Epuka Mtego huu Jakaya

Hivi ni nini hasa kinachomfanya Kikwete ashindwe kuwaondoa Nkya na Mponda? Kama ni wazuri sana kwenye utendaji si awahamishie wizara nyingine?
Tatizo ni kiburi kilichopitiliza, umesahau wengi ya wale wanaokataliwa kwenye sanduku la kura yeye huwachagua kuwa wakuu wa mikoa,wilaya au kuwa mabalozi?
 
Wana JF
Nawaomba sana tuboreshe uchangiaji wetu kwenye jukwaa letu hili maana tumepewa uhuru wa kutoa mawazo kwa mujibu wa Katiba yetu.
Maana yangu hasa ni kuheshimu mawazo ya kila mmoja wetu bila kutukana kupitia kwenye jukwaa hili maana linatumiwa na watu wengi kupata habari, aidha kama mawazo ya mwenzetu yanakukwaza ni bora kutumia lugha nzuri au kupenda kupata ufafanuzi juu ya post yake lakini matusi si mazuri.
Nawaomba tuwe waungwana tukosoane, tushauriane, tupeane habari zinazojiri kwa mustakabali wa nchi yetu sote.
Suala la haki za Madaktari ni changamoto kwa Rais wala haitaji kuambiwa moja jumlisha moja ni mbili, yeye atoe maamuzi kulingana na aonavyo. Muda wa kuogopa uliisha enzi za mkoloni wakati huu ni enzi za NGUVU ZAIDI, ARI ZAIDI NA KASI ZAIDI.
JAKAYA FUKUZA HAO MAWAZIRI WASIOWAJIBIKA KTK WIZARA NYETI
.
 
je haiwezekani kampeni za uchaguzi mdogo arumeru ukafanyika kwa kujitolea na hizo fedha zoke zikatumika kulipia madai ya madr,na kununulia madawati ya shule za watoto wetu wa shule za msingi na sekondari jamani mie mimesema tu :flypig:
 
Hainiingii akilini eti kuwawajibisha Mawaziri kunahitaji faili kuletwa kwa Rais mwezi mzima. Nashangaa kuna watu wanatetea maovu ingawa Kamati ya Bunge ilibainisha uozo pamoja na Waziri mkuu mwenyewe. Tufike mahali tuweke ushabiki pembeni, tuangalie maadili na uwajibikaji kwa dhamana tulizonazo. Mh. Rais sasa masikio yetu sote yapo kwako ili utuokoe na jambo hili, tujaribu kuweka siasa pembeni na tuone matunda yake.
 
madai ya madaktari yanafanyiwa kazi na serikali.nyie mnaotaka majibu baada ya siku tatu mjue kuwa utendaji na maamuzi ya nchi sio sawa na maamuzi ya familia ambayo wewe na mkeo mnaamka na kuamua jambo.hili ni suala la kitaifa linahitaji mambo mengi.subira inahitajika

Subira inahitajika hata kwa Mponda na Nkya wanaojua wazi kuwa Madaktari wamewakaataa?!!! very funny!!!
 
Nahisi kama akitekeleza ili Mateacher nao watasema Kawambwa asepe.
Usikute asiwaondoe akina MPONDA akiwa na mtazamo huo
 
Serikali ya Tanzania haiwajibiki kwa wananchi!, ndio maana tunaona mawaziri wengi tu wanaboronga lakini hakuna wakuwawajibisha!!! aliyewateua alifanya hivyo kwa sababu zake tofauti na uwajibikaji wao kwa wananchi!! Hivyo wawezi kuwawajibisha wala wao hawezi kuwajibika kwa sababu si wananchi waliowateua!!!!!
 
Mbona mnatanguliza siasa au mnajua suala hili lina wanasiasa nyuma? manake kiongozi hawezi kufanya siasa kama hajachokzwa na wanasiasa wenzake. Tumabizane wakuu akina nanihii wako na Madaktari, jambo linalomkera Mkuu? Najua ndo zao kutafuta umaarufu.
Wewe endelea tu kutumika mpaka mimacho yote ifumbike. Usipoangalia mwaka huu watakutumia mpaka masaburi. Wewe huoni hatari ya Mgomo wa madaktari? Au wewe na wanao mnatibiwa India?
 
je haiwezekani kampeni za uchaguzi mdogo arumeru ukafanyika kwa kujitolea na hizo fedha zoke zikatumika kulipia madai ya madr,na kununulia madawati ya shule za watoto wetu wa shule za msingi na sekondari jamani mie mimesema tu :flypig:

Bora wewe useme tu wengine wanaropoka,suala la kipaumbele tz hakuna ni vizuri wagome tu kwani kiukweli madai yao ni ya msingi na wakati mwingine ili mabadiliko yapatikane kunahitaji maumivu kidogo ikibidi sana especially ukipata viongozi wabishi na wapuuziaji
 
Kwani Mponda,Na Nkya hawawezi kujiondoa wenyewe,ukweli walishindwa kabisa kuzuia maafa kutokana na kushindwa kufanya maamuzi sahihi,sasa nhi hii imefika mahala wananchi wanaona watadai haki zao kwa namna yeyote ile kwa sababu hakuna anaye jali
Hii serikali ikiruhusu huu mgomo utokee tena ,yatakuwa maajabu mengine ya saba,kwa sababu sioni mantiki kabisa, serikali ipunguze dharau
 
Rais hawezi kuwaondoa watendaji wake only kwa sababu madokta wanataka, akishamuondoa Nkya na Mponda watataka amuache na mama Salma Kikwete.
nasubiri kwa hamu siku ambapo itafika Watanzania tukaambiwa kuna bajeti ya 11 trillion na baada ya mwaka tukaletewa matumizi halisi ya hizo pesa.

....mkuu namaanisha KUWAJIBIKA kwa viapo walivyokula wakati wanaingia hizo ofisi za umma!
 
Najaribu kulinganisha madhara ya mgomo wa madaktari uliopita na thamani halisi ya madai yao naona kwamba watu/ndugu zetu waliopoteza maisha yao kutokana na kukosa matibabu mahospitalini ni zaidi ya hicho wanachokidai. Wanatishia kugoma tena ili wananchi waendelee kufa kana kwamba hawakuridhika na vifo vilivyotokea katika mgomo wa awali. Kwa mtu yeyote mwenye kupenda haki na kujali wenzake hawezi kudai haki yake kwa kusababisha vifo vya wengine.
 
Mtoa maada, la kuvunda halina ubani. Umeona maoni ya mmoja wa "washauri" wake (anajiita maundumula) hapo juu?
Hivi unategemea mtu mwenye upeo finyu kama huyu kuna akili imesalia kichwani kwake!!??


  • user-online.png
    Maundumula

    28th February 2012 15:53
    #1
    JF Senior Expert Member Array


    Join Date : 4th November 2010
    Posts : 1,384
    Rep Power : 546



    icon1.png
    JF na Chadema


    Ndugu Moderator,

    Nina kitu kimoja nashindwa kuelewa vizuri. Mimi naamini JF ni mtandao wa kijamii hivyo unachukua mawazo , fikra za watu wote bila kujali itikadi.

    Sasa kule kwenye siasa kuna mada kama 2 au 3 ambazo zipo Sticky na moja ni yakukusanya maoni ya chadema. Sasa swali je utaratibu wa kufanya mada iwe "STICKY" upoje? ni maombi au?

    Je kama ni maombi, CCM, CUF,NCCR nk nao wanaweza kuanzisha mada pale kwenye jukwaa la siasa mkaifanya iwe sticky?


    user-offline.png
    Invisible

    28th February 2012 20:13
    #7
    Robot Array


    Join Date : 11th February 2006
    Location : Here...!
    Posts : 8,550
    Rep Power : 100000



    [h=2]
    icon1.png
    Re: JF na Chadema[/h]
    Mkuu,

    Thread ilianzishwa na marehemu Regia, matatizo ya wananchi yaloongelewa hayakuwa na vyama; hayailengi CCM wala CHADEMA bali Tanzania.

    Jaribu kuweka kando kidogo imani na itikadi za kisiasa na vyama utaubaini ukweli; title ya thread imekaa vibaya kama walivyosema wengine lakini si neno.​


    Buchanan and Shark like this.

    Ficha Upumbavu wako; Usiifiche Hekima yako!
    24/7 Email SUPPORT: support@jamiiforums.com















 
Nchi inapoingia vitani bila shaka inajua kuwa kuna raia na askari watakaokufa na kujeruhiwa. Aidha inajua kuwa kuna rasilimali zitaharibika. Lakini hufanya uamuzi huo mgumu kwa maslahi ya nchi na TAIFA.

Madaktari wanapoamua kufanya mgomo wanajua kuwa kuna watu wataathirika na kufa! LAKINI WANAFANYA UAMUZI MGUMU WA KUGOMA KWA MASLAHI YA NCHI NA TAIFA.

Madaktari aluta continua kwa maslahi ya nchi na Taifa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom