Epuka Mtego huu Jakaya

Nahisi kama akitekeleza ili Mateacher nao watasema Kawambwa asepe.
Usikute asiwaondoe akina MPONDA akiwa na mtazamo huo

Kwani hao akina Mponda wanamtumikia nani?wanaowatumikia ndio hawawataki sasa kwa nini asiwaondoe?
 
Kwanini wizara ya afya tu yenye uongozi mbovu?
Ngoja tuone madaktar watakomaaje hawa majaamaa waondoke.Ngoja tutaona.
 
najaribu kulinganisha madhara ya mgomo wa madaktari uliopita na thamani halisi ya madai yao naona kwamba watu/ndugu zetu waliopoteza maisha yao kutokana na kukosa matibabu mahospitalini ni zaidi ya hicho wanachokidai. Wanatishia kugoma tena ili wananchi waendelee kufa kana kwamba hawakuridhika na vifo vilivyotokea katika mgomo wa awali. Kwa mtu yeyote mwenye kupenda haki na kujali wenzake hawezi kudai haki yake kwa kusababisha vifo vya wengine.
kabla ya kujiunga na hii forum wewe ni kati ya watu walinisisimua sana!kwa hii post ya leo umeitesa sana nafsi yangu!!labda hujajua haswa ni nini madrs wanataka ktk madai yao ya msingi.na declare interest,mimi niko ktk afya!pamoja na maslahi,hoja ya kwanza ya msingi ya madrs ni kufanyika kwa mabadiliko ya msingi kabisa ktk secta ya afya yenye lengo la kuokoa na kuboresha maisha ya watz!nitakupa scenarios ambayo naamini itakusaidia kujua mgomo huu inasababishwa na mdrs kutaka kuokoa maisha ya watu na si vinginevyo!
Mkuu sijui una access kiasi gani na mahospitali yetu,lakini watu wanaokufa kila siku kwa kukosa huduma stahiki kutokana na upungufu wa vifaa ni kubwa kuliko ambavyo mtu yeyote amewahi kusema.aisee wagonjwa wanakufa kwa kukosa vitu kama adranaline,lasix na vitu vidogo sana ingawa wewe huwezi jua.mimi binafsi nimeshatoa pesa yangu mara nyingi sana ktk juhudi ya kuokoa maisha ingawa hata malipo yangu hayaji kwa wakati na kuna wakati unakopa ili kukabiliana na hali harisi.
Hosptali kuu kama muhimbili inafikia mahali haina gloves ,thitre gowns na vinginevyo ni hali ya kawaida kabisa,fikili m/nml,temeke na amana kuna nini.!ct scan muhimbli huwa ni ishu wkt,m/nyamala ndio usahau.
Sasa sijui unalisemeaje na hili juu ya hawa watu wanaokufa kimyakimya bila ya wewe kujua.
Mi nafikili wataz tuache kuamini kauli za ki propaganda hata kwenye mambo ya kitaaluma.mimi na amini mkuu wangu uko uninformed juu ya hali halisi na unatoa maoni yako juu ya yanayotokea ndani ya kabuli na ilhali wewe si maiti.kaka matukio ya op kufanyika na tochi ni mambo ya kawaida sasa.mbaya zaidi waheshimiwa hutoa kauli kama secta ya afya imeimalika,huduma ya mama na mtt ni nzuri ilhali hali ni tofauti kabisa na wakati mwingine ma drs na wana afya wengine kutupiwa lawama.tukikaa kimya ndio watu watakufa zaidi kuliko mgomo ukifanyika tena kwa muda mrefu.lakini pia hivi kuna gharama gani hawa jamaa wakijiuzuru na kuzuia mgomo bdala ya ksbr hao wauwaji kama unavyowaita watimize azma yao ya kuua!?hivi unaweza kumtuma mtt wako apite njia ambayo unajua kuna mmbwa mkali na bado ukasema unampenda mtt wako.!?aisee kujiuzuru kunahitaji masaa mangapi!?embu nijuze wakulaumiwa atakuwa ni nani mgomo ukitokea maana hata serikali imekili madai ya drs ni ya msingi,kwa nini inakuwa vigumu kutekeleza makubaliano!!??kwa maneno mengine wewe hujali ile halaiki ya watu wanaokosa huduma stahiki na kufa hata hapa wakati mimi naandika na ambao walikosa msemaji au ku act kwa vitendo maana kama kwa maandishi imeandikwa sana na ahadi kedekede kutolewa bila utekelezaji kama inavyotokea sasa.mkuu afya ya mtu haihitaji siasa na kama unasukali na ukapiga siasa babu wa samunge atakuponya ukweli utabaki palepale!achana na propaganda na utimize wajibu wako.
 
Rais hawezi kuwaondoa watendaji wake only kwa sababu madokta wanataka, akishamuondoa Nkya na Mponda watataka amuache na mama Salma Kikwete.
Hata huyo kama hawezi mshauri mzee na yeye ni mwalimu piga chini................. abaki na vicheche..............
 
mtu mwenye akili timamu hawezi kushabikia mgomo wa madaktari.mleta mada we ni mchochezi na wala huishi hapa tanzania huathiriki na matokeo ya mgomo wa madaktari.

Mtu mwenye busara hatawaonea huruma madaktari peke yao ambao ndio wanaolipwa pesa nyingi zaidi
katika kada ya utumishi wa uma, kisha akawasahau manesi, mahakimu, mapolisi, waalimu, na wengineo
ambao mishahara yao haifikii hata nusu ya madaktari....kuwasikiliza madaktari peke yao na kuwapuuza watumishi wengine ni sawa kabisa na kukaribisha mgomo mwingine mkubwa nchini ambao utakuwa na madhara makubwa
zaidi... Ni kweli JK anatakiwa awe makini na huu mtego wa madaktari!!!!
 
Kwani hao akina Mponda wanamtumikia nani?wanaowatumikia ndio hawawataki sasa kwa nini asiwaondoe?

Kina Mponda wanampa Rais wakati mgumu bila sababu, pengine kwa kujua hana uwezo wa kuuma mfupa.

Kama Rais angekuwa mkali basi hawa jamaa wala wasingesubiri JK awafukuze.

Enzi zile.... tungewasikia kwenye taarifa ya habari saa 2 usiku wamestaafishwa kwa manufaa ya Umma.
 
Rais hawezi kuwaondoa watendaji wake only kwa sababu madokta wanataka, akishamuondoa Nkya na Mponda watataka amuache na mama Salma Kikwete.

Njaa zenu ndio zinawafanya mumshauri mkweeree vibaya; hamjui kuwa maisha ya binadamu ni tunu toka kwa MUNGU na yeyote anaehusika na kukatisha maisha ya watu kwa uamuziusio kuwa wa busara, atajaa damu ya hao watakaokufa mikononi mwake!! Hiyo ni laana ambayo hakuna sangoma anayeweza kuisafisha milelel. Hopefully Kikwete atafunguka na kuona mwanga.
 
Naamini u mzima, na najua huwa unapita hapa kama baadhi ya watendaji wako wanavyopita kwa majina bandia.

Mgomo wa madraktari ndo ushatangazwa naamini mkuu utaweka siasa na kiburi chako pembeni katika kutatua swala hili, japo ulijaribu kuwatuliza kwa maneno yaliyojaa siasa kwenye hotuba yako ya mwisho wa mwezi amini mkuu haijasaidia kitu, kwani makubaliano ilikuwa ni within a month baadhi ya matatizo yawe yameshatatuliwa, swala la kutangaza kwamba waziri mkuu ndo kapokea faili dakika za mwisho za mwezi huo mliokubaliana ni uthibitisho wa kwamba mliwadanganya madaktari, mlitumia siasa kukubaliana nao huku mkisahau mwezi mmoja ni siku thelathini tuu.

Chief najua wewe ni mbishi na utaacha madaktari wagome kwani wewe huumii kwa lolote, najua utataka kuweka muscle kidogo kwa kutishia kuwafuta kazi, mkuu Stuka maamuzi ya hovyo katika swala hili yatagharimu maisha ya wengi, yataibua migomo toka kada nyingine na amini nalokuhasa itakugharimu mkuu.

Enzi za bora liende zimekwisha, fanya kazi kama ulivyoomba wananchi wakuamini na kukupa madaraka.

Ikulu si mahali pa kupatia visa za kwenda kuzurura nje ya nchi kila kukicha, Ikulu ni nyumba inayokutanisha Pure cream and Think Tanks ya taifa.

Penye nyekundu natofautiana na wewe kidogo waliompa madaraka ni tume ya Taifa ya Uchaguzi na siyo wananchi kama wengi wanavyo dhania.
 
Kazi kweli kweli. Swala la kuwaachisha kazi na kumwacha mke wake mpendwa wapi na wapi?
 
Naunga mkono mgomo wa madaktari kwa asilimia zote. Kama viongozi wabovu hawawezi kuwajibika basi acha damu ya watakaokufa iwatese mioyoni mwao hata kama itakuwa damu yangu maana naweza kuwa mgonjwa wakati wa mgomo.

Napinga kila kukicha viongozi na marafiki na ndugu wa viongozi kwenda nje kwa matibabu na ndicho kinacholeta kiburi kuboresha healthy system ya hapa nyumbani.

Doctors!!! Go go go! We are behind you to support you for the better Tz.

Mungu tubariki sana.
 
Rais hawezi kuwaondoa watendaji wake only kwa sababu madokta wanataka, akishamuondoa Nkya na Mponda watataka amuache na mama Salma Kikwete.

Si lazima kuwafuta kazi(kuwa-fire, sack), wanaweza kumuandikia barua ya kujiuzulu kwa manufaa ya umma na yeye kusema kwa 'kwa shingo upande na kinyongo kikubwa kwani bado ninaamini wanauwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi-nimekubali maombi yao'. Huo utakuwa mwisho wa mjadala na kumpatia mwanya wa kuwapeleka sehemu ingine kama suala ni kulindiana ulaji. Hivyo kuacha precedent kuwa wamejiuzulu na hivyo ni uamuzi wao wenyewe si shinikizo la aliyewateua.
 
Wahadhiri wa chuo kikuu Mlimani mpka leo hii ninavyoandika hapa hawajalipwa mshahara wa mwezi wa pili, duh kweli hii serikali ina hali mbaya.
 
Mtoa maada, la kuvunda halina ubani. Umeona maoni ya mmoja wa "washauri" wake (anajiita maundumula) hapo juu?
Mkuu huyo bwana/bibi anacho kiandika ni propaganda naye anajua hilo, sihamini kuwa hawezi ku link utekelezaji wa makubaliano na uongozi wa wizara, kaamua kukomaa na dai 1 tu la kumwondoa waziri na naibu, kaamua kutojikumbusha makubaliano ya pinda na drs. In short huyu naye ni fisadi ambao huona makosa kama tija mpuuzeni tu. Mimi kama mgonjwa mtarajiwa naunga mkono ma dr. Kugoma.
 
mh rais usikubali kuburuzwa na mtu yoyote..hao ma dr kwani ndo waliokutelia huyo waziri? ukiwakubalia tu next target utakua wewe mwenyewe..hata kama kuna haja ya mabadiliko hekima na busara vitawale na wala sio mashinikizo.
 
Wee Mtu weee, Acha kuwa Fisi anayetamani Mkono wa Binadamu ukatike.

Watu wanaongelea migomo, wee unaongelea mke wa mtu aachwe. Endelea na ndoto zako za alinacha usiku kwa huyo mama Salma na Kikwete ndiyo hamwachi ng'oo. Wachafua mashuka utawajua tu.
Rais hawezi kuwaondoa watendaji wake only kwa sababu madokta wanataka, akishamuondoa Nkya na Mponda watataka amuache na mama Salma Kikwete.
 
Hivi ni nini hasa kinachomfanya Kikwete ashindwe kuwaondoa Nkya na Mponda? Kama ni wazuri sana kwenye utendaji si awahamishie wizara nyingine?

Jibu ni kwamba walimapatia asilimia 10% ambayo alikwisha kutoa kwa Ridhwani afanyie biashara za kununua na kuuza unga aweze kutajirika kama wenzake. Sasa akiwatimua wakidai chao atawalipa na nini wakati kuna Mzigo uliokamatwa na Wazee wa kazi atautoaje? Madaktari walie tu Kama Wabunge walimtaka awafute kazi Ngeleja, Malima , Jairo,Utouh pamoja na Luhanjo akakataa na wasimfanye kitu sembuse hao Madaktari. Lucy na Mponda you can keep your posts Hadi 2015 the Doctors can go to hell tutaleta Madaktari kutoka Cuba. Kuna wakati JK alikwenda Cuba nassikia alitimuliwa mpaka Leo hajasema alifanya kosa gani Mimi ni mdaku tu nassikia yuko Moshi mabwanamiti wanamtoa jasho! Let's wait and see jumatano sio mbali tuone nani zaidi?
 
Naamini u mzima, na najua huwa unapita hapa kama baadhi ya watendaji wako wanavyopita kwa majina bandia.

Mgomo wa madraktari ndo ushatangazwa naamini mkuu utaweka siasa na kiburi chako pembeni katika kutatua swala hili, japo ulijaribu kuwatuliza kwa maneno yaliyojaa siasa kwenye hotuba yako ya mwisho wa mwezi amini mkuu haijasaidia kitu, kwani makubaliano ilikuwa ni within a month baadhi ya matatizo yawe yameshatatuliwa, swala la kutangaza kwamba waziri mkuu ndo kapokea faili dakika za mwisho za mwezi huo mliokubaliana ni uthibitisho wa kwamba mliwadanganya madaktari, mlitumia siasa kukubaliana nao huku mkisahau mwezi mmoja ni siku thelathini tuu.

Chief najua wewe ni mbishi na utaacha madaktari wagome kwani wewe huumii kwa lolote, najua utataka kuweka muscle kidogo kwa kutishia kuwafuta kazi, mkuu Stuka maamuzi ya hovyo katika swala hili yatagharimu maisha ya wengi, yataibua migomo toka kada nyingine na amini nalokuhasa itakugharimu mkuu.

Enzi za bora liende zimekwisha, fanya kazi kama ulivyoomba wananchi wakuamini na kukupa madaraka.

Ikulu si mahali pa kupatia visa za kwenda kuzurura nje ya nchi kila kukicha, Ikulu ni nyumba inayokutanisha Pure cream and Think Tanks ya taifa.

Mkuu hapo unampigia mbuzi jitaa ambae kamwe hatocheza nikimaanisha ni vigumu kuufanyia kazi ushauri wako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom