Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,304
Hapo zamani kabla na baada ya mwalimu na hata wakati wa mwinyi ilikuwa mtoto akizaliwa mvua inanyesha anaitwa "mwamvua" akitanguliza miguu wakati wa kuzaliwa ataitwa "sikitu" akizaliwa ijumaa ataitwa "juma au mwajuma" akizaliwa jumapili ataitwa "pili" akizaliwa jumatatu ataitwa "tatu"
Kuna kipindi kukazuka watoto kuitwa majina ya watawala wa zama husika, hii ilitawala hasa kipindi cha kuanzia mwinyi ila sina uhakika kama bado kuna watoto wanazaliwa wanapewa majina kama Slaa, Mbowe, Kikwete n.k.
Ingekuwa enzi zile za mwalimu tungeshuhudia watoto wanaozaliwa katika kipindi hiki wakiwa wanamajina kama Dowans, Mbagala, Gongo la Mboto, Al adawi, Rostam,google, JF, You tube,hi5,IPTL, Songas, Mwakyembe na kadhalika kutokana na wakati wenyewe.
Jana nimesoma news sehemu nikaona kuwa nchini Misri kuna jamaa amemwita mtoto wake wa kike "facebook" kuapriciate mchango uliofanywa na facebook kwenye maandamano yaliyopelekea HM kuangushwa. Wapashaji habari wanasema mtoto huyo amepokea zawadi kem kem kutoka kwa vijana wengi wa kimisri. Nadhani hapa kwetu katika waliozaliwa kwenye mkesha wa tukio la gongo la mboto angepewa jina la gongo la mboto si ajabu watu wangemiminia mizawadi.