyalali (Mzalendo wa kweli)yalipigwa chini kwa kuwa ni hatari kwa madaraka ya CCM, japokuwa Marehemu anaheshimila sana kwa ukweli wake na uadilifu hakuna wa kubisha hili !!!
  • ZNZ mambo hayakufika hapo yalipofika kama sio kwa njia mbadala ambazo hatimae zililazimisha kukaa mezani.
  • Suala la Mgombea Binafisi linapingwa sana na CCM japo mahakama iliruhusu lakini wamefanya Zengwe hadi limekwama, na kinachoogopwa hapa Rais au Mbunge atawajibika direct kwa wananchi c chama , chama kikileta ujinga mladi tu anakubalika na wananchi basi anawamwaga na anaendelea na kazi yake kama kawa yaani " wananchi wanashika hatamu sio chama kama ilivyo sasa" na hili lingekuwepo tungeona CCM ikisambaratika maana sio ya wananchi anymore ni ya kina RA ,MO Dewji, Lowasa + Manji .................................
  • Issue ya SIX ilivyokuwa handled , hakuwa na ustaarabu pale ubabe , kama ni mwanake angepambanishwa sio kupewa kama kiti maalum , hatuma kiti maalum cha Spika
Kwa mifano hiyo hapo juu, inaonyesha CCM can't enter into discussion unless altenative ways used. It is understood , by calming political adverseness in ZNZ , President Kikwete has risen his reputation internationaly and wanted to set his legacy in that , but the brave walkout by CDM MPs marred that repution.To be honest CDM hit the president on the head .As is a case for Kikwete, CCM don't want to portlay herself a dictatorial party before the internation community, na hii itawalazimu kushugulikia NEC na Katiba.
Checki tu kile kitendo kilvyo zua mjadala mkali sasa wa katiba na NEC huru , naaamini bila kufanya vile kusingekuwepo na huu mjadala , maana siku za nyuma ulikuwepo lakini ulikuwa hauna uzito , hivi sasa hata watu wa kuheshimika Tz na makada wa CCM pia wanakubalia haja ya kuwepo Katiba Mpya .

Kile kitendo kinakwenda kutuletea White paper hivi karibuni



HIYO CHADEMA WAMEFANYA SAFI SAAAANA


na kwa sababu hizo juu , Zitto alikosea lakini personaly naamimi kila mtu anafanya makosa hata Nyerere did many , itakuwa Zitto ?
 
Hali hii kwa Zito ilianza kujionesha na kudhihirika pale alipoaanza mkanganyiko wa kutaka kugombea ubunge mara aseme kinondoni, kahama, nk then akarudi kigoma. hii yote ni dalili za usaliti!

zito shame upon you. ..... nina doubt kama ni mzawa halisi!!!
 
Ze thinker Abduhalim:

Wanasema nchi zilizoundwa na wakoloni na kuunganisha jamii na imani nyingi tofauti, haziendelei. Ingekuwa watanzania wote tuna kabila moja na dini moja, mjadala huu usingekuwepo. Na tungekuwa tunawaza maendeleo. Anyway wacha wengine tuendelee kudunda huku viwanja.

Thinker Za10,

Huenda uko sahihi kwamba historia ina mchango wake, lakini binafsi naamini zaidi maendeleo yanatafutwa mkuu, kwanza kwa kuwa na viongozi wene vichwa vilivyotulia na wasio na papara, pupa wala uchu wa mafanikio binafsi, pili kwa wananchi ambao mindset yao pia imekaa 'kimaendeleo'..kusema tu dini au asili moja ni sababu usiende mbali tazama Somalia uione jehenamu live.

Ok, ngoja kwanza niendelee kudandia bandwagon kidogo hapa kabla ya kwenda kupambana na kaubaridi.
 
Bila hata kutumia muda mwingi saaana wa kufikiri nimekuwa sina sababu ya kumuona Zitto kama mwanasiasa bora.

Kilichomuinua ni udhaifu wa Bunge letu na wabunge wetu. Hawasomi na hawawezi kuchangia la maana bungeni. Zitto akaja na juhudi ya shuleni ya kusomea mtihani. Akafanya hivyo na kuchangia kwa nguvu. Baadaye akaamua kutokuwa mwoga na kuonyesha ubishi (arrogance) kwa spika, tukadhani huo ni ushujaa (strength).

Akatolewa nje ya bunge.

Hiyo ikawa sifa ya Zitto. Sikumbuki kama kuna mchango wowote wa maana ambao Zitto aliwahi kuutoa nasi wananchi tukasema, naam, ametufumbua macho. Upi huo? Nasema tena mchango gani huo? Zitto ni lipi zaidi ya kufukuzwa Bungeni?

Hiyo ndo siasa yetu unasifika kwa kazi nzuri kwa skendo na hata kwa upuuzi wako na jina lako linabaki midomoni mwa wa-TZ mpaka mwaka wa uchaguzi. Najua W. Slaa aliyoyafunua Bungeni hata tukayasikia, Zito ni yapi?

Lakini huenda hajui kwamba ktk siasa unafanikiwa pale unapoweza ku-model political intrigue badala ya kuwa na role models. Huwezi kuwa mwanasiasa kama fulani. Never ever! tuna bongo tofauti.

Tumpe moyo aendelee kuamini kwamba anapendwa na familia ya fulani au eti fulani anajali jimbo lake, mwisho wake tutauona.
 
tumekuwa na serkali toka uhuru vlikuwa na brbr km 6 tu za lami. Havkuwa na attention. Mkapata in ten years kaja kgm once and for a day. Hakuwa na a single dev project. Kama mbunge kipindi hcho nimesaidia that attention. We have a road, quality electricity, new port being built, more access to water. Mkapa didnt, mwinyi didnt and nyerere didnt. Huo ndio ukweli. Meza au tema

Zitto, nadhani hapo kwenye red ndo muhimu. Inawezekana imepata attention sababu ya kind of Mbunge aliyepo, siyo sababu JK ni rais. nadhani ungekuwa mbunge kipindi cha Mkapa/Mwinyi/Nyerere na ukaipa pressure Serikali kama ulivyofanya, inawezekana KGM ingepata hiyo attention
 
nafikri ni utoto akikua ataacha! lakini bado mheshimiwa zitto anayo nafasi kutoa utetezi wake kabla watanzania hawajatoa hukumu yao kwa usaliti wake!
 
Nadhani umejiunga JF juzi juzi lakini nitachambua kukusaidia, baada ya JK kuunda timu yake ya kwenda kuchunguza mikataba ya madini ikiongozwa na mzee Bomani, tulichambua hapa tukasema kwamba ile ilikuwa more political motive zaidi ya realistic. Sababu mikataba ilisha tiwa sign na hakuna la maana tume ingefanya. Tukashauri kwamba Bunge linaweza kutunga sheria ya kuwabana au kuwaita viongozi hawa wamadini na kuwaambia option ni mbili either wakubali kujadili kuhusu mikataba hiyo kubadilishwa au bunge litunge sheria za kuwabana. Ile tume ilirudisha majibu na Zitto akasema yawekwe adharani lakini Bomani aliwakilisha majibu kwa JK ambae ameyakalia mpaka leo.

Kwa vile umeonyesha uungwana naomba nikufafanulie swali. Aliyefaidika na mchakato huu wa mjadala ya madini nani kati yake na walalahoi wa Tanzania? Angalizo si mafisadi wa tanzania maana wao walikwisha nufaika, definetly, na sisitiza walalahoi wa tanganyika. Mwenye macho haambiwi ona, mwenye masikio hambiwi tazama, tumieni akili kufikiri na wala sio viungo vingine vya mwili havikumbwa kwa makusudi hayo, atleast kwa wale tunaoamini kwenye uumbaji.
 
umewasemea wengi. Ndicho kinachosumbua watu wengi. Kama imeandikwa itakuwa tu. Waberoya, naona maswali yamekwisha. Narudi library, Mzee Mahathir alinipa ka assigment ka south south cooperation. Kila la kheri katika mjadala.
Punguza kiburi mh.Rais(of your imagination).Hatujaona busara katika majibu yako.Umejibu ki-bongofleva sana,majibu mepesi kwa mambo ya maana.
Trust me or not,you have messed up big tym in this one...
 
I have always known that Zitto is fishy. As street talk Zitto>>the Late Amina C + JK

Hii ni kali kweli kweli nadhani CHADEMA wana macho pamoja masikio ya kuelewa hilo. Isije kulipuliwa mithili ya NCCR ya wakati ule!
Na Mkuu hii ya Zito > Amina Chifupa >what connection is that, defence of interest or what!!!!?

The vision must be followed by the venture. It is not enough to stare up the steps-we must step up the stairs. Vence Havner.
 
Tuendelee: Role model wa Zitto ni Salim A. Salim, rais bora kwake yeye ni Kikwete, MD bora aliyewahi kumsema yeye ni Rashid Idrisa yule wa TANESCO.

Tie, cord, umoja, Urafiki wa Zitto, Ridhwan, Omar Ilyas ni mkubwa sana kuliko maelezo, hili group lililotaka kuipindua serikali ya Kayombo-DARUSO, ili wao wapate madaraka si tu ni la hatari bali la kuangaliwa sana. Ridhwan amekuwa akijitetea sana yeye anataka ku-practise sheria hili hali kutaka uongozi amekuwa akitamani tangu siku nyingi sana.

You can read from his face Zitto is a double dealer....and Chadema better wake up to this fact.................................I do not trust Zitto at, all............................he is a very cheap politician...................Always weakening Chadema........for me it was when he recommended we buy Dowas jalopies that is when I knew the boy is cursed with consumption. excesses.............................Look at his face very carefully and you will understand where I am driving to.........................without mincing words..............
 
does this artical going to build our only poltical part which we hope ndo itakireplace sisiem...? Big NO!!!
Why! because kwa wenye uelewa kama wangu hii artical sio tu inamshambulia Zitto bali vijana wote wa kiislam wenye infuence kwenye hii nchi and this is typical UDINI..!

Me naomba kabisa niseme kwa uwazi kama chadema hakita learn from what happened to CUF before and after year 2000 wanakosea saaana!
hakuna asiyejua kwamba cuf ilikua na element hizi ambazo naamini sio intrest ya viongozi wa chadema but some memberz wa CDM wanajaribu kuziimpliment na hizi ndo zitakazo tuulia chama. Cuf walijaribu sana kumtumia lwakatare kuziba hili na walifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana but wana chadema wananishangaza saana wanapompiga vita bwana Zitto na hili kwa asilimia themanini ni kwa sababu ya dini yake pamoja kweli kijana anamapungufu yake kama binadamu(kupenda sifa) but its nat directly proportion na the way anavyopigwa vita..!

Zitto tunamuhitaji sana katika hiki chama penda tusipende, amekukua na mchango mkubwa na ambaye hauoni labda ni kipofu. Yeye na viongozi wachache wa chadema ambao ni waislam ndo wanafanya tujitetee kwamba hiki chama sio cha kidini. Tukumbuke sisem inaonekana ya kiislam nw caz top leaderz wake majority ni muslim but WHAT IF ZITTO DECIDED TO DROP OUT FROM CHADEMA O FIRED BY CHADEMA THEN AKAANZISHA CAMPAIGN AGAINST CHADEMA KWAMBA NI CHAKIDINI hayatatukumba yale ya cuf ya year2000!

Ukweli ni kwamba kwa tanzania ya sasa hakuna chama chochote kitachoweza kuja kuiongoza hii nchi kikiwa na element za kidini, either agombee uraisi sheikh ama padri ama mchungaji na campaign ziwe makanisani au misikitini hata shinda kamwe.
Tunapomzungumzia zitto tumzungumzie kama zitto na we have to stop kabisa hii tabia ya kumuhusisha na dini yake...! Penda usipende hii itakiuwa chama....!

Naomba kuwakilisha
 
Kwa vile umeonyesha uungwana naomba nikufafanulie swali. Aliyefaidika na mchakato huu wa mjadala ya madini nani kati yake na walalahoi wa Tanzania? Angalizo si mafisadi wa tanzania maana wao walikwisha nufaika, definetly, na sisitiza walalahoi wa tanganyika. Mwenye macho haambiwi ona, mwenye masikio hambiwi tazama, tumieni akili kufikiri na wala sio viungo vingine vya mwili havikumbwa kwa makusudi hayo, atleast kwa wale tunaoamini kwenye uumbaji.

Ni ukweli usio fichika Watanzania wameliwa kwenye swala hili la madini na hakuna lilo au linalo fanyika. BG group wamesign na serikali ya Tanzania umilikuwa asilimia 60 ya Rig tatu za gesi/mafuta huko kusini mwa Tanzania, na serikali ya Tanzania ina own 12%. Na huu ni mkataba mpya ambao umesainiwa mwaka 2010. Tatizo ni kuwa na Bunge ambalo halina nguvu kikatiba.
 
Kwa kuongezea, katika jimbo la Zitto la Kigoma Kaskazini, Dr. Slaa alipata asilimia 30.7 ya kura zilizopigwa dhidi ya asilimia 63.0 za Kikwete; wakati jimbo jirani la Manyovu, ambako hiyo barabara ya lami na kwenyewe imefika, (na huo ndio mradi pekee anaohubiri Zitto), tena ambako mbunge ni wa CCM, Dr. Slaa alipata asilimia 57.8 dhidi ya asilimia 36.6 za Kikwete. Kwa hakika Zitto amempigia kampeni Kikwete. AENDE CCM HARAKA SANA

Duh, makubwa haya!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom