Ephata Nanyaro ajitosa kugombea uenyekiti BAVICHA Taifa

Mwanza Mageuzi,
unajua kuwa nilikuwa mwenyekiti wa chadema duce. kwa hiyo huo ni ukweli ambao hauwezi kuufuta. pia huyu anayesema nikafundishe,ana mawazo ya ki ccm kuambia watu waache siasa.aibu hii.

wewe ni pmbpimbi tu ....mamaamina wewe....wewe hata hutakiwi CDM..Unachukiwa na kila mtu...kunakostahili wewe ni Jehanam...CCM na washirika wake...sikupendiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Tatizo la chama chetu, busara na hekima za viongozi wetu haziambukizi wanachama wetu.baadhi ya vijana ni aibu tu kama wanywa viroba. sasa ujinga wenu unaanza kuwavutia wapinzani wetu kwenye ccm na vyama vingine kuharibu central theme.
tumaini langu ni kuwa viongozi wetu siyo walevi kama hawa vijana.so kama wanaona kuna mantiki,wataconsider.

Chama chenu? my foot ...chama chako na nani? CDM haiwezi kuwa na wanachama kama wewe...kundi lako ni la kina mchange and Co...Chama chako ni CCM na ACT mamaamina wewe
 
Mwanza Mageuzi,
unajua kuwa nilikuwa mwenyekiti wa chadema duce. kwa hiyo huo ni ukweli ambao hauwezi kuufuta. pia huyu anayesema nikafundishe,ana mawazo ya ki ccm kuambia watu waache siasa.aibu hii.
Halafu ukaanza usaliti, ukaomba kitendea kazi kwa mwigulu akakupa, ukatekeleza kazi ya Mwigulu.


Hivi ukisikiliza Mwigulu anavyojigamba namna alivyokutumia unajisikiaje?
 
Last edited by a moderator:
Wakuu,
Natoa ushauri mwingine kwa chama changu kwa nia njema ili tuvuke salama.

Nanyaro nimemfahamu kitambo,amekuwa nguzo muhimu CHADEMA Arusha kuliko hata Godbless Lema. Ni muaminifu na mtiifu sana kwa chama. Kama CHADEMA inataka baraza hili litende kama CHADEMA yenyewe,basi Nanyaro anafaa.

Uongozi wa Heche umekuwepo kuwepo tu. Ilitarajiwa maana ilijulikana awali hana uwezo bali wagombea wenziye akina Ben Saanane walikuwa wasaliti. Nilitahadharisha siku zile kuhusu Shonza, lkn baada ya Gwakisa Nyamsendo kutoroka ukumbini tukakosa namna ya kumkataa Shonza.

John Shibuda aliingilia sana uchaguzi ule akiwatumia Saanane na Shonza baadaye Shonza alionesha uharamia wake.Leo yuko kwao CCM, Saanane hatujui bado kilichomfanya ageuke masalia wenzie,bado tunamfuatilia.

Heche anataka kumpa zawadi ya uenyekiti rafiki yake Daniel. Uongozi wawe macho sana this time.Daniel haaminiki.Hoja kwamba Nanyaro anatokea Kaskazini haina mashiko kwani ni propaganda za CCM.

Nadhani hili nalo uongozi utaliangalia.

Ludovick

Upo ACT, halafu bado unaifuatilia CHADEMA, kweli wewe kamanda wa poyoyo
 
Halafu ukaanza usaliti, ukaomba kitendea kazi kwa mwigulu akakupa, ukatekeleza kazi ya Mwigulu.


Hivi ukisikiliza Mwigulu anavyojigamba namna alivyokutumia unajisikiaje?

Joseph Ludovick ni mnyama wa hatari kwa afya ya binadamu..... anabweka, he is half donkey, half snake
 
Last edited by a moderator:
MAELEZO YA MGOMBEA WA BAVICHA TAIFA FRANCIS BONIFACE MARWA

UTANGULIZI

Ndugu zangu watanzania, awali ya yote niwashukuru sana, ninyi nyote mtakaobahatika kukutana na huu ujumbe wangu mahususi ndani ya mitandao hii ya Kijamii, magazetini ama kupitia chombo kingine chochote kile cha habari ambacho nitaweza kumudu gharama zake ili kuifanikisha azma hii ya kuwafikishieni ujumbe wangu, juu ya nini hasa kimenisukuma kuingia katika kinyang'anyiro hiki cha kuiwania nafasi ya "Mratibu wa Hamasa" BAVICHA ngazi ya Taifa.

Natambua macho yote ya watanzania ndani ya mipaka ya Taifa letu, yameelekezwa kwenye chaguzi za Chama chetu zinazoendelea Nchini kote hivi sasa, ama wapo wanaozitakia mema, na wapo wanaozitakia shari, ili kesho wapate jambo la kuupotoshea umma, kupitia majukwaani, na vijiwe vyao vya kahawa, uji, Draft na Pool table.

Kutokana na hayo yote, na mengine mengi zaidi, ndio sababu wengi wetu hususani sisi vijana, tumechukua maamuzi magumu ya kuomba nafasi za uongozi ndani ya Taasisi hii pendwa kuliko zote Nchini, ili tupate fursa za kuitetea na kuilinda kama mboni ya Jicho.

Baraza letu la Vijana (BAVICHA), ni moyo wa Chama hiki, na hii ndio sababu, upo ulazima wa kuijenga na kuiimarisha BAVICHA na iwe imara, yenye misimamo isiyoyumbishwa na dola, tena yenye maamuzi magumu kwa maslahi ya Chama na wazalendo wa Taifa hili kwa ujumla wao, ambao ndio walipa kodi.

NIMEFANYA NINI NDANI YA CHAMA

Nimeichukua rasmi Kadi ya Chama mwaka 2001 huko kwetu Serengeti Mara, mwishoni mwa mwaka 2009 kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa nikiwa Shuleni Kidato cha Pili, nikachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa Chama ndani ya Kata yangu. Baada ya kukabidhiwa majukumu hayo ya kuibeba dhamana ya Chama, licha ya kwamba nilikuwa Shuleni, nilijituma kadri ya uwezo wangu kukijenga na kukieneza Chama ndani na nje ya kata yetu, kupitia michezo ya Shule za Sekondari, kwa kukutana na watu Sokoni, minadani na hata pia kupitia Vikundi rika vya Maendeleo huko vijijini, ambavyo huko kwetu Mara tunaviita "Saiga".

Uchaguzi ulipotangazwa rasmi, tukawaandaa wagombea wetu, na tukaingia msituni kupambana, baada ya uchaguzi, tukashinda wenyeviti wawili wa vitongoji kati ya watatu waliopo kijijini kwetu, cha kushangaza, CCM wakashinda nafasi moja ya kitongoji, ila wakamtangaza Mwenyekiti wa Kijiji kigumashi, jambo lililonikera sana, haijawahi kunitokea.

Baada ya uchaguzi huo wa Serikali za mitaa, ikafata zamu ya uchaguzi wa Serikali Kuu, madiwani, wabunge na Rais. Hapa sasa, ilikuwa ni patashika nguo kuchanika, kwa kuwa walitunyang'anya nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji kwa mabavu, ikabidi tuwaandae vijana wenzetu kuhusu namna ya kukabilisna na uchaguzi Mkuu uliokuwa mbele yetu ili kuhakikisha kwamba Diwani wetu wa CHADEMA anashinda nafasi hiyo.

Licha ya kwamba ilikuwa ndio mara yetu ya kwanza kuwasimamisha wagombea wa CHADEMA ndani ya Kata yetu na Jimboni kwetu tangu Nchi ipate uhuru, lakini nadhibitisha hili hadharani kwamba, Kata yetu ya Nyansurura ambayo mimi ndiye Kiongozi wa Chama mwenye dhamana ya Uenezi, ni miongoni mwa Kata 6 pekee zinazoongozwa na CHADEMA kati ya Kata 28 za Jimbo la Serengeti huko Mkoani Mara.

Jimboni kwetu (Serengeti) nako pamoja na kwamba ndio uliokuwa mwanzo wa kumsimamisha mgombea wa CHADEMA kwa nafasi ya Ubunge, nilikuwa miongoni mwa vijana walioshiriki kikamilifu katika kumpambania mgombea wetu, mpaka hatua ya mwisho. Nafarijika sana kutamka kuwa, pamoja na masahibu mengi tuliyokumbana nayo katika kipindi chote cha uchaguzi, tulifanikiwa kupata kura 19,700 ambazo ni sawa na 41% ya kura zote, ili hali mgombea wa CCM akatangazwa kigumashi kwa 54% ya kura zote, huku mwenzetu wa CUF akipata 5% ya kura zote.

Licha ya kwamba mpaka leo hii sikuwahi kukata au kukatishwa tamaa na mtu yeyote yule, lakini nimeendelea kuwa mwaminifu, mtiifu, mwadilifu, mjukumikaji katika shughuli zote za kichama popote pale zinapotokea ndani ya mipaka ya Nchi yetu, na hata wakati mwingine nimeendelea kuwa msiri sana kwenye mambo muhimu na nyeti ya Chama chetu, tena mambo yanayohitaji vikao maalumu vya Chama ili kuyazungumza, ili kuilinda heshima na hadhi ya Chama chetu, maana ninaamini kuwa wasakatonge watabana sana ila mwisho wao utakapofika wataachia.

Nje ya Jimbo na Katani kwetu, nimekuwa miongoni mwa vijana wenye nia na moyo wa dhati katika kukipigania Chama masaa 24. Ninaendelea kushiriki harakati zote za kukijenga na kukieneza Chama hiki, kila ninapokutana na harakati hizi ndani ya Nchi yetu.

Ninaendelea kushiriki Mikutano mbalimbali ya kukijenga Chama, nimekuwa nikishiriki katika midahalo, matamasha na makongamano mbalimbali yaliyofanyika Nchini kwa ajili ya kutoa elimu kwa watanzania, juu ya mchakato wa Katiba mpya unaoendelea Nchini hivi sasa, mchakato ambao Chama changu ni miongoni mwa Taasisi zinazoitetea Rasmu ya Tume ya Jaji Warioba, yenye maoni ya wananchi yaliyokusanywa kwa mujibu wa Sheria.

Nitaendelea kukitetea, kukijenga na kukilinda Chama hiki kama Mboni ya Jicho, popote nitakapokuwa, iwe ndani au nje ya mipaka ya Nchi yetu.

NITAFANYA NINI NDANI YA BAVICHA TAIFA NA CHAMA KWA UJUMLA

Sote tunatambua kuwa, CHADEMA bila Mabaraza haya ya BAVICHA, BAWACHA na WAZEE tena yaliyo imara, ni sawa na Bunge la Katiba bila Tundu Lissu, Halima Mdee na Jussa Ladhu wa Zanzibar.

Kwa kushirikiana na Viongozi wenzangu wa Baraza na Chama kwa ujumla, tutakwenda kuangalia namna bora ya kukitafutia wigo mpana kitengo hiki cha hamasa Nchini, ili huduma iweze kuwafikia walengwa kwa haraka na wepesi zaidi, tofauti na ilivyo sasa kwa mfano kwamba, mtu wa Uhamasishaji aliyeko Makao Makuu ya BAVICHA Taifa, ndiye atakayefika Songea, Pemba, Mwanza, Tabora, Lindi au Tarime, ndipo huduma ya hamasa iwafikie wananchi wa eneo hilo husika.

Hapa namaanisha nini, namaanisha kwamba, kwenye kitengo hiki cha hamasa ndani ya BAVICHA Taifa, tutafanya ugatuaji wa madaraka kutoka Makao Makuu ya Baraza na kukasimisha mamlaka hayo katika ngazi zote za uongozi wa Chama, kuanzia Taifa, Kanda, Mikoani, ndani ya Wilaya/Majimbo, Kata/Shehia, Matawi na Misingi.

Utaratibu huu mpya nitakaokwenda kuuanzisha,utafanikiwa kwa kutoa elimu kwa watu maalumu watakaoteuliwa na wataalamu wa mafunzo ya Chama kwa kushirikiana na Baraza, ili kusudi, baada ya wao kupata mafunzo hayo kutoka kwa wataalamu wa mafunzo wa Makao Makuu ya Chama, nao watapelekwa kwenye Kanda.

Baada ya watu wa Kanda kupata mafunzo hayo ya Uhamasishaji, nao watapelekwa Mikoani, ili kusaidia kutoa elimu kwa watu wa Wilaya/Majimbo, nao watu hawa wataipeleka elimu hii ya hamasa kwa watu wa Kata zao, na hawa wa Kata watakwenda kutoa elimu ngazi ya Matawi na hawa wa Matawi nao, watatusaidia kuipeleka elimu hii ya hamasa kwa watu wa ngazi ya msingi.

Ndugu zangu watanzania, yapo mengi naamini kwa kushirikiana nanyi, naamini nitayafanya, ila kikubwa zaidi, natambua ni uaminifu, uwazi, uwajibikaji, uadilifu, heshima na utii wa kanuni na taratibu za Chama chetu, zilizoainishwa katika Katiba yetu ya Chama.

Nihitimishe kwa kuwatakia kila la kheri ninyi nyote mnaoendelea na chaguzi za ndani ya Chama, sio tu kwa wale wa ngazi za Wilaya/Majimbo, hata pia ninyi wa chaguzi za ngazi za Mikoa.

Ahsanteni sana!!!

Francis Boniface Marwa, Mgombea wa nafasi ya Mratibu wa Hamasa BAVICHA Taifa 2014. 0785881009/0767881009 01/09/2014. *****************

Aluta Continueeee........
 
Msichagulie wana CDM viongozi nyie toeni sifa za kila mgombea wapiga kura wataamua!
 
WAJUMBE WA MKUTANO MKUU
BAVICHA TAIFA 2014

Na;
Francis Boniface Marwa,
Mgombea wa nafasi ya
Mratibu wa Hamasa
BAVICHA Taifa

Awali ya yote, kwenu ninyi Waislam Asalaam Aleikum, hata pia kwenu ninyi Wakristo Bwana Yesu Asifiwe.

Poleni sana kwa maandalizi na hekaheka mlizonazo hivi sasa huko Mikoani zenye lengo la kuifanikisha Safari ya kwenda Dar Es Salaam kwa ajili ya kujumuika nasi pamoja katika tukio hili la kipekee na adimu sana linalotokea kila baada ya miaka mitano, tena miaka mitano ambayo ndani yake wanakuwemo washiriki wapya ama hata kwa kutegemea mapenzi yake mola, ni dhahiri wapo wanaoikosa fursa hii kutokana na kutangulia mbele ya haki ili kupumzika ahela, tukio ambalo ni la kuiandika historia ya Baraza letu na Chama kwa ujumla.

Kwa kuyasema hayo, nachukua fursa hii kwa niaba yenu nyote mliopo ndani ya Taasisi hii pendwa, ili kuwakumbuka mashujaa wetu wa Soweto Jijini Arusha, Mwandishi wetu Daudi Mwangosi kule Nyololo Iringa na wenzetu wote waliopoteza uhai wao kwa kuipigania, kuijenga, kuitetea na kuilinda CHADEMA kama Mboni ya Jicho.

Hata pia katika Siku hii ya kipekee tunayokwenda kujumuika pamoja, tunawiwa na roho ya huzuni na huruma kuu, kuwapeni pole na kuwatia moyo wa ushujaa ninyi nyote mliopata ulemavu wa maisha wakati wa harakati za kukipigania Chama hiki.

Baada ya maneno hayo machache yaliyogusa mioyo yetu, nipende kuzungumzia mambo mawili kama sio matatu kulingana na kadri nitakavyoweza,

Kwanza, kila mmoja wetu popote pale alipo, ambaye ni sehemu ya wapigakura ndani ya chaguzi hizi za Kitaifa ndani ya Chama, sio ndani ya Mabaraza ya Wazee, Bavicha na Bawacha au Chama kwa ujumla, unapaswa kutambua kuwa, tayari unayo dhamana kubwa ya kuifanya CHADEMA iwe Chama dola ndani ya Chaguzi zijazo, hata pia wewe unayo dhamana ya kuidhoofisha CHADEMA kutokana na Kura yako moja utakayoipiga Siku ya uchaguzi, pengine kwa kutofanya analysis nzuri kwa wagombea ama kwa kutoutambua umuhimu wako katika kuibadili CHADEMA ili iwe na Taswira ya utaifa na yenye nguvu.

Pili, tunapokwenda kupiga kura ili kuwapa ridhaa viongozi wa kuliongoza Baraza letu la Vijana, upo ulazima sana wa kutambua kuwa, tutalazimika kuwapa ridhaa watu mahili na wachapakazi watakaotuvusha katika kipindi hiki kigumu cha Chaguzi za Kitaifa ndani ya Serikali.

Watu hawa, upo ulazima wa kuijua historia yao katika utendaji kazi, tena utendaji kazi wenye u-serious ndani yake katika kukijenga, kukipigania, kukitangaza na kukilinda Chama hiki.

Hapa pia ni lazima tuwapime wagombea hawa, juu ya nini walichokifanya ndani ya maeneo wanayotokea, sio ngazi ya msingi, Tawi, Kata hata Jimbo pia.
Kwa sababu unaweza unajikuta unamchagua mtu kisa anaonekana kwenye magazeti na runingani kila wakati, na ukipima utendaji wake kiundani zaidi, wazi unagundua kwamba ni kutafuta umaarufu bila utendaji wenye maslahi kwenye Taasisi yetu.

Tunahitaji kuwa makini
sana ili tusije tukafanya kosa la kuwapoteza watu muhimu ndani Chama, wanaoonekana kukipigania Chama usiku na mchana tena kwa nguvu Kazi na rasrimali zao, kisha tukazuzuliwa na mtu, eti kisa ana kitambi kikubwa, ana gari/magari ya kifahari, ana fedha nyingi, anaonekana magazetini na runingani n.k.

Hakika hakuna kosa baya ambalo tunaweza kulijutia, endapo tutasahau jukumu lililoko mbele yetu, na kuwapa watu ridhaa kwa kigezo cha ukwasi wa fedha na magari, au kuonekana magazetini na runingani, bila kumpima mtu kutokana na matendo yake ndani ya Chama.
Kiuhalisia, kuna watu mpaka hivi sasa ni wagombea ndani ya Chama, lakini ni dhahiri pasi na shaka kuwa wamekaa tenge, nadhani mnanielewa vizuri.

Wapambanaji, huu ni wakati muhimu sana kwetu, kuhakikisha kwamba tunaendelea ku-scan virus zote zenye chembe chembe za unafiki na usaliti ndani ya Chama, ili Chama kiendelee kukua, kuimaarika na kibakie salama na chenye nguvu.

Ndugu zangu,
nimeyasema haya kwa sababu natambua kuna mamillioni kwa mamillioni ya wazalendo wa Taifa hili, waliopanga foleni na misururu nyuma ya migongo yetu, wakiomba msaada wa kufunguliwa pingu na minyororo waliyofungwa kwa hila, uongo na unafiki wa CCM na vibaraka wao TLP, UDP na hao viroboto wanaojiita ACT.

Taifa letu kwa hatua lilipofikia
hivi sasa, wanahitajika watu wenye misimamo isiyoyumbishwa na watawala, watu wasio na chembe chembe za unafiki na usaliti kama tunavyoona kwa baadhi ya wenzetu tulionao ndani ya Taasisi, tena watu ambao tulijitoa mhanga kuwapigania ili wapate fursa za kuendelea kukijenga Chama hiki, lakini wamejisahau baada ya kupata fursa hizo, cha ajabu, baadhi yao tena wanaomba fursa ya kuchaguliwa tena katika nafasi zingine, licha ya kwamba wanatambua kuwa hawajafanya lolote ndani ya Taasisi hii, unafiki wa namna hii, huwa naufananisha na dharau iliyopita kiasi, na ifike mahala, tuseme hapana kidemokrasia.

Mwisho niwashukuru sana,
wale wote mliokilea na kukilinda Chama hiki kama mtoto mchanga, hususani pale tulipokumbana na upepo mkali wa dhoruba, hakika mlisimama kidete, na hakuna aliyedhubutu kutetereka, isipokuwa baada ya upepo ule mbaya uliokuwa na vumbi jingi kupita, naona mlijipangusa nyuso zenu uli kuondoa vumbi machoni, na tukaendelea na Safari ya kuitafuta Nchi yetu ya ahadi.

Niishukuru Kamati tendaji ya BAVICHA Taifa kwa nzuri na ya mfani wa kuigwa iliyofanya kwa kipindi hicho chote mpaka leo.
Tunaamini kwa wale tutakaobahatika kuwapokea mikoba yenu kwa ridhaa ya wajumbe wa Mkutano Mkuu, hakika tunaendeleza jahazi hili kwa kuanza na hapa mlipofia leo.

Tunawaahidi hatutawaangusha, bali tutaendelea kuwajaza matumaini ya ukombozi ulioko mbele yetu kwa vitendo bila kumung'unya maneno na wala hatutakuwa na muda wa kuwaonea haya wale wote watakaokuwa na malengo ya kutaka kukidhuru Chama hiki.

Francis Boniface Marwa,
Mgombea
Mratibu wa Hamasa
BAVICHA Taifa
0785881009/0767881009
04/09/2014.
*******************

Ahsanteni sana!
 
Baada ya Chaguzi za Baraza la Wazee ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ngazi ya Taifa hapo jana, utafuata Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na kisha Baraza la Wanawake (BAWACHA) na kuhitimishwa na Uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa mwezi huu wa Septemba.

DSCN5598.JPG
Ephata Nayaro (pichani juu) ni mmoja wa wagombea wa Nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa. Ana nia na Dhamira ya Kushinda Nafasi hiyo ili kulifanya Baraza la Vijana kuwa la manufaa zaidi. Anasababu nami nazikubali.. Anauwezo na amethibitisha hilo kwa vitendo.

Akiwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha Mjini na Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Arusha ameweza kuongoza chama kuimarika na kuwa eneo la kuogopwa na CCM. Bila kusahau kuwa ni Uongozi wa Nanyaro Jijini Arusha ndio ulifanikiwa kutetea Kata nne zote za waliokuwa madiwani wakafukuzwa uanachama na pia kuchukua Kata mbili zikizokuwa za CCM! Kwa ufupi ni mafanikio makubwa sana chini ya Uongozi wake. Namkubali. anafaa, anaweza na anastahili kuongoza BAVICHA mpya kwa mafanikio zaidi!

Nikushirikishe hapa mengine usiyoyajua kuhusu Ephata Nanyaro.
********************
SAM_6003.JPG
SIFA BINAFSI
-Ephata Nanyaro amezaliwa tarehe 27.11.1984
-Ana mke mmoja na watoto wawili.
-Elimu yake ni ya Shahada ya kwanza.
-Ni mcha Mungu
- Ana Certificate ya Campaign for Change

UZOEFU WA KIUONGOZI NDANI YA CHAMA
-Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Arusha (2009-2014)
-Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Arusha Mjini(2011-2014)
-Diwani wa Kata ya Levolosi Arusha Mjini (2010 hadi sasa kuelekea 2015)
-Mbunifu wa Siasa ya Uchumi kwa Viajana wa Chadema Jijini Arusha kwa kuasisi VIPATU (Vijana Kwa Pamoja Tunaweza)
- Taasisi ya vijana ambayo imeinua vijana wengi kiuchumi mkoa wa Arusha.

KWA NINI ANAFAA KUWA MWENYEKITI BAVICHA TAIFA
10625061_542533232515569_1989449309245340711_n.jpg
1.Uwezo wa Kiuongozi
Amekiongoza Chama Wilaya ya Arusha Mjini kwa mafanikio makubwa sana. Katika kipindi cha uongozi wake Chadema ilifanikiwa kushinda chaguzi zote ndogo, na kuongeza Kata za Sombetini na Daraja mbili ambazo awali zilikuwa zinaongozwa na CCM, pia kuzitetea Kata nne za Kimandolu, Kalolei, Themi, na Elerai ambazo madiwani wake walifukuzwa kwa kukosa ndiahmu kwenye chma.

Aimewatumikia wanawanchi wake wa Kata ya Levolosi kwa uaminifu na uwezo mkubwa,ambapo ameweza kutekeleza ahadi kwa wastani wa 80% hadi sasa.

2.Ubunifu
Amebuni miradi mbalimbali ya BAVICHA Mkoa wa Arusha, yenye malengo ya
(a)Kuboresha na kuinua maisha ya vijana kiuchumi
(b)Kukifanya chama kuwa relevant kwa wananchi wengi. Chini ya mpango huu alianzisha VIPATU(Vijana Pamoja Tunaweza)

3.Oganizesheni imara ya BAVICHA
Kwa kuwa malengo makuu ya chama ni kuchukua DOLA,na BAVICHA ina jukumu kubwa la Kuhakikisha malengo makuu ya chama yanafikiwa.

Hivyo tunahitaji kujenga oganaizesheni imara ya BAVICHA kutoka chini hadi juu.BAVICHA itakayokuwa mhimili mkuu wa CHAMA katika kufikia malengo,hili tutalijenga katika misingi ya Uadilifu,Uwajibikaji,Uwazi,Utu na Ujasi ri mkubwa sana

Kwa heshima sana anaomba KURA kwa vijana wenzake, wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa BAVICHA, na wasio wajumbe annawaomba sana mumuunge mkono katika kuwatumikia vijana.

Hakika ukimchagua Nanyaro hutoijutia kura yako.
View attachment 183457
CHAGUA NANYARO BAVICHA 2014-2019

Malengo na dira yake katika kuliongoza baraza la vijana wa CHADEMA (BAVICHA) yanampambanua yeye kama mgombea pakee mwenye mikakati thabiti ambayo ikimpata msimamizi, BAVICHA itaonekana katika sura mpya hasa wakati huu ambao CHADEMA ni chama kinachosubiri kuongoza DOLA.

Dhamira ya Nanyaro ni kuhakikisha mipango kazi yote inayoandaliwa na baraza la vijana Taifa inaanzia kwanza kwenye ngazi ya MATAWI na MISINGI kwakuwa huko ndiko wanachama waliko.

-Kuhakikisha vijana wanajitegemea kiuchumi, kwa kuanzisha fursa za uchumi kama kuwekeza katika kilimo, viwanda vidogo na ufundi, na kupunguza vijana kutumiwa na wazee kwa malengo yao ya kisiasa.
-Kuhakikisha Bavicha inakuwa taaisis inajiyotegemea kiuchumi na kifikra bila kutegemea ufadhili toka chama, hii itawezesha baraza kujitegemea kimajukumu na kufanikisha malengo yake yote na kufanya kazi zake kwa uhuru.
-Ni BAVICHA ya vijana walio jitambua, BAVICHA inayo fanya kazi kwakusimamia Misingi, Falsafa na Itiadi ya CHADEMA.
-Demokrasi, Uadilifu, Uwajibikaji, Uwazi, Uzalendo na Ujasiri uliotukuka kwa maslahi mapana ya chama na Taifa letu ni TUNU zinazo muongoza Ephata Nanyaro mtakapompa ridhaa ya kuliongoza baraza la vijana wa CHADEMA (BAVICHA)
-Kuhakikisha dira kuu ya BAVICHA inafikiwa yaani vijana kuwa nguvu ya mabadiliko ya kidemokrasia kwa maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla-Kuwezesha sera sahihi, uongozi bora na kujenga oganizesheni dhabiti yavijana kwa maendeleo endelevu
-Mafunzo ya maswala ya kijamii (afya,uchumi,demokrasia,na uongozi)
-Chemichemi ya uongozi

Ni Ephata Nanyaro Mwenyekiti BAVICHA Taifa 2014 – 2019 kwa Baraza la Vijana imara na lenye uthubutu katika kupigania maslahi mapana ya vijana ndani ya Taifa letu kupitia CHADEMA.
*****************
10592887_542533219182237_6626805832997756445_n.jpg
"And there comes a time when one must take a position that is neither safe, nor politic, nor popular but he/she must do it because CONSCIENCE tells him it is RIGHT" - Ephata Nanyaro BAVICHA 2014-2019


View attachment 183459
 
Ni vizuri nanyaro akatafutiwa kitengo kingine, lakini suala la uenyekiti wa bavicha iende kwenye kanda nyingine, tusibeze jambo hilo lina madhara makubwa kwa wapiga kura wa kawaida!
 
Back
Top Bottom