Mhandisi Ndolezi Petro atangaza nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti Ngome ya Vijana ACT Wazalendo Taifa

DodomaTZ

Member
May 20, 2022
71
107
Hili hapa andiko la Mhandisi Ndolezi Petro ambaye ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti Ngome ya Vijana ACT Wazalendo Taifa katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 29 Februari, 2024:

Ndolezi Petro.jpg

UONGOZI NI VIJITI VYA KUPOKEZANA NAMI NAJIANDAA KWENDA KUCHUKUA KIJITI

Mhandisi Ndolezi Petro, Waziri Kivuli Sekta ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Katika Baraza Kivuli la Mawaziri wa ACT Wazalendo nina tangaza nia rasmi ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti Ngome ya Vijana ACT Wazalendo Taifa Katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 29 Februari, 2024.

Muda wa kampeni tutazungumza mengi lakini kwa uchache yaliyonisukuma ni dhamira na nia ya dhati ya kuwatumikia Vijana wenzangu na Watanzania kwa ujumla.

Ikumbwe kuwa kwa mujibu wa sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 takwimu zinaonyesha wenye umri chini ya miaka 36 ni aslimia 77% hivyo kwa kiwango hiki Vijana tunakila sababu ya kujipambanua na kuingia kwenye majukwaa yatakayotupa nafasi ya kupaza sauti zetu juu ya changamoto tunazozipitia.

Ndolezi Petro2.jpg

ACT Wazalendo muda wote kimeendelea kuwa chama ambacho kinajipambanua kwamba ni chama Cha masuala ya Wananchi na kimeendelea kutupa fursa Vijana kuonyesha vipawa vyetu. Hivyo nataka kutumia fursa hii kutia nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti Ngome ya Vijana ACT Wazalendo Taifa ili nitakapopata fursa ya kugombea na kushinda nikaungane na Vijana wa Mikoa na Majimbo na Watanzania kwa ujumla ili tuendelee kuunganisha nguvu ya pamoja kupaza sauti ya kutoa majawabu mbadala ya kisera juu ya changamoto mbalimbali zinazotukabili Vijana.

Vijana sio Taifa la kesho ni Taifa la leo na kesho kwani huko nyuma iliwezekana kwa viongozi wengi Kupambana kusaka ukombozi wa Bara la Africa wengi wao walikuwa Vijana na mfano mzuri ni Baba wa Taifa na Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere amekuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika akiwa na miaka 39 tu na kabla ya kufika umri huo alikuwa akipambana kuhakikisha Tanganyika inakuwa huru na aliweza kufanya hivyo 1961 tukapata Uhuru.

Ndolezi Petro1.jpg

Tubebe wajibu Vijana maana tunachangamoto nyingi zinazohitaji majawabu na tuweze kunufaika.

Wito wangu kwa Vijana wote tuendelee kujitokeza kushiriki mchakato huu wa kidemokrasia na tuendelee kujiweka pamoja kwenye jukwaa la ACT Wazalendo ili tuweze kuwakwamua Watanzania.

Waziri Kivuli Sekta Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Eng. Ndolezi Petro.
6 Februari, 2024.
 
Back
Top Bottom